..Ilikuwa
ni maji siyo chanjo…
..Mbona
kipindi cha Rais Magufuli tena bila hata ya chanjo Korona ilipungua haraka na
haikusambaa kama sasa hivi…?
Kiukweli kabisa
makala hii unayosoma sasa niseme wazi kabisa kwamba nimeiandika kiupendeleo (biased) kinyume kabisa na vile
nilivyofundishwa katika uandishi wa habari na sababu nitaielezea.
Nimeegemea upande ule
wa wanaohitaji kuchanjwa Korona kwa udi na uvumba na hata ingeliwezekana
kuchanjwa mara tu baada ya Mama samia jana kuchanjwa basi ningechanjwa.
Waswahili husema aisifuye mvua imemnyea, kama alivyosema Rais Mama Samia Suluhu
Hassan jana wakati akifanya uzinduzi wa chanjo dhidi ya covid-19 ya Johnson
& Johnson chini ya mpango wa chanjo wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wa
Covax kuwa kama hujaguswa na hili janga kwenye ukoo au familia yako unaweza
ukasema lolote, lakini likikugusa unajua hatari ya hili janga.
SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza korona Tanzania kubusti uchumi wako unaosambaratika.
Binafsi mimi janga la
corona limenigusa, ndugu yangu kaugua ijapokuwa amepona lakini najua wasiwasi
na hekaheka ndugu na jamaa tulizopitia kwa takriban wiki zaidi ya 2 alizoumwa
achilia mbali yeye mwenyewe maumivu na hali aliyopitia. Inatosha na wala
sihitaji kuwa Tomaso kwa suala hili.
Ushahidi pia wa watu
ninaowajua kufa kwa korona ninao lakini sina ushahidi wa mtu hata mmoja
aliyefariki kwa athari za chanjo yeyote iwe ya corona au hata ya magojwa yale
mengine kama polio na surua ijapokuwa tangu nikiwa shule ya chekechea uvumi wa
hatari za chanjo nimekuwa nikiusikia tu mitaani na miaka yote tumekuwa
tukitumia chanjo mbalimbali kutoka kwa hawahawa wazungu, iweje sumu waje
watutilie kwenye hii ya corona tu? Chanjo ya korona Kenya na Uganda zimetangulia
kabla yaTanzania lakini hatujasikia bado madhara ya kutisha yaliyotokea mpaka
sasa hivi zaidi ya faida za chanjo ya corona zenyewe, hivyo usalama wa chanjo
hii kwa kiasi kikubwa hauna mashaka kama Wizara ya Afya na shirika la afya Duniani WHO wanavyosisitiza.
Mimi siyo daktari
wala sina taaluma yeyote ile ya uuguzi, lakini kama muelimishaji ninao wajibu
wa kuhakikisha natoa taarifa zilizokuwa sahihi kwa jamii yangu kuhusiana na jambo
lolote lile likiwemo na hili la kiafya kwa malengo ya kuwafanya watu wachukue
maamuzi sahihi yanayohusu usalama na ubora wa maisha yao. Siwezi kuhubiri
mafanikio ya kifedha tu peke yake huku watu wakiangamia kwa korona au magonjwa
mengine yanayoweza kuzuilika kwa urahisi kabisa kisayansi.
SOMA: Aina (4) za biashara zenye kinga ya majanga vikiwemo virusi vya corona(covid-19)
Wakati Rais Samia
Suluhu Hassan akihutubia kwenye uzinduzi wa chanjo ya covid-19 nikiwa na kisimu
changu kidogo chenye redio, kama kawaida yangu nilipita mitaani nikitaka kujua
kilichokuwa kikisemwa juu ya zoezi lile. Nilichogundua ni kwamba, wananchi
wengi mitaani wala hawakuwa na habari, wengi walikuwa wakiendelea tu na mishemishe
zao, wengine wakipiga story mitaani na kwenye vijiwe.
