Mpenzi msomaji wa makala hii,
Natanguliza kwanza Pole kwa msiba
uliotupata sisi sote kama Taifa la Tanzania. Natambua hali ngumu tunayoipitia
sasa hivi lakini sina budi kusema chochote kama mtu ninayeandika makala za
maendeleo na mafanikio ya watu. Hayati Rais wetu John Pombe Magufuli kwa kweli
alikuwa ni Mwana Mafanikio aliyewavutia na kuwatia moyo watu wengi sana muda
mfupi aliokaa madarakani kwa staili yake ya kufanya mambo kwa haraka na ubora
wa kiwango cha juu.
JINSIYA KUTUMIA MAAJABU YALIYOPUNGUZA CORONA TANZANIA KUBUSTI UCHUMI WAKOUNAOSAMBARATIKA
na
nyingine inayosema;
TULIKOSEAWAPI TANZANIA CORONA IKARUDI TENA KWA KASI HII?
Katika Makala hizi zote mbili kuhusianana na mapambano dhidi ya Covid 19, kipekee kabisa nilimhusisha Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli na juhudi mbalimbali alizozichukua licha ya kelele nyingi hasi dhidi yake tokea Mataifa ya kigeni. Magufuli alidiriki kujisacrifice (kujitoa mhanga) maisha yake kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, amebeba lawama nyingi mno!, mafanikio bila gharama tungeliendelea kuyasikia kwenye bomba tu.
Masikini kumbe hata wengi hatukuwa na
habari ya kuwa Rais alikuwa na tatizo la muda mrefu tena ambalo lilihitaji
apumzike muda mwingi lakini yeye aliamua tu kuzunguka kila mahalali nchini, jamani
huku si kujitoa mhanga? Ni nani ajuae ziara zake za mwisho Dar pamoja na stress
za kufiwa na wasaidizi wake Balozi Kijazi na Maalim Seif pengine ndizo zilikuwa
chanzo cha kuutibua Moyo wake uliokuwa tayari na hitilafu? Naandika haya si kwa
nia nyingine yeyote ile, bali kuonyesha tu kiwango cha kujitoa mhanga Rais
alichoonyesha kwetu.
Ndio maana mimi binafsi kwa kweli
nachelea hata kumpa lawama yeyote ile mtu huyu kwa yale mambo ninayoamini
hakuyafanya kwa usahihi uliotakiwa. Hakuna binadamu mkamilifu chini ya Jua
lakini inapotokea mtu akafanya mambo mema mengi kuliko mabaya yake, basi yale
mabaya hufutwa na yale mema.
Mungu ailaze Roho ya Mpendwa wetu Rais
John Pombe Magufuli Mahali Pema Peponi AMINA.
Dhana ya uwekaji malengo na utekelezaji wake
kwa muda mrefu limekuwa ni suala lenye mijadala mirefu sana, wengine wakisema
ni sahihi kujiwekea malengo lakini kundi jingine la watu likikataa katakata na
kudai kujiwekea malengo maishani ni kujipotezea tu muda bure kwani baada ya
muda mfupi kupita ile hamasa ya kutimiza malengo hayo huyeyuka ama kuishia
njiani huku mhusika akirudia mambo yaleyale ya zamani aliyozoea kufanya. Mfano
mzuri kundi hili hutumia malengo ya mwaka mpya yanayowekwa na watu wengi
Januari lakini mpaka Machi - Aprili yameyeyuka yote.
Ikiwa kama kuweka malengo watu wengi huishia njiani sasa ndio kusema malengo hayafai kabisa kuwekwa? Jibu ni hapana, watu wataendelea tu kujiwekea malengo hata ikiwa ni wachache wanaofanikiwa kuyatimiza kama walivyoyaweka.
Katika suala zima la kujiwekea malengo na
hatimaye kuyatimiza kuna vitu viwili (2) muhimu sana ambavyo inatakiwa mtu
kuvifahamu vizuri ikiwa atataka kuondokana na utata uliopo. Na hapa nitakwenda
kuvielezea vitu hivyo huku nikionyeshana tofauti iliyokuwepo baina yake.
