Inawezekana ulipata taarifa juu ya offa hii
na bado hujaamua kuchukua hatua, unajua ni sababu ipi kubwa iliyokufanya
usichukue hatua licha ya offa yenyewe kuwa ya kipekee na ambayo ikishapita
haitarudi tena? Sababu zaweza kuwa ni nyingi na tofauti kulingana na mtu na mtu
lakini kusema ule ukweli asilimia kubwa ya watu jambo kama hili wanakuwa na
sababu za kushangaza sana ukifanikiwa kuzijua.
SOMA: Download / pakua hapa kitabu Fikiri Utajirike (Think and Grow Rich) kwa Kiswahili, sura zote 15 bure
SOMA: Download / pakua hapa kitabu Fikiri Utajirike (Think and Grow Rich) kwa Kiswahili, sura zote 15 bure
Simply itakuta ni hofu tu au wasiwasi, na
sababu za hofu unaweza kukuta ni kutokana na offa yenyewe kuwa imetangazwa
mtandaoni hivyo mtu anahofia kutapeliwa basi, ingawa kweli wapo wenye sababu za
msingi kama kukosa pesa kwa muda huo, mwingine anaweza kuogopa tu kuwa labda
hatapata faida iliyoahidiwa nk.
Lakini ikiwa una hofu yeyote nikuhakikishie
tu kwamba offa hii ni ya kweli(Genuine) na wale wote waliojipatia tayari, kamwe
hawawezi kujutia kwani thamani waliyoipata ni kubwa mara 20 kuliko gharama
waliyotoa. Nimetoa zaidi ya vitabu na michanganuo 20 kwa sh. Elfu 10 tu, vitu
ambavyo mtu angelipia karibu shilingi Laki 2. Nimepata jumbe nyingi watu
wakishangaa ni kwa vipi niuze vitu vingi kama hivyo kwa bei ya kutupa namna
hiyo
SOMA: Jinsi unavyozuia mafanikio makubwa maishani kwa kuhangaika na vitu vidogovidogo
SOMA: Jinsi unavyozuia mafanikio makubwa maishani kwa kuhangaika na vitu vidogovidogo
MZIMU
WENYEWE NI HUU HAPA;
Tukiachana na masuala hayo ya offa hebu sasa tuone
mada yetu ya leo inazungumzia kitu gani hasa;
1) Una
ndoto kubwa maishani lakini kila ikija fursa kitu fulani kinakuvuta kwa nyuma
usiijaribu?
2) Kila
ukitaka kujaribu fursa fulani unahisi watu wengine watakuonaje au ukifeli
itakuwaje na kisha unaachana nayo?
3) Hata
ulipojaribu sana kuchukua hatua ukakamilisha baadhi ya malengo uliyojiwekea
baadae ulibaini wala hujaridhika moyoni baada ya malengo mengine kuibuka upya?
4) Kutafuta
suluhu ya hali hiyo umejaribu mbinu nyingi za utatuzi kutoka kwa washauri na
makocha mbalimbali bila ya mafanikio yeyote?
Tutayajibu maswali hayo baadae kidogo
mwishoni mwa hili somo ila kikubwa ninachotaka kukizungumzia hapa leo ni hiki
kifuatacho;
Akili zetu wanadamu zina nguvu sana kuliko
vile tulivyokuwa tukifikiria na hata wakati mwingine akili yako mwenyewe
inaweza kuwa inakuhujumu usiweze kuyafikia mafanikio yale unayostahili. Unaweza
kuwa usiwe unalifahamu hili lakini linapokuja suala la kufanya mabadiliko ya
kweli katika maisha yako akili yako ndiyo adui yako mkubwa. Na usije ukadhani
labda hili hutokea kwako tu hapana, hutokea kwa watu wengine wengi nikiwemo
hata na mimi mwenyewe ninayekuandikia huu ujumbe.
