Mazingira ya biashara ni nini?
Mazingira ya biashara ni jumla ya nguvu
mbalimbali zinazobadilika muda wote kutoka ndani au nje ya biashara zinazoweza
kuiathiri biashara ikashamiri au kudumaa.
Mazingira
ya biashara ya ndani (Internal business environment)
Mazingira ya ndani ya biashara hujumuisha nguvu au mambo yote yanayohusisha maamuzi ya kila siku ya biashara na ambayo mmiliki au meneja wa biashara anao uwezo wa kuyathibiti kwa mfano;
· Bidhaa
· Wateja
· Mmiliki
wa biashara
· Uongozi
· Mtaji
· Wasambazaji
bidhaa(suppliers)
· Ugavi
na mahitaji na
· Vyombo
vya habari
Mazingira yote haya ya ndani ya biashara
yanaweza yakathibitiwa na biashara au mmiliki
2.
Mazingira ya nje ya Biashara (External business environment)
Hizi ni nguvu au mambo ambayo yapo nje ya biashara na huwa hayawezi kuthibitiwa na uongozi wa biashara kirahisi. Kitu pekee uongozi au mmiliki wa biashara unachoweza kukifanya ni kujibadilisha wewe mwenyewe na biashara yako ili kuweza kuendana na mazingira hayo jinsi yanavyotaka huku ukitumia fursa zozote zile zinazoweza kuwepo katika mazingira hayo kwa faida ya biashara yako. Mazingira ya nje ni kama vile mazingira ya;
· Kiuchumi
· Kisiasa
na kisheria
· Kijamii
· Ushindani
· Majanga
ya asili
· Kiteknolojia
· Kidemografia(kitakwimu)
MAELEZO YAFUATAYO YENYE RANGI YA BLUU
HAYAKUWA SEHEMU YA MAKALA HII TANGU AWALI NILIPOKUWA NAANDIKA HII MAKALA,
NIMEYAONGEZEA LEO HII BAADA YA TATIZO LA KUTOFANYA KAZI VIZURI KWA MITANDAO YA
KIJAMII KUMALIZIKA
Wakati naandika makala hii siku ya tarehe 1 NOVEMBA 2020 nilipanga kuwa ndio iwe siku ya kuipost katika blog hii lakini ilishindikana kutokana na mtandao wa intaneti kutokufanya kazi vizuri, ilinibidi tu kuituma kwenye listi yangu ya email ya watu ninaowatumia masomo kwani ni email peke yake iliyokuwa inafanya kazi tena kwa kusuasua na kwa bahati nzuri email hiyo ilikuwa tayari nimeshaingia “sign in” kabla ya tatizo la mtandao kuanza. Tatizo hili lilikuwa ni mfano dhahiri wa mazingira ya nje ya biashara (External business environment) niliyoyataja hapo juu katika makala ya awali hasa mazingira yale ya kiteknolojia kwani kama tulivyoshuhudia hakukuwa na mtu hata mmoja aliyeweza kubadilisha kitu kwenye tatizo hili zaidi ya kusubiria tu ni lini mitandao ya kijamii itafanya kazi vizuri.
Katika makala hii ya leo ingawa nimeyataja mazingira ya aina zote mbili, ya nje na ya ndani, lakini lengo langu kubwa lilikuwa ni mazingira ya nje ya biashara hasa hasa katika kipengele cha mazingira ya Kisiasa na kisheria.
SOMA: NUFUVI(SWOT ANALYSIS) Tathmini muhimu kabla hujaanza kuandika mchanganuo wa biashara yako
Bila shaka sote tunakumbuka kipindi cha miaka
mitano iliyopita jinsi tulivyoshuhudia mabadiliko makubwa na ya haraka katika
mazingira mazima ya kisiasa na kisheria ya biashara. Mabadiliko hayo ya kisiasa
na kisheria yaliathiri karibu kila biashara iwe ni katika muelekeo chanya ama
muelekeo hasi kulingana na vile wamiliki wa biashara hizo walivyoweza
kujibadilisha ili kuendana na mazingira hayo ama kinyume chake na hivyo
kusababisha kudorora au kushamiri kwa biashara zao.
