Ukisikia biashara ya mtaji mdogo yenye faida
kubwa basi biashara ya kuuza chipsi ni moja ya biashara hizo. Hivi ulikuwa unajuabiashara ya chipsi kuku, soda
inavyolipa dar? Basi kama ulikuwa hulijui hilo fuatana na mimi leo
katika Makala hii ili uweze kulijua, unakula sahani ya chipsi kavu au chipsi
mayai huku ukishushia na soda baridi, je wajua sahani hiyo moja ya chipsi mpaka
inaingia mezani imegharimu kiasi gani cha fedha?.
Unamuona muuza chipsi akipokea hela nyingi
unasema, “Du jamaa anapiga pesa sana ngoja na mimi nianzishe banda langu la
kuuza chipsi, je unajua ni mahitaji ya shilingi ngapi utakayotakiwa uwe nayo
kabla hujaanza? Na je unajua mtaji wako wa chipsi utarudi baada ya muda gani kupita?
Unajua ili uweze kurudisha ghara zote za siku ulizotumia unatakiwa uuze angalao
sahani ngapi za chipsi kwa siku(Break eve point)?. Vipi kuhusiana na vifaa vya
kupikia chipsi, unajua bei ya jiko la kukaangia chipsi ni shilingi ngapi, jiko
la kupikia chipsi na mayai, bei ya kabati la chipsi, makarai, jiko la kuchomea
mishikaki, frying pan, sahani nk.?
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya car wash, kuosha magari mtaji na vifaa vinavyohitajika.
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya car wash, kuosha magari mtaji na vifaa vinavyohitajika.
Je unajua ni gharama zipi za uendeshaji wa
biashara ya chipsi unazotakiwa kuzilipa? Unatakiwa kujua gharama kwa mfano, bei
ya gunia la viazi mbatata/viazi ulaya, bei ya mafuta ya kukaangia chipsi, bei
ya mkaa au nishati utakayotumia iwe ni umeme, gasi au Maranda ya mbao. Bei ya
trei la mayai, bei ya viungo mbalimbali utakavyotumia kutengenezea saladi(kachumbari)
au chachandu kwa ajili ya kuongeza hamu na ladha kwenye chipsi zako wateja
wavutiwe zaidi kwako nk.
Baada ya kufahamu vitu vyote hivyo sasa
utatakiwa kujua unaweza ukapata faida kiasi gani katika mradi wako huu wa
kukaanga chipsi au Vihepe kama watoto wa mjini wanavyoita hasa wanafuzi wa
mashule na vyuo ambao ni wateja wakubwa sana wa chipsi katika miji mikubwa kama
Dar es salaam na kwingineko.
SOMA: Biashara ya mgahawa wa chakula, mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanzia
SOMA: Biashara ya mgahawa wa chakula, mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanzia
Faida utakayoipata itategemea sana ENEO lako
la biashara likoje, ikiwa ni eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu mfano stendi ya
mabasi, katika eneo la starehe na burudani kama bar au club, karibu na shule au
karibu na chuo, basi mauzo na faida yako itakuwa kubwa sana na nzuri. Lakini
ikiwa ni eneo tu la kawaida mtaani faida inaweza kuwa ya kawaida(wastani)
Ili kunogesha biashara yako ya chipsi
unatakiwa kama unao uwezo basi uweke na bidhaa nyingine mfano juisi, soda au
vinywaji vingine vya kushushia, kuwa na biashara ya juice pembeni au hata
biashara ya kuuza soda na maji sambamba na biashara yako ya chipsi itakuongezea
faida zaidi. Biashara ya chipsi vilevile inataka uwe na bidhaa ambatani kama
vile mishikaki, kuku wa kukaanga au wa kuchoma, firigisi, samaki, soseji na ndizi.
Bidhaa hizi ambatani zitaifanya faida yako kuongezeka zaidi.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
Sasa ili kujua hayo yote unapaswa kwanza
kufanya utafiti wa biashara ya chipsi ambao kwa mujibu wa kitabu cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIMALI Utafiti wa biashara yeyote ile siyo
chipsi tu, mtu unatakiwa kuuliza watu mbalimbali, kutembelea sehemu mbalimbali
kupata taarifa anuai zinazohusiana na biashara unayotaka kuifanya pamoja na
kusoma au kusikiliza machapisho yeyote yenye taarifa za biashara yako unayotaka
kuifanya. Kwa kifupi kabisa hivyo ndivyo utafiti wa biashara au upembuzi
yakinifu unavyoweza kufanyika wala huhitaji kuwa na digrii ya uchumi ndipo
ufanye utafiti wa biashara yako.