Ni watu wangapi umewahi kuwasikia wakipanga
hili na lile katika juhudi za kutaka kubadilisha maisha yao? Ukimsimamisha mtu
yeyote leo njiani, atakueleza mipango lukuki na malengo aliyojiwekea toka
Januari, na hii ni Julai muulize sasa ametekeleza mangapi, nakuambia
utashangaa! Si kama nasema ni kila mtu hapana ila ni asilimia kubwa sana ya
watu.
SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini ujiwekee malengo makuba maishani
SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini ujiwekee malengo makuba maishani
Sasa ni kitu gani kinachotokea kwenye akili
zetu? hicho hasa ndio mchawi mwenyewe anayeharibu kila kitu na si mwingine bali
ni HOFU au WOGA. Hofu ndio mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya ndoto zetu.
Woga unazima ndoto za watu wengi duniani na hatimaye kuwafanya waingie
makaburini mwao na ndoto zao hizo, ndio maana waswahili husema kuwa Makaburini
ndio mahali palipolala mabilionea wengi zaidi hata kuliko duniani penyewe.
Hofu ina tabia ya kujivika tabia ya huruma na
kukudanganya kama vile ina nia ya kukukinga na hatari fulani inayokunyemelea
hata kama hatari yenyewe siyo hatari ni fursa kubwa kwako. Kazi yote hii hufanywa
na akili yako mwenyewe katika harakati ‘feki’ za kutaka kukulinda na madhara
mbalimbali, mengine yakiwa wala si madhara asilani. Ni sawa na Mwanamke (Mama) anayehofia
kumpeleka bintiye mdogo akaanze shule ya chekechea siku yake ya kwanza kabisa
kwa hofu kuwa mwanaye huyo anaweza kudhurika njiani kwa namna moja au nyingine.
SOMA: Kwanini huruma na upendo wa wazazi kwa watoto hupita kiasi?
SOMA: Kwanini huruma na upendo wa wazazi kwa watoto hupita kiasi?
Wazazi wengi (mimi hii iliwahi kunikuta) hukaribia hata kuahirisha mwaka
kuwaanzishia watoto wao chekechea kutokana na sababu hii, mama atahakikisha
siku ya kwanza anashinda hata nje ya geti la shule akiogopa tu mwanaye muda wa
kutoka anaweza kubakwa, kuibiwa na watu wasiojulikana au hata kugongwa na gari
au pikipiki hata kama shule yenyewe ina utaratibu mzuri tu wa kuwapeleka watoto
makwao muda wa kutoka.
Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi sana vile
vitu akili zetu hutudanganya kuwa ni vya hatari tusivifanye, mara nyingi
utakuta ndiyo fursa za mafanikio zilipolala. Woga wa mama kumpeleka bintiye
akaanze chekechea siku yake ya kwanza kabisa hajui kama kumbe anamyima mtoto
fursa ya ‘dhahabu’ ya kujifunza mapema, kukua na kukomaa kiakili. Vipi kama
ataendelea kumwacha tu nyumbani mwaka mmoja tena zaidi akaja kukuta watoto wa
rika lake wameshafika darasa la kwanza au la pili?
SOMA: Mchanganuo wa biashara: Kuanzisha shule ya chekechea(Day care Centre)
SOMA: Mchanganuo wa biashara: Kuanzisha shule ya chekechea(Day care Centre)
Mara nyingi akili zetu hudhania zinajua kila
kitu kinachoendelea katika mazingira yetu na kutufanya tuamini kuwa jambo fulani
haliwezekani kabisa hata kama katika jambo hilo hakuna kitu chochote kile
kilichoziba mbele yake. Akili zetu hutupofusha tusiweze kuziona fursa sahihi
zilizoko mbele yetu.
Hii ndiyo sababu kubwa sana ni kwanini watu
wengi tunashindwa kuufikia uwezo wetu wote tuliokuwa nao pale tunapotaka
kutimiza malengo tuliyojiwekea ili tuishi maisha yenye mafanikio tunayotamani
kila siku na kuendelea tu kubakia kuwa watumwa wa akili zetu wenyewe.
