Kabla
hatujaendelea na sehemu yetu hii ya 4, ningependa kusisitizia kidogo mambo haya
mawili yafuatayo;
1. Kumbuka
kwamba sehemu hii ya soko ndiyo muhimu sana kwa mjasiriamali yeyote yule kwani
biashara bila soko la uhakika haiwezi kuwa endelevu. Lakini soko halizuki tu
hivi hivi kama uyoga porini hapana. Ni lazima ulitengeneze, ni biashara chache
sana siku hizi hupata bahati ya kujiuza zenyewe, usemi ule wa kale, “Kizuri chajiuza, na kibaya chajitembeza”
umegeuka “vice versa”.
2. Pia
nikukumbushe tena kwamba, jipatie mchanganuo kamili wa USADO Milling kwani
licha ya kuutumia ukifuatilia semina hii lakini utajifunza mambo mengi
kuhusiana na ubunifu katika kiwanda chochote kile kidogo. Unaweza ukatumia baadhi ya mikakati iliyotumika
katika mchanganuo huu kwenye biashara yako unayotarajia au uliyokwisha ianzisha
tayari hata kama siyo ya usagishaji nafaka. Bei yake ni sh. Elfu 10 tu,
nakutumia kwenye simu yako pamoja na offa ya vitabu na michanganuo mingine
mizuri.
Hebu sasa tuendelee na semina yetu………
4.0
TATHMINI YA SOKO
Maelezo mengi kwenye Sura hii yanatokana na majibu ya utafiti
ule wa soko. Vipengele vinavyotakiwa kuelezewa ni hivi vifuatavyo ingawa katika
Mpango wa USADO inawezekana kuna vilivyoachwa au kuna vilivyoongezeka pia;
4.1
Mgawanyo wa soko
4.2
Soko lengwa
4.2.1
Mahitaji ya soko
4.2.2
Mwelekeo wa soko
4.2.3
Ukuaji wa soko
4.3
Tathmini ya sekta
4.3.1
Washiriki katika sekta
4.3.2
Usambazaji
4.3.3
Ushindani
4.3.4
Washindani wako wakubwa
Kama kawaida baada ya kuacha nafasi ndogo ya Muhtasari nitaenda
kuanza moja kwa moja na kipengele kidogo cha “4.1”
4.1
Mgawanyo wa soko
Kwenye mgawanyo wa soko nimeelezea kwanza soko USADO
inalolilenge kwa ujumla kwamba ni eneo zima la jiji la Dar es salaa na Mkoa wa
Pwani. Lakini nazidi kuchuja soko hilo kwa kutaja vipande au makundi 3 ya
wateja inaowalenga ambao ni Maduka ya rejareja, Maduka ya jumla na Wanunuzi
mmoja mmoja wa dona. Kisha kila kundi au kipande nimekielezea sifa zake zikoje.
4.2
Mkakati wa Soko lengwa
Hiki ni kipengele kingine kidogo kwenye Soko na kama tulivyoona
kile kilichotangulia, hiki tunazidi kuchuja ili kupata kipande cha soko
kinacholengwa zaidi ambacho ni kundi au kipande cha “Maduka ya rejareja”. Naweza pia kuelezea ni kwanini kampuni
imeamua kuchagua kipande hiki cha soko, uhusiano wake na vitu kama bei, ubora
nk.
4.2.1
Mahitaji ya Soko
Hiki ni kipengele kidogo kwenye soko lakini chini ya kipengele
kidogo cha soko lengwa hapo juu na kinaelezea namna soko lengwa linavyohitaji
bidhaa ya unga wa dona. Nilionyesha kulingana na utafiti uliofanyika wingi wa
watu au kaya zinazohitaji unga wa dona kila siku katika mikoa ya Pwani na Dar
es salaam hivyo kufanya maduka ya rejareja kuwa na mahitaji makubwa ya kuuza
unga wa dona.
Nikaelezea pia ni kwanini wateja hupendelea sana kula dona
lakini ajabu ni kwamba huwa hawanunui dona na badala yake hununua zaidi sembe. Katika
utafiti unajua wateja walipoulizwa walijibu kitu gani? Basi ndicho nilichokiandika
hapo kisome.
4.2.2
Mwelekeo wa soko
Ni kipengele kingine kidogo chini ya soko lengwa na nimeelezea
mielekeo kwa maswala mbalimbali yanayoweza kuliathiri kundi hili la soko
linalolengwa. Masuala hayo 3 niliyataja kuwa ni, Hali ya kisiasa, Hali ya hewa
na Hali ya Ulaji wa watu.
4.2.3
Ukuaji wa Soko.
Katika kipengele hiki nimejaribu kuonyesha
jinsi soko linalolengwa na USADO uwezekano wake wa kukua ulivyo na nikataja
takwimu mbalimbali kwa mujibu wa Mamlaka ya Takwimu ya Taifa (NBS), mamlaka
nyingine za serikali kuu na serikali za mitaa. Takwimu hizi hupatikana kwenye
utafiti wa dawati uliofanywa kabla ya zoezi hili kuanza.
4.3
Tathmini ya Sekta
Hiki ni kipengele kidogo kinachojitegemea
katika Sura ya soko na nimeielezea sekta nzima ya Usagishaji nafaka nchini,
washiriki wake na muelekeo wake kwa ujumla ulivyo.
4.3.1
Ushindani
Ni kipengele kidogo cha Soko lakini chini ya
kile cha ‘Tathmini ya Sekta’ na katika hiki nilitaja ushindani kwenye sekta ya
usagishaji nafaka, wadau hasa hushindania kitu gani. Pia nikataja washindani
wakuu wa USADO Milling ni kina nani, wana sifa zipi na USADO Milling
wanatofautiana vipi na hawa washindani wote watatu.
SEMINA SIKU-2 SEMINA SIKU-4
SEMINA SIKU-2 SEMINA SIKU-4
Mpaka kufikia hapo ndugu msomaji wangu sehemu hii ya 4, Tathmini ya soko ndio tunafika tamati lakini sehemu ya 5, Mikakati na Utekelezaji ni siku ya kesho Mungu akitujalia afya.
Usisahau kujikinga, Barakoa ni muhimu
hata ukikosa ya kununua kuwa mbunifu mwenyewe, jitengenezee hata ya leso na
raba bendi inasaidia ilimradi iwe na layer 2 kuliko kutembea bila kinga yeyote hasa maeneo hatarishi
kama sokoni, stendi za mabasi na hospitalini. Mtu anaweza akapiga chafya ghafla
au kukohoa matonetone yatatua juu ya leso au barakoa yako badala ya puani au
mdomoni moja kwa moja.
…………………………………..
0 Response to "SEMINA SIKU YA 3: MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUSAGA NAFAKA (DONA) HATUA KWA HATUA"
Post a Comment