Kwanza
kabisa ndugu mdau wa blogu hii napenda Kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa
kutuvusha salama mwaka 2019, ni imani yangu kama unasoma hapa basi ni miongoni mwa waliovuka
salama hata ikiwa kulikuwa na changamoto za hapa na pale.
Kipekee
pia nikushukuru wewe kwa kuwa nasi 2019 yote na nikuombe kwa mara nyingine tena
kuendelea kuwa nasi 2020 kwani tunatarajia kuwa na mambo mzuri na muhimu zaidi
hasa katika sekta ya Viwanda (The 2020
Tanzania Industrial Revolution is Possible, Play your Part ! )
Pamoja na kwamba kila
mwaka inapofika mwezi January tumekuwa tukijiwekea Malengo lakini wengi wetu
inakuuwa vigumu kuyatimiza yote kikamilifu ifikapo Desemba. Pamoja na hayo
lakini malengo yatabakia kuwa ni kitu muhimu na kisichoweza kukwepeka kabisa
katika maisha.
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi
Watu wataendelea
kujiwekea malengo iwe ni January, June au Oktoba lakini tu kitu kimoja
kinachowatofautisha wale wanaofanikisha malengo yao kikamilifu na wale wasiofanikisha
vizuri ni njia wanayotumia(approach) katika kuyatekeleza malengo yao. Nakumbuka mwaka jana muda sawa na huu baada ya kuwatakia wasomaji wa blogu hii heri ya Krismasi na Mwakampya niliandika makala ambayo nilisisitiza umhimu wa mtu kuishi kama Mbayuwayu(Mwaka 2019 ishi kama mbayuwayu)
Mengi sana yamewahi
kuzungumzwa kuhusiana na suala hili la kujiwekea malengo lakini mimi hapa leo ningependa
kulizungumzia katika mtazamo wa ndege maarufu aitwaye Tai, jinsi anavyoendesha
maisha yake kwa kuwa kiumbe anayesifika zaidi Duniani kutokana na umahiri wake
wa kutimiza lengo lolote lile analojiwekea la kuwinda kwa ufanisi mkubwa.
TUNAJIFUNZA
MBINU ZIPI KUTOKA NA TABIA ZA NDEGE HUYU TAI?
Pamoja na nguvu na
uwezo mkubwa aliokuwa nao Tai wa kuona na kuruka juu angani lakini anazo pia
mbinu za ziada anazozitumia katika kutekeleza malengo yake wakati wa mawindo.
Mbiu hizo baadhi nitazitaja hapa chini;
(1) Tai haishi kwa hamasa wala mihemko bali yeye hujijengea mazoea
mazuri tokea utotoni akiwa kinda.
Tofauti na walivyo
ndege wengine kama Kunguru ambao ni mpaka pale wanapoona mzoga ndipo hupata
hamasa na kuanza kushangilia kwa kuitana, Tai yeye tayari anajua kabisa wajibu
wake kila siku ni kuwinda kitoweo hai siyo mizoga. Tai wanaanza kujifunza
kutoka kwa mama zao namna ya kuwinda na kuruka juu angani wakiwa na wiki 10 –
12 na baadae kuishi maisha yao yote katika mazoea hayo waliyofunzwa.
SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.
SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.
Kwa upande wetu sisi
Binadamu huwa tunafanya makosa makubwa sana tunapojikuta tukihusudu sana HAMASA
kama njia kuu ya kupata mafaniko na kusahau kujijengea MAZOEA ambayo ndiyo hasa
kiini cha mafanikio ya watu wengi unaowaona wamefanikiwa.
Unapojijengea mazoea
ya kufanya jambo fulani, jambo hilo hunasa katika akili yako ya ndani. Jambo
unalolifanya kama mazoea kila siku huwezi kuacha kulifanya hata siku moja,
lakini lile unalolifanya kwa hamasa ya muda mfupi, siku ukija kuamka huna
hamasa hutaweza kulifanya. Si kama nasema hamasa(mhemko) ni kitu kibaya hapana,
bali iambatane na kujijengea tabia ya
kutenda jambo kidogokidogo kila siku.
Mfano mzuri sana ni
ni wale watu wanaofanya mazoezi ya viungo maarufu kama watu wa ‘gym’. Watu hawa
huwa hawaoni kama ni kazi ngumu hata kidogo kuhudhuria gym kama ilivyo kwa watu
wengine wa kawaida wasiokuwa na mazoea hayo kutokana na mazoea
waliyokwishajijengea taratibu kwa muda mrefu. Kwa yule anayekwenda gym siku
mojamoja kutokana tu na pengine amehamasika baada ya kumuona baunsa aliyetuna
kifua akadhani na yeye anaweza akawa hivyo siku hiyohiyo, mara hamasa hiyo
itakapopoa na yeye unakuwa ndiyo mwisho wake wa kuonekana gym.
SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
(2) Tai
hawana wivu wa kijinga
Ukifanikiwa kuwaona
Tai wadogo wanapokuwa wakijifunza kuruka na kuwinda unaweza kucheka kwa jinsi
wanavyofanya makosa. Huanza kwa kuruka kidogokidogo kwenye miti ya karibukaribu
huku wakiwatazama mama zao vile wanavyoruka na kuwinda wakijua kabisa kwamba
kwao hakuna maisha bila ya kujua kuruka juu na kuwinda.