Kubadilika kwa mazingira ya kisiasa na
kisheria kulileta pia mabadiliko katika sera mbalimbali za kiuchumi za serikali
ambazo zimesababisha kuwepo kwa fursa mbalimbali lakini pia Vikwazo/hatari
mbalimbali. Kwa mfano sera ya serikali kuhimiza wafanyabiashara kulipa kodi
halali kwa kiasi fulani imesababisha wale waliokuwa wakikwepa kodi kuwa na
wakati mgumu wakati huohuo ikiwa ni fursa kwa wale waaminifu wanaolipa kodi zao
kihalali kwani ushindani umepungua wa wale waliokuwa wakiibia serikali mapato.
Mfano mwingine wa mabadiliko ya mazingira ya
biashara kisiasa na kisheria tunaweza kuuona katika suala zima la usajili wa
biashara Tanzania, mnamo mwaka 2018 serikali ilianzisha utaratibu mpya wa
kusajili biashara Mtandaoni kwa mfumo uitwao, Online Registration System(ORS),
mfumo huu ulitamatisha ule wa zamani ambao mtu alitakiwa kwenda hadi ofisi za
Brela akiwa na makaratasi yake mkononi.
SOMA: Fursa za mafanikio kamwe hazitakaa ziishe lakini pia hazichumwi mtini kama embe
Moja ya fursa kubwa mfumo huu uliokuja nayo
kwa wamiliki wa biashara ni urahisi wa kusajili biashara zao na kufanya
marekebisho ya nyaraka za usajili hata baada ya usajili wenyewe. Mtu hata uwe
kule Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Kagera nk. Unao uwezo wa kufanya usajili wa
biashara yako ilimradi tu uwe na kompyuta na mtandao wa intaneti
Lakini pia kuna vikwazo ama ugumu mabadiliko
ya mazingira haya kisheria yaliyokuja nao, moja ni kwamba Mfumo wa ORS unamtaka
kila anayetaka kusajili biashara/kampuni au kufanya marekebisho baada ya
kusajili basi awe na namba ya Utambulisho wa Utaifa NIN wakiwemo pia wale
wanahisa wote wa kampuni. Jambo hili limesababisha kutokuwepo tena na fursa ya
mtu kumsajili mwanaye au ndugu yeyote wa karibu mwenye umri chini ya miaka 18.
SOMA:Hatua zipi nifuate kuanzisha kampuni na ni jinsi gani ya kuiendesha?
Zamani mtu uliweza kuunda kampuni hata na
mwanao wa miaka 2 mkiwa kama wakurugenzi. Aidha mfumo huu pia umeziba fursa ya
mtu yeyote yule mgeni asiye Mtanzania kusajili jina la biashara au Ubia kwani
kigezo cha kusajili majina ya biashara na ubia mtu ni lazima awe na namba ya
kitambulisho cha Taifa NIN kitu ambacho wageni hawawezi kuwa nacho.
Mabadiliko mengine ni katika sera na taratibu
za serikali kwenye sekta ya fedha, kwa mfano hapo zamani kabla ya mabadiliko
hayo yaliyokuja kipindi cha awamu ya tano ya serikali, wajasiriamali wengi na
wafanyabiashara walikuwa na fursa pana ya kuchukua mikopo wapendavyo.
Mtu mmoja aliweza kuomba mikopo hata kutoka
taasisi tofauti zaidi ya nne bila ya kujulikana
wala kufuatiliwa na mtu yeyote yule lakini sasa hivi serikali kupitia
Benki kuu imeanzisha utaratibu wa Taasisi za kifedha hasa Mabenki kuwasilisha
taarifa za wakopaji wote kusudi taasisi hizo kabla ya kumkopesha mtu kuchunguza
kwanza historia yake ya ukopaji kama ni nzuri au mbaya. Utaratibu huu kwa kiasi
Fulani umepunguza mzunguko wa fedha kwani umeminya fursa iliyokuwepo ya watu
wasiokuwa waaminifu kupata mikopo kirahisi.
