Katika safu yetu ya maswali na majibu leo kutokea Mkoani Dodoma (Makao
makuu ya nchi), msomaji wetu mmoja kwa jina Janeth,
ameuliza kama ifuatavyo;
“Habari! Naomba ushauri wako, Nina mtaji wa laki tatu nitafanya
biashara gani itakayoniingizia hela? Nipo kijijini siyo mjini.”
Na hii hapa ni ‘Screenshot’
ya swali hilo alilonitumia kwa SMS ya kawaida.
Nilimjibu kama
ifuatavyo:
Mimi siwezi kuzijua fursa zilizoko hapo kijijini kwenu kwakuwa
sijafanya utafiti. Mimi naweza tu kukutajia kwa ujumla fursa zinazoweza
kupatikana katika vijiji vyote siyo kimoja tu
Unatakiwa utafiti ni fursa za biashara zipi zilizoko hapo
kulingana na mazingira yaliyopo. Lakini pia ni lazima ujitathmini wewe
mwenyewe binafsi ikiwa una uwezo au nguvu katika aina gani ya biashara.
Nguvu ninazozizungumzia hapa namaanisha vile vitu ambavyo una uwezo
navyo kwa mfano ikiwa wewe umewahi kusomea kozi fulani labda tuseme ‘course’ ya matumizi ya compyuta, basi
wewe biashara unayoweza kuanza kuifikiria ni biashara ya steshenari au biashara
ya graphic designing. Ikiwa wewe
uliwahi kuajiriwa katika duka fulani la rejareja lakini baadae ukaacha, wazo
lako la biashara utakalolipa kipaumbele ni kufungua duka la rejareja.
Kitu kingine kinachoweza kukupa wazo la biashara ni hobi au
mapenzi na biashara fulani. Jiulize mwenyewe je, ni biashara gani
unayoihusudu Sana? Kile unachokiwaza mara kwa mara akilini kwako kina uwezekano
mkubwa wa kugeuka kuwa wazo lako la biashara.
Kitu kingine ni mahitaji au shida za watu. Jiulize hapo
hapo kijijini watu wanahangaika sana kutafuta bidhaa/huduma gani. Au hata wewe
mwenyewe ni kitu gani ukikihitaji unazunguka mwendo mrefu kukipata? Basi ujue
ikiwa utaanzisha biashara ya bidhaa ama huduma hiyo utakuwa umetatua shida za
watu wengine wengi na hivyo watu hao watakupa fedha kama malipo. Na hii
itageuka biashara inayolipa hapo kijijini kwenu
Biashara za vijijini zipo nyingi kutegemeana na mahitaji ya
kijiji husika lakini kwa ujumla orodha ya biashara nyingi zinazofanyika
vijijini na kuwalipa watu vizuri ni hizi zifuatazo;
Biashara za kununua na kuuza mazao ya vyakula yanayotokana na
kilimo au ufugaji. Biashara hii italipa vizuri zaidi ikiwa unanunua mazao na
kuyapeleka maeneo ya mjini. Unaweza pia kununua mazao hayo msimu wa mavuno kwa
bei ya chini kisha kuyahifadhi ukaja kuyauza kipindi cha uhaba wa chakula kwa
bei ya juu.
Biashara nyingine unayoweza kufanya kijijini ni biashara ya kuuza
bidhaa zitokazo mijini. Ukifungua duka la rejareja au hata duka la jumla
kijijini na kisha bidhaa zako ukawa unazifuata mjini unao uwezekano wa kupata
faida mara mbili ya mfanyabiashara anayenunua kwa jumla hapohapo kijijini.
Biashara hizi kubwakubwa nilizozitaja hapo juu zinataka uwe na
mtaji mkubwa wa kutosha lakini nakumbuka wewe umeniambia mtaji wako ni lakini
tatu tu. Biashara ndogondogo unazoweza kufanya kijijini na zikakupatia faida
zipo pia ingawa haziwezi kufanana na biashara nyingi ndogondogo zinazoingiza
fedha nyingi mjini.
Biashara kama za kuuza vitafunwa na biashara za vyakula kwa
ujumla zinalipa sana mijini lakini biashara hizi vijijini haziwezi kutamba sana
kutokana na watu wengi kutegemea milo inayopikwa majumbani mwao zaidi.
Biashara ya kuuza vyombo nayo inalipa kijijini. Lenga vile
vyombo vinavyopatikana kwa shida na vilivyo na uhitaji mkubwa mfano, mapipa,
ndoo, mifuko ya kuhifadhia mazao, madumu ya maji, kamba za manila na mashine
ndogondogo za kurahisishia kazi za shamba kama vile mabomba ya kunyunyizia
madawa, mitego na sumu za kuulia wadudu/wanyama waharibifu nk.
