Kwa jinsi suala la utekelezaji wa mipango na malengo tunayojiweka kila MWAKA MPYA linavyochukuliwa na baadhi ya watu kuwa gumu, imeonekana sasa na watu wengi kwamba ili mtu uweze kufanikisha malengo yako ya mwaka mpya basi ni sharti utumie Sayansi mithili ya ile itumikayo kurushia maroketi mwezini.
Lakini unaweza usiamini hata kidogo jinsi siri zenyewe za wale wanaotekeleza kirahisi malengo yao ya mwaka mpya zilivyokuwa ni vitu vya kawaida kabisa tena vilivyoko ndani ya uwezo wa kila mtu mwenye uwezo wa kufikiri. Leo hii katika makala hii nitakwenda kukushirikisha HATUA MUHIMU 3 ZA KUWEKA MALENGO pamoja na KANUNI KUU 10 ZA KUFUATA ili malengo na mipango yako ya mwaka mpya yaweze kutimia kwa urahisi zaidi.
SOMA: Mwaka 2020 ishi kama Tai,usikubali tena kuishi kama Kunguru
Unaweza kujiuliza kwani Mipango ndio nini na Malengo ni nini lakini wala usibabaike kwani vitu hivi, Mipango, Malengo, Maono, Dhamira, Ndoto, Mikakati, sijui Maazimio na hata Dhima, msingi wake mkubwa upo kwenye Juhudi za binadamu kusaka mafanikio hapa Duniani, ni nguzo kuu za mafanikio katika nyanja yeyote ile ya maisha ya mwanadamu.
Katika vitabu vyangu, MIFEREJI 7 YA PESA na kile cha MICHANGANUO YA BIASHARA & UJASIRIAMALI, maneno hayo ndiyo yaliyobeba maudhui makubwa ndani ya vitabu hivyo kwahiyo makala hii sehemu fulani nimeitoa katika vitabu hivi 2, na naamini waliowahi kuvisoma ni mashahidi.
SOMA: Heri ya Krismasi na Mwakampya wenye mafanikio tele, 2019 ishi kama Mbayuwayu
Kama ilivyokuwa ada, Jifunzeujasiriamali kila mwaka kipindi kama hiki ni lazima tutoe tathmini, mikakati na muelekeo wetu kwa mwaka mpya unaoenda kuanza Januari ikiwa ni pamoja na Kaulimbiu yetu ya Mwaka. 2021 Kaulimbiu yetu kuu itakuwa hivi;
2021
ASIKUTISHE MTU, AMUA HATMA YAKO, TENGENEZA MWAKA ULIOKUWA BORA ZAIDI KUSHINDA
MINGINE YOTE!
Kwa kimombo kidogo;
2021 DO NOT BE INTIMIDATED, DECIDE YOUR DESTINY AND CREATE YOUR BEST YEAR EVER!
Haijalishi ni miaka mingapi umekuwa ukiweka malengo ya mwaka mpya yakaishia hewani February na March, hata kama unakaribia miaka 70 bado unaweza ukatumia kanuni sahihi za uwekaji wa Malengo yako na hatimaye kufanikiwa.
Usimwangalie mtu yeyote aliyefanikiwa ukadhani wewe huwezi kufanikiwa kama yeye, hakutumia miujiza wala maji spesho ya baraka(upako), bali kanuni ni hizihizi ndio maana nakuambia kataa kabisa kutishika na maneno ya watu sijui, ….OOO….ulishindwa masika, kiangazi utaweza….? Umeshindwa na taa ya Mungu, utaweza kwa taa ya mzungu….? nk.
….na maneno chungu nzima kama hayo ya
kukukatishana tamaa.
SOMA: Ni robo ya mwaka sasa, bado upo kwenye mstari wa malengo uliyojiwekea January?
Kama una afya yako maridhawa, wewe piga mzigo tu ukitumia kanuni sahihi za uwekaji malengo nitakazokwenda kukupa pale chini mwishoni mwa makala hii, na nataka nikueleze, hii kasumba ya malengo ya mwaka mpya kuanzia leo usiitilie maanani sana kwani malengo unaweza ukayaweka siku, saa, mwezi au majira yeyote yale ya mwaka na wala si lazima iwe ni Januari tu.
