Bila shaka umewahi kusikia au hata kualikwa
kwenye mikutano ya wanabiashara za mtandao maarufu kama Netwok Marketing au
Mult-level Marketing(MLM). Biashara za namna hii zimeenea karibu mabara yote
Duniani huku zikihusisha biashara ya mamilioni ya pesa.
Maana
hasa ya biashara ya Mtandao/Mult-level marketing au network marketing
Biashara hii imekuwa ikipewa maana nyingi na
hivyo pia kumekuwa na majina tofauti yanayoielezea. Wapo wanaoiita Network
marketing, wengine Direct selling na wengine, Multlevel marketing. Biashara ya
mtandao pia imekuwa ikinasibishwa na upatu ujulikanao kwa kimombo kama Ponzy
cheme au Pyramid schemes jambo linaloifanya biashara hii kutiliwa mashaka na
watu wengi japo ni halali na inayokubalika kimataifa.
Ili kutofautisha mbichi na mbivu, hebu kwanza
tuone maana halisi ya dhana hizi mbili, biashara halali ya mtandao(Mult-level
Marketing) au Network Marketing na ile isiyokuwa halali ya upatu wa Pyramid
scheme.
Biashara
ya mtandao maana yake ni biashara inayohusisha watu wengi katika
kuuza bidhaa ama huduma na mara nyingi huwa ni bidhaa za afya, urembo, chakula
na hata vitabu. Mshiriki anaweza
akaingiza pesa kwa njia mbili, yakwanza kwa kuuza bidhaa au huduma lakini ya
pili ni kila pale anaposhawishi mwanachama mpya kujiunga hukatiwa kamisheni.
Upatu
wa pyramid/ponzy scheme kwa upande mwingine ni biashara haramu
ya kitapeli ambayo malengo yake makuu siyo kuuza bidhaa au huduma bali
wanaingiza pesa kwa kuwahadaa wanachama wapya wanaojiunga na kampuni kuwa
watavuna gawio kubwa pasipo hatari yeyote ile. Wakati huohuo kiingilio chao
kikitumika kuwalipa gawio wale wanachama waliotangulia kujiunga. Kampuni
inaweza kuzuga hata inauza bidhaa au huduma lakini kumbe hilo siyo lengo lao
kuu.
Hapa unaweza ukaona kwamba kuna makampuni
mengi yanayokuja kwa mgongo wa network marketing lakini kumbe agenda yao kubwa
ni kuendesha upatu wa pyramid/ponzy scheme biashara ambayo mwisho wake ni
kuanguka na wanachama wengi wale wa mwisho kuambulia kupoteza fedha zao zote
walizowekeza kama mtaji baada ya kudanganywa wangevuna faida mara mbili(2)au
hata mara kumi ya mtaji waliowekeza.
Utaitambuaje kampuni ya biashara mtandao kama
ni halali au ni matapeli wa upatu wa Pyramid scheme?
· Kampuni
halali huwa haitoi ahadi za mtu kupata utajiri wa haraka, ukiona wawakilishi wa
kampuni wakikukazaia ujiunge kwa ahadi ya kutajirika ghafla(kuwa milionea siku
moja au mbili), fikiria mara mbilimbili kujiunga.
· Kampuni
halali wanachama wake wanategemea zaidi katika uuzaji wa bidhaa/huduma na wala
siyo kuingiza watu wapya. Kipato kutokana na kuingiza watu wapya kwao ni kama
ziada tu.
· Kampuni
Itakutaka kununua bidhaa za kuanzia, kifurushi hicho cha kuanzia huwa kimebeba
pia na matangazo yatakayotumika kuvutia wateja
Mambo
ya msingi ya kuzingatia kabla hujajiunga na kampuni ya mtandao;
· Zingatia
gharama za kununulia bidhaa za kuanzia kama ni shilingi ngapi, ikiwa ni kubwa
sana, jiulize utazirudisha vipi?
· Ni
mauzo kiasi gani utakayofanya ili kurudisha kianzio chako ulichotoa?
· Je
mauzo ni kweli yanawezekana? bidhaa au huduma ni vitu vinavyoweza kuhitajika na
jamii inayokuzunguka?
· Utahita
muda kiasi gani kuingiza faida, je muda huo ukilinganisha na kazi au biashara
zingine kweli kuna tija?
· Ili
kutengeneza pesa ni lazima uingize wanachama wapya?
· Je
upo tayari kushawishi ndugu na jamaa zako wa karibu kujiunga na kampuni hiyo
bila hatari ya kuja kutokea ugomvi au kutokuelewana hapo baadae?
· Zingatia
athari zozote zinazoweza kuja kukupata katika mahusiano yako na ndugu, jamaa na
marafiki.
Biashara
ya mtandao (MLM) ni kweli inaweza kumpa mtu kipato cha uhakika na haraka?
Ukiachana na ahadi nyingi hasa…………….
..................................................................
Ndugu msomajia somo hili bado halijafika mwisho hapa, litaendelea kwenye group la Michanganuo-online leo hii usiku. Kujiunga na group hili la masomo ya fedha kila siku kuna kiingilio sh. elfu 10 ada ya mwaka mzima. Pamoja na masomo ya kila siku lakini pia kuna semina za mara kwa mara juu ya uandishi wa michanganuo ya biashara zinazolipa. Ukijiunga pia unapata papo hapo vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara iliyoandaliwa tayari.
Kulipia namba zetu ni 0765553030 au 0712202244 jina: Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma ujumbe watsap 0765553030 usemao; "NIUNGE MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE2021"
0 Response to "NI KWELI UNAWEZA KUTENGENEZA PESA NYINGI HARAKA KWA BIASHARA YA MTANDAO, MULT LEVEL MARKETING?"
Post a Comment