Nani
kakuambia fursa za biashara Tanzania zipo chache? Zimejaa tele, kila siku
nakutana na maswali mengi watu wakitaka kupata taarifa kuhusiana na biashara
mbalimbali zenye faida ya haraka. Miongoni mwazo ni biashara ya vinyaji vya
jumla, kuuza bia za jumla na soda aina zote, biashara ya kuuza
maji ya kunywa pamoja na jinsi ya kupata uwakala wa kuuza
vinywaji mbalimbali mfano kuwa wakala wa makampuni kama ya pepsi, cocacola nk.
Leo kwenye safu yetu hii ya uliza ujibiwe nitajibu swali kutoka kwa msomaji wetu mmoja ambaye swali lake ametuma kupitia njia ya whatsap kama ifuatavyo;
Naomba
ushauri kaka,
Nataka kufanya biashara ya
vinywaji ya kuuza kwa jumla sasa nina mtaji wa million moja, je naweza
nikafanikiwa kuanza hata kidogo?
Majibu ya swali hilo
ni haya hapa:
Ndugu msomaji,
Ingawa sijafahamu
ikiwa biashara yako hiyo ya kuuza vinywaji vya jumla utaifanyia katika eneo au
mazingira ya namna gani lakini nitajitahidi kukupa majibu kwa kuzingatia
mazingira yote, iwe utafanyia kwenye eneo maalumu kama vile dukani au hata kwa
njia ya kuwasambazia wateja wako watarajiwa wa vinywaji mpaka mlangoni kwa
kutumia usafiri.
SOMA: Nina mtaji wa milioni moja ya mkopo, nifanye biashara gani inayolipa?
Siku zote mimi huwa
nasema ikiwa una mapenzi na biashara fulani na unajua una uwezo nayo
nikimaanisha unazijua mbinu zote muhimu za kuifanya na kuingiza faida basi
mtaji siyo tatizo hata kidogo. Kwanini nasema hivyo? Inawezekana wewe una wasiwasi
mkubwa juu ya kiwango chako cha mtaji ambacho umeshakitaja kuwa ni shilingi
milioni moja tu. Mtu mwingine hapa anaweza akakushauri milioni moja ni kiasi
kidogo mno kuweza kutosha kuanzisha biashara ya jumla ya kuuza vinywaji iwe ni
vinywaji baridi kama soda na maji au hata vinyaji vikali kama bia na aina
nyinginezo za pombe.
Yamkini hujui hata
kreti ya soda jumla inauzwaje, usijiloge ukaingia kichwakichwa biashara hii
kwani utakuwa na wakati mgumu sana wa kujifunza kwanza kabla hujaanza.
Hakikisha una uelewa wa kutosha nayo kwa kufanya utafiti wa soko kama ilivyoainishwa
vizuri katiaka kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako
Kuanzisha biashara ya
aina yeyote ile ikiwemo pia na biashara ya kuuza vinywaji vya jumla ni
lazima mtu uorodheshe katika karatasi
mahitaji yako yote muhimu ambayo yatakuwezesha wewe kuianza biashara husika.
Huo ndio mpango wako wa kwanza kabisa rahisi wa biashara.
Fikiria akilini mwako
ni vitu gani utahitaji kwa makadirio ya chini kabisa ili uweze kuanza japo hata
ikiwa ni kwa kiasi kidogo kabisa iwezekanavyo. Ikibidi hata unaweza kuanza na
kreti za soda tano, ilimradi tu ufahamu kuwa utapata mteja atakayezinunua.
