Maswali mengi yanayofanana na hili yamewahi kuulizwa hapa
na wadau wengine mbalimbali na siku za nyuma nimewahi pia kutoa majibu yake katika blogu hii ya
jifunzeujasiriamali likiwemo hili la Mtaji wa kuanzisha biashara ya kuuzavochaza simu jumla, million mbili inatosha?
Sababu kubwa iliyonifanya leo kujibu swali lililoulizwa
na mdau wetu mmoja ajulikanaye kwa jina la James ni kuwa kuna kitu kimoja cha
tofauti nilichokiona katika swali lake hili nacho ni kuwa, ana mtaji wa milioni
moja lakini alioipata kwa njia ya mkopo kutoka mahali fulani na anataka
auzungushe mtaji huo ndani ya miezi mitatau tu kabla hajatakiwa kuurejesha wote
kwa wenyewe.
Maswali mengine mengi niliyokuwa nikiwajibu wadau
hapo kabla yali ‘base’ zaidi kwenye mitaji waliyojidundulizia wenyewe kutokana
na shughuli zao mbalimbali, zawadi au ruzuku na hakuna wa kuwadai endapo mitaji
hiyo ingemezwa kwenye biashara walizotaka kufanya.
Bwana James kupitia njia ya watsap aliuliza kama
ifuatavyo,
“Nina
mtaji wa Milioni 1 kwa sasa. Hiyo hela nimekopa kwa miezi 3 riba yake 10% kwa
muda huo. Malengo niliyokuwa nimejiwekea
yamekufa hivyo nimebaki na pesa hiyo ambayo natakiwa kuirejesha kwa
wausika. Je nifanye nini kwa hiki kipindi kilichobaki kuhakikisha narejesha
mkopo, riba pamoja na kupata faida kidogo?”
Majibu
kwa swali la Bwana James;
Habari Mr. James na nashukuru kwa kuuliza swali juu ya
changamoto ya kimtaji inayokukabili kwa sasa.
Ijapokuwa pesa za mkopo ni chanzo kizuri sana cha mtaji
wa kuanzisha na kuendeshea biashara mbalimbali, lakini pia ni vigumu sana
kuzitumia fedha za mkopo kuanzishia biashara mpya kabisa tena ambayo wala hukuwa
na malengo ya kuifanya muda ulipokuwa ukikopa hizo fedha. Isitoshe pia
haishauriwi mahali popote pale Duniani mtu kwenda kukopa kwanza ndipo uje
ufikirie biashara ya kufanya na huo mkopo. Kanuni inamtaka kila mkopaji awe na
chakufanya kwanza kabla hajainua mguu wake kwenda benki au taasisi yeyote ile
ya mkopo.
Kwa mantiki hiyo, fedha za mkopo watu hufanyia biashara
ambazo tayari zilishaanza kuzalisha faida, au la basi ikiwa utaamua kuanzishia
mradi mpya kabisa, basi uwe tayari unao mradi mwingine kama “back up” ambao
utatumika kufanya marejesho ya mkopo endapo itatokea huo mradi mpya umefeli
kuzalisha faida ya lulipa marejesho ya mkopo.
Hata hivyo Bwana James ikiwa tayari umejikuta katika
situesheni kama hiyo kama ulivyoeleza, basi mimi nakushauri, jitahidi kutafuta
walau njia yeyote ile utakayoitumia kujiingizia kipato bila ya kuhatarisha
kabisa hiyo hela ya mkopo uliyonayo uhakikishe umelipa kwanza denial watu kasha
sasa ndipo uje ujipange mwenyewe upya kwa ajili ya malengo mengine ukiwa hauna
deni lolote linalokupa msongo wa mawazo. Ukisha hakikisha sasa una chanzo cha
kipato ambacho kina uwezo wa kuzalisha pesa pasipo kutegemea mkopo basi unaweza
kwenda kukopa ili kutanua zaidi wigo wa biashara hiyo na kwa kufanya hivyo
haitakuwa tena rahisi mtaji wako au mkopo kumezwa katika biashara.
Nikutakie shughuli njema,
Peter Augustino Tarimo.
Mshauri
Biashara & Ujasiriamali na Mwanaviwanda 2020
WHATSAPP: 0765553030
SIMU: 0712202244
Nikiwa na millioni moja na nusu ila co za mkopo ni zangu binafsi,,,je nifanye biashara gani ambayo inaweza kuniridhisha ndani ya miezi 6?
ReplyDelete