Hatua ya pili unatakiwa uandae mpango wa
biashara yako, hii ukiweza kuandika katika karatasi ni vizuri zaidi lakini pia
watu wengi huifanya tu vichwani mwao na kuanza ndio maana utakuta watu wengi
hawana kitu kinachoitwa mpango wa biashara ulioandikwa, siyo hawafanyi kabisa
mpango wa biashara hapana, bali hufanyia vichwani na kutekeleza moja kwa moja
kuokoa muda.
SOMA: Sababu kuu tano(5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaianzisha biashara yenyewe
SOMA: Sababu kuu tano(5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaianzisha biashara yenyewe
Kinachosababisha watu wengi kutokuandika
mipango ya biashara zao kwenye karatasi mara nyingi ni udogo wa biashara
zenyewe, utakuta mtu anataka kufanya biashara ya mtaji wa laki moja sasa anaona
yanini kusumbuka na tafiti na michanganuo, ila ukweli ni kwamba vitu hivyo huwa
anavifanya kimya kimya kichwani mwake bila hata ya yeye mwenyewe kujua kama
amevifanya. Ni lazima vifanyike, kamwe hamna namna nyingine unavyoweza kuanza
biashara bila utafiti na mpango.
Sasa tukirudi kwenye mchanganuo wa biashara
yetu ya chipsi kuku, mayai na chipsi kavu, hapa nitaanza kwa kuweka mahitaji ya
kuanzisha biashara ya chipsi ya mtaji wa kawaida kwenye eneo la kawaida uswahilini,
siyo maeneo ya ‘kishua’ yanayohitaji mtaji mkubwa sana.
SOMA: Naanza hatua kwa hatua kuandika mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama
SOMA: Naanza hatua kwa hatua kuandika mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama
Mchanganuo kamili wa biashara yetu ya chipsi
tutaandika hatua kwa hatua kwa njia rahisi kwenye group letu la Whatsapp la
MICHANGANUO-ONLINE siku ya leo tarehe 3/6/2020 usiku saa 3 mpaka saa 4 lakini
hapa chini nitakwenda kuweka mahitaji yote na gharama za kuanzia tu, nitaweka
gharama za kudumu za mradi wa chipsi, gharama za uendeshaji na pia nitaainisha
ni gharama zipi za moja kwa moja na zipi ni gharama zisizokuwa za moja kwa moja
katika mradi/biashara hii. Ndani ya group tutafafanua zaidi pamoja na kuandika
hatua kwa hatua kuanzia muhtasari mpaka ripoti ya faida na harasa.
Katika group la MICHANGANUO-ONLINE tumeanzisha
utaratibu wa kuandika michangauo ya biashara zenye fursa kubwa na faida hatua
kwa hatua, michanganuo hii inaweza kuwa mifupi au mirefu kulingana na aina ya
biashara husika lakini tutajitahidi michanganuo hiyo iwe mifupi na iliyo na
maana kwa mjasiriamali anayetaka kuiweka katika vitendo mara moja bila
kuchelewa. Tutakuwa tukizingatia zaidi vipengele vile vya mpango wa biashara
muhimu vinavyomrahisishia mtu kufanya utekelezaji haraka. Michanganuo hiyo mtu
anaweza akaiendeleza na kuifanya michanganuo kamili mirefu kwa urahisi zaidi.
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara? tumia njia hizi 3
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara? tumia njia hizi 3
Kabla sijaorodhesha mahitaji ya mradi wetu wa
chipsi katika eneo la uswahilini lakini lililo na watu wa kutosha, nitaainisha
kwanza Gharama mbalimbali ambazo mara nyingi watu huwa zinawachanganya. Kumbuka
nimesema mradi huu ni wa uswahilini lakini hata ikiwa unataka kuanzisha
biashara yako ya chipsi ‘ushuani’, tuseme labda maeneo ya watu wenye kipato
kikubwa kama vile masaki, Sinza, Ilala nk. basi unaweza tu ukatumia mfumo
huohuo wa kuorodhesha mahitaji yako yote na kitakachobadilika hapo ni bei tu za
vitu mbalimbali mfano wewe badala ya kuweka kabati la chipsi la shilingi laki
mbili basi weka la laki 8 au milioni kabisa. Na katika listi ongeza na gharama
za vitu kama AC, mayonnaise, sofa na kodi ya eneo kubwa kuanzia laki 2,3 mpaka
5 kwa mwezi badala ya elfu 50 au laki moja nk.