SULUHISHO
Napoleon Hill katika kitabu chake, Think and Grow Rich anafundisha njia
sahihi zitakazokuwezesha kuitumia akili yako vizuri na kuondoa kabisa hofu zile
zisizokuwa na msingi wowote kwani zipo hofu za kweli na zile za uwongo (fake).
Siwezi kukusimulia hapa ni kwa namna gani, ila ukisome mwenyewe kitabu hicho na
hata ikiwa ulishakisoma lakini hujakielewa vizuri basi nakushauri ukisome tena
na tena kama njia sahihi ya ‘kumaster’
yale yaliyofundishwa humo.
Toka sura ya kwanza mpaka ya kumi na tano
kina shuhuda na mifano ya watu wengi waliofanikiwa au kufeli kutokana na jinsi
walivyozitumia akili zao kufikiri na katika Sura ya 15 yenyewe imezungumzia
mahsusi kabisa jinsi mtu anavyoweza kuondokana na Mzimu wa woga unaotuhumiwa
kukatisha ndoto za watu wengi Duniani.
SOMA: Think and Grw Rich kwa ufupi: Mapitio ya vitabu vya mafanikio(Book Review)
SOMA: Think and Grw Rich kwa ufupi: Mapitio ya vitabu vya mafanikio(Book Review)
Basi ndugu yangu chukua hatua leo usikubali
tena kumruhusu adui HOFU kuendelea kukudanganya kila mara kwamba unaibiwa,
unadhulumiwa, unahujumiwa, unatapeliwa na ‘kekundu’ na karata tatu nk. kwa
kisingizio eti cha kukulinda uwe salama kumbe ndio kwanza inazidi kukudidimiza,
hofu zingine kweye maisha yetu ni za ukweli lakini nyingi kwa kweli ndio hizi
kama tulizoona hapa.
Wala si kama nakushauri kila fursa uingie
kichwakichwa tu bila ya kufanya utafiti wa kina hapana, bali ninachotaka ujue
ni kwamba chukua hatua ya zile fursa zinazoonekana bayana kabisa kwako bila
kusitasita ndio mafanikio utayaona maishani.
Na mwisho kabisa usisahau hili, kama bado
hujajipatia OFFA yangu ya mwisho kwa mwaka huu, basi ufanye hivyo leo kabla ya
siku ya Jumatatu tarehe 6, 2020. Zimebakia siku 2 tu toka siku ya leo offa
ifungwe rasmi. Ukitaka kujua thamani halisi ya Vitabu, Michanganuo na Seminars
nilizokuwekea katika offa hii ya kipekee, tembelea ukurasa huu hapa wa DUKALANGU LA VITABU MTANDAONI kujua kila kitu kinauzwa shilingi gani.
Hutaamini! Unaweza ukasema hivi, “Ni mwendawazimu pekee anayeweza kutoa offa
kama hii”
“Peter
are you Crazy? what kind of that OFFA are you giving to people.” Mimi
wala siyo mwendawazimu kama alivyoniuliza rafiki yangu huyo whatsap juzi, bali
napenda tu kushea maarifa na wenzangu kwani naamini hata watu wa Magharibi
wangelikuwa wachoyo wa maarifa leo hii wala usingelisikia Wachina na Mataifa
mengine tukiwemo na sisi huku Afrika tukijivunia Gunduzi za kushangaza kabisa
za kisayansi na elimu nyinginezo nyingi kubwakubwa za kistaarabu.
