Bada ya kutangaza tungekuwa na somo la mchanganuo wa biashara yenye faida kubwa na
mtaji mdogo, darasa lilikuwa moto! Kila mtu(members) alikuwa na
shauku kubwa sana (over excited) ya kufuatilia kwa umakini somo la
kuandika mchanganuo wa biashara ya chipsi iliyopo eneo la stendi ya Buguruni-Muhimbili.
Kwa kweli wengi walionekana kutokuamini kama biashara ya chipsi ni biashara inayohitaji
mtaji mdogo sana lakini yenye kulipa faida kubwa kiasi ambacho ndani
ya mwezi mmoja tu na siku tano mtaji wote uliowekeza unaweza ukarudi.
Kabla sijaenda kukuonyesha jinsi wanagroup
walivyohamasika mpaka mtoa somo akaamua kuanza somo hilo saa 12 jioni badala ya
saa 3 usiku, ngoja kidogo nielezee jinsi biashara hii ya chipsi inavyolipa haraka kwa
mtaji kidogo. Zipo biashara nyingi zenye faida ya haraka unazoweza ukaanzisha
na mtaji mdogo lakini kulingana na utafiti tulioufanya biashara ya chipsi inashika
nafasi ya juu kabisa miongoni mwa orodha ya biashara ndogondogo zenye faida kubwa mara mbili ya mtaji unaowekeza.
Biashara ya nguo kwa mfano, iwe ni nguo za mitumba au
hata nguo za spesho za kushona nayo ni biashara nyingine ya uhakika isiyopitwa
na wakati muda wote, kuna biashara ya duka la rejareja, hali kadhalika na
biashara ya kuosha magari. Biashara zote hizi na nyingine tunazoandikia
michanganuo ya biashara zake kila siku katika group letu zipo katika orodha ya
biashara ndogo zinazolipa faida haraka kwa mtaji kidogo.
Biashara kama hii ya chipsi kwa mfano unatumia kiasi cha
fedha chini ya shilingi milioni moja lakini faida yake kwa siku unapata hadi
shilingi elfu 30. Hapo kwa haraka haraka hebu chukua tu lali 9 (900,000/=)
kisha gawa kwa elfu thelathini(30,000). Hapo jibu utapata 30, maana yake ni
kwamba kwa muda wa siku 30 tu zile laki 9 zinakuwa zimesharudi na faida hiyo ya
elfu 30 kuipata ni rahisi sana, utauza chipsi ndoo mbili au tatu tu, kuku
wasiozidi 2, mayai trei 2 na nusu, mishikaki kama kilo moja, pengine na ndizi
mbili tatu tu hivi.
Katika group la masomo ya kila siku ya Fedha na Michanganuo ya biashara la
MICHANGANUO-ONLINE, tumeanzisha utaratibu wa kuandika hatua kwa hatua
michanganuo ya biashara ndogondogo zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo wa
kuanzia. Michanganuo hiyo huwa tunaiandika kwa kutumia njia rahisi sana ambayo
mjasiriamali anaweza akajifunza njia hiyo na kuweza kuandika mwenyewe
mchanganuo wa biashara nyingine yeyote ile inayolipa na aipendayo.
Baada ya kuandika kwa njia rahisi pia huwa tunaonyesha jinsi
ya kuandika mchanganuo huo kwa njia ile ya kawaida (traditional business plan
writing) njia ya kuandika mchanganuo wa biashara iliyozoeleka na wataalamu (Business plan Experties). Kwahiyo
utaratibu huu ni mzuri siyo tu kwa wajasiriamali wadogo bali hata kwa wafanyabiashara
walio na mawazo mazuri ya biashara lakini wangependa andiko la biashara zao kwa
njia nyepesi kwa wafadhili, benki au wabia ili kuweza kupa mitaji ya kuendeshea
biashara za ndoto zao. Baada ya hayo machache sasa hebu tukaone jinsi darasa
letu la whatsapp lilivyohamasika jana;
Darasa lilianza hivi;
Karibuni
members kwenye darasa letu la Michanganuo,
Leo
tunachambua biashara ya chipsi iitwayo AMANI CHIPS CENTRE iliyopo stendi ya
Buguruni-Muhimbili. Tutaanza kwanza na mchanganuo mfupi kama trela vile, kisha
baada ya hapo tutakwenda kuona mchanganuo kamili mrefu wenye vipengele vyote
muhimu.
1.
Utambulisho wa biashara
Hapa kama kawaida
tuielezea kwa maneno machache kabisa biashara.
Amani Chips centre ni
biashara itakayotoa huduma bora za chipsi kwa madereva na makondakta katika
stendi ya Buguruni Muhimbili wasio na muda wa kwenda kula majumbani
Hapa
ni wanagroup wakisubiri kwa shauku somo:
Mchanganuo wenyewe kamili wa Amani Chips centre huu hapa;
Asante sana nina ndugu alikuwa anataka kuanzisha biashara
hii, mchanganuo huu utamsaidia sana;
Nashukuru kaka Peter kwa mchanganuo huu. Kuna kitu kikubwa nimejifunza. Asante
Mimi binafsi nimeupenda huu uchambuzi na mpango. umekaa vizuri na umezingatia vigezo muhimu katika mchanganuo wake;
Mimi pia nasubiria kwa hamu nimefungua kama mara mbili lakini nafeli, nataka kujua kinachonikwamisha ni nini? nasubiri somo;
.....................................................
Je, unahitaji kuandikiwa mchanganuo wa biashara
yako au kujifunza kwa njia rahisi namna ya kuandika mwenyewe?
1. Tunaandika
mipango ya biashara za aina zote kwa gharama nafuu sana kuanzia asilimia 1%
mpaka 2% tu ya mtaji wa biashara unayotaka tukuandikie. Cha kufanya tu ni
kwamba, tukishakubaliana na kututumia mahitaji ya mpango wako online, unalipia
nusu ya gharama kisha tunaaza mara moja kazi kwa siku 3 – 5. Baada ya hapo
tunakutumia mchanganuo wako kamili.
2. Ukitaka
kuandika mpango wa biashara yako mwenyewe pia unaweza ukawasiliana na sisi(watsap:
0765553030) tukakutumia resources zote muhimu, vitabu, seminars, templates na
michanganuo ya mfano/business plan samples, za Kiswahili na kiingereza
vitakavyokurahisishia kazi ya kuandika mchanganuo wako kwa wepesi.
.WASILIANA NASI KWA NAMBA:
0765553030 au 0712202244
WASAP: 0765553030
Jina: Peter Augustino Tarimo
.Kupata vitabu vyetu mbalimbali na Michanganuo tembelea
Duka la vitabu mtandaoni la; SMART BOOKS TANZANIA
.Kujiunga na group letu la whatsapp la masomo ya kila siku, lipia ada ya mwaka sh. elfu 10 kisha unitumie ujumbe nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia offa ya masomo, michanganuo na vitabu muda huohuo
0 Response to "BIASHARA YA MTAJI MDOGO YENYE FAIDA KUBWA ZAIDI TANZANIA ILIVYOSHANGAZA DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA"
Post a Comment