Katika maswali ya wasomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali wanayoniuliza, nimekuwa napata maswali yanayojirudia mara kwa mara kuhusiana na jinsi ya kujenga mabanda ya kuku. Wakati fulani hata niliandika Makala hii isemayo, UJENZI WA MABANDA YA KUKU ISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUANZISHA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU. Hata hivyo siku za hivi karibuni nimeendelea kupokea maswali na changamoto kutoka kwa wafugaji wa kuku wapya na hata wale wa zamani pia wakitaka kufahamu au kupata ramani, michoro na hata vipimo vya banda bora na la kisasa la kuku linavyoweza kuonekana.
Hapa nitaanza kwanza na maswali waliyoniuliza
wadau hao wa kuku kwa kuyaandika ikiwa ni pamoja na kuweka screenshots za meseji walizonitumia,
1. Mdau wa kwanza aliuliza hivi;
1. Mdau wa kwanza aliuliza hivi;
Je,
naweza kupata ramani au mchoro au picha za banda la kuku la kuanzia ambalo
linaweza kuchukua kuku 1000 hadi 2000?
Na screenshot yake ni hii hapa;
2. Mdau wa pili yeye aliniuliza kama ifuatavyo;
Hi
Mr. Tarimo, nimesoma taarifa zako kwenye Google nimezipenda sana. Mimi nataka
kuwa mjasiriamali wa ufugaji wa kuku tena mkubwa ila sijui chochote kuhusu kuku
na nataka nianze kwenye ujenzi wa banda la kuku la kisasa na la bei nafuu.
Nahitaji msaada wako nianzeje pia niwe
kwenye group?
Screenshot yake ilikuwa hivi;
Baada ya kuona maswali
hayo kwanza ningependa kuandika kile nilichowajibu kwa haraka haraka halafu
tena nitaelezea kwa ufasaha kabisa banda la kuku 100 linatakiwa kuwa na ukubwa
kiasi gani.
SOMA: Ujenzi wa mabanda ya kisasa ya sungura ulivyo rahisi na nafuu kwa mfugaji anayeanza
SOMA: Ujenzi wa mabanda ya kisasa ya sungura ulivyo rahisi na nafuu kwa mfugaji anayeanza
1. Majibu kwa mdau wa kwanza
Banda la kuku
halihitaji kuwa na shepu au mtindo wa kipekee Sana bali tu liwe imara,
sehemu za kulia chakula, kunywea maji, kulala mfano mabembea nk. Pia lipitishe
hewa safi vizuri na sakafu nzuri.
Vipimo vya banda
zingatia kuku 6 mpaka 10 kwenye mita moja ya mraba. Yaani mita 1 upana kwa mita
1 urefu.
Kama ni kuku wa
kienyeji ni vizuri ukatumia kuku 6 kwenye mita moja ya mraba ambapo kwa idadi
ya kuku 2000 utahitaji mita za mraba; 2000/6 sawa na mita za mraba 333. Mita za
mraba 333 ni sawa na urefu,(makadirio) mita 18 na upana mita 18 au urefu mita
20 na upana mita kama 16 hivi.
SOMA: Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku wa asili)
SOMA: Kilichokuwa nyuma ya pazia, ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku wa asili)
2. Majibu ya swali kwa mdau wa
pili 2
Mabanda si lazima yawe
ya hali ya juu sana, cha kuzingatia kwanza ni vipimo, saizi ya banda
inayoendana na idadi ya kuku unaotaka kuwafuga na kingine ni uimara wa banda wa
kuwakinga na hatari zozote zile kama vile wanyama hatari, baridi, jua, upepo na
mvua.
SOMA: Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? Naomba mchanganuo
SOMA: Shilingi milioni 5 itatosha kufuga kuku wangapi wa mayai? Naomba mchanganuo
Unaweza kujenga kwa
kumtumia fundi yeyote mtaani kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi
kwenye mazingira uliyopo.
