Kuna watu mpaka sasa hivi Duniani wanaitukana
Tanzania kwamba imekataa kuchukua tahadhari zote zilizowekwa na shirika la Afya
Duniani WHO. Watu hao hawaamini hata kidogo kile kilichotokea Tanzania na
wanachukulia korona kuisha Tanzania kama vile ni maajabu ya Dunia. Lakini kwa
wachache wanaoelewa kama Donald Trump wa Marekani wameishia kimyakimya kufuata
nyayo Tanzania ilizopitia.
Naomba usije ukaninukuu vibaya hapo, mimi
sijasema Tanzania corona imekwisha kabisa hapana, bali imepungua kwa kiasi cha
kustaajabisha na watu wengi kutokuamini kabisa wakiwemo majirani zetu Kenya,
Uganda, Rwanda na wengineo. Ingawa Imani za kidini zimetajwa kuhusika na hili
lakini mimi katika makala hii sitajikita sana kwenye Imani za kidini ingawa pia
kile nitakachokwenda kukizungumzia(IMANI / BELIEF) kinaweza kuhusika na dini
kwa namna moja ama nyingine kulingana na mtazamo wa mtu ulivyo.
Kumbuka tu kwamba Imani siyo lazima ihusiane
na dini, unaweza ukaweka Imani kwa jambo lolote lile lisilohusiana na dini na
ikafanya kazi. Imani ni hali inayofanya kazi ndani ya akili ya Mwanadamu na ina
athari kubwa sana kwenye kufanikiwa ama kutokufanikiwa kwake kimaisha. Sibezi
Imani za kidini hapa bali nataka tu kuelezea jinsi vile Imani inavyofanya kazi
kwa namna ya ajabu katika akili zetu.
Ikiwa majirani zetu Kenya na Uganda hawaiamini
Tanzania kama kweli Corona imepungua sembuse nchi zilizokuwa mbali kama
Marekani, Ulaya na Asia? Sasa basi ni kitu gani hasa kilichotokea Tanzania hata
Corona ikapungua kisi hicho na kuna ukweli wowote kwamba Corona imepungua ama
ni propaganda tu za viongozi wa Tanzania kutaka kuficha ukweli wa mambo kijanja
kusudi taswira ya Tanzania kibiashara huko nje isije ikaharibika tukakosa hela
za utalii, ndege na nyinginezo?
Kujua ikiwa kama ni kweli Tanzania Corona
imepungua kwa kiasi kikubwa au la ni rahisi sana kwa mtu unayeishi hapahapa
Tanzania lakini siyo kwa mtu aliyeko ughaibuni. Unatakiwa tu kujiuliza maswali
machache yafuatayo pale ulipo; Je, ni watu wangapi unaowajua mtaani kwako
waliokufa kwa korona ndani ya wiki hii? Au ni watu wangapi maarufu nchini
waliokufa au kuambukizwa corona siku za hivi karibuni? Na Je, siku mbili tatu
hizi umeshuhudia watu wangapi wakiwa na mafua makali, kikohozi au hata homa
kali na matatizo ya kupumua kwa shida?.
Kiukweli nilichoshuhudia mimi binafsi kwa
macho yangu hospitali moja ni kupungua sana kwa wagojwa na sababu kubwa
inatajwa kwamba ni watu wengi kutouguaugua tena ovyo mafua, vikohozi na minyoo
kulikosababishwa na watu kunawa mikono kila mara.
Nilikuwa mmoja kati ya wabishi sugu kwamba
corona haiwezi kupungua Tanzania ili-hali wenzetu Kenye wagojwa bado
wanaongezeka, lakini baada ya kujiuliza maswali hayo machache niliamua mwenyewe
kukaa chini na kuanza kuandika makala hii lengo langu likiwa si kupamba wala
kusifia hapana, bali kuchunguza na kuibuka na majibu ya ni mbinu gani hasa
iliyotumika mpaka corona Tanzania ikapungua kwa namna ya kustaajabisha hivyo na
wala siyo kwa majirani zetu au nchi nyingine yeyote ile Duniani.
Kisha basi mbinu hiyohiyo bila shaka inaweza
ikatumiwa na watu mbalimbali kuboost hali zao za kiuchumi zikiwemo pia biashara
zao zinazozorota kwa kasi ileile Corona au Covid 19 ilivyosambaratishwa.
