Mtandao wa GetValue
ni jukwaa(Online Digital Information Products Retailer) la kuuza bidhaa za
mawasiliano za kidijitali kama vile vitabu, muziki, kozi mbalimbali na vitabu vya sauti kwa wateja
mmoja mmoja popote pale walipo duniani. Hii ni njia mpya ya uuzaji wa vitabu na
course ambayo haijaanza siku nyingi hapa Tanzania ingawa Kimataifa tayari
ilishaanza siku nyingi na mifano mizuri unaweza kuona mitandao ya Amazon, Lulu,
Create Space, ibooks, IngramSpark, Smashwords, Barnes and Noble Press, Bookbay
na wengineo.
Lengo kuu la majukwaa
haya ni ili kuwarahisishia watumiaji wa kazi za kidigitali hususani vitabu
waweze kuzifikia kwa urahisi na kwa gharama ndogo, lakini pia wakati huohuo
kuwawezesha watunzi wa kazi mbalimbali vikiwemo vitabu kuweza kuwa na uthibiti
wa kazi zao hususani kupunguza usambaaji holela wa kazi zao jambo linalowafanya
wengi wao kufa masikini wakati walitumia muda wao mwingi kuziandaa kazi hizo.
Watanzania wengi njia
hii mpya ya kununua vitabu au bidhaa zingine za kidigitali kupitia mitandao
rasmi kama huu wa GETVALEU hatujauzoea na kwa kweli nikiri hata mimi mwenyewe
binafsi wakati nilipofanya manunuzi ya kitabu katika mtandao huu kwa mara ya
kwanza kabisa nilikutana na changanoto kadhaa ambazo zinatosha kumfanya mtu
yeyote yule wa kawaida kuona ni kwanini tu njia ya kizamani ya kununua PDFs
isiendelee kama kawaida.
Lakini ni ukweli
mchungu kwamba Dunia sasa hivi tumeshafika, na tunaelekea moja kwa moja kwenye
matumizi ya Mtandao kufanya karibu kila aina ya manunuzi muhimu(transactions) kwenye maisha yetu ya kila
siku. Njia hii haina tofauti sana na ile mtu unapokwenda kulipia bili
mbalimbali za serikali kisha wanakuambia
“chukua hii control namba” ukalipie
kwa kutumia simu yako ya mkononi.
Baada ya kukutana na changamoto hizo nilizosema hapo juu ambazo nitazieleza hapa, mwishowe nilibaini kuwa changamoto hizo ni za kawaida sana na wala si ngumu kama nilivyokuwa nafikira kabla.
Kabla ya kuona changamoto mbalimbali unazoweza kukutana nazo, hebu kwanza tuone hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kununua kitabu kutoka GETVALUE. Hatua zimegawanyika katika sehemu kuu tatu((3), Kufungua account, Kununua kitabu na ya tatu ni Kusoma kitabu kwenye app yako.
SEHEMU YA KWANZA (KUFUNGUA ACCOUNT)
Hatua ya Kwanza(1)
Ili kufungua akaunti ya GETVALUE, unatakiwa kwanza kuingia katika mtandao huo kwa kwenda moja kwa moja Google ukatype neno GETVALUE au kwa kutumia link/kiungo cha ukurasa wa mwandishi wa kitabu unachotaka kununua kwa mfano link hii hapa ya kitabu cha THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION. Baada ya kubonyeza link hiyo utakutana na ukurasa kama huu ufuatao;
NB: Juu ni ukurasa wa kompyuta ya mezani, kama unatumia smartphone muonekano wake unaweza kuwa tofauti kidogo lakini cha muhimu unatazama kwenye screen kulia kwako pale juu kabisa mwishoni palipoandikwa "sign in" bonyeza hapo.
Hatua ya Pili(2)
Utaona ukurasa huu ufuatao, kisha bonyeza palipoandikwa "Buyer Registration;" picha hii ni screen ya simu ila haina tofauti sana na ikiwa unatumia kompyuta ya mezani/laptop
Hatua ya TATU(3)
Utaona ukurasa kama huu hapa wenye sehemu ya kujaza vitu vifuatavyo;
FIRST NAME:
SURNAME:
E-MAIL:
PHONE:
PASSWORD:
Jaza sehemu zote kisha chini kabisa mwishoni kulia bonyeza neno "Register" NB: Kwenye password chagua nenosiri lolote jingine na si lazima liwe sawa na lile la kawaida unalotumia kulog-in katika email yako hiyo kila siku.