Watanzania tumezowea
kushabikia mno habari na taarifa feki(potofu) kuliko taarifa rasmi za ukweli,
tumekuwa wavivu hata kusikiliza tu taarifa ya habari redioni. Kwa hali hiyo
unakuta jambo la uzushi ndilo hubebewa bango na kila mtu hata kama watu hao
hawajajiridhisha kutoka katika vyanzo vya habari vya uhakika. Taarifa kama
chanjo ya corona kuongeza maumbile ya kiume hata ‘ugoogle’ mitandao ya Kimataifa
huwezi kukuta kitu kama hicho kutoka kwa vyanzo makini zaidi ya wazushi(Conspiracy theorists)
Katika kijiwe kimoja
maeneo ya stendi ya Mbezi mwisho nilikuta kina dada fulani wakinunua samaki mahali huku mjadala mkali
ukiendelea juu ya suala la chanjo ya corona baina yao na muuza samaki. Dada
mmoja alikuwa akipinga kabisa chanjo na kusema,
“mimi hata waniwekee panga shingoni sichanjwi ng’o! mbona Rais Magufuli enzi zake alikataa hayo
machanjo na hatukuona korona ikisambaa kama sasa hivi? Hayo machanjo Wazungu wawetuwekea humo virusi vya corona”
Sikuweza kuvumilia
ikabidi nisogee karibu nijiunge na mjadala ule kwa lengo la kusahihisha kauli
ile potofu.
Muuza samaki naye
akadakia,
“Unafikiri
Mama Samia pale amechanjwa dawa yenyewe wanayosema…...yale yalikuwa ni maji
matupu, amezuga tu ili wananchi tukubali kiurahisi kuingia mtegoni…..hawezi
kukubali kitu cha kumuua taratibu…….”
Kifupi pale mtetezi
wa chanjo nilijikuta ni mimi peke yangu, nikapata picha jinsi serikali ilivyo
na kibarua kigumu kuwaelimisha wananchi wake kusafisha uwongo waliopandikiziwa
vichwani mwao na wapinga chanjo. Kauli ya Hayati Rais Magufuli juu ya chanjo ya
korona nakumbuka hata makala zangu za nyuma kwenye lile wimbi la pili niliwahi
kuandika; TULIKOSEA WAPI TANZANIA CORONA IKARUDI TENA KWA KASI HII? Mimi sikusikia mahali Magufuli alipokataza chanjo isipokuwa serikali
kujiridhisha kwanza na usalama wake jambo ambalo leo kweli limetekelezwa, rejea
makala hiyo utafahamu ukweli wa mambo ulivyo.
Siku hizi kutokana na
karibu kila mtu mwenye simu ya mkononi na akaunti ya mtandao wa kijamii kuwa
“mwandishi wa habari”, kutofautisha taarifa potofu na zile za ukweli limekuwa
ni jambo gumu hasa kwa watu wa kawaida wasiokuwa na taaluma ya uanahabari.
Na taarifa potofu
zisizokuwa na uthibitisho wowote huwa zinazidi kupata nguvu kwa wananchi wa
kawaida pale zinaposhadidiwa na baadhi ya watu kwenye jamii ambao kutokana na
dhamana au nyadhifa fulani walizonazo, wanaaminika kirahisi na kwa kiasi
kikubwa na makundi makubwa ya watu. Watu hao wanaweza wakawa Wanasiasa wenye
ushawishi, viongozi wa dini(dini zote kuu, Uislamu, Ukristo, na Dini za
kienyeji), Wasanii na Wanamichezo.
Watu hao maarufu
wanaweza wakapotosha jambo si kama hawajui kuwa wanapotosha hapana, wanajua
fika lakini wanafanya hivyo kutokana na maslahi fulani ambayo wanajua kabisa
wafuasi wao au wale wanaowashabikia wakiujua ukweli basi kwa namna moja ama
nyingine wanaweza wakapunguza ufuasi au kiwango cha kuwaamini kutokana na
sababu kwamba msingi mkuu wa ufuasi wao umesimama katika taarifa au mambo
potofu waliyowahi kuwaaminisha hapo kabla.
SOMA: Puuza Imani na dhana hizi potofu ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula
Kwa mfano kiongozi wa
dini ambaye wafuasi wake wengi amewapata kwa njia za kuwahadaa na miujiza
mbalimbali feki mfano uwezo wa kutibu, kufufua wafu, misukule nk. kiongozi kama
huyo katu hawezi kukubali wafuasi wake waambiwe ukweli katika jambo lolote
ambalo ameshawaaminisha kuwa yeye ana uwezo wa kulitatua.
