Bila shaka yeyote ile kama hujawahi mwenyewe kuwa na
biashara iliyoanguka chini ilihali ina faida kubwa basi umewahi kusikia watu
wengine ambao biashara zao ziliwahi kufa au kuporomoka kabisa na sababu kubwa
ikiwa si kukosekana wateja wala faida ya kutosha bali sababu nyingine kabisa
tofauti.
Linaweza likawa ni jambo la kusikitisha sana kuona
biashara nzuri unayoipenda na yenye faida kubwa tu ikikushinda na kuiacha
hivihivi kwa sababu ambayo inaweza kuonekana ni nyepesi lakini ni sababu nyeti
pengine kuliko sababu nyingine zozote zile zinazochangia kuyumba au
kutokuendelea mbele kwa biashara nyingi za wajasiriamali wadogowadogo.
Ili kuielezea sababu hiyo vizuri zaidi itanibidi kutumia
mahesabu kidogo ya mpango wa biashara ingawa sitaingia kwa undani sana. Sababu
hii ya biashara kufa hata ikiwa ina uwezo wa kuingiza faida nyingi mara nyingi
sana mtu unaweza ukaibaini kabla pale unapokaa chini na kuandika
mpango/mchanganuo wa biashara yako kabla haujaianza au hata biashara ikiwa
tayari inaendelea lakini ukaamua tu kufanya makisio ya mzunguko wa fedha
taslimu(cash flow) katika biashara yako jambo ambalo siyo gumu hata kidogo.
Sababu kubwa kwanini baadhi ya biashara zenye faida
hufilisika inatokana na biashara hizo kushindwa kulipa baadhi ya gharama zake
kunakotokana na ukata au ukosefu wa mtaji wa kutosha kuendeshea kazi au working
capital kwa kimombo, maana yake ni fedha ambazo mfanyabiashara
inakubidi uzitenge kabisa mapema kwa ajili ya kuja kulipia gharama mbalimbali
wakati biashara ikiendelea. Kukosekana kwa fedha hizi maana yake biashara nayo
imekufa kwani hutaweza kulipa wanaokusambazia bidhaa wala madeni mengine
yatokanayo na uendeshaji wa biashara yako.
Kumbuka biashara kabla haijatengeneza faida ni lazima kwanza ununue malighafi kwa fedha
taslimu. Hata ikiwa ni biashara ya huduma ni lazima kwanza ulipie vitu
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujilipa wewe mwenyewe ili uweze kuiendesha hiyo
biashara nk. Sasa ikiwa hauna mtaji wa kulipia hivi vitu kabla ya kulipwa na
wateja uliowakopesha utaona kwamba biashara ni lazima itafeli tu.
Ili kuweza kuielezea vizuri dhana hii, nitatumia
majedwali ya ripoti za mahesabu ya mfano wa biashara ya mtaji wa laki moja
(100,000/=) ambayo mjasiriamali aitwaye Juma ananunua vyombo vya ndani na
kwenda kuviuza ili kupata faida. Biashara ya Juma ina faida nzuri tu, akinunua
vyombo vya mtaji wa shilingi laki moja akienda kuuza anapata faida ya shilingi
elfu hamsini(50,000). Huu ni mfano rahisi wa haraka haraka na ambao
unatuonyesha uhusianao uliopo kati ya ripoti zote 3 za biashara, Faida
na hasara, Mizania(Rasilimali na madeni) na ile ya Mzunguko wa Fedha taslimu
Sasa kabla Juma hajanunua chochote hebu tuone ripoti za
biashara yake za Faida & Hasara na ile ya Mali & madeni(Mizania)
zipoje;
1.
Kabla Juma hajafanya muamala wowote ule.
Ripoti
ya Faida & Hasara
Mauzo
|
0
|
Gharama
zamauzo
|
0
|
Faida
|
0
|
Ripoti
ya Mali na Madeni;
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
100,000
|
Wadaiwa
|
0
|
Jumla
|
100,000
|
MADENI & MTAJI
|
|
Madeni
|
0
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
0
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
100,000
|
Hapo juu kwenye Fida na hasara tunaona hamna kitu kwani
biashara bado haijafanyika. Katika mizania au Mali na madeni tumeona upande wa
Rasilimali jumla yake ni sh. 100,000 na kwenye Mtaji na madeni Jumla yake sh.
100,000 pia. Kumbuka kimahesabu, RASILIMALI = MADENI + MTAJI
2. Muamala
wa kwanza wa Juma.
Ni pale Juma atakapokwenda kununua vyombo na kuviuza kwa
mara ya kwanza.