Majibu kwa ujumla ya jinsi ya kujenga banda la
kuku linalofaa kufugia kuku: ujenzi, vipimo, ramani na picha ya mabanda
Ukitazama katika
majibu yote mawili kwa wadau hapo juu utagundua kwamba kitu cha msingi sana
kabla hujajenga banda lako la kuku ni idadi ya kuku unaotaka kufuga pamoja na
saizi ya banda. Ni lazima kwanza ujue katika eneo la ukubwa fulani wanatakiwa
kukaa kuku wangapi. Kwa kifupi unatakiwa kujua kuku mmoja anatakiwa aishi
kwenye eneo la ukubwa gani.
Sasa kitaalamu kabisa
ni kwamba kuku wa umri/aina tofauti watahitaji pia eneo la ukubwa tofauti,
mathalani banda la vifaranga 100
haliwezi kuwa sawa na banda la kuku wa mayai 100. Halikadhalika pia banda la
kuku wa kienyeji 20 haliwezi kulingana na banda la kuku wa kisasa 20 walio na
umri huohuo sawa na wenzao wa kienyeji. Hivyohivyo banda la kuku wa nyama 200
haliwezi likawa sawa na banda la kuku chotara 20 ingawa idadi na umri vinaweza
kuwa ni vilevile.
Lakini kwa ujumla ni
kwamba mabanda ya kuku wakubwa kitaalamu wawe ni kuku wa kisasa, wa kienyeji au
wa mayai, katika mita moja ya mraba wanatakiwa kuishi wastani wa kuku 6 mpaka
10. Hii inamaana kwamba kwa kuku wa kienyeji watahitaji eneo la nafasi kubwa
zaidi kushinda wale kuku wa kisasa.
Hivyo katika wastani huo, ule wa chini kabisa kuku 6 ndio utakaofaa zaidi kwa kuku wa kienyeji na ule wa juu zaidi kuku 10 utafaa zaidi kwa kuku wa kisasa wawe wa nyama au hata wa mayai. Na kwa upande wa kuku chotara basi unaweza ukawaweka hapo katikati labda tuseme kuku 7 au 8 katika mita ya mraba moja .Mita ya mraba 1 hapa namaanisha (Mita moja urefu x Mita moja Upana).
SOMA: Chakula cha kuku wa kienyeji kina tofauti yeyote na kile cha kuku wa kisasa?
Hivyo katika wastani huo, ule wa chini kabisa kuku 6 ndio utakaofaa zaidi kwa kuku wa kienyeji na ule wa juu zaidi kuku 10 utafaa zaidi kwa kuku wa kisasa wawe wa nyama au hata wa mayai. Na kwa upande wa kuku chotara basi unaweza ukawaweka hapo katikati labda tuseme kuku 7 au 8 katika mita ya mraba moja .Mita ya mraba 1 hapa namaanisha (Mita moja urefu x Mita moja Upana).
SOMA: Chakula cha kuku wa kienyeji kina tofauti yeyote na kile cha kuku wa kisasa?
Kwa upande wa kuku
wadogo vifaranga unaweza ukapunguza vipimo hivyo banda la ukubwa wa mita moja
mraba likawa na vifaranga hata zaidi ya 15 hamna shida ingawa pia kuna vipimo
vyake maalumu.
SASA NI VIPI UTAJUA
UKUBWA WA BANDA KULINGANA NA IDADI YA KUKU UNAOTAKA KUFUGA?
Njia nyepesi zaidi na
rahisi ya kukuwezesha kujua idadi ya kuku wako itahitaji eneo la ukubwa wa mita
ngapi za mraba ni hii ifuatayo;
Kwanza weka msimamo
unataka kuku wako wabanane au wawe huru kiasi gani. Ukitaka wawe huru sana
tuseme kama kuku wa kienyeji basi wewe weka idadi ya kuku wako kwenye mita moja
ya mraba kuwa 6 au hata 5 ukitaka. Kisha sema hivi;
Ikiwa kuku 6 = Mita 1 ya mraba, Je kuku(…………) (taja idadi ya kuku wako hapo) watahitaji mita ngapi za mraba? Kisha chukua idadi ya kuku wako gawa kwa 6 na jibu ndio mita za mraba unazohitaji.
