Bila ya kupoteza wakati hebu tuanze na swali lenyewe, na mimi naliweka hapo chini kama alivyouliza kupitia watsap bila ya kuongeza wala kupunguza chochote;
Habari yako ndugu Tarimo,
ni namna gani rahisi, nzuri ya kujua faida ya biashara ya duka kwa siku??
Je
nipo sahihi.?
Nilipoanza kununua bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kufungua duka, niliorodhesha bidhaa zote bei ya kununulia na bei ya kuuzia, mwishoni nikapata jumla kuu na kuchukua jumla ya kuuzia nikatoa na jumla ya kununulia, hiyo tofauti niliyoipata nikaiita faida ghafi.
Sasa hiyo faida ghafi nikagawanya na ile jumla ya kununulia, hapo nikapata asilimia ya ile faida ghafi kama 33%, sasa hapo nikasema asilimia 14% ni gharama za kila siku za duka na asilimia 19% ni faida baada ya matumizi (net profit)
Sasa
kila siku wakat wa kufunga duka ninachukua mauzo ya siku husika ninazidisha na
ile 33% hapo napata fedha kama faida ,alaf natafuta tena 14% hiyo nasema ni
gharama na asilimia 19% ndio faida yangu ambayo itanisaidia kupata mlo wa
familia kwa kesho yake.
Je
nipo sahihi?
MAJIBU:
Ingawa katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA tumeweka njia sahihi zaidi ya kujua faida unayopata katika duka larejareja kila siku lakini kwa ujumla njia yako ya kujua faida halisi ya duka unayoipata kwa siku ipo sahihi kiasi fulani isipokuwa tu kuna baadhi ya sehemu ambazo ningependa kushauri ufanye marekebisho kidogo;
Vilevile pia njia ya kutumia asilimia ya mauzo ni ya makadirio zaidi hivyo faida utakayokuwa ukikata inaweza isiwe sahihi kwa asilimia 100% ingawa itakaribiana sana au kupungua kidogo kutokana na sababu kwamba umetumia asilimia ya mauzo jambo ambalo siyo kila siku utakuwa ukiuza bidhaa zenye kiwango cha faida kinachofanana kwa asilimia 100%. Kuna njia sahihi zaidi unayoweza kutumia.
SOMA: Aina za bidhaa za duka zenye faida ndogo lakini hutoka harakaharaka
Kumbuka pia kwamba unapokadiria faida ghafi ni asilimia 33% ya mauzo yote, zipo siku nyingine utauza bidhaa zenye faida ghafi kidogo zaidi na kuna siku pia utauza bidhaa nyingi zilizo na faida ghafi iliyo juu kidogo ya wastani uliokadiria wa 33%.
Hata hivyo pamoja na
kasoro hiyo ndogo bado wastani huo hautapishana sana na hali halisi iwapo mtu
utaamua kuitumia kwani bidhaa za duka la rejareja nyingi huwa asilimia ya faida
inalingana au kukaribiana sana.
Marekebisho ninayopendekeza katika njia yako
hii ni haya hapa chini:
Kwa kawaida vipengele
vya Hesabu za Faida na Hasara, ukiacha MAUZO,
vitu vingine vyote huwa chini yake kuanzia faida ghafi mpaka faida halisi.
Kwahiyo vitu hivyo vingine mara nyingi huwa vinatafutiwa asilimia zake katika Mauzo na siyo katika bei ya kununulia (gharama ya mauzo) kama wewe
ulivyofanya kwenye mfano wako pale juu (ingawa unaweza kufanya hivyo pia). Kwahiyo pale uliposema hivi;
“Sasa hiyo faida ghafi nikagawanya na ile
jumla ya kununulia, hapo nikapata asilimia ya ile faida ghafi kama 33% “
Kwa mujibu wa kanuni yako asilimia 33 ijapokuwa ni faida ghafi lakini imeelezewa katika gharama za mauzo (Mark up percenage %) na siyo mauzo (gross profit margin %), siyo vibaya lakini mpaka hapo. Unaponunua bidhaa na kuja kuiuza huwa kunakuwa na ongezeko la thamani / faida ghafi. Faida ghafi hii au kwa kimombo "Mark up" unaweza ukaielezea katika Asilimia ya mauzo au katika Asilimia ya Gharama za mauzo. Wewe hapa uliielezea katika asilimia ya gharama za mauzo ndipo ukapata asilimia 33%
….Siwezi kusema hukuwa sahihi lakini mara nyingi zaidi huwa yanatumika mauzo kutafuta asilimia ya faida ghafi, badala yake nafikiri ungegawa faida ghafi uliyoipata kwa jumla ya bei ya kuuzia na kuzidisha mara 100, ili kupata asilimia 33% au yeyote nyingine kulingana na kiasi chako cha mauzo.
Nasema hivyo kwa sababu sisi hapa katika mfano wetu tunadili zaidi na matokeo ya mwisho ambayo ni faida halisi kuliko faida ghafi pekee ndiyo maana ni lazima tuhusishe faida ghafi na mauzo. Kwahiyo ni sahihi zaidi tutumie asilimia ya faida ghafi kwa mauzo na siyo kwa gharama za mauzo kama ulivyofanya wewe.
