Hivi karibuni msomaji wetu mmoja alinitumia swali lake kama ifuatavyo kupitia whatsapp, maswali kama haya kwa kweli ni mara nyingi tumewahi kuyajibu hapa lakini si vibaya tukaendelea kuyajibu kwani wajasiriamali wengine ni wapya na hatuna budi kuendelea pia kuwaelimisha. Nimeweka screenshot ya swali na jibu kisha maelezo nimeyaandika kwa kirefu chini yake;
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
SWALI
hello habari,,,
natumai u mzima! Tafadhali naomba msaada wako nina mtaji
wa milioni mbili sielewi nifanye biashara gani naomba msaada
MAJIBU
Mzima kabisa, za kwako;
Wazo la biashara linatakiwa litokane na wewe mwenyewe kwa kufanya utafiti kujua ni mahitaji gani yanayokosekana katika jamii iliyokuzunguka. Ukiweza kubaini mahitaji hayo na kisha ukaweza kuyatimiza jamii itakuwa tayari kukulipa pesa na hilo ndio libaloweza kuwa biashara nzuri kwako.
Aidha tafakari ni kitu gani unachokiweza zaidi ya vingine au kushinda watu wengine na unaweza kukitumia kitu hicho kama wazo lako la biashara. Mfano labda una kipaji cha kuzungumza mbele za watu, unaweza kugeuza kipaji chako hicho kuwa biashara ya ushereheshaji(u-mc) kwenye mashughuli mbalimbali kama harusi, kipaimara, kitchen party, ubarikio, maulidi nk..
Vilevile unaweza kubuni biashara inayoendana na fani au taaluma uliyosomea kwa mfano ikiwa wewe umesomea ualimu, unaweza kuanzisha madarasa ya tuisheni nyakati za likizo au muda wa jioni. Na ikiwa labda umesomea mambo ya kilimo unaweza ukaanzisha biashara yeyote ile inayohusisha utaalamu kwenye fani ya kilimo kama uuzaji wa dawa za kuulia wadudu na pembejeo zingine au ukaamua kuanzisha huduma za ushauri wa masuala ya kilimo nk.
Mtu akikushauri kwa kuwa una huo mtaji wa milioni 2 kaanzishe ufugaji unalipa, wakati wewe mawazo yako yote yapo kwenye kufungua genge la matunda na mbogamboga, ni wazi ufugaji utakwenda kukushinda na utaona kwamba pengine mtu huyo alikuingiza 'choo cha kike' jambo litakalokufanya uwaone watu hawakutakii mema hata kidogo.
Baada ya kupata wazo la biashara unaloona litakufaa kulingana na mazingira yako sasa unaweza kukaa chini na kutafakari ni nini hasa kinachohitajika ili uweze ukaanzisha biashara hiyo. Orodhesha mahitaji yako yote ambayo hayataweza kuzidi mtaji wa shilingi milioni mbili uliokuwa nao. Hatua hii kwa biashara kubwa naweza kusema ni hatua ya kuandika mpango wa biashara lakini kwa ngazi ya biashara ndogo tu ya mtaji mdogo unaweza usijisumbue kuandika mpango kamili wa biashara na badala yake mpango wako ukauweka kichwani kama wajasiriamali wengi wadogowadogo wanavyofanya siku zote.
Katika mpango wako huo jaribu kufikiria kila hatua biashara yako itakayopitia, fikiria jinsi ya kupata mtaji au kuongeza mtaji huo wa milioni mbili uliosema tayari unao, tafakari ni nani atakayehusika katika uendeshaji wa biashara yako ikiwa kama siyo wewe mwenyewe, jiulize ni bidhaa ama huduma zipi utakazouza, utawauzia kina nani, wateja wako walengwa wana sifa zipi, je ni wanaume, wanawake au mchanganyiko? Utatumia mbinu zipi kujitangaza.
Fikiria pia juu ya wale watakaokuwa washindani wako ni nguvu zipi au udhaifu waliokuwa nao. Tafakari juu ya vihatarishi mbalimbali vinavyoweza kuja kuikumba biashara yako na njia utakazotumia kupunguza hatari hizo na mwisho jiulize ikiwa biashara hiyo ni endelevu na itakayoweza kukupatia faida ya uhakika.
SOMA: Biashara ndogondogo zenye faida ya haraka Tanzania ni hizi hapa zipo nne(4)
Baada ya kutafakari hayo yote na kufikia muafaka kuwa biashara hiyo ya mtaji wa milioni mbili (2) ina uwezekano wa kukupatia faida, basi huna muda wa kupoteza tena zaidi ya kuianza mara moja kwa vitendo. Hakuna biashara rahisi ni lazima uanze kwanza kwa ugumu bila ya kuona faida harakaharaka mpaka pale wateja watakapoizoea na wewe mwenyewe kutengeneza mazoea ya kuifanya kila siku bila kukosa. Wateja hupendelea kununua kutoka kwa mtu waliyemzoea na kumuamini hivyo jenga kwanza kuaminika kwa wateja wako.
.............................mwisho……………......
Katika biashara ndogondogo wajasiriamali wengi hawana muda wa kuandaa michanganuo kamili ya biashara zao, kwanza wengi hawana uelewa na michanganuo ya biashara na pili wengine hawana rasilimali za kutosha kumlipa mtaalamu wa kuwaandikia.
Hivyo kwa kulitambua hilo katika kitabu chetu mashhuri cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMLI TOLEO LA 2021 tumeongeza kipengele muhimu sana kwa wajasiriamali wale wadogo kinachohusu jinsi ya kuandaa mwenyewe mpango rahisi kabisa wa biashara ndogo kwa muda mfup usiozidi nusu saa.
Mpango huo mfupi wa biashara unaoweza ukachukua ukurasa mmoja au zaidi, kimsingi unabeba karibu vipengele vyote muhimu vinavyopatikana kwenye mchanganuo wa kawaida mrefu wa biashara na faida zake ni sawasawa tu na zile zilizoko kwenye mchanganuo mrefu wa biashara. Kipengele hicho kipo katika ukurasa wa 344 – 352 na kuna malezo pamoja na mifano halisi.
Kukipata Kitabu hiki kwa sasa tunaweza kukutumia kupitia email au watsap na malipo ni kwa njia ya simu. Namba yetu ni, 0765553030 Tunatuma kitabu dakika 3 baada ya kufanya malipo na BEI ni sh. 10,000/=
0 Response to "BIASHARA YA MTAJI WA MILLION MBILI (2) NINAYOWEZA KUFANYA NI IPI? NAOMBA MSAADA"
Post a Comment