Jana katika sehemu ya kwanza ya somo hili (Usilaumu kukosa pesa bali njia iliyokufikisha pale ulipo) tuliishia kwa kuahidi kwamba leo tungeendelea na sehemu ya pili inayoelezea hatua za kuchukua ili kuzuia mtu kujikuta katika hali ngumu ya kifedha baada ya kupita nyakati na vipindi vyenye fursa mbalimbali za kiuchumi.
Hatua hizo pia zinaweza zikachukuliwa hata na
mtu ambaye tayari ameshajikuta yupo kwenye hali kama hiyo ya mkwamo mbaya wa
kiuchumi katika harakati zake za kujinasua ili kuweza tena kusonga mbele. Hatua
zenyewe ni hizi zifuatazo;
1. Jiwekee
kinga na wale wanaokutegemea(Familia)
Kabla hujaanzisha kuwekeza au kufanya
biashara hakikisha unajiwekea bima mbalimbali kama vile,bima ya maisha, bima ya
matibabu na hata ikiwezekana bima kwa ajili ya nyumba na gari yako.
2. Anza
Mapema.
Kuna maajabu katika kuanza jambo lolote lile
mapema. Hakikisha unaanza tabia ya kujiwekea akiba kungali bado mapema
iwezekanavyo. Yamkini wewe ni mwanafunzi sasa hivi na miaka yako pengine ni 20,
22, 25 nk. huu ndio muda muafaka wa kujizoesha tabia hiyo. Haijalishi pia hata
ikiwa tayari umri wako umeshasonga, bado unaweza ukaanza sasa kabla muda
haujakwenda zaidi kwani hi heri kuanza leo kuliko kuja kuanza baada ya tuseme
miezi miwili au mitatu ijayo.
3. Omba
au tafuta Msaada/Ushauri
Siyo kila mtu anao uwezo wa kupanga na
kusimamia fedha zake mwenyewe inavyotakiwa. Kama katika eneo hilo unajijua
haupo vizuri basi tafuta ushauri wa kitaalamu mahali au hata unaweza kujifunza
mwenyewe kwa kusoma vitabu mbalimbali na kuhudhuria semina zinazohusiana na
usimamizi mzuri wa fedha. Usiogope kutumia gharama kidogo kupata ushauri bora
wa kifedha. Jiunge na magroup makini ya whatsapa, facebook nk.
SOMA: Maajabu ya Nguvu ya Ushirika, Umoja ni nguvu
4. Fuatilia
na Kuweka Kumbukumbu za Mali na Madeni uliyokuwa nayo.
Thamani halisi ya mali zako unazomiliki
utaijua kwa kuchukua thamani ya mali zote ulizonazo na kutoa thamani ya madeni
yote unayodaiwa na watu au taasisi mbalibali zikiwemo zile taasisi za fedha
kama vile benki, vicoba au saccos. Fuatilia na kujua pia mtiririko wako wa
fedha upoje. Baadhi ya mambo haya tulishajifunza hapa katika group hili la
Michanganuo-online.
5. Hakikisha
biashara au Uwekezaji wako unakua na kuongezeka hata unapokuwa umelala usiku
Maana yake ni kwamba unatakiwa uhakikishe
unawekeza katika biashara au vitegauchumi vilivyokuwa na uwezo mkubwa wa
kurudisha fedha zako ulizowekeza. Buni mfumo wa biashara au miradi ile
isiyokulazimisha kuwepo pale muda wako wote.
6. Orodhesha
Matumizi yako yote ya Mwezi.
Zoezi hili litakuwezesha kujua ni wapi fedha
zako zinakotumika kwa wingi kusudi uweze
kubalansi matumizi yako na kuelekeza fedha nyingi zinazotokana na mapato
yako kwenye maswala yale ya msingi zaidi kama vile uwekezaji na kuweka akiba. Unaweza
kuamua labda tuseme mapato yako asilimia 35 ukayapeleka katika kulipia gharama
na matumizi mbalimbali, asilimia 30% kwenye kulipa madeni, asilimia 30% mpaka
32% kwenye uwekezaji na kiasi kinachobakia ukakiingiza kwenye akiba yako.
7. Mshirikishe
Mwenzi wako.
Kama unaye mwenzi mshirikishe vitu mbalimbali
vya msingi kama vile nywila/password muhimu za benki na za accout zako za simu kuhusiana
na Madeni na mali uliyokuwa nayo kwani huwezi kujua leo na kesho kitatokea
nini. Unaweza ukadondoka ghafla halafu baadhi ya mali zako nyingine zikaishia
kupotea hivihivi tu ikiwa hukuchukua tahadhari muhimu kama hizo.
8. Nidhamu
ya Pesa.
Hakuna njia ya mkato kwenye maisha, hakikisha
fedha unazozipata kwa jasho unazitumia pia kwa umakini wa hali ya juu. Kamwe
usitumie zaidi ya kile unachoweza kuingiza kama faida katika biashara zako na zaidi
ni kwamba bana matumizi kusudi uweze kutimiza malengo yako ya kifedha
uliyojiwekea kwanza.........
...............................................
Somo hili bado halijaisha na somo zima linapatikana kwenye Group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE.
Unaweza kuyapata masomo yote kamili tunayojifunza kila siku kwenye group hili kwa kulipa ada/kiingilio ambacho ni shilingi 10,000/= kwa mwaka huu mzima wa 2020
Pamoja na kuwa mwanachama wa group lakini pia punde baada ya kujiunga tunakutumia vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali kwenye simu au kompyuta yako.
Namba zetu za kulipia ni 0765553030 au 0712202244 Jina Peter Augustino Tarimo
Kisha baada ya malipo tuma ujumbe wa wasap au sms ya kawaida ukisema; NIUNGE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO"
Kwa vitabu na Michanganuo zaidi Tembelea DUKA LETU LA MTANDAONI (SMART BOOKS TZ)
................................................
0 Response to "HATUA 11 ZA KUJINASUA KWENYE MKWAMO WA KIFEDHA (USILAUMU KUKOSA PESA.. (PART II)"
Post a Comment