Kwani Serikali na Mabunge yanavyoweka malengo yao June huwa hayatimiziki? Kwa taarifa yako Duniani kuna “Miaka Mipya” lukuki na wala yote haianzii Januari lakini ni Miaka mipya kulingana na tamaduni za wenye miaka hiyo, kuna mwaka mpya wa Kiislamu, Mwaka mpya wa Kichina, Kihindi, mwaka mpya wa Kiyahudi nk.
Yote hiyo ina miezi yake ya kuanza siyo Januari.
Januari haina rangi maalumu, jua hukuchwa na kuzama kama tu ilivyo kwa miezi mingine, haya ni mazoea tu tumejiwekea wanadamu, hivyo malengo yako unaweza hata kuyaanza Novemba hii hii, Desemba, Januari au hata Aprili ukipenda. Cha msingi tu ni kuzingatia hatua na kanuni nitakazokudondolea pale chini.
SOMA: Sababu kubwa ni kwanini mwaka 2017 sikufanikisha malengo yangu yote niliyojiwekea Januari
Nilitangulia kusema nitatoa muelekeo wetu wa
2021 kama blogu ya Jifunzeujasiriamali
na mitandao yake yote ya kijamii likiwamo Group la Masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE.
Tutaendelea kuweka makala kamili(nzima) za thamani katika blogu yetu bila malipo yeyote pamoja na Makala chache(NUSU) zenye mwendelezo wake kwenye Group la MICHANGANUO-ONLINE (hizi ni exclusive-hazipatikani kokote kwingine).
“Makala chache NUSU” huwa zinachochea wale wanaopenda kujifunza kwa kina zaidi masomo yetu kulipia gharama kidogo kwa mwaka (sh. Elfu 10 tu) kwakuwa ukitoa kila kitu bure si kila mtu atatilia maanani.
Tunafanya usajili mpya kwa washiriki wa group la 2021 kuanzia leo Alhamisi, 26/11/2020 na kwa wote watakaowahi nafasi kabla ya Alhamisi Desemba 10, 2020 (Wiki 2 tu tokea sasa) nitawatumia ile OFFA ya mwisho ya mwaka huu iliyomalizika wiki 2 zilizopita. OFFA hiyo ilikuwa na vitu vifuatavyo, lakini nimeongezea hapo Kitabu cha MIFEREJI 7 YA FEDHA.
Hii ni nafasi nyingine ya dhahabu kwa wale walionilalamikia kuwa OFFA ilichukua muda mfupi mno kumalizika (Kumbuka offa zetu hujirudia kwa nadra sana!). Group likiwahi kujaa(watu 250) na nafasi zitakuwa zimemalizika, tuna uwezo wa kuhudumia group moja tu kwa ufanisi, na hatutakuwa na magroup zaidi ya hili.
Kupata OFFA hii pamoja na nafasi ya kuungwa
group mwaka mzima wa 2021 lipia ADA
yako sh. Elfu 10 kwa kutumia namba zetu, 0765553030
au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma
ujumbe kwa watsap au sms kupitia 0765553030
usemao;
“NATAKA
OFFA YA MWISHO 2020 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO”
Muda huohuo nitakutumia offa zako na kukuunga kundini. Yale Masomo ya kipekee ya fedha na Ujasiriamali kila siku tayari yameshaanza katika group.
Kwa yeyote yule ambaye hatumii WHATSAPP hakuna shaka kwani kila kitu
natuma pia kwa njia ya EMAIL, nitumie anuani yako ya email kwa meseji ya
kawaida na kila kitu kitakuwa shwari.
OFFA
KUBWA YA MWISHO 2020 NI HII HAPA;
1.
KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
(New special edition 2021) –cha kiswahili
2.
KITABU
mashuhuri zaidi
duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio
kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA FEDHA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
Semina
nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili
5.