Mabadiliko hayo ya sera na taratibu za
serikali kwenye sekta ya fedha pia yalisababisha taasisi mbalimbali za kifedha
zilizokuwa zinafanya vizuri hapo kabla kushindwa kumudu mazingira ya biashara
na hata nyingine kufikia hatua ya kufilisika na kufunga shughuli zao, kulikuwa
na taasisi mfano, PRIDE Tanzania na nyinginezo ambazo zilikuwa chanzo kizuri
sana cha mitaji kwa wajasiriamali wadogo kwa masharti nafuu lakini mabadiliko
hayo na wamiliki wake pengine kushindwa kwenda sambamba nayo hayakuziacha
salama hata kidogo
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake, nkoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima
Kwa ujumla kuna mambo mengi sana kutokana na
mabadiliko ya Kisiasa na kisheria yameziathiri sana biashara iwe ni katika
mlengo chanya au mlengo hasi lakini cha msingi zaidi hapa ni Je, mjasiriamali
ni kwa namna gani unazitumia fursa zinazotokana na mabadiliko hayo na kukwepa
au kupunguza hatari zilizopo?.
Ingawa hatuna uwezo kabisa wa kuzuia sera na
kanuni za serikali lakini tunaweza kutumia kila fursa zitokanazo na sera hizo
kuhakikisha biashara zetu zinashamiri na siyo kufa. Badala ya kufunga maduka
kwa kuhofia kudaiwa kodi na leseni za biashara, tujifunze namna ya kuweka
kumbukumbu za biashara zetu vizuri kusudi serikali iweze kukata kodi yake
halali na sisi tubakie na faida tunayostahili kuipata.
SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza corona Tanzania kuubusti uchumi wako unaosambaratika
Watanzania ndani ya miaka 5 iliyopita
tumejifunza kwamba serikali hii haipendi wala kuvumilia vitendo vya mkato mkato,
kwa hiyo katika awamu hii nyingine inayoanza sasa hivi ni lazima tukitaka
biashara zetu kushamiri basi tuhakikishe tunafanya mambo yetu pasipo kuwa na
kona kona kwani hakuna namna tunaweza kubadilisha sera na misimamo ya serikali.
Serikali inapoweka sheria hizo si kwa lengo la kuwakomoa wananchi wake hapana
bali lengo lake ni kuhakikisha kunakuwa na utawala wa sheria unaomlinda kila
mtu na kwa maslahi ya kila mwanachi.
Serikali ikikubali mambo yajiendee kama kila
mtu ambavyo angependa yajiendee matokeo yake ni kuvurugika kwa kila mfumo
katika jamii na matokeo yake ni kuwa na Taifa lisilojali taratibu na sheria,
jambo ambalo linaweza kuibua madhara makubwa mwisho wa siku. Kila mtu ataamua
kujifanyia anavyotaka na mwishowe hata kila mtu kuamua kujianzishia ‘kataifa’
kake ndani ya Taifa. Kwa mantiki hiyo nchi haitakuwa tofauti na Mataifa mengine
yaliyofeli kama vile Somalia, Afghanistan, Libya na Syria.
SOMA: Kati ya Obama na Putin ni nani aliyeisaidia IS
Marekani Taifa linaloongoza kwa wananchi wake kuishi maisha
ya viwango vya hali ya juu zaidi pia ndio Taifa linaloongoza duniani kwa
kuzingatia sheria na taratibu za kibiashara. Ingawa kuna nchi nyingine za Ulaya
kama vile Uswizi, Ujerumani, Norway, Sweden na nyinginezo
zinazosemekana wananchi wake wanaishi maisha bora zaidi kwa kupata vipato
vikubwa kupita Wamarekani lakini ni ukweli usiopingika kuwa katika nchi hizo
bei za bidhaa na huduma mbalimbali zipo juu mno kushinda zile za Marekani na
matokeo yake ukiwa na dola moja ya Kimarekani Uswizi utanunua vitu vichache
zaidi kuliko utakavyonunua nayo ukiwa Marekani kwenyewe.
Wamarekani ndio watu wa kwanza duniani kuhakikisha maadili ya
biashara na Ujasiriamali yanapewa uzito unaostahili na kwa Wamarekani Biashara
ndiyo kigezo kikubwa kinachoamua ubora wa maisha ya watu kwa kutengeneza ajira,
bidhaa mbalimbali na huduma katika jamii.
