Leo mmoja wa wadau wetu kwa jina Luca M. (Huwa hatutaji jina kamili bila ridhaa ya muulizaji) ameuliza swali lake katika safu hii na bila ya kuongeza au kupunguza chochote kile swali hilo naliweka hapa chini na majibu yake yatafuata chini yake;
SWALI:
“Nataka
kufungua duka la rejareja la mahitaji ya kila siku katika jamii mbinu gani
naweza kutumia kufanikisha”
MAJIBU:
Duka la rejareja ni biashara rahisi sana
kuanzisha ikiwa tayari unao mtaji na eneo la kuweka duka lako. Yapo mambo
muhimu 10 unayopaswa kuyazingatia kabla hujaanzisha biashara yako ya duka la
rejareja na mambo hayo niliyaelezea kwa kirefu katika kitabu changu cha SIRI YA
MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA katika ukurasa wake wa 7
SOMA: Kuwa Bilionea naweza kutumia mbinu zipi?
SOMA: Kuwa Bilionea naweza kutumia mbinu zipi?
Nitaelezea mambo machache lakini mengine kwa
kirefu unaweza ukatafuta kitabu hicho kwani sitaweza kuyaeleza hapa yote.
1. Kwanza
kabisa kama ilivyo kwa biashara nyingine zozote zile unahitaji kufanya utafiti
pamoja na kuandaa mpango wa biashara yako utakavyokuwa.
Zoezi hili usiniambie eti hutaliweza au ni mambo ya kitaalamu yanayomhitaji
msomi aje akufanyie, la hasha. Utafiti na mchanganuo wa biashara hata mtu
ambaye hajakanyaga shule ya vidudu hufanya kabla hajaanzisha biashara yeyote
ile. Hapa ndipo maswala kama utapata vipi mtaji, utauza bidhaa zip nk. yanapojibiwa
na katika kitabu yameainishwa yote hasa katika shuhuda mbalimbali za watu.
Hivi kuna mtu ambaye katika Ulimwengu wa leo
hajawahi kufanya biashara hata ya kuuza karanga hata kama hajasoma? Ni dhahiri
kabisa kwamba biashara na ujasiriamali hauchagui kiwango cha elimu ya mtu hivyo
na utafiti au mchanganuo nao pia haujalishi umesoma au hujasoma ni lazima mtu
afanye kabla hajaanzisha biashara yeyote ile. Kwa kifupi kabisa utafiti na
mchanganuo wa biashara ni karibu kitu kimoja hichohicho na ikiwa hujui uanzie
wapi basi nikuambie tu si kitu kigeni kwako kwani umeshawahi kufanya pasipo
hata wewe kujua kama uliwahi kufanya.
SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu
SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu
Utafiti au mchanganuo wa biashara kwa kifupi zaidi
ni maswala yote unayoyawaza juu ya biashara yako na kutaka kujua yanafanywa
vipi kabla hujaanza kuifanya biashara yenyewe na wala siyo sayansi ya kwenda
mwezini au sayari ya Mars. Ili uweze kuifanya biashara au shughuli yeyote ile kwa ufanisi wa
kutosha ni sharti kwanza uchunguze biashara au shughuli hiyo
inafanyikafanyikaje, na huo ndio utafiti au mchanganuo wa biashara yako.
2. Pointi
ya pili ni kuirasimisha biashara yako.
Hata ikiwa hautasajili kampuni lakini ni
lazima ukitaka biashara yako ya duka isiwe na vikwazo basi angalau uhakikishe
unaisajili katika ngazi ya serikali za mitaa kwa kwenda katika manispaa yako
wakupe leseni ya biashara. Kuna suala pia la namba ya utambulisho(TIN namba)
kwa ajili ya kulipa kodi ya mapato ikiwa biashara yako ni kubwa kidogo nk. Ukipenda unaweza ukasajili Brela jina la biashara yako pia.
3. Pointi
ya tatu ni kuchagua eneo la biashara yako,
Watu
husema “Biashara ya duka la rejareja ni eneo” Eneo
utakalochagua kuweka duka lako, litaathiri kila kitu utakachokifanya katika biashara yako yote. Mafanikio au kuanguka kwa biashara yaduka la rejareja kunategemea kwa asilimia kubwa sana sehemu ulipoiweka biashara hiyo. Usikurupuke wakati wa kufanya uamuzi wa eneo utakaloweka biashara yako ya duka, chukua muda wa kutosha kufanya utafiti
na kuwa mvumilivu.
SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?
utakalochagua kuweka duka lako, litaathiri kila kitu utakachokifanya katika biashara yako yote. Mafanikio au kuanguka kwa biashara yaduka la rejareja kunategemea kwa asilimia kubwa sana sehemu ulipoiweka biashara hiyo. Usikurupuke wakati wa kufanya uamuzi wa eneo utakaloweka biashara yako ya duka, chukua muda wa kutosha kufanya utafiti
na kuwa mvumilivu.
SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?
Ukigundua
eneo halifai, basi ni bora ukaahirisha na kuangalia uwezekano
wa eneo jingine kuliko baada ya
muda mfupi kuja kuanza kuzozana na mwenye nyumba akurudishie kodi au hata biashara yako kufia njiani.
Usikubali presha za madalali ambao hutumia ujanja kwa
kukuambia eti, eneo/fremu fulani inagombewa na watu
zaidi ya watatu na wewe ni wa nne,
hivyo ukichelewa kidogo tu hutaikuta.
Katika toleo jipya la kitabu hicho la mwaka
2020 tumeongeza shuhuda mbalimbali za watu jinsi walivyoanzisha maduka yao ya
rejareja ukiwemo ushuhuda wake mwenyewe binafsi mwandishi wa kitabu hiki Bwana
Peter Augustino Tarimo. Ushuhuda huo upo katika picha za rangi.
SOMA: Tunatuma vitabu vya ujasiriamali mkoa wowote ule Tanzania kwa usalama wa asilimia 100% wa fedha ya mteja
SOMA: Tunatuma vitabu vya ujasiriamali mkoa wowote ule Tanzania kwa usalama wa asilimia 100% wa fedha ya mteja
Basi naamini mpaka kufikia hapo ndugu Lukas
utakuwa umeshapata mwangaza walau ni mambo gani ya msingi zaidi mtu unayopaswa
kuyazingatia ikiwa una ndoto za kuanzisha duka lako la rejareja mtaani.
Tunakaribisha maswali mafupimafupi kama haya na
tutayajibu bila ubaguzi wowote ule. Lakini pia ukipenda kuwa karibu zaidi na
sisi ili kujifunza mambo mengi zaidi kutoka kwa watu mbalimbali unaweza kujiunga
katika magroupu yetu ya Watsap na Telegramu ya MICHANGANUO-ONLINE. Masomo ni kila siku na mada zetu ni Michanganuo
ya Biashara mbalimbali pamoja na masomo yenye maudhui ya Pesa yasiyopatikana
mahali kwingine kokote.
SIMU/WATSAP: 0765553030
SIMU/SMS:
0712202244
0 Response to "NATAKA KUFUNGUA DUKA LA REJAREJA LA MAHITAJI YA KILA SIKU KATIKA JAMII, MBINU GANI NAWEZA KUTUMIA KUFANIKISHA?"
Post a Comment