Kuna biashara nyingine ndogo yenye faida kubwa ambayo malighafi
zake wala hununui unapata bure ardhini, hii ni biashara ya kutengeneza majiko
sanifu na vifaa vya ufinyanzi kwa kutumia udongo wa mfinyanzi. Kama kijiji
chenu kimebarikiwa kuwa na aina hiyo ya udongo basi kumbuka mnaukalia utajiri
pasipo kujua. Maeneo ya mijini wanahitaji sana majiko sanifu ya kutumia mkaa
kidogo, ukijifunza kuyatengeneza na kuyatafutia soko maeneo ya mijini umeula!
Ikiwa kijijini kwenu mikate ni ya shida pia unaweza kuanzisha
biashara ya kuoka na kuuza mikate kwa kutumia oven rahisi za mkaa.
Kwa mtaji wa laki 3 pia kijijini unaweza ukaanzisha biashara ya
kununua na kuuza matunda. Lakini pia biashara hii unatakiwa ukishanunua matunda
yako kijijini basi soko lako liwe ni mjini. Tafuta mji uliokuwa karibu na wewe
au hata ikiwa ni mji wa mbali basi pawe na usafiri was uhakika. Matunda mijini
yana soko kubwa ukiwa na mahali pa uhakika pa kushushia matunda yako kisha
wateja wakaja kuyachukulia pale isijekuwa tena ukishayafikisha mjini unawaita madalali wanakuja kukuupangia bei.
Matunda na mbogamboga ni aina ya mazao ya biashara yenye faida kubwa nje na
ndani ya nchi.
Mwisho Janeth nakushauri fikiria wazo la biashara unayoona
utaimudu, ifanyie utafiti kuijua nje ndani na baada ya hapo sasa ianze taratibu
kwa kutumia kiasi kidogo kwanza cha huo mtaji wako(300,000/=) unaweza kutumia
hapo laki na nusu kisha ukiona biashara inakupa matumaini kwa kuingiza faida
basi ndipo uongeze taratibu kiasi kingine cha mtaji uliobakia.
…………………………………………………………
Ndugu msomaji wa makala hizi, ikiwa
ungependelea kujifunza zaidi kwa makala nzuri kila siku zinazohusu fedha na
ujasiriamali basi nakukaribisha katika darasa letu ndani ya group la Whatsap la
MICHANGANUO-ONLINE. Ada ni sh. Elfu 10 tu kwa mwaka mzima na tayari sasa hivi
masomo yakiwa yameshaanza tunaendelea na usajili wa wanachama wapya kwa ajili
ya mwaka 2021
FAIDA
UTAKAZOZIPATA
1. OFFA
ya vitabu na michanganuo, ni items
zipatazo 20
2. Kuwa
member wa group kwa mwaka mzima bila malipo ya ziada.
3. Semina
za jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara zinazolipa
4. Fursa
ya kuuliza swali lolote lile kuhusiana na Mpango wa biashara na Ujasiriamali na
kujibiwa kwa kina
5. Fursa
ya kutangaza bure katika group
6. Fursa
ya kuchangia chochote, kutoa somo au semina nk.
Offa ya kupata hivyo vitu 20 kikiwamo kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI mwisho wake ni tarehe 10 Desemba
2020 siku ya Alhamisi usiku. Baada ya hapo kama nafasi zitakuwepo bado utaweza
kulipia kujiunga na group lakini offa hii haitakuwepo tena.
Kulipia tumia namba zetu; 0765553030 au
0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe kwa meseji
au watsap usemao;
“NATAKA
OFFA YA MWISHO 2020 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”
Baada ya hapo nitakutumia offa zote na
kukuunganisha na group la masomo uanze kujifunza siku hiyohiyo.
Ikiwa
hutumii WATSAP hamna shida kwani tunatuma kila kitu pia kwa njia ya E-mail.
NA IFUATAYO NDIO ORODHA YA OFFA NITAKAZOKUTUMIA!
1.
KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
(New special edition 2021) –cha kiswahili
2.
KITABU
mashuhuri zaidi
duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio
kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA FEDHA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
Semina
nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili
5.
Kifurushi
cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-zote kwa kiswahili
6.
Mchanganuo
kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA
WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili
7.
Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa Kiswahili &
kiingereza
8.
Mchanganuo
kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks) -Kiswahili
9.
Mchanganuo
kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-Kiswahili
10. Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha
kwako binafsi na kwa biashara
yako-kwa kiswahili
11. Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha
kuandika michanganuo kwa muda mfupi. -
Kiswahili & kiingereza
12. Mchanganuo mfupi wa biashara
ya Steshenari (One page Business plan)
(NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
13. Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara
kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan
unaweza kuvifuatisha ukaandika.
14. Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2021
(MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu
michanganuo na ujasiramali kwa ujumla
0 Response to "ORODHA YA BIASHARA ZA VIJIJINI UNAZOWEZA KUANZA NA MTAJI WA SH. LAKI 3 (300,000/=)"
Post a Comment