Hakuna mtu yeyote leo hii Duniani hata awe
Donald Trump mwenyewe anayeweza akasimama na ‘kujimwambafy’ kuwa eti biashara
yake inadunda kama kawaida wala Covid 19 haijaitikisa. Hata ukiangalia zile
biashara zenye kinga maalumu dhidi ya majanga nilizoziandikia makala wiki
chache zilizopita, tayari sasa nazo zimekwishaanza kusukwasukwa na mawimbi ya
corona mithili ya meli kubwa inayokumbwa na dhoruba kali.
Wengi wetu tumebakia tu tumeduwaa tusijue ni
nini cha kufanya. Hakika haijawahi kutokea miongo ya hivi karibuni!
Pamoja na hali hiyo ya kutisha ngoja
nikusimulie mkasa wa ndege mmoja mpole sana lakini cha kusikitisha mpaka
ninapoandika hapa sasa tayari ndege huyo alishatoweka katika uso wa dunia hii
siku nyingi na inasemekana kuwa ni sisi Binadamu tuliochangia kutoweka kwake.
SOMA: Wanasayansi wagundua mnyama wa ajabu
SOMA: Wanasayansi wagundua mnyama wa ajabu
DODOO ni ndege wakubwa walioishi katika
mapori na misitu ya Kisiwa cha Mauritius kilichopo katika Bahari ya Hindi.
Kabla ya Wazungu kuingia katika kisiwa hiki miaka ya 1500, Mauritius kilikuwa
hakijawahi kukaliwa na binadamu yeyote yule wala wanyama zaidi ya aina chache
tu za ndege akiwamo na huyu Dodoo.
Hivyo Dodoo waliishi Mauritius kwa Amani na
utulivu pasipo hatari yeyote ile kwa mamilioni ya miaka iliyopita huko nyuma.
Kwa mara ya kwanza kabisa Wareno ndio waliokuwa binadamu wa kwanza kukanyaga
katika kisiwa hiki hapo mwaka 1505 na mara moja Kisiwa cha Mauritius kikaanza
kuwa kama kituo kikubwa cha Meli zilizokuwa zikifanya biashara ya viungo baina
ya Ulaya na nchi nyingine za Mashariki ya mbali na Asia.
SOMA: Kumbe sokwe hugawana vitu sawa na binadamu.
SOMA: Kumbe sokwe hugawana vitu sawa na binadamu.
Dodoo waliokuwa na uzito hadi kilo 20
wakaanza kugeuka wahanga kwa kuwa kitoweo cha Mabaharia wa meli zilizotia nanga
katika kisiwa cha Mauritius. Baadae Wadachi nao walikitumia kisiwa hiki kama
makazi kwa wafungwa waliohamishwa kutoka huko kwao. Wafungwa hawa walihamia
huko wakiwa na wanyama mbalimbali wafugwao na wasiofugwa kama vile Nguruwe,
Nyani, Paka na mbwa.
Taratibu ndege Dodoo waliendelea kupungua
siyo tu kwa sababu ya kufanywa kitoweo bali pia wanyama waliohamia na Wadachi
nao walianza kuwawinda Dodoo kila kona na kuwatafuna. Ndani ya kipindi cha takribani
miaka 100 tu mpaka kufikia1680 Dodoo wakawa ni ndege waliotoweka kabisa
Duniani.
SOMA: Njia mpya za kufanya mambo, Dunia, Biashara, Ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
SOMA: Njia mpya za kufanya mambo, Dunia, Biashara, Ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
Sasa
basi stori hii inatufunza nini kuhusiana na biashara zetu wakati huu mgumu wa
Janga la Corona (Covid 19)?
Sawa tu na Dodoo walivyoishi kisiwani
Mauritius kabla ya Wazungu kuingia kisiwani humo, biashara nyingi kabla ya Desemba
2019 zilikuwa zikishamiri kama kawaida na hakukuwa na hatari kubwa
iliyozikabili na uchumi kote duniani ikiwemo Tanzania ulikuwa ukikua kwa
viwango vya kuvutia.
Lakini ujio wa Corona tangu December 2019 ilikuwa
sawasawa na kipindi cha ujio wa Wareno kule Mauritius mikaka ya 1500. Mpaka
kufikia hii Apili 2020 biashara karibu zote zinachechemea, zimepoteza wateja na
hazina tena uwezo wa pesa wa kujitangaza wala muda kwani watu kote duniani
imewabidi wajifungie majumbani mwao.
