Ikiwa ni siku ya mwisho ya semina yetu
hii, leo tunaangalia sura ya mwisho ya mchanganuo wa biashara ya kiwanda cha
Usagishaji unga wa dona cha USADO Milling, Vielelezo au Viambatanisho.
Sura hii huwa haina vitu vingi sana
labda tu mchanganuo wako nao uwe mrefu sana. Kimsingi huwekwa au kuambatanishwa
vile vitu ambavyo hukuweza kuviweka ndani ya mchanganuo wako kutokana na urefu
au umuhimu wake kutokuwa mkubwa sana kwa ajili ya msomaji wako kufanya marejeo
atakapohitaji kufanya hivyo.
9.0
VIELELEZO
Katika kipengele hiki cha vielelezo kuna vitu
vingi ningeweza kuambatanisha lakini hapa nimeweka Majedwali mbalimbali ya
hesabu ambayo sikuweza kuyaweka ndani ya sura za ndani za mchanganuo wenyewe.
Ningeliweza pia kuweka, mikataba ya biashara
USADO iliyofanya na wadau wake mbalimbali, picha na ramani, kopi za matangazo,
CV za viongozi, nyaraka za dhamana za mikopo, nyaraka za utafiti uliofanyika nk.
Mpaka kufikia hapa ndugu msomaji wangu nimefikia tamati ya mafunzo haya yaliyochukua siku 7. Mafunzo haya utanufaika nayo zaidi endapo tu utayafuatilia huku ukiwa na Mpango kamili wa biashara ya kiwanda cha USADO Milling pamoja na Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
Kitabu ambacho kina mafunzo ya kina kabisa
juu ya uandaaji wa michanganuo ya biashara. Kitabu hiki kinafundisha namna mtu
anavyoweza kuandika Mpango wa biashara yeyote ile kwa njia rahisi pamoja na
mifano ya Michanganuo ya biashara mbalimbali zilizofanyiwa utafiti wa kina.
Kitabu pia kina course nyingine zote
za Biashara na ujasiriamali mjasiriamali yeyote anazohitaji.
Karibu pia katika magroup yetu ya Whatsap na
Channel ya Telegram kwa ajili ya mafunzo zaidi ikiwa utahitaji. Magroup yetu ya
MICHANGANUO-ONLINE ukijiunga mafunzo
ni mwaka mzima kwa malipo ya mara moja tu sh. 10,000/=, huwa hatuna malipo yaliyojificha nyuma ya pazia.
Masomo yetu makuwa kila siku yanahusu vitu
viwili vifuatavyo
(1) Michanganuo ya Biashara bunifu
zinazolipa
(2) Fedha/Financia Literacy.
Aidha mada nyinginezo kuhusiana na biashara,
ujasiriamali na maendeleo binafsi kwa ujumla vinapewa nafasi.
Asante sana.
PETER AUGUSTINO TARIMO
WHATSAPP/CALL: 0765553030
SMS/CALL: 0712202244
SEMINA SIKU-6
0 Response to "SEMINA SIKU YA 7: MPANGO WA BIASHARA, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA HATUA KWA HATUA (USADO MILLING)"
Post a Comment