Kukopa au kukopesha pesa ndugu, jamaa na rafiki wakati wa kuanzisha biashara ni hatari, je nini kifanyike? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Kukopa au kukopesha pesa ndugu, jamaa na rafiki wakati wa kuanzisha biashara ni hatari, je nini kifanyike?

Kumkopesha rafiki, ndug au jamaa

Upo usemi kwamba kumkopesha ndugu au rafiki matokeo yake ni kupoteza vyote viwili, pesa zako pamoja na undugu au urafiki wenyewe. Kauli hii binafsi nimewahi kuishuhudia kivitendo katika pande zote mbili, kumkopesha rafiki na pia kukopeshwa na ndugu/jamaa.  

Kama mojawapo ya njia ya kupata mkopo wa haraka, kukopeshana baina ya ndugu, jamaa au rafiki mara nyingi hakuambatani na masharti yeyote yale yanayolenga kuja kumbana mkopaji ili aweze kuona umuhimu wa kulipa wala huwa watu hawawekeani muda maalumu wa marejesho zaidi ya kila mmoja kujua tu ipo siku watarejesheana.

SOMA: Kutumia kiwanja, nyumba au ardhi kama rehani kuomba mkopo ni sahihi? Naomba ushauri.

Katika upande nilioona ni mgumu zaidi ni ule wa kumkopesha ndugu au rafiki. Ijpokuwa inaweza kudhaniwa kuwa mkopaji ndiye anayeteseka zaidi pale anaposhindwa au kuchelewesha kulipa, ukweli ni kwamba wewe mkopeshaji unaweza kuwa ndiye mhanga zaidi wa adha hii. Ikiwa unajua ni nini maana ya ndugu au maana ya rafiki utaelewa kile ninachotaka kukisema hapa. 

Unaweza hata usiwe na mawazo ya kumdai lakini kila utakapomuona mdaiwa wako unahisi kama vile hajisikii vizuri, unatamani hata kumwambia nimekusamehe deni lenyewe lakini unashindwa. Hali hii mwishowe humfanya mkopeshaji kumkwepa mkopaji na mkopaji naye anapoona hivyo hupatwa na wasiwasi na kujisikia mnyonge muda wote. 

SOMA: Kuendeha biashara bila mtaji au mtaji kidogo ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.

Hatari nyingine ya kumkopesha ndugu, jamaa au rafiki ni kwamba huwezi kumchaji riba. Kwanza kumtajia tu sual la riba tayari ataona kama vile unataka kumfanya yeye kama kitegauchumi chako jambo litakaloleta manunguniko makubwa ndani ya familia, ukoo au baina ya pande mbili na hasa ikiwa hawana uelewa mpana ama kuwahi kujifunza jinsi ya kupata mkopo wa biashara mahali pengiine 

Familia hushindwa kukaa pamoja hata katika vikao kutokana na mdaiwa kuwa na hofu ya kukaa karibu na mdai hasa ikiwa mdai ni mtu asiyeweza kujizuia kuwatangazia wanafamilia au wanandugu wengine. Mdaiwa hatimaye anaweza akatengwa hata na wanafamilia wengine wakidai ni kwanini hataki kulipa deni.

SOMA: Sababu kubwa 9 duniani kwanini watu hukopa pesa, 4 kati yake ni za kuogopa kama ukoma.

Utatamani hata ni kwanini hukuenda kuomba kupata mkopo kwa simu ama kuomba mkopo online katika app za mikopo Tanzania na hata nje, au mikopo binafsi benki kwani hamna udugu wa karibu au urafiki hapo na hata ikitokea umesuasua kulipa marejesho yao ndiyo watakufuatilia lakini siyo kufedheheshana namna hiyo.

Mithali kabla ya kukupa mkopo walihakikisha ulikuwa na vigezo vya kupata mkopo toka kwao, wao watakachozingatia kwanza ni kuangalia dhamana ulizoweka na siyo undugu wala urafiki kwenye mikopo ya biashara.

Lakini pia hatari nyingine ni kwamba mkopaji hugeuka kama mtumwa kwa mkopeshaji kwani hujikuta akilazimika kukubaliana na kila kitu atakachosema mkopeshaji hata kama hoja zenyewe siyo sahihi, huwezi kumpinga kwa lolote.

 SOMA: Kabla ya kukopa mkopo wa biashara yako, pambana kiume kwanza usije kuumbuka bure!

Mkopaji pia anaweza akaja na kuomba kupewa tena mkopo mwingine. Badala sasa ya kuwa umemsaidia inakuwa ndiyo njia ya kumfanya asijishughulishe tena na kazi bali kila mara arudi kwako kutaka msaada. Anageuka mwiba kwako.

Si hivyo tu kwani wanandugu au marafiki wengine wakishajua ya kuwa wewe unakopesha kirahisi, nao humiminika kwako kuja kuomba mkopo nafuu usiokuwa na masharti ya kuwabana kama ilivyo mikopo ya mabenki mfano CRDB, NMB, ACCESS, AKIBA, DCB, EQUITY na mengineyo mengi nchini Tanzania. Wanaambiana, ‘twende shambani kwa bibi tukachukue hela za dezo’

Wewe uliyekopesha hali yako kifedha bahati mbaya inaweza ikageuka na kuwa mbaya ghafla ukahitaji kurudishiwa fedha zako na mkopaji/wakopaji lakini itakuwa vigumu sana kukulipa na hata wengine watakubeza usiamini kabisa kama ni wao waliokuja mikono nyuma kutaka uwakopeshe.

SOMA: Ili ufanikiwe kuwa tajiri mkubwa jiepushe kabisa nakauli hizi 4

Kabla ya kumfuata ndugu, jamaa au rafiki na kumtamkia, nataka mkopo, hebu kwanza soma suluhisho la tatizo hili hapo chini kwa umakini mkubwa. 

Suluhisho la Yote haya

Mapenzi yako kwa ndugu, jamaa au marafiki hayapaswi kabisa kupimwa kwa ukarimu uliokuwa nao, lakini pia kwa kuwa ni vigumu..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Ndugu msomaji wangu somo hili bado halijamalizika na unaweza kulisoma lote ukijiunga na masomo yetu ya kila siku ya fedha. Somo hili tutajifunza leo tarehe 15/07/2023 katika group la Michanganuo-online.

Kujiunga mwanachama unalipia shilingi elfu 10 tu ada ya mwaka mzima. Tunakutumia muda huohuo OFFA ya vitu 12 vikiwa ni vitabu na michanganuo kamili ya biashara mbalimbali kama uonavyo hapo chini mwisho. Unapata pia na masomo mengine yaliyokwishapita ndani ya group

Namba za kulipia ni; 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma meseji sms au watsap isemayo, "NATAKA OFFA YA VITU 12, NIUNGE NA GROUP LA MASOMO"

Ikiwa hupendelei magroup basi unaweza kulipia tukakutumia offa zako tu

Karibu tukutane saa 3 usiku kila siku.


VITU 12 VYA OFFA NI HIVI VIFUATAVYO;-

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)


Imeandaliwa na:

Peter A. Tarimo

Mtaalamu wa michanganuo ya biashara aina zote

Call/watsapp: 0765553030 / 0712202244

0 Response to "Kukopa au kukopesha pesa ndugu, jamaa na rafiki wakati wa kuanzisha biashara ni hatari, je nini kifanyike?"

Post a Comment