Faida
& Hasara
Mauzo
|
150,000
|
Gharama
zamauzo
|
100,000
|
Faida
|
50,000
|
Mizania
(Mali na Madeni);
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
150,000
|
Wadaiwa
|
0
|
Jumla
|
150,000
|
MADENI & MTAJI
|
|
Madeni
|
0
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
50,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
150,000
|
Hapo juu inamaana kwamba Juma alitumia mtaji wa shilingi
laki moja (100,000/=) kununulia vyombo vya ndani na alipoviuza alipata faida ya
shilingi elfu hamsini (50,000/=) sawa na kusema, MAUZO – GHARAMA ZA MAUZO =
FAIDA. Kwa upande wa Mizania ataishia kuwa na fedha taslimu sh. 150,000/=
wakati Madeni na mtaji ikiwa pia ni jumla sh. 150,000 na pande hizo mbili
zinalingana.
SOMA: Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ni moyo wa mpango wa biashara (The heart of a business plan)
Juma anarudi tena mara ya pili kwenda kununua mzigo (vyombo)
kwa mtaji uleule wa shilingi laki moja na kwenda kuviuza tena kama alivyofanya
mwanzoni. Anarudia zoezi hilo mpaka anafikisha mara tatu na ripoti zake sasa
zitasomeka kama ifuatavyo baada ya miamala hiyo mitatu;
Faida
& Hasara
Mauzo
|
450,000
|
Gharama
zamauzo
|
300,000
|
Faida
|
150,000
|
Mizania
(Rasilimaliali na Madeni);
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
250,000
|
Wadaiwa
|
0
|
Jumla
|
250,000
|
MADENI
& MTAJI
|
|
Madeni
|
0
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
150,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
250,000
|
Hapo juu ni ripoti za Faida na Hasara na Mizania ya
biashara ya Juma baada ya kuuza vyombo mara 3 kwa mtaji wa laki moja aliokuwa
nao. Lakini ukiangalia katika uhalisia wa biashara ulivyo, biashara haiwezi
kuwa namna hii, kwa mfano mauzo mengine unaweza kufanya kwa mkopo wateja wakaja
kukulipa baada hata ya siku 30 au zaidi ya hapo.
Kwa hiyo kwa mfano ikiwa kama Juma atakuwa aliuza kwa
mkopo vyombo vyake hatuwezi tukasema kwenye mizania yetu hapo juu Juma atakuwa
na fedha taslimu zote mfukoni au benki shilingi laki mbili na nusu, 250,000/=.
Atakuwa akidai na hivyo ni lazima katika mizania yetu tufanye marekebisho kama
ifuatavyo ingawa faida itabakia kuwa vilevile,
3.
Mauzo ya Juma kwa mkopo;
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
0
|
Wadaiwa
|
150,000
|
Jumla
|
150,000
|
MADENI & MTAJI
|
|
Madeni
|
0
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
50,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
150,000
|
Juu: Mauzo na faida vipo vilevile lakini mfukoni Juma
hana kitu, amekopesha vyote. Sasa hapo ndipo shida inapoanzia, Juma atakwenda
kununua mzigo mwingine kwa pesa ipi wakati hajalipwa na wateja wake? Ili
kusuluhisha tatizo hili kwa muda Juma anaamua kununua baadhi ya vyombo kwa
mkopo pamoja na kuomba mkopo benki wa sh. 200,000 na majedwali yataonekana kama
ifuatavyo;
Faida
& Hasara
Mauzo
|
150,000
|
Gharama
zamauzo
|
100,000
|
Faida
|
50,000
|
Juma
anakopa mali na fedha;
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
0
|
Mali
za stoo(alizokopa)
|
100,000
|
Wadaiwa
|
150,000
|
Jumla
|
250,000
|
MADENI
& MTAJI
|
|
Madeni(wadai)
|
100,000
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
50,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
250,000
|
Hapo biashara angalao sasa inaoneka ni nzuri baada ya
Juma kukopa vyombo vya shilingi 100,000(Wadai) vyombo hivi vitamwezesha
kuendelea na biashara hata kama bado wadaiwa wake hawajamlipa deni la sh.
150,000. Sasa anavyo vvyombo vya shilingi laki moja stoo huku akisubiri kulipwa
sh. 150,000 zake.
