JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA KWA MUDA MFUPI NDANI YA NUSU SAA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA KWA MUDA MFUPI NDANI YA NUSU SAA


MPANGO RAHISI WA BIASHARA-ONE PAGE BUSINESS PLAN
Mpango kamili(Sanifu) wa biashara(traditional business plan) ni andiko linalohitaji muda wa kutosha kulikamilisha jambo linalowafanya watu wengi kukwepa kuandika michanganuo ya biashara zao na hata wengine kuchukia michanganuo ya biashara. Lakini kuna njia unaweza kuitumia na ukaweza kutimiza azma yako ya kuwa na mpango wa biashara pasipo ugumu wowote ule na kwa muda mfupi usiozidi saa moja.


Unaweza ukauita “Mchanganuo rahisi wa biashara”, “Mchanganuo mfupi wa biashara” au “Ukurasa mmoja wa mchanganuo”.  Unaandika mpango wa biashara yako vipengele vyote muhimu lakini kwa kifupi kadiri inavyowezekana, na ikiwezekana hata mchanganuo huo uenee katika ukurasa mmoja tu ingawa unaweza kuurefusha zaidi ya hapo. 

SOMA: Jinsi mango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako

Unaweza ukauita “Mchanganuo rahisi wa biashara”, “Mchanganuo mfupi wa biashara” au “Ukurasa mmoja wa mchanganuo”.  Unaandika mpango wa biashara yako vipengele vyote muhimu lakini kwa kifupi kadiri inavyowezekana, na ikiwezekana hata mchanganuo huo uenee katika ukurasa mmoja tu ingawa unaweza kuurefusha zaidi ya hapo.

Kwa wafanyabiashara hasa hasa wale wadogo(sole proprietorship) na hata ubia wa watu wawili watatu, mpango mrefu na wa kina sana hauhitajiki, wanaweza tu wakaandika aina hii ya mpango rahisi wa biashara na ukatosha kabisa hasa ikiwa hautatumika kuombea fedha mahali kama benki au kutafuta wawekezaji.

SOMA: Sababu kuu tano(5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaanzisha biashara yenyewe

Mchanganuo mfupi/rahisi wa biashara unafanana na muhtasari ule wa kawaida wa mpango mrefu wa biashara kutokana na sababu kwamba unagusa sura zote kwa kifupi lakini msomaji anapata picha nzima ya biashara yake ilivyo au itakavyokuwa.

Ukishamaliza kuandika mchanganuo wako rahisi au ukurasa mmoja wa mchanganuo, baadae unaweza ukaamua kuongezea maneno zaidi (nyama) na kuufanya ukawa mchanganuo kamili wenye maelezo ya kina na kazi hiyo sasa huwa rahisi zaidi kuliko kama ungelianza moja kwa moja toka mwanzo kuandika mchanganuo mrefu.

SOMA: Je, huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara yako? Tumia njia hizi 3 rahisi 

Faida za mchanganuo rahisi wa Biashara.
1.  Husaidia hasa ikiwa msomaji wa mpango wako hapendi kusoma maelezo marefu.

2.  Ikiwa wewe mwenyewe huna muda mwingi wa kuandika mpango mrefu wa biashara yako kwa kina

3.  Una faida zote zinazopatikana kwenye mchanganuo mrefu pasipo kutumia nguvu nyingi na muda

4.  Inakusaidia kutambua kabla hujapoteza muda mwingi ikiwa biashara italipa ili uweze kuandika mpango mrefu wa biashara yako.

5.  Ikiwa hutarajii kuutumia kuombea mkopo benki au taasisi za fedha basi hamna haja ya kuandika mpango wa biashara mrefu na wa kina sana, mpango rahisi unatosha kuendesha biashara yako.

JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA
Vipengele ni vile vile vinavyotumika katika kuandika Mpango wa biashara wa kawaida(mrefu) isipokuwa tu huandiki kwa undani sana. Unaweza ukagusa kila kipengele sentensi moja moja tu au mbili na unaweza kuingia ndani kidogo ikiwa kipengele kina umuhimu mkubwa sana kwenye biashara husika.

SOMA: Jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara yenye mafanikio, maeneo 6 muhimu ya kuzingatia

Hapa chini nitaorodhesha vipengele vinavyotakiwa kufuatwa kwa Kiswahili na kwa Kiingereza kabla hatujakwenda kuandika mfano wake.