Ikiwa kuku 6 = Mita 1 ya mraba, Je kuku(…………) (taja idadi ya kuku wako hapo) watahitaji mita ngapi za mraba? Kisha chukua idadi ya kuku wako gawa kwa 6 na jibu ndio mita za mraba unazohitaji.
MFANO: BANDA LA KUKU
WA KIENYEJI 100 LIWE NA UKUBWA WA MITA NGAPI ZA MRABA?
Kuku 6 = Mita ya mraba 1
Kuku 100 =
Mita ? za mraba?
Chukua kuku 100
/6 = 16.6
Kwahiyo kuku 100
watahitaji mita za mraba 16.6 ambazo ni sawa na wastani wa Mita 4 upana na Mita
4 Urefu au Mita 8 urefu na mita 2 upana.
Unaweza ukaamua
kutafuta ukubwa wowote ule wa eneo linalohitajika kulingana na idadi yako ya
kuku unaotaka kufuga.
SOMA: Hydroponic fodder: jinsi ya kuotesha majani ya mifugo katika trei za aluminium na plastiki bila udongo
SOMA: Hydroponic fodder: jinsi ya kuotesha majani ya mifugo katika trei za aluminium na plastiki bila udongo
Ikiwa unataka pengine
kufuga kuku wa kisasa wa nyama punguza ukubwa wa banda na ufanye angalau kuku
10 wakae kwenye mita moja ya mraba hivyo kwa kuku 100 wa kisasa watahitaji
banda la ukubwa wa; 100/10 = mita za mraba 10 au (Upana mita 2 x Urefu mita 5)
nk.
JINSI YA KUJENGA BANDA
LA KISASA LA KUKU
Hakuna kanuni/formula
maalumu inayotakiwa kufuatwa ili mtu aweze kutengeneza banda la kuku iwe ni
banda la kuku wa kienyeji, banda la kuku wa nyama, banda la kuku wa mayai,
banda la kuku wa kisasa, banda la kuku chotara banda la vifaranga au hata banda
la bata na ndege wengineo wafugwao, ila kitu kikubwa tu cha kuzingatia hapa ni
uimara wa banda kuhakikisha kuku wanakuwa salama wasidhurike na hatari zozote
wala hali mbaya ya hewa lakini pia wapate eneo la kutosha la kucheza, kula na
kulala.
Materials za kujengea
mabanda ya kuku yaweza kuwa ni kitu chochote kile kinachofaa kujengea mfano
kuna mabanda ya kuku ya mbao na misumari, mabanda ya kuku ya udongo(tofali za
udongo au za sementi), banda la kuku la mabanzi na hata mabanda ya kuku ya
nyavu na miti au mbao. Kuna watu wengine
hufikiri banda la kuku la ghorofa ndio zuri na la kisasa zaidi lakini wala siyo
lazima liwe ni banda la ghorofa, banda la kuku la gharama nafuu tu linatosha
kabisa endapo litakidhi sifa zote zile zilizotajwa pale juu bila kusahau bembea wajirushe hapo usiku wakati wa kwenda kulala.
RAMANI YA BANDA LA
KUKU LA KISASA
Watu wengine hufikiria
labda kuna ramani za kisasa sana za mabanda ya kuku kama zilivyokuwa ramani za
kisasa na tata(complex) za majumba ya kulala au ya kuishi binadamu. Lakini
ukweli ni kwamba, kwa mfugaji wa kawaida unayetaka pengine kufanya ufugaji wa
kuku wa kienyeji kibiashara kama ule niliouelezea katika mchanganuo wangu
maarufu wa ufugaji bunifu wa kuku wa
kienyeji, basi huna haja ya kumtafuta mkandarasi wa majengo akudizainie banda
lako la kuku, wala vifaa na material za bei ghali.