Hatua ya nne(4) ya mwisho(sehemu ya 1)
Hatua ya mwisho kwenye sehemu hii ya kwanza utaona ukurasa ufuatao unaokuonyesha umeshakuwa registerd sasa. Utajua umeshajiunga kikamilifu kwa kuona juu kulia kwako katika screen maneno. "My Account(JINA LAKO)"
SEHEMU YA PILI (KUNUNUA KITABU)
Hatua ya Kwanza(1)
Hatua ya Tatu(3)
Baada ya malipo, utapata meseji ya udhibitisho kwenye simu yako na hapo unakuwa umeshamaliza kununua kitabu chako. Sasa utaingia katika sehemu ya Tatu na ya mwisho ya kukifungua na kukisoma kitabu chako ndani ya APPLICATION YA GETVALUE.
SEHEMU YA TATU (KUFUNGUA NA KUSOMA KITABU NDANI YA APP YA GETVALUE)
Kama bado ulikuwa hujadownload App ya GETVALUE ingia Playstore tafuta GETVALUE na kisha uipakue(install) kwenye simu yako. Ukishaipakua itakutaka kujisajili, weka taarifa zako zilezile, E-mali na Password ulivyotumia wakati unajisajili kwenye mtandao wa Getvalue kununua kitabu. Hakikisha App hiyo hujaisajili kwa e-mail nyingine tofauti. Baada ya kufunguka moja kwa moja nenda menyu ya My Products, utaona kitabu chako ulichonunua na utaweza kukisoma bila wasiwasi wowote.
.......................................................
Pale mwanzoni nilisema mtu unaweza kukutana na changamoto kadhaa lakini ambazo pia unaweza kuzirekebisha kirahisi sana, baadhi yake ni kama hizi hapa ;
KUWEPO KWA MAJUKWAA MAWILI TOFAUTI YA GETVALUE, WEBSITE NA APP.
· Unaweza kufanya kila kitu ikiwemo kulipia kitabu chako katika website ya kawaida ya GETVALUE lakini mwisho wa siku ni lazima udownload APP ya GETVALUE kutoka Playstore katika simu yako ya smartphone ili uweze kusoma kitabu ulichonunua. Huwezi kabisa kusoma kitabu ulichonunua nje ya simu-janja yako.
· E-mail unayotumia kujisajili pamoja na neno-siri(password) zinakuwa ni zilezile kote, kwenye mtandao wa getvalue na pia kwenye app ya getvalue.
· Ukishalipia bidhaa yako(kitabu na kufuata hatua zote) mwishoni unapata meseji katika simu yako kuwa umeshalipa. Sasa hapa ndio muda wa kufungua app yako kwa kutumia email na password ileile uliyokuwa ukitumia katika mtandao wa kawaida.
Hapa ndio nilikutana na changamoto kwani sikuweza kuona kitabu nilichokinunua mara moja hata baada ya kubonyeza kwenye “My products”
“NAMNA YA KUNUNUA BIDHAA KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU-GETVALUE”
Getvalue
katika channel yao ya You tube wameweka masomo mbalimbali yanayoelezea jinsi ya
kutumia mtandao wao uwe mnunuzi au muuzaji.
Kama umekutana na changamoto yeyote ile wakati wa kununua kitabu hiki kwenye mtandao huu, unaweza kuwasiliana na sisi kwa namba zilizoko hapo chini.
Kupata kitabu cha karatasi-hardcopy wasiliana nasisi utaletewa ulipo au unaweza kukipata Bright Future Books & Stationery iliyopo Mbezi-Kimara, Kibanda cha mkaa karibu na St. Augustine Secondary School (Tagaste) Unaweza pia kupitia njia yaTemboni.
SIMU/WATSAP: 0765553030 au 0712202244
0 Response to "JINSI YA KUNUNUA KITABU CHA THINK AND GROW RICH-SWAHILI KATIKA MTANDAO WA GETVALUE"
Post a Comment