SOMA: Kufa au kuanguka kwa biashara yako ndogo fanya vitu hivi 9 kujiepusha
SOMA: Kufa au kuanguka kwa biashara yako ndogo fanya vitu hivi 9 kujiepusha
Hamna tofauti na jinsi ndege Dodoo
walivyopoteza uhuru wao wa kutembea kokote wapendako kisiwani Mauritius.
Imekuwa ni sawa na kipindi kile cha ujio wa Wadachi wakiwa na wanyama kama
nguruwe, nyani, paka na mbwa kuja kupiga kambi kwenye kisiwa hicho kilichokuwa
hakikaliwi na mtu kwa mamilioni ya miaka hapo kabla.
Sasa
basi tunaweza kufanya kitu gani kuweza kuzinusuru biashara zetu kama hali
yenyewe ndio hivyo ilivyo?
Hakuna njia nyingine zaidi ya kubadilika na
kuendesha biashara zetu kulingana na mazingira yalivyo. Badala ya kuanza
kujifungia majumbani na kusubiri serikali ije ituletee unga, ni lazima tuwe
wabunifu, tusibakie tu kuwa wapole kwa corona kama Dodoo walivyoendelea kubakia
kuwa wapole mpaka wakamalizwa wote.
SOMA: Unawezaje kuyakabili magumu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
SOMA: Unawezaje kuyakabili magumu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
Wangelijua mapema wakajifunza hata kujificha
kwenye mapango au kuruka juu kama ndege wengine mfano Tai nk. pengine Dodoo wangelikuwa
wanaishi mpaka leo hii. Lakini badala yake Dodoo hawakufanya mabadiliko yeyote zaidi
ya kuendelea kuishi maisha waliyozoea kuishi hapo kabla
Mwanasayansi mashuhuri Charles Darwin aliwahi
kusema hivi;
“Viumbe
watakaopona na kuishi duniani siyo wale wenye nguvu nyingi sana bali ni wale
watakaojibadilisha ili kuendana na mabadiliko ya kimazingira wanayoishi”
Tusikubali kuwa kama Dodoo, tubadilishe namna
ya kufanya biashara zetu kabla hazijafa.
Tutafute njia mbadala za kufanya biashara
zetu sasa kwa mfano, tuvae barakoa(mask), tuoshe mikono kila mara, tuzingatie
umbali wa mita moja na hata zaidi ya huo. Ikiwa biashara inafaa kutumia mtandao
wa intaneti basi tuitumie zaidi nk. Cha kutia faraja ni Serikali yetu kutambua
umuhimu huo wa kutumia njia mbadala za kupambana na janga hili kuliko kufungia watu
moja kwa moja (total lock down).
SOMA: Usiogope, mabadiliko katika maisha ni kama plasta, ikishabanduka kidonda hupona chenyewe.
SOMA: Usiogope, mabadiliko katika maisha ni kama plasta, ikishabanduka kidonda hupona chenyewe.
Basi na sisi wananchi tujiongeze maambukizi yasiongezeke ili tuendelee kuwa angalao na huru tukifanya biashara
zetu. Katika nyumba zetu za ibada pia tuwe makini tusali tukiwa na tahadhari
zote, tofauti na wanyama Mungu ametupa akili na maarifa yote ya kisayansi kwa
lengo la sisi kuyatumia maarifa hayo kujisaidia na siyo kujibweteka na kusubiri
Mungu atuokoe na Janga pasipo sisi kuwajibika.
Kitu kingine cha msingi sana cha kufanya kipindi
hiki ili biashara zetu zisiwe kama Dodoo ni KUTOA THAMANI KWA MTEJA. Uza thamani na wala siyo bidhaa au huduma,
kwa kuwauzia thamani wateja wako hawatakusahau kamwe hata baada ya janga hili
kupita. Kuwauzia wateja thamani maana yake ni kutatua shida walizokuwa nazo kwa
weledi kushinda matarajio yao.
…………………………………….
TANGAZO MUHIMU
2. Kujiunga
na Group letu la Watsap na Telegram la masomo ya Fedha na Michanganuo kila
siku, lipa kiingilio shilingi 10,000/= kupitia namba; 0765553030 au 0712202244
kisha utume ujumbe usemao, “NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE NA OFFA YA VITU 6”
3. Unaweza
pia kujipatia vitabu vyetu vifuatavyo (softcopy) kwa bei ya punguzo, ukinunua
vyote 3 ni shilingi elfu 15 tu badala ya elfu 18. Punguzo hili ni kwa muda
mfupi. Hardcopy pia vinapatikana .
0 Response to "NDEGE WA AJABU ALIYETOWEKA DUNIANI NI FUNZO KUBWA KWA BIASHARA ZETU KIPINDI HIKI CHA JANGA LA CORONA (COVID 19)"
Post a Comment