1. Gharama
za kudumu:
Hizi ni zile gharama za vifaa, banda na
vyombo kama majiko, makarai, kabati, meza na viti ambavyo hutumika zaidi ya
mara moja na pengine vinaweza kukaa hata zaidi ya mwaka mmoja
2. Gharama
za uendeshaji:
Huu ni mtaji wenyewe wa kuendeshea biashara,
ni zile gharama za uendeshaji biashara (vitu au shughuli zinazotumika kwa muda
mfupi mfupi, zinaisha na kwenda kununua vingine)
3. Gharama
za moja kwa moja:
Gharama hizi zinaweza kuwa pia katika upande
wa gharama za uendeshaji au za kudumu lakini ni zile tu zinazohusiana moja kwa
moja na uzalishaji wa bidhaa au huduma kwa mfano gharama za ununuzi wa viazi,
mafuta, saladi, chumvi, na mkaa.
SOMA: Jinsi ya kuandika mpango rahisi wa biashara kwa muda mfupi ndani ya nusu saa.
SOMA: Jinsi ya kuandika mpango rahisi wa biashara kwa muda mfupi ndani ya nusu saa.
4. Gharama
zisizokuwa za moja kwa moja:
Gharama hizi pia zaweza kuwa pande zote
mbili, upande wa gharama za kudumu au za uendeshaji lakini hazihusiani moja kwa
moja na uzalishaji wa bidhaa ama huduma inayozalishwa na mfano mzuri ni gharama
kama vile za uchakavu wa vifaa, mishahara, kodi ya pango na matangazo. Gharama
hizi hata usipozalisha kitu siku hiyo, mithali umeshaanza biashara yako ya
chipsi basi zitatumika tu na hamna namna ya kuzikwepa.
Jinsi ya kutumia aina zote hizo nne za
gharama zilizoainishwa hapo juu na ni wapi kila moja inatakiwa kutumika kwemye
mpango tutakwenda kuona kwa vitendo katika mchanganuo wetu huo wa biashara ya
kukaanga na kuuza chipsi katika Group la Michanganuo-online leo. Vitu vyote
tunavyojifunza katika group hili vinahifadhiwa na mara unapojiunga kwa mara ya
kwanza unapata fursa ya kuvidownload na kuvisoma hivyo hamna shaka ikiwa
ulipitwa na Michanganuo iliyopita.
MCHANGANUO WA MAHITAJI YA KUANZISHA BIASHARA
YA CHIPSI ENEO LA KAWAIDA LAKINI LENYE WATU WENGI KAMA BUGURUNI, MANZESE,
TANDIKA, MBAGALA RANGI TATU, MBEZI-KIMARA NK.
Nimetaja maeneo yaliyopo Dar es salaam lakini
si lazima iwe ni Dar, hata mikoani(mikoa yote) pia mfano huu unafanya kazi
hamna shida. Vile vile bei ya vitu mbalimbali na gharama zingine nimekadiria
tu, si lazima iwe hivyo kwa upande wako, itategemea maeneo ulipo na jinsi
ulivyoufanya utafiti wako. Hata hivyo bei hizi ni za wastani.
Jedwali
la mahitaji:
Gharama za kudumu/Vifaa:
|
|
Kabati la chipsi 1
|
150,000
|
Jiko la kukaanga chipsi 1
|
65,000
|
Jiko la kuchomea mishikaki na kuchaganyia
chipsi mayai 1
|
25,000
|
Karai kubwa 1
|
18,000
|
Meza 2 kubwa @ 50,000 na ndogo@20,000
|
70,000
|
Viti 4 @ 10,000
|
40,000
|
Benchi 1
|
5,000
|
Koleo la kuchotea chipsi 1
|
4,000
|
Frying pan ya chipsi mayai 2 @ 15,000
|
30,000
|
Sahani dazani 2 @ 800
|
20,000
|
Beseni
|
4,000
|
Vijiko, umma na chuma za mishikaki
|
10,000
|
Visu 2 @ 1,500
|
3,000
|
Ndoo 2 @ 3,000
|
6,000
|
Jumla ndogo
|
450,000
|
Gharama za
uendeshaji(mtaji)
|
|
Kodi (pango) miezi 6 @ 50,000
|
300,000
|
Mshahara wa msaidizi siku 3 @ 5,000
|
15,000
|
Viazi ndoo 2 @ 15,000
|
30,000
|
Mafuta lita 5 @ 3,000
|
15,000
|
Nyama ya mishikaki kilo 1
|
7,000
|
Kuku 1
|
6,500
|
Mkaa gunia moja
|
45,000
|
Mayai Trei 2 @ 6,000
|
12,000
|
Tomato source 1
|
2,000
|
Chili sorce
|
2,500
|