Baadhi ya viongozi wa
dini kwenye janga kama hili la korona hutafuta kila aina ya fursa ya kunufaika
nalo, na kwa sababu korona ni ugonjwa hatari unaoua haraka hamna namna mhubiri
au mganga wa jadi anaweza akapata nafasi ya kuwahadaa waumini wake kuwa ana
uwezo wowote wa kusaidia, kinachobakia sasa unakuta mtu anaanza kutapatapa,
mara ..ooo… chancho haifai, …..chanjo ya corona ina madhara makubwa…, masuala
sijui ya namba 666…, sijui vinasaba vya mwili kubadilika….. na mambo kibao
yanayofanana na hayo yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Ndio maana utakuta
sasa hivi kuna wimbi kubwa la watu kama hao wanaojitangaza kuponyesha ukimwi na
magojwa hatari kama kansa na kisukari kwa kuwa wanajua fika magojwa haya kwanza
mgojwa hawezi kufa mara moja na kuna dawa za kufubaza nk. Wewe subiri korona
chanjo ifanye kazi vizuri, utawaona tu wajanja hawa wakiibuka na kuanza
kujitangaza kuwa hata korona wanatibu wakitumia mgongo na fursa ya ugonjwa huo
kupunguzwa makali na chanjo, utasikia tu shuhuda kibao watu wakidai oo…, “mimi niliugua korona lakini baada ya kuja
kwa nabii/mtaalamu/ustaath/mganga/mtume/ Askofu fulani. sasa nimepona kabisa”
SOMA: Jinsi ya kutambua na kuacha fikra hasi ulizonazo juu ya pesa zinazokurudisha nyuma usifanikiwe
Kwa hiyo ukiona
kiongozi au mtu mwenye ushawishi katika jamii akitumia nguvu nyingi sana
kupinga jambo la kisayansi kama hili la chanjo ya korona bila ya kuonyesha njia
yeyote ile mbadala ya kukabiliana nalo zaidi ya kudai watu wamtegemee Mungu
peke yake, malimao na kufukiza wakati Mungu mwenyewe ndiye aliyeweka wataalamu
ili wawatibu watu wake, basi ujue kiongozi au mtu huyo anacho hofia ni hatima
yake(legitimacy) Anajua fika watu
aliozowea kuwaaminisha kuwa yeye ndiye dawa ya matatizo yao yote sasa
watamdharau baada ya kuona kwenye korona hawezi kuwakinga wala hawezi tena
kutengeneza shuhuda za uwongo kuwahadaa.
Ni nani atakayekubali
tena kuwa Nabii/Askofu/Mganga/Shehe/Padre au Mtume anaweza kuondoa korona
ilihali chanjo tayari imeshakubalika ndiyo suluhisho la korona? Baadhi yao hata
wamefikia hatua ya kuchukua nafasi ya ukuu wa Mungu kwa mfano utasikia baadhi
ya waumini au wafuasi wakitaja maneno kama vile, “Mungu wa Nabii/Mtume/Askofu
fulani” wakiwa na maana kwamba kiongozi wao huyo anaye Mungu wake spesho
tofauti na Mungu yule wa watu wote aliyeumba kila kitu.
SOMA: Dhana potofu ya ushirikina ni hatari kushinda ushirikina wenyewe
Kwa hali kama hii
utagundua kabisa kwamba kiasi kiongozi huyu alivyowakamata wafuasi wake(brainwash) kwa kauli mbalimbali za
kizushi hawawezi kuchomoka hata kidogo pindi atakapowaagiza jambo lolote lile
hata kama liwe ni la hatari na la kuwaangamiza kama alivyofanya Kibwetere kule
Uganda.