Kifurushi
cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-zote kwa kiswahili
6.
Mchanganuo
kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA
WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili
7.
Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa Kiswahili &
kiingereza
8.
Mchanganuo
kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks) -Kiswahili
9.
Mchanganuo
kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-Kiswahili
10. Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha
kwako binafsi na
kwabiashara yako-kwa kiswahili
11. Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha
kuandika michanganuo kwa muda mfupi. -
Kiswahili & kiingereza
12. Mchanganuo mfupi wa biashara
ya Steshenari (One page Business plan)
(NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
13. Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara
kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan
unaweza kuvifuatisha ukaandika.
14. Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2021
(MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu
michanganuo na ujasiramali kwa ujumla
OFFA
HII SI YA KILA MTU !
· Ikiwa wewe ni miongoni mwa wale wasioamini kama mipango mizuri na utekelezaji wake ndio kiini cha mafanikio katika biashara yeyote ile, basi usipoteze ada na muda wako bure kujiunga
· Ikiwa
tayari wewe ulishakuwa mwanafunzi wangu wa Michanganuo, ni hiyari yako kujiunga
tena kwa ajili ya baadhi ya mambo mapya hasa hasa masomo ya fedha na
Michanganuo mipya, vinginevyo unaweza kuhisi tunarudia baadhi ya mada hasahasa
zile courses na semina za jinsi ya kuandaa michanganuo.
Nisiendelee kukuchosha, hebu sasa turudi kwenye mada yetu kuu, ni sanaa gani inayotumika na wale wanaofanikisha malengo yao ya mwaka mpya?
Sababu kubwa inayowafanya watu kushindwa
kuendelea kutimiza malengo yao ya mwaka mpya muda mfupi tu baada ya kuyaweka
haitokani na ugumu au ukubwa wa malengo yenyewe bali hutokana zaidi na
kutokuzingatia kanuni au taratibu za uwekaji wa malengo hayo.
SOMA: Jinsi unavyozuia mafanikio makubwa maishani kwa kuhangaika na vitu vidogovidogo
HATUA
KUU 3 UNAPOTAKA KUWEKA LENGO LOLOTE MAISHANI:
1. Hatua ya kwanza kabisa, tengeneza akilini mwako picha kubwa ya lengo lako kuu unalotaka kulifikia na uanze kulifikiria
2. Hatua ya pili, tengeneza mpango wa utekelezaji kwa kulivunjavunja lengo lako kubwa katika malengo madogomadogo mfano lengo la miaka 10, weka malengo ya miaka 5, Mwaka 1, miezi 6 hadi vitu utakavyovifanya kila siku kwa ajili ya kufikia lengo lako kuu. Kinachokatisha watu tamaa ni kule kutaka kulifikia lengo kuu haraka jambo ambalo haliwezekani, badala yake inashauriwa kufikia sehemu ndogondogo kwanza za lengo ambazo baada ya muda huungana na kukamilisha lengo zima. Hii itakupa hamasa muda wote na hautaishia tena njiani Machi na Aprili
3.
Hatua
ya tatu: baada ya kuwa na mpango sasa anza kuufanyia kazi ili
kulifikia lengo lako kuu huku ukidumu katika malengo uliyojiweka
MFANO:
Nitakupa mfano mmoja, tuseme mwaka 2020 umejiwekea lengo lako kubwa la kuwa Mheshimiwa mbunge wa jimbo fulani unakotokea ifikapo uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025. Tayari hapa utakuwa umeshavuka hatua ya kwanza ya kuweka lengo lako kubwa la miaka 5.
Hatua ya pili sasa hebu tuone jinsi utakavyolivunjavunja lengo lako hili kubwa la kuwa mbunge 2025 katika malengo madogomadogo ambayo yatakuwa rahisi kwako kutimiza bila ya kukuchosha. Unaweza` kuamua kama ifuatavyo;
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi
Lengo la Miaka 3 ya mwazo: Kujiboresha kielimu
Kujiunga chuo au masomo huria ili kukamilisha hitaji la angalao kuwa na shahada ya kwanza katika fani uliyosomea na wakati huohuo ukijinoa katika midahalo mbalimbali ya chuo na ile ya kijamii ili kuhakikisha unakuwa mzungumzaji mzuri.