Chumvi, pilipili, nyanya na viungo vyote
kwa ajili ya kachumbari jumla
|
6,000
|
Foil paper/vifungashio
|
5,000
|
Dharura
|
54,000
|
Jumla ndogo
|
500,000
|
JUMLA KUU
|
950,000
|
Kwa hiyo kama uonavyo kwenye jedwali letu la
mahitaji ya kuanza biashara ya kukaanga
na kuuza chipsi, mtaji unaohitajika ni shilingi laki tisa na nusu(950,000/=)
Gharama za uendeshaji zimekadiriwa kiasi
kinachotosha kuanzia, na kwa kuwa kunakuwa na mzunguko wa pesa kila siku vitu
viunauzwa na kununuliwa vingine basi mzunguko utaendelea hivyohivyo huku faida
ikizidi kuongeza mtaji. Gharama za kudumu hazina haja ya kuongeza nyingine
zinatumika zilezile mpaka zitakapochakaa baada ya kipindi cha muda mrefu ambao
tutakuja kuona kwenye uchakavu. Tutakwenda pia kuona hatua kwa hatua jinsi ya
kukokotoa gharama ya sahani moja ya chipsi mpaka inamfikia mteja mezani ni
shilingi ngapi.
SOMA: Ni lini biashara yako itarudisha gharama zote ulizotumia?(break even analysis)
SOMA: Ni lini biashara yako itarudisha gharama zote ulizotumia?(break even analysis)
Kuhusu gharama za moja kwa moja na zisizokuwa
za moja kwa moja pia tutakwenda kuzionyesha kwenye mchanganuo wetu kamili
wakati tukiandika hatua kwa hatua kwenye group la MICHANGANUO-ONLINE, hapa
tumeziweka kwa ujumla tu.
Mpaka hapo ndugu msomaji wa blogu hii ya
jifunzeujasiriamali nimefika mwisho wa Makala hii lakini nakusihi
hakikisha umejiunga na group letu hili
kwa masomo zaidi ya michanganuo ya biashara na masomo mengine ya fedha
yasiyopatikana mahali kwingine kokote. Karibu sana!
...............................................................................
KULIPIA KUJIUNGA NA GROUP UPEWE NA MASOMO NA
SEMINA ZOTE ZILIZOPITA, TUMA NENO, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO NA
OFFA ZOTE MPYA”
*Ratiba ya Group la Michanganuo-online
*Ratiba ya Group la Michanganuo-online
SIKU
|
SOMO/MADA
|
Jumatatu
|
Somo la fedha
|
Jumanne
|
General/Vitu mchanganyiko
|
Jumatano
|
Michanganuo
|
Alhamisi
|
General/Vitu mchanganyiko
|
Ijumaa
|
Somo la Fedha
|
Jumamosi
|
General/Vitu mchanganyiko
|
Jumapili
|
Michanganuo
|
Siku za vitu mchanganyiko au general huwa
tunajifunza chochote kutoka kwa yeyote katika group pamoja na matangazo
mbalimbali ya biashara za wadau
Siku za masomo ya fedha na Michanganuo masomo
maalumu kuhusiana na mada hizo hutolewa na wataalamu mbalimbali usiku kuanzia
saa 3 mpaka saa 4 au 5
NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA ZOTE MPYA
ReplyDeleteUnakaribishwa, lipia kiingilio sh. elfu 10 utaunganishwa pamoja na kupata offa ya kitabu cha Michanganuo.
Deleteunalipajee
DeleteNiunganishe na group la michanganuo na ofa zote mpya
ReplyDeleteUnakaribishwa sana kwenye familia yetu: 0712202244
DeleteNiunganishe na mimi kwenye group 0685130309. Nataka mchanganuo wa biashara ya chipsi.
ReplyDeleteKaribu tuwasiliane michanganuo ipo ya aina mbalimbali ukiwemo wa chipsi: 0712202244
Deleteadd 0699539013
ReplyDeleteNiunganishe na group la michanganuo na offa zote mpya 0627701738
ReplyDeleteNiunge kwa group 0767022000
ReplyDeleteUnakaribishwa tuwasiliane tu kwa 0765553030
DeleteNiunge 0675 275 986
ReplyDeleteKarbu Anonymous tuwasiliane kwa namba 0712202244
Delete