Umefika wakati sasa
watu makini kuwaeleza ukweli watu hawa ambao wengine wanajificha kwenye koti la
Dini au Utumishi wa Mungu huku wakiwatisha wale wanaowaeleza ukweli eti
watapata laana ya Mungu kwani wanakufuru. Na Wafuasi wengi kweli wanakubaliana
nao kwa kuwa Imani huwa hazina kawaida ya kuhojiwa. Ukihoji unaambiwa wewe
utaishia motoni, utapata laana, utakufa, nk. Hebu jiulize mbona hao viongozi na
wao pia huwa wanakufa na kupata matatizo sawa tu na watu wengine wa kawaida?
Uvumi na taarifa
zenye utata(Conspiracies) nchi hii,
nyingi huwa zinaanzia kwenye imani mbalimbali,
za kidini na hata za kijadi pia. Simaanishi ni imani hizo kwa ujumla
wake hapana bali baadhi tu ya vikundi au madhehebu machache. Kwa mfano
madhehebu mengi ya dini wanaendesha mambo yao kwa kuzingatia ukweli pasipo
mambo ya kuhadaa hadaa waumini. Kinachofanya baadhi watumie mbinu chafu za udanganyifu
ni suala zima la kutaka wafuasi wengi. Hakuna tofauti na biashara, ili dhehebu,
kikundi, au mganga apate wafuasi, kunahitajika mbinu mbalimbali za kimasoko
zikiwemo na hizo mbinu feki.
Mbinu
kubwa inayotumika
Motivational
Speeches(Kauli za kushawishi), hapa ieleweke sipigi vita motivational Speakers
kwani na mimi pia nimo katika kundi hilohilo kama Motivational writer(mwandishi
mshawishi). Kushawishi siyo jambo baya hata kidogo lakini jambo hili
linapotumiwa vibaya kama vile kwenye masuala ya kitaaluma kama vile utabibu, sheria
na uandishi habari, linaweza likaleta madhara makubwa na ndio maana utakuta
katika taaluma nyingi wamezuia sana maswala haya ya kushawishishawishi ovyo au
kujitangaza kwa kuwa wanafahamu fika madhara yake.
SOMA: Je, biashara ya kilimo cha matikitimaji ni hadithi zilezile za mayai ya kware, sungura na kuku?
Kwa mfano hata kwenye
uandishi wa habari ni tofauti sana na uandishi wa kawaida wa kushawishi,
wenyewe msingi wake upo katika ukweli zaidi(facts) kuliko utiaji chumvi na
ushawishi.
Sasa wahubiri wengi
na watu wenye ushawishi kwenye jamii hupata wafuasi wao kwa njia hii ya
ushawishi pasipo kuzingatia kile wanachoshawishi kama kina ukweli kiasi gani.
Imani iwe na ukweli au isiwe haijalishi, ilimradi imeshaitwa ni imani na haina
madhara ya moja kwa moja kwa watu.
Mambo yahusuyo imani
mtu usipokuwa makini unaweza ukajikuta unayumbishwa kama kishada, badala ya
kumwabudu na kumsujudia Mungu asiyekuwa na mfano utajikuta ukiwasujudia
binadamu wenzako waliozaliwa kama wewe, wenye shida kama za kwako na
watakaokufa kama wewe, kisa tu wenzako hao ni motivational speakers wanaojua
kushawishi na kutumia mbimu mbalimbali za kimasoko kukuhadaa na kukuchota
kisaikolojia kwa maslahi yao wenyewe binafsi ya kiuchumi, kijamii au kisiasa.
Chanjo ya corona
Uingereza, Marekani na nchi nyingine mbalimbali imeonyesha mafanikio makubwa,
wanaokufa kwa korona katika Mataifa hayo sasa hivi ni wale tu ambao bado
hawajachanja aidha kwa ukaidi kama huu tunaoushuhudia hapa Tanzania au tu
pengine kwa kutokufikiwa na vyombo husika vinavyohusika na chanjo hizo.
SOMA: Kwanini chanjo ya malaria imekuwa ngumu hivyokupatikana?
Akikuhubiria mtu
yeyote eti chanjo ya covid-19 haifai inaua naomba umfungulie habari ya muumini huyu wa dhehebu fulani la dini aliyekuwa akipinga sana chanjo ya korona lakini akaja kujutia
ukaidi wake dakika za mwisho alipokuwa akipigania uhai wake kwenye mtungi wa
gesi ya oksijeni dakika chache kabla hajakata roho kwa covid-19 huku akiwaomba
wafuasi wake kumuombea apone bila mafanikio.