(a) KWA KISWAHILI

1. Utambulisho au Thamani unayotoa kwa mteja
Ielezee biashara yako katika sentensi moja ni kitu gani unachokifanya. Kwa mfano utambulisho wa duka la nguo za wanawake unaweza kuwa hivi; “Tunauza nguo zinazomfanya mwanamke kujiamini muda wote”. Utambulisho wako ni kile kitu kinachokutofautisha na washindani wako,ni ile thamani unayoitoa kwa mteja. Ni namna unavyojipanga(kujiposition) sokoni

2. Tatizo unalotatua & Suluhisho lake
Tatizo ni hitaji lile ambalo wateja wako watarajiwa linawasumbua. Na Suluhisho ni Bidhaa au huduma unayoitoa, Ielezee huduma hiyo hapa na jinsi itakavyotatua shida ya wateja wako.

SOMA: Kuandika mchanganuo wa biashara yako kwa kiswahili kuna faida nyingi.

3. Soko unalolilenga & Ushindani
Kwenye soko unalolenga, taja wateja wako ni kina nani, sifa zao ni zipi na wapo wangapi. Katika Ushindani bainisha ni bidhaa au huduma gani wateja wako watarajiwa wanaitumia kwa sasa kukidhi mahitaji yao? Eleza utakavyowahudumia kwa ufanisi zaidi kuwashinda washindani wako. Taja na washindani wako wakubwa.


4. Mahitaji ya fedha & matumizi ya fedha hizo
Biashara huhitaji rasilimali mbalimbali zitakazosaida kuanza na kuendesha biashara, zitaje hapa, thamani yake pamoja na vyanzo vyake.

5. Mikakati ya Soko & Mauzo
Katika mkakati wa masoko taja njia utakazotumia kuwajulisha wateja juu ya bidhaa/huduma zako. Je, utatangaza kupitia vyombo vya habari, promosheni au mahusiano mazuri na umma?

SOMA: Shindano la kuandika mchanganuo wa biashara, wajasiriamali walivyohamasika!

Kwa upande wa mkakati wa Mauzo Eleza jinsi utakavyowauzia wateja wako. Wateja wako utawauzia moja kwa moja kutoka dukani au kwa njia ya mtandao?  Jumla au rejareja? Elezea mchakato mzima wa mauzo utakavyokuwa.

6. Mauzo & Gharama za mauzo.
Kwenye Mapato (mauzo), eleza njia zako za msingi za kuingiza mapato ni zipi? Hapa utaeleza jinsi utakavyoingiza pesa na ni bidhaa au huduma zipi zitakazozalisha hayo mapato. Kisia pia mapato yako kwa mwaka au mwezi

Kwa upande wa Gharama, orodhesha gharama zako kubwa ni zipi. Onyesha gharama za mauzo na gharama za uendeshaji.

7. Vitendo & Utekelezaji.
Orodhesha vitendo au malengo yako ya msingi utakayotekeleza siku au miezi michache kabla biashara haijaanza rasmi na jinsi unavyotarajia kuyakamilisha. Eleza namna utakavyobadilisha mpango wako kuwa kitu halisi(uendeshaji)

8. Timu nzima na Majukumu yao.
Ikiwa unaye mshirika/mbia au labda umepanga kuajiri watu wa kukusaidia kuanzisha biashara, wataje pamoja na nafasi zao hapa.




9. Mpango wa Fedha
Hapa unaweza ukaweka ripoti fupi ya faida na Hasara kwa mwaka au mwezi pamoja na mauzo ya kurudisha gharama zote(Break even Point). Huna haja ya kuingia ndani sana.


(b) KWA KIINGEREZA

1. Identity / Value Proposition

2. Market needs & Your solution

3. Target Market & Competition

4. Funding needs & Use of funds

5. Sales & Marketing Strategies

6. Sales goal & Budget

7. Milestones & Operation

8. Your Team & Employees

9. Projected Profit & Loss 

..........................................................

Kwenye group la Masomo ya kila siku ya fedha na Michanganuo la "MICHANGANUO-ONLINE" tumekuwa na zoezi la kuandika hatua kwa hatua mchanganuo wa Biashara ya Stationery kwa kutumia mtindo huu rahisi kuanzia tarehe 11/5/2020 mpaka 13/5/2020

Ikiwa unapenda kuona jnsi tulivyoandika pamoja na mchanganuo wenyewe mzima, unaweza kujiunga na group hilo ambalo ada yake ni sh. elfu 10 kwa mwaka mzima pia unapewa masomo yote, vitabu na michangnuo mbalimbali tuliyokwishajifunza.

Namba za kulipia ni 0765553030 au 0712202244 Peter Augustino Tarimo. kisha tuma ujumbe wa, "NIUNGANINSHE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA YA VITU 7" 


0 Response to "JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA KWA MUDA MFUPI NDANI YA NUSU SAA"

Post a Comment