Mtu mwingine anaweza
akadhani biashara ya mtaji wa laki tano au milioni moja basi ni lazima tu iwe
ni biashara ndogo mfano wa mama lishe au baba lishe lakini niamini, hiyohiyo
milioni yako moja unaweza ukaanzisha biashara ya jumla ya vinywaji kwa kiwango
kidogo kabisa huku ukiwa na maono ya mbali zaidi (Start small but think Big)
SOMA: Huna mtaji wa kutosha, hukopesheki? jaribu njia hii ya kufunga mkanda(Bootstrapping)
Ni sawa kiasi hicho
cha fedha hakitoshi kuchukua fremu ya duka la kuuzia vinyaji, unaweza
kuwatembelea wenye maduka ya rejareja ukawauliza kama wanahitaji vinywaji, wakijibu
uwaletee, unakwenda maduka makubwa kununua mzigo na kuwapelekea. Cha msingi
ujue tu unapata hapo faida kidogo.
Kidogokidogo
utajikuta unapata mtaji mkubwa au unapata ‘mchongo’ wa kupata mtaji mkubwa
zaidi hata wa kufungua duka kubwa la vinywaji jumla kupitia njia nyinginezo tofauti
kwakuwa sasa utaweza kuaminika kutokana na watu kuona kwa macho utendaji wa
biashara zako.
Kiukweli changamoto
kubwa kwenye biashara hii ya jumla ya vinywaji ni mtaji, ili upate faida kubwa na
ya haraka zaidi inakubidi uwe na kiasi kikubwa cha mtaji lakini kwa kuanza si
lazima uanze na kiasi hicho kikubwa cha mtaji. Unachopaswa kufanya kwanza ni
kutengeneza msingi wa wateja, wateja ndio kila kitu mengine huja taratibu.
Unaweza hata kuanza biashara yako ya vinywaji kama dalali usiyekuwa hata na
senti tano mfukoni.
SOMA: Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti
Kuna jamaa yeye kazi
yake ilikuwa ni kuzunguka maduka ya rejareja, mabaa na grocery akiwa na sample za
vinywaji kama vile, red bull, malta na aina nyinginezo za vinyaji vinavyobebeka
kwa urahisi, akipata oda hata ya pc 6 anakimbia kwa wenye maduka ya jumla ya
vinywaji anawaomba wamuamini mzigo, akishaenda kuuza anarudi kuwalipa chao na yeye
anabakia na faida yake.
Kidogokidogo hivyo
akajikuta anapata mtaji kiurahisi kabisa baada ya muda kupita. Sasa hivi
ninavyoandika hapa anamiliki duka la kuuuza bia za jumla pale Mbezi mwisho na
duka jingine kubwa la kuuuza maji ya jumla pale Kiluvya madukani. Ndugu msomaji wangu
nikutie tu moyo kuwa million yako hiyo moja unaweza ukatimiza azma yako ya
kumiliki biashara ya jumla ya vinywaji ikiwa utaamua kuwa mbunifu na
kuhakikisha unaishi chini ya kipato chako hadi pale utakapohakikisha mtaji
umetengemaa vya kutosha.
………………mwisho……………..
Una swali lolote lile
kuhusiana na Biashara na Ujasiriamali? Tutumie maswali yako kupitia Watsap au
Sms ya kawaida, 0765553030 au 0712202244 na tutakujibu kupitia safu hii.
Masomo ya fedha(Basic
& Advanced Financial Education) yanapatikana ndani ya MASTERMIND GROUP la
MICHANGANUO-ONLINE kila siku saa3 usiku. Kujiunga kiingilio cha mwaka(miezi 12)
ni sh. Elfu 10 tu. Uwe na account watsap na Telegramu lakini ikiwa huna basi
E-mail inatosha, tutakutumia kila kitu kupitia email yako-nijulishe mapema
kupata utaratibu.
VITABU vyetu vyote pia
vinapatikana;
1. THINK & GROW RICH-SWAHILI
EDITION
2. MICHANGANUO YA
BIASHARA & UJASIRIAMALI
3. MAFANIKIO YA
BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
4. MIFEREJI 7 YA PESA
NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
0 Response to "BIASHARA YA VINYWAJI JUMLA, MTAJI MILIONI MOJA (1) NAOMBA USHAURI"
Post a Comment