Siandiki Makala hii kiushabiki hata kidogo
naomba nirudie tena, bali naiandika kisayansi kabisa baada ya kufanya utafiti
wa kutosha. Mtu mwingine anaweza akasema labda Peter anataka kuleta tu siasa
kwenye jambo hili, pengine kwakuwa kipindi cha kampeni kinakaribia na mengine
kibao ya namna hiyo, hapana, hata kidogo, ukilipinga hili ni shauri lako mimi
siwezi kukulazimisha, kwanza sina chama mimi bali muumini wa maendeleo ya binadamu.
SASA
BASI NI KWA NAMNA GANI UNAWEZA KUTUMIA MAAJABU YALIYOMALIZA UGOJWA WA CORONA
TANZANIA KUBUSTI UCHUMI WAKO?
Kwanza kabisa niweke wazi kwamba
kilichosaidia sana mapambano ya covid 19 hapa Tanzania ni IMANI waliyojengewa
Watanzania juu ya janga hili. Haijalishi ni kiongozi gani aliyebuni mbinu hii
lakini mbinu ni mbinu tu ilimradi isaidie kushinda vita.
Ijapokuwa waswahili husema Mnyonge mnyongeni
ila haki yake mpeni, siwezi nikasema ni Rais Magufuli aliyefanikisha hili peke
yake kwa kuwa tulishuhudia hata viongozi wengine akiwemo Waziri mkuu Mh. Kasim
Majaliwa, Waziri wa afya mama Ummy Mwalimu na hata Waziri wa Tamisemi
Mheshimiwa Sulleiman Jafo wakihamasisha kauli mbalimbali zilizowajengea
Watanzania Imani ya kuushinda ugojwa huu hatari kama vile, “Corona isitutishe”,
“zingatieni masharti yote ya shirika la afya Duniani huku mkiendelea kuchapa
kazi” “Pigeni nyungu kwelikweli msione aibu” “Kujifukiza, malimao, tangawizi, michaichai,
muarobaini bila ya kusahau kumuomba MWENYEZI MUNGU” na mengineyo mengi.
Kilichowasaidia watu kwa kiasi kikubwa siyo
malimao, tangawizi na kupiga nyungu vyevyewe kama vilivyo hapana bali msaada
mkubwa ulitokana na ile Imani iliyojengeka akilini mwa watu kwamba Corona
isingeliweza kuwadhuru kwa kiasi kile walichokuwa wakidhania kabla. Wasiwasi
ungeliweza kupandisha juu idadi ya vifo na wagojwa wa corona lakini Watanzania
hawakuruhusu jambo hilo kutawala katika akili zao.
SOMA: Jinsi ya kutambua na kuacha fikra hasi ulizonazo juu ya pesa zinazokurudisha nyuma usifanikiwe
Jinsi
imani ilivyo na nguvu ya kubadilisha matokeo ya jambo lolote lile chini ya jua
Kile unachokiamini huwa ndicho kinachokuwa kweli
mara zote. Imani zina athari kubwa sana kwenye namna tunavyohisi, kufikiri na
kutenda. Ndiyo hutoa taswira ya mambo yote tunayopitia katika maisha yetu;
Ø Imani
ndiyo inayotengeneza mawazo/fikra
Ø Mawazo
hutengeneza Hisia
Ø Hisia
hubadilika kuwa vitendo/kutotenda
Ø Na
vitendo sasa ndiyo vinavyohusika na matokeo yeyote yale katika maisha yetu
Mlolongo uko hivi;
IMANI
→ FIKRA
→ HISIA → VITENDO
→ MATOKEO
Watu kimakosa huwa mara kwa mara tunadhania
kwamba vitendo ndiyo vyenye uwezo wa kuleta matokeo lakini ni kama
tunajidanganya kwa kusahau vitu vingine 3 nyuma yake. Ndiyo sababu
tunastruggle(kuhangaika) sana kutafuta matokeo mazuri pasipo mafanikio makubwa
kwani vitendo tu bila kingine chochote haviwezi kukufikisha mbali, utakwama
njiani.