SOMA: Rais Obama: Kila mtu duniani anatakiwa apewe nafasi nyingine ya kurekebisha maisha yake
Ubora wa maisha kwa ujumla unahusiana na furaha ya mwanadamu
katika vitu kama vile, viwango vya elimu, makadirio ya umri wa mtu wa kuishi,
afya, usafi na muda wa burudani. Hivyo ili kujenga maisha yenye ubora wa hali
ya juu ni lazima kuwe na juhudi za pamoja za Wananchi wenyewe, Serikali,
Mashirika mbalimbali na wadau wengine wa nje.
Kama kinavyoelezea vizuri kabisa kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI toleo jipya maalumu la mwaka 2021, biashara ndio kila kitu. Uwe umeajiriwa ama huna ajira. Ikiwa umeajiriwa kuna siku tu utajikuta unafikiria kufanya biashara kwa namna moja ama nyingine na hivyo utahitaji maarifa ya kufanya biashara kama siyo leo basi kesho.
SOMA; Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?
Hebu fikiria baada ya kustaafu kwa mfano, utaniambia.. oo, mimi
bwana nitakuwa nimeshawekeza kwenye majumba na viwanja kwahiyo biashara
hainihusu kabisa, lakini kumbuka kuwa pia hizo ni aina ya biashara (Real
estate business) tena ni aina ya biashara zinazohitaji mtu uwe na
weledi mkubwa nazo, tazama mtu kama Donald Trump, hizi ndio biashara
zilizomjengea heshima kubwa hata akaukwaa urais wa Marekani.
Katika toleo hili la kitabu cha Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali, mbali na mada zote zilizokuwepo katika toleo lililopita vitu vya
kipekee vilivyoongezwa ni hivi vifutavyo;
1.
JINSI YA KUANDIKA MPANGO RAHISI WA BIASHARA YAKO KWA MUDA MFUPI (Ndani ya nusu saa tu)
Suala la kuandika mpango wa biashara au
kutokuandika limekuwa na mjadala mwingi, wajasiriamali wengi hasa wale wadogo
ikiwawia vigumu kuandaa michanganuo ya biashara zao kwenye karatasi.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako
Kwa kuwa haiwezekani mtu yeyote yule chini ya
jua kuanzisha biashara bila ya kuwa na mpango wa biashara, wanachofanya
wajasiriamali wengi ni kuweka mipango ya biashara zao vichwani hata pasipo wao
wenyewe kujua wanafanya hivyo. Kupanga mpango wa biashara kichwani na
kuuhifadhi akilini ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa siku zote tokea enzi na
enzi, siyo jambo baya kupanga kichwani lakini katika mazingira ya sasa na hasa
biashara inapokuwa kubwa mahitaji ya kuandika mpango katika karatasi yanakuwa
makubwa zaidi.
Hata hivyo kwa mjasiriamali mdogo mdogo
kuanza kuandika mchanganuo katika karatasi ni kama vile kupoteza muda wake
ambao ni heri angeliutumia kuendesha biashara yake akapata faida chapchap. Kwa
kulizingatia hilo, katika toleo hili maalumu la 2021 tumeongeza mada mahsusi
inayoelezea namna mjasiriamali mdogo anavyoweza akayaweka mawazo yake yote ya
biashara kwenye ukurasa mmoja tu wa karatasi kwa muda mfupi ajabu! Haichukui
zaidi ya nusu saa kukamilisha zoezi hilo.
Njia hii inampa mjasiriamali faida zote za
kuandika mpango wa biashara hasa umakini(Focus)
wakati huohuo ikimpa muda mwingi zaidi wa kuihudumia biashara yake changa
inayohitaji zaidi rasilimali ya muda kama mtaji pekee. Kumbuka mjasiriamali
mdogo mtaji wa pesa kwake ni kitu adimu mno hivyo ni lazima ajitahidi kuzitumia
ipasavyo rasilimali zingine rahisi kupatikana alizokuwa nazo hasahasa MUDA.