Biashara inapozidi kushamiri baada ya kukopa bidhaa, Juma
anaamua kukopa tena pesa nyingine benki sh. 200,000 kusudi aweze kununua vyombo
zaidi na ripoti zitakuwa hivi;
Mauzo
|
450,000
|
Gharama
zamauzo
|
300,000
|
Faida
|
150,000
|
Juma
anakopa fedha;
RASILIMALI
|
|
Fedha
taslimu
|
0
|
Wadaiwa
|
450,000
|
Bidhaa
stoo
|
100,000
|
Jumla
|
550,000
|
MADENI & MTAJI
|
|
Madeni(wadai)
|
100,000
|
Deni
benki
|
200,000
|
Mtaji
|
100,000
|
Faida
|
150,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
550,000
|
Lakini hata hivyo bado katika biashara hii ya Juma hakuna
uhalisia sana kwani bado kuna vitu kama vile gharama za uendeshaji wa biashara
hiyo mfano pesa za kujilipa mshahara wakati akifanya biashara kwani ni lazima
ale apande daladala nk. gharama za mawasiliano kama bando la simu na hata fedha
za dharura ikiwa lolote linaweza kutokea, Vile vile wakopeshaji wake (Wadai) ni
vipi watakubali kumkopesha Juma ikiwa hana rasilimali zozote zile zinazoonekana
kama dhamana? Au hata ni benki gani itakubali kumkopesha mtu asiyekuwa hata na
mali au akiba kidogo?
Jibu la maswali hayo yote ni MTAJI WA KUENDESHEA
KAZI(Working Capital). Hiki ndio kitu kilichokosekana kwenye biashara hii ya
Juma tangu anaianza. Mtaji wa kuendesha biashara ndiyo kitu kinachosababisha
mzunguko wa fedha wa biashara yako uweze kuwa mzuri na ni lazima uhakikishe
tangu mwanzo unao, vinginevyo hautaweza kudumu kwenye biashara hata kama
biashara yenyewe ina faida nusu kwa nusu kama ilivyokuwa kwa biashara ya Bwana
Juma hapo juu.
Mtaji wa kazi(Working capital) katika miamala yote 3
Faida
& Hasara
Mauzo
|
450,000
|
Gharama
zamauzo
|
300,000
|
Faida
|
150,000
|
Mizania
ya Biashara;
RASILIMALI
|
|
Fedha taslimu benki(working capital)
|
300,000
|
Wadaiwa
|
450,000
|
Mali
za stoo
|
100,000
|
Jumla
|
850,000
|
MADENI
& MTAJI
|
|
Madeni(wadai)
|
100,000
|
Deni
la benki
|
200,000
|
Mtaji
|
400,000
|
Faida
|
150,000
|
Jumla Madeni na Mtaji
|
850,000
|
Kama uonavyo jedwali letu hapo juu, Biashara ya Juma
ilihitaji kuanzishwa na mtaji wa shilingi laki nne (400,000/=) badala ya mtaji
wa shilingi laki moja, 100,000/= za pale awali. Kwa hali hii sasa biashara ya
Juma inaweza kuwa na uhalisia kwani mtaji wa kuendeshea biashara(Working
capital) ni shilingi,
850,000 - 300,000
= 550,000/= badala ya shilingi
250,00 za awali. Kumbuka Mtaji wa kuendeshea kazi = (Jumla ya mali za muda
mfupi – Jumla ya madeni ya muda mfupi).
HITIMISHO
Majedwali hayo yote tuliyoyaona hapo juu yanatuonyesha
uhusiano ulokuwepo baina ya ripoti zote tatu za fedha kwenye mpango wa
biashara.
Ili kufahamu zaidi kuhusiana na Michanganuo ya Biashara
na jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yeyote ile kwa njia rahisi kabisa,
jipatie kitabu chetu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Ni Kitabu
pekee Afrika Mashariki cha Michanganuo kilichoandikwa kwa lugha adhimu ya Kiswahili.
BEI
NA JINSI YA KUKIPATA:
22,000/=
Kitabu cha karatasi(Hardcopy) tunakuletea popote ulipo jijini Dar es salaa. Kwa
mikoani tunatuma kifurushi ila gharama ya basi huongezeka kutegemeana na umbali
na aina ya basi.
10,000/=
Kitabu kwa njia ya mtandao(Email) (SOFTCOPY) Tunatuma kitabu ukiwa mahali
popote pale Duniani kwa njia ya email
MAWASILIANO:
Watsao/simu: 0765553030
Simu/sms:
0712202244
Pia masomo ya kila siku kwenye Group letu la Whatsapp la
Mchanganuo-online bado yanaendelea na leo hii tarehe 18 June 2020 tutakuwa na
somo lisemalo;
“IKIWA
ADUI MKUBWA WA FEDHA ZAKO NI WEWE MWENYEWE UFANYEJE ILI ZIWE SALAMA?”
Kujiunga na group hilo lipa kiingilio chako sh. 10,000/=
kupitia namba zetu; 0765553030 au 0712202244 kisha tuma ujumbe usemao; “NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA MPYA YA MASOMO NA VITABU” Baada ya kujiunga
tunakutumia Michanganuo, Vitabu na Masomo yote yaliyopita siku za nyuma.
0 Response to "SABABU KUBWA KWANINI BIASHARA INAWEZA KUFA HATA KAMA INA FAIDA NZURI TU NA YA UHAKIKA?"
Post a Comment