Na hii ndiyo sababu umeona nchi kama
Marekani, Uingereza Italia na nyinginezo zilizokimbilia kutekeleza vitendo kama
lock down nk. hazikuweza kupata matokeo mazuri pamoja na kuwa wana rasilimali
nyingi. Walisahau vitu vingine 3 nyuma, Imani, fikra na hisia. Hapa chini
nitaonyesha hatua zote 5 jinsi Tanzania ilivyozitumia kikamilifu na kufika hapa
ilipofikia na janga hili la corona, na kisha baadae nitakwenda kutoa mfano
mwingine wa mtu anavyoweza kupata matokeo bora kabisa kwenye jambo jingine
lolote lile kama biashara, uchumi nk.
Kwenye matokeo yeyote yale maishani yawe
mabaya au mazuri, hebu rudi kinyumenyume ukianza na MATOKEO yenyewe kisha
chunguza matokeo hayo yametokana na VITENDO gani?, halafu Vitendo
vilisababishwa na HISIA zipi, hisia hizo zilitokana na FIKRA zipi na mwisho
tafuta Fikra zilitokana na IMANI ipi. Baada ya kugundua Imani iliyosababisha
matokeo, sasa ndipo unapoweza kuamua kubadilisha matokeo hayo ikiwa ni mabaya
kwa kubadilisha Imani na si vinginevyo. Ukijidanganya kuanzia kwenye vitendo
narudia tena kusema ni lazima tu utafeli kwa mara nyingine, anzia kwenye mzizi
wa fitina “IMANI”
Imani
ilivyopunguza Corona Tanzania.
Tutaanza na MATOKEO kisha tutarudi
kinyumenyume mpaka kwenye IMANI.
MATOKEO:
Matokeo yetu kwenye hili suala la korona ni
KUPUNGUA KWA HALI YA UGOJWA/NAFUU KUBWA-Visa siyo vingi tena.
KITENDO:
Ni
kitendo gani au vitendo gani Watanzania wanavifanya sasa ambavyo ndio
vinavyotupatia matokeo haya tuyaonayo? Bila shaka vitendo ni Kufanya
kila aina ya jitihada zinazochangia katika kumaliza janga la corona huku
shughuli nyingine za kiuchumi zingali zikiendelea kama kawaida.
HISIA:
Ni
hisia zipi Watanzania walizokuwa nazo juu ya vitendo hivyo?
Watanzania hawana wasiwasi na korona
wanafanya mambo yao kama ilivyokuwa kabla ya ujio wa corona, hawahofii tena
kama corona itawaua wala njaa kutokana na lockdown
FIKRA:
Ni
fikra au mawazo gani yanayosababisha hizi hisia?
Corona itaisha kwa kuchukua tahadhari zote za
kisayansi, kumtegemea Mungu lakini pia hatua za kienyeji bila ya kujifungia
ndani na hata tukiugua tutapona hatutakufa.
5.
IMANI
Ni
Imani ipi inayosababisha fikra hizo?
Corona isitutishe na wala haina nafasi
Tanzania, ni ugonjwa ulioletwa na watu kutoka mataifa ya nje kwa makusudi au
bila kukusudia kwa lengo la kutufanya tuogope, tujifungie ndani na mwishowe tufie
huko kwa njaa.
Katika kutia Imani hiyo nguvu Rais John Pombe
Magufuli alifikia hatua ya kupima corona kwenye mapapai, mbuzi na sungura
akakuta vitu hivyo pia vina maambukizi jambo lililowashangaza watu wengi na
kuwaongezea Imani kwamba ugojwa huu si bure ni kama vile umepandikizwa.
Walizidisha Imani kuwa corona haina madhara kwa kiwango kilichokuwa
kimetabiriwa na Mataifa makubwa na matokeo yake ni huu ushindi tunaouona japo
corona haijamalizika kwa asilimia 100%. Tungelikazania kwenye vitendo vya 'kujilockdown' leo hii tungelikuwa wapi?
Hivi karibuni Mataifa mengi yamegundua siri
kuwa lockdown zisingeliweza kuwa suluhu endelevu ya corona bali suluhu ni
kuwajengea watu Imani ya kuishinda corona wakati huohuo shughuli nyingine
zikiwa zinaendelea kama kawaida mbinu ambayo Tanzania tulianza nayo tangu janga
hili linaanza mpaka sasa hivi ambapo maambukizi yameanza kupungua.