Maelezo hayo pamoja na mfano mzima wa mpango
huo mfupi yamechukua takriban kurasa 8 kuanzia ukurasa wa 343 – 352 ikiwemo pia
nukuu moja ya maneno yenye busara ambayo,
acha kusoma kila kitu kinachohusiana na
mpango wa biashara kwenye kitabu hiki lakini siyo hii nukuu ya busara yenye aya
mbili tu iliyopo uk. Wa 352.
2. JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI/BIASHARA KWA
KUTUMIA NJIA MPYA YA KISASA MTANDAONI (ORS)
Tangu mfumo huu uanzishwe rasmi na serikali
chini ya Mamlaka ya leseni na usajili wa biashara BRELA mnamo hapo tarehe1
February 2018 bado kuna watu wengi wameendelea kupata changamoto mbalimbali kwa
kutokujua tu vizuri jinsi ya kufanya usajili huo mtandaoni.
SOMA: Kuanzisha kiwanda rahisi cha juisi ya matunda, Tanzania ya viwanda yaja jiandae
Ingawa kuna watu mbalimbali na taasisi
wanaotoa huduma hiyo kwa malipo lakini ikumbukwe pia kwamba kuna wajasiriamali
wadogo ambao bajeti zao ni finyu, wana ada tu ya kulipia usajili Brela lakini
hawana uwezo wa kupata ada ya kulipia huduma hiyo kwa “mawakala” au wawakilishi.
Katika maelezo yangu haya mbali na kuelezea
Utaratibu wote kama ulivyo kwa lugha rahisi pia tumejaribu kutaja changamoto
mbalimbali wanazokutana nazo wajasiriamali wanaotaka kusajili biashara zao iwe
ni majina au Kampuni kwa mfumo mpya na jinsi ya kuzitatua wenyewe bila ya
msaada wa mshauri au mwakilishi yeyote.
SOMA: Jinsi ya kuuza wazo lako la biashara au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine
Brela wenyewe wamejitahidi kuhakikisha
taarifa zote za namna ya kusajili biashara zipo katika mtandao wao wa
https://www.brela.go.tz/ lakini katika maelezo yetu haya kuna vitu vingine vingi
ambayo aidha brela hawakuvifafanua kwa kirefu au hawakuviweka kabisa. Sisi siyo
mawakala wa Brela isipokuwa kazi yetu ni kuhakikisha msomaji anapata taarifa
kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi.
Maelezo yetu haya ya kipekee usiyoweza
kuyapata mahali kwingine kokote yanalenga hasa kumsaidia mjasiriamali asiyekuwa
na bajeti ya kutosha ya kumlipa mshauri kumsaidia katika mchakato huu, kwa
walio na bajeti zao napendekeza maelezo haya hayawahusu kwani kumlipa mshauri
ni njia fupi na ya haraka zaidi.
Aidha pia maelezo haya yamelenga kuwasaidia
wale wajasiriamali ambao mchakato wa kufanya jambo lao muhimu kama hili la kusajili biashara zao za kwanza
kabisa, kama tu lilivyokuwa tukio la kuoa mke, mume au kupata mchumba linakuwa
ni la kwao binafsi pasipo kuwashirikisha watu wengine wa pembeni. Maelezo ya
mchakato mzima pamoja na mawaidha mbalimbali yamechukua takriban kurasa 7
yameanzia ukurasa wa 354 – 362.
Ikiwa unayo shauku ya kujua vyema jinsi ya
kusajili biashara yako kwa njia ya kisasa mtandaoni ORS basi unaweza kujipatia
nakala yako ya kitabu hiki na moja kwa moja ukafungua ukurasa huo uliotajwa tu
hata kama huna shida na mambo mengine yaliyoko ndani ya kitabu. Maelezo ni
mafupi na yaliyolenga zaidi utatuzi wa changamoto zile zinazowasumbua zaidi
wajasiriamali katika mchakato huu wa kusajili kampuni na majina ya biashara
mtandaoni.
Toleo hili jipya maalumu (New Special Edition)
ingawa litatoka rasmi hapo January 2021 lakini kwa sasa hivi lipo tayari na kwa
wale wateja watakaowahi kabla ya muda huo wataweza kukipata kwa njia ya nakala
tete(Softcopy).