JINSI SASA YA KUJUA FAIDA YA DUKA LA REJAREJA KILA SIKU JIONI
UNAPOFUNGA HESABU ZAKO
Sasa ukitaka kujua kwa siku umepata faida kiasi gani, tafuta kwanza faida ghafi kama ulivyoeleza pale mwanzoni kwamba;
"Nilipoanza kununua bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kufungua duka, niliorodhesha bidhaa zote bei ya kununulia na bei ya kuuzia, mwishoni nikapata jumla kuu na kuchukua jumla ya kuuzia nikatoa na jumla ya kununulia, hiyo tofauti niliyoipata nikaiita faida ghafi"
Kisha tena hiyo faida ghafi toa gharama zote za kudumu za uendeshaji mfano pango, umeme, ushuru wa taka na mshahara (gharama hizi za kudumu kwa siku itakubidi uchukue za mwezi ugawe kwa siku 30) ambapo sasa utapata faida halisi kwa siku. Hiyo faida halisi tena itafutie asilimia yake katika mauzo kwa kuigawa kwa jumla ya bei ya kuuzia.
Asilimia utakayoipata sasa ndiyo unayoweza kuitumia kila siku kama kanuni yako ya kutafutia kiasi cha faida unayopata kwa siku na ndiyo pia unayoweza kuichanganua kwa usahihi kama wewe mwenyewe ulivyoelezea kwa mujibu wa maelezo yako ya asilimia 14% na 19% hapo chini. Kwa kuwa hapa tayari tumeshatoa gharama za uendeshaji za kudumu za mwezi, huna teana haja na ile asilimia 14% utadili na asilimia 19% ambayo ndiyo faida yako halisi
SOMA: Hatua kumi (10) za kuanzisha biashara ya rejareja - DUKA
Tuna "assume" sasa asilimia ya faida halisi yako uliyopata ni 19% kama ulivyosema.
Asilimia 14% ya gharama za kudumu za uendeshaji mfano kodi ya pango, umeme na ushuru wa taka, ambazo hazitegemei kama umeuza au haujauza ukijumlisha na asilimia 19% ya faida halisi ndipo unapata faida ghafi. Hapo ulikuwa sahihi ingawa “fiqure” zako zaweza kuwa tofauti ikiwa utagawa faida kwa bei ya mauzo na wala si bei ya manunuzi (gharama za mauzo).
Pia hii asilimia 19%(Faida halisi) uliyodai ni kwa ajili ya mlo wa kila siku wa familia, mimi ningeshauri pia kwa ajili ya uendelevu wa duka lako basi usiimalizie kwenye mlo bali tenga tena hapo kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kuongezea mtaji wako wa duka, ili nalo liweze kukua vinginevyo itafika siku litazidiwa na kuzorota au hata kufa kabisa.
SOMA: Puuza Imani na dhana hizi potofu ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula
Kwa ufafanuzi zaidi wa hesabu ya faida na hasara pamoja na kanuni rahisi zaidi ya hii ya kujua faida kamili ya duka lako kila siku jioni unapofunga mahesabu yako, soma katika kitabu changu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA Toleo jipya la mwaka 2024 kwenye sura inayohusiana na Usimamizi na Hesabu za duka la rejareja hasa kurasa za 82 – 83 pamoja na uk. 92
Mbali na kujibu changamoto mbalimbali kubwa za biashara ya duka la rejareja na biashara nyingine zote za rejareja lakini pia kitabu hiki kina mifano ya vitabu au madaftari ya hesabu zote muhimu za biashara hii za siku na za mwezi kama vile, Mfano wa daftari la mauzo, mfano wa daftari la manunuzi ya bidhaa la kila siku, mfano wa daftari la gharama za kudumu, mfano wa daftari la wakopaji (wadaiwa), mfano wa daftari la wadai, mfano wa daftari la fedha taslimu, mfano wa daftari la mali za kudumu nk.
Tumeshauri pia mifumo ya kihasibu inayofaa na kutumiwa zaidi na watu hapa Tanzania kwa ajili ya kurahisisha na kutunza hesabu katika biashara za rejareja hususani maduka.
SOMA: Jinsi ya kusimamia hesabu katika biashara ndogo unayomwachia mfanyakazi
Tumeangazia pia kwa kina sana changamoto sugu ya namna ya kupata mtaji wa kuanzisha duka la rejareja pamoja na mfano halisi katika picha za rangi na maandishi jinsi mwandishi wa kitabu hiki alivyoweza kuvuka kihunzi kigumu mno cha kupata mtaji wa biashara yake ya kwanza kabisa ya rejareja akianzia na sifuri kabisa mitaa ya msimbazi Kariakoo mpaka kumiliki duka lililotoa ajira kwa watu wengine wawili.
Upekee wa kitabu hiki ni lugha rahisi iliyotumika inayoweza kueleweka kwa mtu yeyote yule hata asiyewahi kusomea mahesabu ya biashara. Katika toleo la 2024 tumeongeza sura inayohusu matumizi ya Akili bandia (Artificial Intelligence AI)
JINSI YA KUPATA NAKALA YA KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA KWA NJIA YA MTANDAO (NAKALA-TETE) ;
Lipia sh. elfu 6, (6,000/=) kwa Tigo-pesa au M-pesa na namba zetu ni, 0712202244 au 0765553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha nitakutumia kitabu kupitia simu yako ya mkononi au kompyuta ndani ya dakika 3 mpaka 5 tu
Vile vile unaweza kukinunua moja kwa moja kutoka katika mtandao wa GETVALUE kwa shilingi elfu 10 kupitia smartphone yako, bonyeza maandishi haya GETVALUE kuingia ukurasa wa kitabu moja kwa moja.
0 Response to "JINSI YA KUJUA FAIDA YA DUKA LA REJAREJA KILA SIKU JIONI UNAPOFUNGA HESABU"
Post a Comment