SOMA: Vitabu Chanzo cha maendeleo na mafanikio makubwa ya binadamu duniani
SOMA: Vitabu Chanzo cha maendeleo na mafanikio makubwa ya binadamu duniani
Asili ya elimu na maarifa MWENYEZI MUNGU hajaviwekea mipaka hata
kidogo na ndio maana hata uliona pamoja na Wamarekani kuwa watu wa kwanza
kabisa duniani kuunda Nyuklia, lakini Urusi haikushindwa nayo kupata teknolojia
hiyo ngumu ingawa walikuwa mahasimu wakubwa, halikadhalika Korea ya Kaskazini
na sasa Irani. Maarifa hayabagui dini, rangi wala kabila, hayajali unatoka
kusini, kaskazini au Mashariki na wala hayaangalii kama wewe ni bepari au
mkomunisti
Pia nimalizie na yale Masomo ya kila siku ya
fedha na michanganuo kwenye lile group letu la masomo la (MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP) Yameanza tena na wote wanaochukua
offa hii wanaunganishwa moja kwa moja bureee! mwaka mzima, somo letu la leo
lina kichwa kisemacho, “MBINU ZA KUBAJETI FEDHA KIDOGO KWENYE
BIASHARA MPYA INAYOANZA.”….na kesho Jumamosi tutakuwa na Mchanganuo wa biashara ya kuuza mchele wa
jumla na rejareja hatua kwa hatua. Hivyo
unakaribishwa sana.
OFFA ina
vitu vifuatavyo;
1. KITABU: Tafsiri nzima ya
Think & Grow Rich (Fikiri Utajirike)
Ndio kitabu mashuhuri zaidi cha fedha na mafanikio kuwahi kuandikwa duniani
–cha Kiswahili & cha kiingereza
2. KITABU cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI - cha
kiswahili
3. KITABU: Mifereji 7 ya pesa
na siri matajiri wasiyopenda kuitoa- cha
kiswahili
4. KITABU mashuhuri zaidi
duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio
kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.- cha
kiingereza
5. KITABU: Masomo
ya fedha yaliyofundishwa watsap Part 1–cha
kiswahili
6. KITABU: Masomo ya fedha
yaliyofundishwa watsap Part 2 -cha
kiswahili
7. KITABU: Michanganuo
hatua kwa hatua, watsap, part 3 –cha kiswahili
8. Semina ya siku 7 na mpango kamili wa
biashara ya usagishaji nafaka - unga wa dona (USADO
Milling) )-kwa kiswahili
9. Kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji
wa kuku (MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa
nyama na kuku wa kienyeji-zote
kwa kiswahili
10.
Mchanganuo
kamili wa kilimo cha Matikiti maji (KIBADA WATERMELON BUSINESS
PLAN) -kwa kiswahili
11.
Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingereza
12.
Mchanganuo
kamili wa Biashara: Kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)
-kwa Kiswahili
13.
Mchanganuo
kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE) -kwa Kiswahili
14.
Somo
maalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwa
biashara yako-kwa
kiswahili
15.
Vielezo
(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha
kuandika michanganuo kwa muda mfupi. kwa
Kiswahili & kiingereza
16.
Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA
SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato
yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5–kwa
kiswahili
17.
Ukurasa
mmoja wa mchanganuo(One
page Business plan).(Njia fupi zaidi ya kuandika mchanganuo
wa biashara yako kwa nusu saa tu, na mfano)
–kwa kiswahili
18.
Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan)
(NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
19.
Vipengele / (Outlines) vya Mpango
wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa
kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika mwenyewe bila mtaalamu.
20.
Kuungwa group la Michanganuo
la mentorship mwaka mzima(michanganuo-online
mastermind group) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu
michanganuo na ujasiramali kwa ujumla
Kupata
offa mara moja, lipia sh. Elfu 10 kupitia namba zangu; 0712202244 au 0765553030
Tuma pia na ujumbe watsap: 0765553030 au SMS ya kawaida usemao, “NATAKA OFFA YA
MWAKA 2020 YA VITU 20” Ikiwa utapenda nikuunge pia na Master Mind Group la
MICHANGANUO-ONLINE naomba uniambie tafadhali manake watu wengine haapendelei kuwa
kwenye magroup bali wanahitaji tu OFFA yenyewe.
Siyo lazima uwe na Watsap, hata Email peke
yake inatosha nitakutumia kila kitu kwa email yako.
Asante sana,
Asante sana,
PETER AUGUSTINO TARIMO
0 Response to "MZIMU HATARI UNAOONGOZA KUZIMA NDOTO ZA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI NA NJIA ZA KUUKWEPA"
Post a Comment