Tanzania imepokea
chanjo zipatazo milioni moja aina ya Johnson, taarifa kuhusu korona duniani
zinasema kwamba kuna aina nyinginezo za chanjo mbali na Johnson Jansen kama
vile chanjo za Pfizer, Moderna,
Novavax, Sinovac, AstraZeneca,
Wataalamu
wanapendekeza chanjo hizi kwa mtu yeyote wa umri juu ya miaka 12 na
wanasisitiza kwamba aina bora zaidi ya chanjo kwa mtu ni ile inayopatikana
kwake kwa wakati muafaka, usije eti ukakaa ukisubiria aina fulani ya chanjo
ambayo bado haijafika ulipo kwani aina zote zilizoidhinishwa na Shirika la WHO
zote ni salama, zilizo na ufanisi wa kukabiliana na aina mpya ya virusi vya
corona (Delta variant) na
zinazopunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuugua corona ile kali inayoweza
kuondoa uhai wako.
"Chanjo" yangu binafsi, haikupendekezwa na WHO wala Wizara ya Afya lakini inafanya kazi pia
Leo hii Kuna dawa
moja kubwa sana nitakayoipendekeza kwako kama kinga ya kukuzuia usiyumbishwe
wala kubabaishwa na wajanja wanaotumia vivuli vya imani mbalimbali ziwe za kidini
au zile za kijadi. Dawa hiyo ni maarifa sahihi ya kujitambua, Kujitambuni ni
kinga ya magojwa mengi hata zaidi ya corona, na maarifa sahihi unaweza ukayapata
mahali popote na kwa mtu yeyote lakini napendekeza kuyapata kutoka katika
kitabu kimoja mashuhuri kiitwacho THINK AND GROW RICH (FIKIRI NA UTAJIRIKE)
SOMA: Jinsi ya kununua kitabu cha Think & Grow Rich-swahili edition katika mtandao wa Getvalue
Kitabu hiki kina sura
maalumu ya IMANI, hapa utajifunza jinsi imani mbalimbali duniani zinavyofanya
kazi kuanzia dini zote kubwa mpaka zile za kienyeji, athari zake na namna mtu
unatakiwa kuzichukulia. Imani hasa za dini zile rasmi zina mambo mazuri sana
zikitumika vizuri kama waanzilishi wake walivyokusudia, lakini zinapotumiwa
kinyume chake hazina tofauti na bomu la nyuklia.
……………………….
JINSI
YA KUKIPATA KITABU HIKI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
NAKALA YA KITABU HALISI CHA KARATASI (HARDCOPY)
Bei yake ni sh. elfu 20 na tuna huduma ya
kukuletea ulipo(Delivery) ikiwa upo Dar es salaam ila gharama ya daladala sh. Elfu
mbili huongezeka.
Mikoani, mkoa wowote
Tanzania Bara na Zanzibar tunatuma kwa njia ya basi au boti lakini pia gharama
za usafiri zitaongezeka na hutegemea aina ya basi lakini mara nyingi huwa ni
sh. Elfu 10.
NAKALA
YA KITABU PEPE (SOFTCOPY)
Unaweza kukinunua
kitabu hiki mara moja(instantly)
kwenye simu-janja yako kupitia mtandao uitwao GETVALUE kwa kupitia kiungo/link ifuatayo hapo chini, lakini kabla
hujanunua ni vizuri kwanza ukapitia kidogo video hii inayoelezea jinsi ya kununua kitabu kutoka mtandao wa Getvalue.
THINK & GROW
RICH-SWAHILI EDITION 2021(TAFSIRI ORIJINO YA MWAKA 1937 NA NAPOLEON HILL)
Bei ya nakala tete ni
shilingi elfu kumi na tano (15,000/=)
KWA MAWASILIANO YA SIMU AU WATSAP TUMIA NAMBA HIZI: 0765553030 au 0712202244
0 Response to "CHANJO YA COVID-19 ALIYOCHANJA RAIS SAMIA SULUHU ETI SIYO YA KWELI ILIKUWA FEKI?"
Post a Comment