Bila shaka duniani hakuna
mtu ambaye hajawahi kukumbana na tatizo la kifedha angalau mara moja. Lakini unafikiria ingelikuwaje
ikiwa matatizo hayo yasingelikuwa na mwisho na hata ujaribu vipi kuyatatua
huwezi kurekebisha chochote? Basi leo katika somo letu hili tunakwenda kupata
majibu ya maswali hayo lakini katika mtizamo wa kisaikolojia zaidi.
Saikolojia ya pesa ni moja
kati ya matawi ya saikolojia inayoshughulika na tabia za watu kwenye fedha
pamoja na athari za fedha kwenye haiba ya mtu. Tawi hili lina uhusiano wa
karibu na uchumi.
SOMA: Kuvalia vizuri huongeza kipato
Saikolojia ya pesa itadumu
katika maisha yetu muda wote ilimradi tu kuna mzunguko wa fedha miongoni mwa
jamii inayozunguka na pia kuna kipimo cha fedha katika kila huduma na bidhaa
zinazozalishwa. Fedha na binadamu ni vitu viwili vinavyotegemeana na hakuna
kimoja kati yake kinachoweza kujidai kuishi bila mwenzake. Pesa bila ya
binadamu ni makaratasi matupu yasiyo na thamani yeyote ile na binadamu naye
bila pesa hawezi kujenga mahusiano yake ya kawaida ya kibiashara na binadamu
wenzake.
Je, inawezekana kwa kiasi
fulani kufahamu chanzo cha matatizo ya kifedha na kwa kiasi fulani kuweza kuyatatua?
Kitu kikubwa tunachojifunza
kwenye saikolojia ya pesa ni tabia ya binadamu kwenye fedha, kila mtu
huichukulia pesa tofauti na mwenzake na kila mtu anaweza akaielezea pesa kwa
namna tofauti anavyoichukulia mwenyewe. Mzunguko wa fedha kwa mtu yeyote yule
unategemea uwepo kwa kiasi fulani cha uwajibikaji hasahasa katika eneo la elimu
ya fedha. Pasipo kujifunza vizuri jinsi ya kusimamia mtiririko wa fedha na mali
zako ni vigumu sana kuviondoa vyanzo vya matatizo ya kifedha. Pesa zinahitaji
uwajibikaji, utulivu, usimamizi na uthibiti. Lakini mambo hayo yote mtu huwezi
kuyatekeleza ikiwa kama hujajijengea aina fulanifulani ya tabia.
Ni tabia zipi unazozihitaji
ili kutokomeza matatizo ya kifedha na uwe mtu uliyefanikiwa?
Unahitaji kuishi tabia za
kitajiri lakini pia usije ukasahau, kila mtu anao uelewa wake mwenyewe kwenye
dhana nzima ya Mafanikio sawasawa na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya pesa kama
tulivyoona hapo juu. Kwa baadhi ya watu kuwa na milioni kadhaa kwenye akaunti
ya benki kwao ndio kilele chao cha mafanikio, Wengine kilele cha mafanikio kipo katika maendeleo yao ya
kiroho.
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi
Hivyo usijilinganishe na
watu wengine linapokuja suala la
mafanikio. Isitoshe wala hatuwezi kujua kwa yakini ni njia ipi ya maisha mtu aliyopitia katika kufanikisha hili au lile maishani.
Fuata ndoto zako, malengo yako na katu usiige malengo na ndoto za mtu mwingine
huku ukidumisha tabia zote za kitajiri tunazokwenda kujifunza leo kwa matokeo
bora zaidi. Iga tabia zao lakini siyo njia walizotumia kutajirika utapotea.
Tabia ndiyo kila kitu kwenye mafanikio ya jambo lolote lile maishani.
Kuna ukweli watu
waliofanikiwa kifedha wana fikra tofauti – zile zijulikanazo kama tabia za
kitajiri?
Ukweli upo asilimia 100%,
ingawa mitazamo ya watu kwenye pesa na namna wanavyofikiri juu yake ni tofauti
sana. Na mara nyingi fikra na tabia hizi zinaweza kurithishwa katika familia
kutoka kizazi kimoja hadi kingine, Ni muhimu kutambua kwamba kila mtu yuko peke
yake na kile kinachofanya kazi vizuri kwa mtu mmoja kinaweza kisifanye vizuri
kwa mwingine. Ni ukweli kuna tabia za kitajiri ambazo mtu yeyote yule akiamua
kuziishi na kuziweka katika vitendo hamna shaka yeyote kwamba siku moja atapata
utajiri, mafanikio na furaha maishani. Mtu unapofanikiwa kuzifahamu tabia za
kitajirii ni nusu ya kuigundua kanuni kuu ya kupata mafanikio ya kifedha.
SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unazotaka maishani
Baba wa vitabu vyote vya
mafanikio duniani, THINK & GROW RICH katika sehemu mbalimbali za kitabu
hicho mashuhuri zaidi mwandishi wake Napoleon hill amezitaja tabia zote za
kitajiri na katika makala hii ya leo pamoja na kwamba nitakutajia baadhi ya
tabia za kitajiri(kama 12 zile muhimu zaidi) lakini pia nitakutajia
kurasa ambazo unaweza kujifunza kwa kina zaidi tabia nyinginezo. Nitatumia
kitabu hicho katika toleo la Kiswahili sanifu la mwaka 2021 lakini kikiwa ni
tafsiri orijino ya lile toleo mama la mwaka 1937 lililoandikwa na Napoleon Hill
mwenyewe.
Ingawa tabia za kitajiri
zipo, lakini kwa kweli ni lazima tabia hizo ziende sambamba na mpango mzuri na
usimamizi thabiti wa fedha zako. Tabia hizo mtu yeyote yule anaweza akajifunza
na kuzifanyia kazi kama nilivyotangulia kusema pia kwamba zinaweza
zikarithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kama wafanyavyo baadhi
ya makabila.
SOMA: Ili ufanikiwe kuwa tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi nne (4)
Watu wengi tunaposikia kuna
tabia za kitajiri ambazo mtu ukiziishi kila siku hatimaye unapata utajiri, mafanikio na furaha
tunaweza tukadhani labda ni tabia ngeni kabisa ambazo sisi ndio mara yetu ya
kwanza kabisa kuzisikia masikioni. Mimi kwa mfano ni mpaka baada ya kukisoma
vizuri kitabu cha Think and Grow Rich(Fikiri na Utajirike) ndipo nilipogundua
kumbe tabia zenyewe ni zilezile za kawaida tunazohimizwa hata katika maisha tu
ya kawaida tuziishi.
Tabia na mienendo yote
inayosaidia mtu kupata pesa, kuzisimamia fedha zake vizuri hasa katika upande
wa matumizi, kuweka akiba na uwekezaji kwenye miradi ya faida zinaingia katika
kundi la tabia za kitajiri. Tabia tunazozizungumzia hapa ni tabia zote nzuri
zinazosaidia mtu kupata epesa, kuzisimamia na hatimaye kumfikisha kwenye uhuru
kamili wa kifedha.
SOMA: Utajuaje kama umeufikia uhuru kamili wa kifedha? Kanuni hii hapa
Kuingia kwenye matatizo ya
kifedha siyo mwisho wa dunia na wala usikatishe uhai wako bure, ipo njia
unaweza kutoka kwa kubadili tabia kutoka zile zinazokuzuia usipate pesa kwenda
zile zinazokupeleka kwenye kupata pesa kama hizi tutakazoelezea hapa
Sitapoteza muda mwingi zaidi
hebu kwanza nizitaje moja baada ya nyingine;
1.
Haiba nzuri
Utaniambia haiba inahusiana
vipi na kupata pesa?
Haiba nzuri(muonekano
nadhifu )-kama tabia niliyochagua ya kwanza kabisa miongoni mwa nyinginezo
nyingi, ndiyo inayoamua mwajiriwa alipwe kiasi gani, mfanyabiashara alipwe
kiasi gani nk. Haiba njema maana yake ni pana na inajumuisha vitu vingi ndani
yake na wala siyo muonekano tu, hata vaa yako, namna unavyowasiliana na watu,
ongea yako, ‘body language’ nk. vyote huingia katika haiba yako.
Motivational speakers na
writers wengi wanatilia sana mkazo tabia hii kwamba
ndio msingi mkubwa wa mtu kufanikiwa. Huwezi kumuuzia mtu kitu kirahisi ikiwa
huna haiba nzuri kama wasemavyo wazungu, “First
impression matters!” Ndani ya Fikiri na Utajirike haiba imezungumziwa
mahali pengi ikiwemo uk. 96 sura ya Tatu “IMANI”........................................
...................
Somo hili kamili unaweza kulidownload ndani ya Channel ya MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE pamoja na masomo mengine adimu ya fedha zaidi ya 70 yasiyopatikana mahali kwingine kokote. Kujiunga na group, lipia kiingilio cha mwaka mzima(miezi 12 tokea siku ya kujiunga) sh. 10,000/= tu kisha tuma ujumbe ukisema; niunganishe na mastermind group-2021" Nitakuunganisha na group na channel pia kukutumia vitabu na michanganuo huku ukipata masomo mapya na semina kwa miezi yote 12 bila ya gharama za ziada au zilizojificha.
0 Response to "JE, IPO KANUNI YA MAFANIKIO YA KIFEDHA?: MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA"
Post a Comment