Kama ilivyokuwa ada
sisi huwa tunapokea na kujibu kila siku maswali na changamoto fupifupi kutoka
kwa wasomaji wa blog ya jifunzeujasiriamali, baadhi ya maswali huwa tunaweka
majibu yake katika blogu hii na mengine tunayajibu tu kwa muulizaji basi. Leo
hii ni zamu ya msomaji mmoja kutoka jijini Dar es salaa na nimeweka mawasiliano
yake ya watsap namimi tangu tunasalimiana mpaka majibu kama ifuatavyo,
MUULIZAJI SWALI: za siku ndugu, nimepata namba
yako kwenye channel yako ya utube
JIFUNZEUJASIRIAMALI: Nzuri
tu ndugu Karibu Sana, Mimi naitwa Peter Tarimo ni mwandishi vitabu vya
ujasiriamali lakini pia blogu iitwayo jifunzeujasiriamali.co.tz
MUULIZAJI SWALI: Ninahitaji
kufanya biashara, lakini mtaji wangu Ni mdogo Sana, na Sina ajira naomba
ushauli wako
Nimekua
nikisoma makala mbalimbali za kutoka kwenye blog yako, vilevile kwenye
utube channel yako , Sasa ninahitaji kusimama na kuanza biashara, lakini kabla
cijaanza biashara nahitaji ushauri kutoka kwako Kama mjasiliamali
ulienitangulia najua utakua na kitu Cha kunishauli
Asante
MAJIBU:
Ikiwa tayari una njia
inayoweza kusapoti maisha yako yaani kupata mahitaji yale ya msingi ya kila
siku halafu umesema kwamba una mtaji kidogo sana, hapo panaweza kuwa na njia ya
wewe kuanza biashara hata kama ikiwa ni kwa ugumu(bootstrapping)
Kitu ninachokushauri
ni kwamba chekecha na upate wazo la biashara ambayo unajua kabisa kwanza ina
uwezekano mkubwa wa kupata wateja.
Biashara ya kufanya ya
namna hiyo mara nyingi sana ni zile biashara za bidhaa ama huduma zinazotumiwa
na watu kila siku, mtu hata akinunua leo lakini kesho au keshokutwa atahitaji
tena kitu hichohicho.
Pia wazo la biashara
hiyo hakikisha aidha unaifahamu au una uzoefu wa namna fulani nayo kusudi iwe
rahisi kwako kuifanya
Wakati wa kufikiria
wazo usijisumbue kabisa kuwaza kama mtaji utautoa wapi, wewe just fikiria tu uwezekano wa wewe
kuifanya hiyo biashara upoje
Ukishajiridhisha
kwamba wazo la biashara uliyokusudia kuifanya linatekekezeka na kuna uwezekano
wa kupata wateja watakaojirudia mara kwa mara, sasa angalia ni kwa vipi au ni
kwa njia gani unaweza ukaianza biashara hiyo katika hatua(level) ya chini
kabisa.
Hatua ya chini kabisa namaanisha
kwamba hata ikiwa kwa mfano biashara uliyowaza ni ya kumiliki kampuni ya utalii
basi hatua ya chini kabisa ni kuanzisha hata blog au ukurasa wako wa facebook
maalumu tu kwa ajili ya kuandika insha na dondoo zinazohusiana na maswala ya
utalii, katika hiyo kurasa au website pia unaweza ukaanza moja kwa moja
kuweka matangazo ya google ya kulipia(AdSense) ili uanze kuingiza chochote
mapema(pesa)
SOMA: Napenda kuanzisha biashara ila sina mtaji wala pesa za kununua vitabu kujiendeleza, nifanyeje?
Baadae utajikuta
taratibu unapata connection mbalimbali zitakazokufanya hatimaye uweze kuifikia
ndoto yako ya kuwa na biashara ya utalii
Huo ni mfano tu lakini
wa mtu ambaye labda ana uzoefu au mapenzi na biashara ya utalii. Zipo biashara
za aina nyingi za mtaji mdogo Tanzania unazoweza kuanzisha ingawa watu wengi
huwa tunazipuuzia au kuogopa watu wengine watatuonaje tutakapokuwa tukizifanya
au watatucheka nk.
Biashara ya duka kwa
mfano, biashara zilizosahauiika kama hii hapa na hata biashara ya kukaanga
mihogo na nyinginezo nyingi nilizowahi kuandika katika blogu yangu ya
jifunzeujasiriamali ni aina za biashara mtu anazoweza akaanza kwa mtaji kidogo
sana huku akijiwekea mipango ya biashara kubwa zaidi. Wakati huo wa kujipanga
usisahau kujifunza mambo yahusuyo ujasiriamali na biashara, unaweza kujifunza
popote pale unapoona ni rahisi kwako kujifunza. Siku hizi kuna mitandao ya
kijamii, vyombo mbalimbali vya habari na hata unaweza kuhudhuria semina za
ujasiriamali na makongamano.
Kumbuka unaweza kuanza
na biashara ndogo sana lakini lengo lako kubwa liwe ni unataka kukuza mtaji ili
uje ufanye biashara kubwa zaidi hapo baadae.
Ninachokushauri ni
kwamba usiogope kuanzia chini. Watu wengi uwaonao leo wana mafanikio makubwa
walianzia chini sana huku wakitengeneza wateja na soko kwanza kabla ya mitaji
mikubwa.
Hakuna njia ya mkato
duniani ya kuanza biashara, ni lazima ukubali kuanza kidogo huku ukifikiria
makubwa(Start small but think big)
Asante, naamini
ushauri wangu ukichanganya na mawazo yako mwenyewe vinaweza vikakupa mwangaza
walao kidogo wa kuanza biashara endelevu na mtaji mdogo uliokuwa nao.
……………………………………………………..
Je, una
swali au changamoto yeyote ile kuhusiana na Biashara na Ujasiriamali? Tuma
swali au changamoto yako fupi kupitia Whatsap: 0765553030 au e-mail: jifunzeujasirimali@gmail.com
tutaijibu hapa. Hatutaji utambulisho wa mtu pasipo ridhaa yake mwenyewe. Asante
Kwa vitabu
vyetu na michanganuo mbalimbali ya Biashara tembelea duka la vitabu la SMARTBOOKS TANZANIA hapa
Unaweza pia
kujiunga na Group letu la Masomo ya kila siku ya fedha na Michanganuo kwa
kulipa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu kwa mwaka, lipia kwa namba 0765553030 au
0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA
GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE”
Pia usisahau, kile kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA toleo la 2020 lililoboreshwa kwa kuongeza mbinu na njia za kuthibiti udokozi na usimamiaji wa mahesabu wenye tija sasa kinapatikana bonyeza Jina la kitabu hapo kukipata.
Pia usisahau, kile kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA toleo la 2020 lililoboreshwa kwa kuongeza mbinu na njia za kuthibiti udokozi na usimamiaji wa mahesabu wenye tija sasa kinapatikana bonyeza Jina la kitabu hapo kukipata.
0 Response to "MTAJI WANGU NI MDOGO SANA LAKINI NAHITAJI KUFANYA BIASHARA NA SINA AJIRA NAOMBA USHAURI WAKO"
Post a Comment