Tabia hii ya ndege
Tai kujifunza kwa weledi na umakini mkubwa haiwaruhusu kabisa kuwa na kitu
kinachoitwa WIVU WA KIJINGA, wala tabia nyinginezo za wizi na kunyanganyana
mizoga kama wafanyavyo kunguru kwa kuwa kila mmoja anakuwa na stadi zinazomwezesha kujitafutia
chakula mwenyewe.
Na sisi binadamu
yafaa sana tuige tabia hii ya tai ya kujifunza kwa bidii kutoka kwa wale
waliofanikiwa pamoja na wale waliotuzunguka, ni njia zipi rahisi wanazozitumia
mpaka wanafanikisha mambo yao kwa ufanisi na wala siyo kuanza kuwaonea vijicho
na husuda au kutafuta mbinu chafu za kuwashusha au kuwaangamiza. Wivu ni mbaya
sana kwani unazuia kabisa mtu kujifunza.
(3) Uwezo
wa kuona lengo lake kabla(VISION)
Macho yenye nguvu ya
Tai(Ana uwezo mara 8 zaidi ya ule wa binadamu) humwezesha kuona lengo (Kile
anachotaka kuwinda) mfano Sungura aliyeko umbali wa maili 2 kutoka alipo yeye
kabla hata ya sungura mwenyewe kushtuka kama ameonwa.
SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha na biashara.
SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha na biashara.
Binadamu na sisi
tunapaswa kujijenga uwezo wa kuyaona maisha yetu miezi/miaka kadhaa ijayo
mbele(na haya ndiyo malengo yenyewe). Ingawa ni kweli kuna mambo hutokea
yenyewe tu bila ya kuyapanga lakini mengi ni yale ambayo tunakuwa tumechagua wenyewe yawe jinsi
yanavyotokea. Mbinu hii inamwezesha mtu kubadilisha njia anazotumia kuyafikia
malengo yake kulingana na umbali au mazingira mengine yeyote yale atakayokutana
nayo njiani kabla ya kulifikia lengo lenyewe, sawa tu na Tai afanyavyo, mfano
kupunguza kasi, kushuka kidogo, kupanda kidogo, ilimradi tu aweze “kutarget” kitoweo
chake kwa usahihi.
(4)Tai
huwa haangalii fursa moja tu.
Tai chakula chake kikubwa ni samaki, lakini
usije ukafikiri anaweza kufa njaa ikiwa atakosa kabisa samaki hapana. Tai
anakula pia wanyama wengine kama vile, sungura, watoto wa nguruwe mwitu, ndege
wengine, nyoka, kobe, nguchiro, vindama vya mbuzi, vicheche na akizidiwa sana
anao uwezo hata wa kuwabeba watoto wa binadamu.
SOMA: Fursa za mafanikio kamwe hazitakaa ziishe lakini pia hazichumwi mtini kama embe.
SOMA: Fursa za mafanikio kamwe hazitakaa ziishe lakini pia hazichumwi mtini kama embe.
Maisha yanatakiwa mtu
ubadilike kulingana na mazingira uliyopo. Ijapokuwa malengo yako unayajua
lakini ni lazima katika mapambano ya kuyafikia utumie stratejia mbalimbali
zinazoendana na mazingira yale uliyopo. Lengo la Tai ni kujipatia mlo lakini si
lazima atumie samaki tu peke yake, halikadhalika na wewe inawezekana unayo
malengo ya kupata kiasi fulani cha pesa, si lazima uuze mchicha tu uliozoea
kuuza ndippo upate kiasi hicho cha pesa, ukiona hata inawezekana kwa kuuza
kahawa ukapata hicho kiasi, basi wewe nenda kauze kahawa ili mwisho wa siku
lengo lako liweze kutimia lakini si kubadilisha gia angani kwa kubadilisha au
kuyaacha malengo yako kirahisirahisi
kabla hujayatimiza na kuweka mengine kabla ya muda kutimia.
Je na wewe 2020
Ungependelea uishi kama ndege yupi? Tai au Kunguru? Binafsi jibu langu nitakupa
siku nyingine.
Asante sana na
tukutane tena wakati mwingine
Mwanaviwanda/Industrialist
Peter Augustino
Tarimo
The
2020 Tanzania Industrial Revolution is Possible, Play your Part !
..................................................................................................
..................................................................................................
1. Mwaka 2020 njia za kupata
Vitabu na huduma zetu zote zimerahisishwa mara dufu baada ya maboresho ya hali
ya juuu;
2.
Kujipatia
vitabu vya karatasi wasiliana nasi au fika BRIGHT BOOKS & STATIONERY, MBEZI(Kibanda cha
mkaa). Kwa softcopy lipia kwa namba, 0765553030 au 0712202244, na utatumiwa ndani ya dk.5 tu
3.
KITABU CHA DUKA LA REJAREJA 2020 KIMEONGEZEWA MAMBO MENGI
MAZURI, HEBU YACHEKI KWA KUBONYEZA JALADA HAPO CHINI;
1. UNAWEZA PIA KUFAHAMU
ZAIDI KUHUSU KITABU CHA MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI KWA KUBOFYA
JALADA HAPA CHINI;
KUPATA MAELEZO YA KINA KUHUSU KITABU CHA MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA BONYEZA JALADA HAPO CHINI;
0 Response to "MWAKA 2020 ISHI KAMA TAI, USIKUBALI TENA KUISHI KAMA KUNGURU"
Post a Comment