Malengo ni matokeo ya mwisho ya kile mtu
unachotamani kukipata, lakini ili kukifikia unahitaji kwanza NJIA ya
kukifikia(Mchakato) au kwa maneno mengine tunaweza tukasema ni ule utekelezaji
wenyewe(MFUMO). Haiwezekani mtu ukaweka lengo kisha ukalifikia pasipokuwa na
mchakato hapo katikati. Kwa kifupi vitu hivyo viwili nitaviita;
1. MALENGO
2. MFUMO
Ili kueleweka vizuri ni ipi tofauti kati ya
Malengo na Mfumo hebu tuitazame mifano ifuatayo;
1) Tuchukulie
mfano wewe ni Mjasiriamali
LENGO
lako ni kumiliki biashara nzuri ya
mamilioni ya fedha
MFUMO
wako ni mikakati yako mbalimbali ya Mauzo na ya Kimasoko
2) Tuchukulie
mfano wewe ni Mtunzi wa Kitabu fulani
LENGO
lako hatimaye ni kuandika kitabu kizuri
MFUMO
wako
ni ratiba ya kuandika utakayoifuata kila siku au kila juma
3)
Tuchukulie mfano wewe ni Kocha/mwalimu wa mpira wa miguu(footboller)
LENGO
lako ni kuchukua Ubingwa
MFUMO
wako ni ratiba ya mazoezi ya timu yako unayoifuata kila siku
4)
Tuchukulie mfano wewe ni Mwanariadha
LENGO
lako hatimaye ni kuibuka kidedea(mshindi)
MFUMO
wako ni ratiba yako ya mazoezi unayoyafanya kila siku, wiki au mwezi.
Duniani kitu cha kushangaza sana katika mambo
haya mawili, Malengo na Mfumo ni kwamba Matokeo ya mwisho ndicho kitu ambacho
kila mtu atapenda kukisikia na kusifia lakini siyo mchakato(Mfumo). Mchakato ni
wewe peke yako utakayeusifia na mfano
mmoja ni pale mtu anapomaliza masomo iwe ni katika ngazi ya Cheti, Stashahada
au Shahada.
Dunia nzima itataka kujua umepata alama gani
lakini hawataki kabisa kusikia mchakato wako uliokufikisha pale ulikuwaje, iwe
ulifaulu kwa kufanya bidii au kuiba mtihani, ulifeli baada ya kuugua au kukosa
pesa za ada na matumizi, hilo haliwahusu.
SASA
MALENGO NA MFUMO NI KIPI MUHIMU ZAIDI YA KINGINE?
Vyote viwili ni muhimu, unaweza kujidanganya
kwamba unashughulika na mfumo peke yake bila ya malengo lakini hilo
haliwezekani, hivi ni vitu viwili vinavyotegemeana isipokuwa tu ni kwamba baada
ya kuwa na malengo mtu unashauriwa usije ukazingatia na kuiweka akili yako yote
kwenye matokeo ya mwisho ya lengo lako kabla hujalifikia, bali lenga na zingatia zaidi mfumo(mchakato) ambao ndiyo
utakaokuwezesha kuyafikia malengo uliyojiwekea.
Kwa mfano unaweza kuwa na malengo siku moja
uwe umetunga kitabu, baada ya kuwa na
nia hiyo achana kabisa na matamanio hewa yasiyoisha ya kuwa mtunzi na badala
yake sasa elekeza nguvu zako zote kwenye ratiba ya kuandika kidogokidogo hata
ukurasa mmoja kila siku huku ukijisomea pia kidogokidogo mambo yanayohusiana na
kile unachotaka kukiandika. Baada ya muda fulani kupita, utashangaa tayari
umekamilisha kuandika kitabu chako.
Katika malengo yako unaweza ukajiwekea muda
maalumu wa kuyatimiza, hilo ni sawa lakini pia hilo lisikuzuie wewe kuzingatia
mfumo uliojiwekea. Ni sawa na kama ilivyo pia kwenye suala la kuandaa Mpango wa
biashara vs kufanya biashara tu bila
kuweka mpango wowote ule, ni vizuri kuwa na ramani ya kule uendako kabisa
mkononi lakini pia ukawa tayari kuachana
nayo au hata kutokuifuata pale inapobidi kwani katika maisha ya binadamu
hatuwezi kubashiri kwa asilimia 100% kile kitakachoweza kutokea wakati ujao hasa
kwenye biashara.
Inawezekana katika mipango yako ulipanga hivi
lakini ukaja kulazimika kufanya vile ili tu malengo yako yatimie lakini hii
haiwezi kuondoa umuhimu wa kuweka mpango wa biashara kabla ya kuanza biashara
yako.
Hatari
za kuzingatia zaidi (focus) kwenye Malengo(Matokeo ya mwisho) kuliko
Mfumo/mchakato
1. HATARI:
Kunapunguza hamasa na furaha ya wakati uliopo. Unapoweka
malengo ni kama vile unaifundisha akili yako kwamba utahamasika na kufurahi
pale tu malengo hayo yatakapotimia. Mtazamo huu akilini mwetu huwa unatufanya
tuahirishe hamasa na furaha zetu hadi pale malengo yatakapotimia jambo
linalosababisha watu wengi kukichukia kitendo cha kujiwekea malengo.
SULUHISHO:
Ukishayajua
malengo yako ni yapi, jikite zaidi kwenye mchakato kwa kuifundisha akili yako
kufanya hivyo
2. Huongeza mzigo wa mawazo.
Mfano unapolenga kupunguza uzito kiasi
fulani, kumiliki biashara ya milioni 50 au kukamilisha kuandika kitabu cha
kurasa 500 baada ya mwaka 1, tunajiongezea tu msongo wa akili huku tukihofia
namna tutakavyoweza kukamilisha malengo
hayo, hofu inachukua nafasi ya muda ambao ulitakiwa tuchape kazi.