Tumetoa pia OFFA ya wiki moja kuanzia leo Jumapili tarehe 1/11/2020 mpaka
Jumamosi tarehe 7/11/2020 (Kutokana na tatizo
la mtandao tumeongeza tena wiki moja mpaka tarehe 14/11/2021)
kwa kila atakayenunua kitabu hiki kupewa vitabu na michanganuo ya biashara
ifuatayo pale chini, pia kuunganishwa na Group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE kwa muda wa miezi 3.
Group hili linaendesha masomo ya kila siku ya fedha na Ujasiriamali pamoja na
semina za mara kwa mara kuhusiana na Uandishi wa Michanganuo ya biashara
zinazolipa.
OFFA
HIYO YA WIKI MOJA NI HII HAPA CHINI;
1. KITABU cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI (New
special edition 2021) –kwa
kiswahili
2. KITABU mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio
kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa
kiingereza
3. Semina ya siku 7 na mpango kamili wa
biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO
Milling))-kwakiswahili
4. Kifurushicha michanganuo 3 ya ufugaji wa
kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wamayai, kuku wanyamana kuku wakienyeji-zote kwa kiswahili
5. Mchanganuo kamili wa kilimo cha
Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili
6. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa Kiswahili &
kiingereza
7. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
8. Mchanganuo kamili wa BiasharayaChipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
9. Somomaalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako
binafsi na kwabiashara yako-kwa kiswahili
10.
Vielezo(Templates)zamichanganuo
ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Kwa Kiswahili & kiingereza
11.
Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari(One page Business plan)
(NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
12.
Vipengele / (Outlines) vya Mpango
wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa
kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.
13.
Kuungwa group la Michanganuo
la mentorship miezi 3
(michanganuo-online) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu
michanganuo na ujasiramali kwaujumla
Siku za nyuma tumekuwa tukitoa offa kama hii
ingawa kila offa huja na vitu tofauti na nyingine, na kwa wale waliokuwa
wakitufuatilia ni mashahidi, huwa tunaposema ni ya wiki moja ni ya wiki moja
kweli hatutanii, na ikishapita imepita hakuna tena namna unaweza kuja kuipata
labda ije nyingine ambayo itakuwa na vitu vingine tofauti.
Kupata toleo hili jipya la kitabu cha MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI-new special edition pamoja na OFFA
zake zote 12, lipia sh. Elfu 10 tu
kwa namba zetu, 0765553030 au 0712202244 jina ni Peter AugustinoTarimo
Kisha tuma ujumbe wa Watsap au Sms
ya kawaida usemao, “NITUMIE OFFA YA MWISHO 2020 YA VITU 12” Ukihitaji na group la
mentoship basi ongeza “…NA GROUP LA
MICHANGANUO” kwenye ujumbe wako. Unaweza pia kutuma kwa Telegram namba ni 0765553030
Ikiwa hutumii watsap wala telegram usijali,
unaweza kututumia anuani yako ya email kwani masomo, vitabu na michanganuo
vyote tunatuma pia kwa njia ya email. Vilevile kwa kipindi hiki mitandao ya
kijamii ipo chini sana, watsap haifanyi kazi maeneo mengi hivyo email inaweza
kufaa zaidi. Wahi offa hii kabla wiki haijakwisha. ASANTE SANA.
HATA HIVYO OFFA HII ITAONGEZEWA TENA WIKI MOJA MPAKA JUMAMOSI IJAYO YA TAREHE 14/11/2020 KUTOKANA NA SABABU KUBWA KWAMBA TAARIFA HII HAIKUWEZA KUWAFIKIA WATU WENGI SHAURI YA TATIZO LA KITEKNOLOJIA LA MTANDAO WA INTANETI LILILOSABABISHA PIA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI TANZANIA KUWA CHINI MNO KIASI CHA KUTOKUFUNGUKA KWA URAHISI
0 Response to "MAZINGIRA YA BIASHARA KUELEKEA MIAKA 5 IJAYO YA UTAWALA WA RAIS JOHN MAGUFULI JE, UMEJIPANGA VIPI?"
Post a Comment