SOMA: Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi
SOMA: Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi
Wewe cha kufanya tu ni
kuhakikisha ukishapata vifaa (material) zako za bei nafuu, unamtafuta fundi au kama wewe
ni mtundu kama mimi wala huna haja ya kumtafuta fundi bali wewe piga hesabu
kuku wako wanahitaji ukubwa wa eneo gani kisha anza kuchimba mashimo au kuweka
msingi na ujenge kitu kama ukumbi(hall). Baadae ndani ya lile hall kata vyumba unavyohitaji kulingana
na aina za kuku uliokuwa nao.
Kama ni kuku wa aina
moja tu basi huna haja ya kukata vyumba wala nini, wewe wawekee mahitaji yao
yote ndani kulingana na idadi yao kisha wamwage huko wahangaike wenyewe. Hakikisha
lakini banda lina vigezo vyote nilivyotaja, usalama, nafasi ya kutosha,
hewa(madirisha ya nyavu), kuwakinga na hali yeyote ile mbaya ya hewa pamoja na sakafu
nzuri, mabembea nk.
…………………………………………
*Ufugaji wa kuku ni
miradi unayoweza kuianza kwa mtaji wowote ule mdogo au mkubwa ulio nao lakini ukitaka mafanikio
makubwa na ya haraka, basi huna budi kutafuta mtaji wa kutosha na uzoefu,
Mafunzo kama haya ya kwenye mitandao si mabaya yanamsaidia mtu kupunguza ule
muda atakaotumia kujifunza kwa vitendo ila vitendo ni lazima piga ua ili
ujifunze mwenyewe changamoto na fursa zilizopo na si kuhadithiwa.
Baada ya muda wa
vitendo angalao kufuga kwanza kuku wachache kwa miezi kadhaa, sasa unaweza
kuwekeza muda na fedha zako nyingi kwenye miradi hii, hapo ndipo unapoweza
kuona mafanikio makubwa na ya haraka ya ufugaji wa kuku, lakini vinginevyo
unaweza kuishia tu kufuga kuku kwa ajili ya kitoweo/mboga au jogoo wa kuchinja Krismasi, Mwakampya na Idi, basi.
Nimeandaa michanganuo
ya biashara hizi za ufugaji wa kuku kitaalamu na kiubunifu yenye kila kitu
kuanzia muhtasari, changamoto mpaka makisio yote ya fedha, michanganuo hiyo ipo
mitatu (3), kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji. Kila mchanganuo
bei yake nauza shilingi elfu 10 lakini nina offa ya muda mfupi kwa wale wote
wanaojiunga na Group langu la Whatsapp la masomo ya kila siku ya Fedha na
Michanganuo.
Kwa members
wanaojiunga nawauzia kwa sh. Elfu 10 tu
michanganuo yote 3, hivyo mtu anakuwa amesevu sh. Elfu 20. Offa kama
nilivyosema haitadumu muda mrefu kwani group lenyewe nalo nafasi zimebaki chache.
Karibu kama utapenda nikutumie na kukuunganisha na group. Mawasiliano yangu ni; Simu/waTsap: 0765553030 au Simu/sms: 0712202244
. Asante sana
Peter Augustino Tarimo
Niwashukuru sana kwa Elimu hii ya kuku
ReplyDeleteAsante nawewe pia ubarikiwe kwa kusoma makala yetu
DeleteKazi mzuri congratulations. Naoomba kupata elimu zaidi namba yangu ni 0682244414
ReplyDeleteKaribu sana ndugu
DeleteNataka kujua kuwalisha kuku wa nyama mpaka niwauze chakula natumia kiasi gani na madawa kiasi gani nataka kuingia kwa biashara hii na pia eneo langu ni dogo lina urefu wa mita 6m na upana 2.5m je hapa naweza kuweka kuku wangapi
ReplyDelete