SULUHISHO:
Badala yake mtu unashauriwa kumega kidogokidogo hilo lengo kila siku mpaka
umelikamilisha huku ukifurahia mchakato huo wakati uleule ukiwa unafanya.
3. Wakati mwingine huondoa furaha ya
kudumu.
Si mara zote kutimiza malengo kunaweza
kukupa furaha ya kudumu. Hebu fikiria mwanariadha anaweza kufanya mazoezi ya
kufa mtu ili kupata ushindi lakini mara tu anapofanikiwa kuchukua kikombe na
mchezo unakuwa umeishia hapo, hafanyi tena mazoezi. Na hii pia ipo kwa
wanafunzi wa mashule na vyuo, wakishafanya mtihani wa mwisho tu hivi ni basi,
madaftari, vitabu na kalamu tupa kule, hamna hamasa tena ya kujifunza.
SULUHISHO:
Malengo
ni ya muda mfupi lakini Mfumo ni wa muda mrefu(Maisha)
Pamoja na hayo yote si kama malengo hayana maana hapana,
ila malengo ni mazuri pale unapopanga mipango yako lakini Mfumo ndio
utakaosaidia wewe kupiga hatua mbele. Unapaswa kuviangalia vitu hivi 2 kama
Kuku na Yai, kila kimoja kikimtegemea mwenzakie ingawa kuku(mfumo) unapaswa
kuzingatiwa muda mwingi zaidi kuliko yai(lengo). Kuna mazingira mengine lakini
kuzingatia sana mfumo nako kunaweza kumfanya mtu aishie kutokulifikia lengo
alilokusudia ndio maana mahali fulani nikasema hivi;
“beba ramani yako lakini ukiona mahali fulani
njiani haifanyi kazi basi achana nayo kwani hiyo siyo msahafu, isije ikakupotezea muda wako
mwingi bure ukachelewa kulifikia lengo ulilokusudia ”
…………………………………………………..
OFFA
KUBWA YA VITABU NA MICHANGANUO YA BIASHARA !
Kuanzia tarehe 20/3/2021 mpaka tarehe 27/3/2021 mtu
atakayejiunga na MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE atapewa kitabu cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na OFFA ya vitu vingine
vifuatavyo;
1. KITABU cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI (New special edition
2021) –cha kiswahili
2. KITABU mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi
duniani.-cha kiingereza
3. Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa
biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO
Milling))-kwa kiswahili
4. Kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji wa
kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wamayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-yote ni kwa kiswahili
5. Mchanganuo kamili wa kilimo cha
Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili
6. Mchanganuo wa biashara ya Mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa
Kiswahili & kiingereza
7. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
8. Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
9. Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha
kwako
binafsi na kwa biashara yako-kwa kiswahili
10. Vielezo(Templates) za michanganuo
ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Kwa Kiswahili & kiingereza
11. Mchanganuo mfupi wa biashara
ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa
Kiswahili
12. Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza.
Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.
13. Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2021 (MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote
lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla
Thamani halisi ya Package hii ni sh. Laki mbili
(200,000/=) lakini mimi nakupatia kwa shilingi elfu 10 tu !. Lipia kabla ya March
27, 2021 kupitia namba zetu, 0765553030 au 0712202244 jina ni PETER AUGUSTINO TARIMO. Ukishalipa tuma
ujumbe watsap au sms ya kawaida usemao; “NIUNGANISHE NA MASTERMIND GROUP2021 NA
OFFA YA VITU 13”
Katika Group la Masomo ya kila siku Watsapp utajifunza masomo yenye maudhui ya FEDHA usiyoweza kuyapata mahali
kwingine kokote pamoja na kupata access ya kupakua(download) masomo zaidi ya 70 ya fedha
yaliyokwishafundishwa katika group siku za nyuma. Kupakua masomo unatakiwa kuwa
na app ya TELEGRAM kwani yapo katika
Channel yetu maalumu kwa ajili hiyo.
Ikiwa hutumii Watsapp wala Telegramu unaweza kujipatia
OFFA hii kisha tukakutumia kupitia E-mail yako kila kitu.
Unaweza pia kujipatia vitabu vyetu vingine mbalimbali
vifuatavyo;
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
BEI SH. 20,000/= HARDCOPY, 10,000/= SOFTCOPY
MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
BEI SH. 10,000/= HARDCOPY. 5,000 SOFTCOPY
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
BEI SH. 5.000/= HARDCOPY, 3,000/= SOFTCOPY
0 Response to "KUFANIKIWA MALENGO YAKO, FOCUS KWENYE MFUMO (UTEKELEZAJI) NA SIYO KWENYE MATOKEO YA MWISHO"
Post a Comment