IMANI,
IMANI, IMANI, iwe ni ya dini au hata katika jambo jingine
lolote lile ikipandikizwa akilini na kugeuzwa hisia mwisho wake hushawishi
vitendo vitakavyoleta matokeo tarajiwa. Haiwezekani ukatenda vitendo pasipo
Imani wala Hisia yeyote ile vikakuletea matokeo unayoyatarajia, utajikuta tu
unaishia njiani, kusuasua au kupoteza kabisa motisha na ari ya kumalizia
vitendo hivyo. Matokeo mabaya ni zao la kupanda Imani ambaya kwenye akili zetu,
Imani ambayo inashawishi hisia mbaya.
Kitu kikubwa sana walichokifanya viongozi wa
Tanzania ni kuwaondolea watu Imani mbaya waliyokuwa wamejijengea kuhusu corona
na kuwavika Imani nyingine nzuri juu ya corona, basi hakukuwa na uchawi wala
mazingaombwe hapo. Watu wa dini mbalimbali hapa msinifikirie vibaya tafadhali,
dini nayo imechangia pakubwa katika vita na janga hili kwani dini pia ni Imani
chanya katika kupambana na jambo lolote lile baya duniani.
UTAITUMIAJE
IMANI KUBUSTI(KUINUA) UCHUMI/BIASHARA YAKO INAYOSAMBARATIKA?
Hatimaye sasa hebu tuone ni kwa jinsi gani
funzo la mapambano ya ugojwa wa corona Tanzania linavyoweza kukusaidia katika
mapambano mengine hasa ya kuondokana na umasikini kwa kuinua kipato chako cha
fedha.
Tutatumia mlolongo kama uleule tuliouona
kuanzia kwenye matokeo kurudi nyuma mpaka kwenye Imani. Tunachokitafuta hapa
zaidi ni Imani kwani pasipo kwanza kubadilisha Imani mtu aliyonayo juu ya
jambo fulani itakuwa vigumu sana kubadilisha matokeo ya jambo hilo, ataendelea
tu kupata matokeo yaleyale milele na milele.
MATOKEO:
Matokeo yetu kwenye suala hili la kiuchumi ni;
Ukata/umasikini/kukosa kipato cha kutosha
kuendesha maisha-
KITENDO:
Ni
kitendo gani au vitendo gani unavyovifanya vinavyokupa matokeo hayo?
Sipati wateja wa kutosha kwenye biashara
yangu kwa sababu sifanyi juhudi za kutosha za masoko kama ambavyo ningelipaswa
kufanya
HISIA:
Ni
hisia zipi ulizokuwa nazo juu ya hali hiyo?
Nina wasiwasi sitopata wateja wa kutosha na
ninaogopa kwamba biashara yangu inaweza ikafa
FIKRA:
Ni
fikra au mawazo gani yanayosababisha hisia hizi?
Mimi siyo mjuzi kwenye suala la masoko na
wala sipendi kazi hiyo kwani inanifanya nionekane kama vile nawalazimisha watu
kununua.
5. IMANI
Ni
Imani ipi inayosababisha fikra hizo?
Kazi ya masoko ni ya kulazimisha watu, haina
uhalisia na ni watu wenye uchu wa pesa tu ndio wanaopaswa kuifanya.
HITIMISHO
Ukishabaini IMANI inayokusababisha usipate
kile unachokitaka maishani basi tayari utakuwa umekaribia sana kupata suluhisho
la tatizo lako na utaweza hatimaye kubadilisha matokeo uliyokuwa ukiyapata kila
mara.
………………………………………
1. Kwa
Makala bora kabisa usizoweza kuzipata mahali pengine popote pale juu ya fedha
na Michanganuo ya biashara, karibu kwenye darasa letu whatsap na telegram,
Group la MICHANGANUO-ONLINE tuna masomo kila siku yatakayokujenga kisaikolojia na
kukuongezea ubunifu kwenye biashara yako. Kiingilio ni sh. Elfu 10 tu kwa mwaka
mzima unapata pia na masomo yote ya siku zilizopita. Lipia kwa 0765553030 au
0712202244 Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP
LA MICHANGANUO-ONLINE2021” pamoja na CHANNEL YAKE
2. Kujipatia
kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA REJAREJA bonyeza link hiyo.
3. Kupata
VITABU NA Michanganuo ya biashara mbalimbali zinazolipa tembelea duka letu la
vitabu mtandaoni la SMART BOOKS TANZANIA
0 Response to "JINSI YA KUTUMIA MAAJABU YALIYOPUNGUZA CORONA TANZANIA KUBUSTI UCHUMI WAKO UNAOSAMBARATIKA "
Post a Comment