Lengo
la mwaka mmoja (1):
Kujitolea katika nafasi mbalimbali za kiuongozi chuoni au kwenye jamii
SOMA: Je, wajua siri ngingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
Lengo
la miezi 6:
Kuandaa mkutano au kongamano la vijana na
kumualika mbunge wenu wa sasa jimboni kwa ajili ya kuzungumza naye masuala
mbalimbali yanayohusu maendeleo ya jimbo lenu
Lengo la mwezi mmoja 1:
Kuandika makala zenye maudhui ya kimaendeleo
katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii
SOMA: Jinsi ya kufanikiwa kufikia malengo katika uwekezaji wowote utakaoufanya
Lengo la siku:
Kujifunza bila ya kuchoka masuala mbalimbali
ya maendeleo na kiuongozi kupitia vitabu na vyombo vingine vya upashanaji
habari
KANUNI
MUHIMU ZA KUFUATA ILI KUTIMIZA MALENGO YAKO KWA URAHISI
1. Weka malengo makubwa na yanayosisimua kwani malengo madogo kila mtu anayaweza(think Big)
2. Malengo
unayoweka ni lazima yawe na sifa kuu 5 zifuatazo;
· Yawe
wazi na yanayoeleweka vizuri
· Yanayopimika
· Yanayotekelezeka
· Yanayofaa
na kuendana na mazingira yako mwenyewe
· Yenye
muda maalumu wa utekelezaji
3. Andika
malengo yako na ikiwezekana yabandike mahali pa wazi unapoweza kuyasoma kila
siku.
4. Elezea
malengo yako kwa lugha chanya mfano, “Naacha sigara kuboresha zaidi afya yangu”
badala ya kusema, “Naacha sigara
nisipate kansa, neno kansa lina mlengo hasi na ukakasi unaoweza kukufanya
uchukie hata na mikakati yenyewe ya kuachana na sigara.
5. Yaeleze
kwa wakati uliopo sasa, mfano usiseme, “Nitaacha kuvuta sigara, sema, “Sasa
hivi naacha kuvuta sigara”
6. Weka
vipaumbele: mfano ukiwa na malengo mengi yapange kufuatana na umuhimu ukianza na
yale muhimu zaidi. Hii itakusaidia kuelekeza nguvu zako nyingi kwanza kwa yale
malengo yaliyo na umuhimu kwako.
7. Lengo
kubwa livunje katika malengo madogomadogo
8. Usijaribu
kuweka malengo yasiyotekelezeka mfano mtu binafsi kuruka kuelekea sayari
nyingine, kuota mabawa kama ndege, kuzunguka dunia kwa miguu nk.
9. Malengo
yako yazingatie zaidi utekelezaji wake na wala siyo matokeo. Kwa bahati mbaya
utakaposhindwa kutekeleza malengo yako kutokana na sababu zilizoko nje ya uwezo
wako mfano kuugua, majanga ya sili, sera za serikali nk. haupaswi kujilaumu
kwamba umefanya uzembe ingawa hili linaweza kukuhuzunisha.
10. Hakikisha
unadumu na malengo uliyojiwekea bila kukata tamaa kirahisi mpaka yanatimia (Don’t Give up)
Nikukaribishe
sana 2021 hii, ili uweze kuwa huru kuamua mustakabali wa maisha yako mwenyewe
bila ya kuingiliwa na mtu yeyote, na hatimaye uweze kutengeneza mwaka bora
zaidi kushinda miaka mingine yote iliyopita !
PETER AUGUSTINO TARIMO
Mwandishi na Mhamasishaji wako.
0 Response to "2021 AMUA HATMA YAKO, TENGENEZA MWAKA ULIOKUWA BORA ZAIDI KUSHINDA MINGINE YOTE!"
Post a Comment