Kabla ya kuanza somo letu la leo rasmi, kwanza nikushukuru kwa kusoma blogu hii, mahali sahihi ambapo siku zote umekuwa na utaendelea kupata makala adimu zinazohusu fedha kwa mapana yake.
Elimu
ya fedha na umuhimu wake limekuwa ni jambo lisiloweza kukwepeka kwa mtu yeyote
yule anayetafuta mafanikio ya kimaisha kwenye Dunia hii ya karne ya 21. Pamoja
na makala tunazoandika hapa kwenye blogu hii, pia ukipenda kupata elimu ya
fedha ile ‘cream’ kwa kina zaidi, basi karibu ujiunge na familia yetu Group na
Channel ya Michanganuo-online.(MASTERMIND GROUP 2021) Kila siku jioni tunakuwa na masomo ya
kipekee(exclusive) yasiyoweza kupatikana mahali kwingine kokote!
Kujiunga
tuwasiliane kwa watsap namba, 0765553030 au 0712202244, tuna maktaba ya masomo
zaidi ya 100 ya siku za nyuma na kila siku tunajifunza somo jipya la kipekee.
Yamkini
wewe ndio kwanza unaanza safari yako ya kifedha, au labda tayari ulishaianza
kitambo lakini bado hujafanikiwa kuufikia ule uhuru wa kifedha unaotamaniwa na
karibu kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke.
Lengo kubwa la kila mtu akiwa hai ni siku moja hatimaye kuja kumiliki
rasilimali(assets) za kutosha zenye uwezo wa kuzalisha au kutengeneza kipato
ambacho kitakuwa chanzo cha pesa za kulipia gharama zote za maisha.
SOMA: Utajuaje kama umeufikia uhuru kamili wa kifedha?
Je
na wewe pia unayo ndoto hii? Basi hapa chini
leo nimekuandalia falsafa 7 ambazo zimejaribiwa na kufanyiwa kazi kwa
miaka mingi na watu mbalimbali waliofanikiwa kifedha miaka na miaka huko nyuma
lakini mpaka hivi leo na hata siku zijazo. Ni imani yangu zitakusaidia katika
safari yako ya kifedha kama na mimi pia zinavyoendelea kunisaidia.
1.
Weka Malengo
Umekuwa
kila mara ukisikia maneno haya, “weka malengo….weka malengo…..weka malengo….”
na naamini mpaka sasa hivi pengine umeshachoka nayo na hutaki tena kuyasikia
lakini nakupa moyo usichoke, endelea tu kuyasikia ila kitu cha muhimu zaidi
lifanyie kazi na ipo siku utakuja kuyakumbuka haya maneno yangu.
Kabla
hujajiwekea malengo yeyote unapaswa kwanza kuwa na maono ya kile unachokitaka,
(Katika kitabu changu kimoja kiitwacho,
MIFEREJI 7 YA PESA, nimeainisha Malengo, Dhamira, Maono, Dira na Ndoto kwa kina
sana) kwanini unakitaka kitu hicho na ni lini unakitaka. Ni vigumu kufikia
mafanikio yeyote ikiwa kama hutobainisha mafanikio hayo kwa uwazi.
SOMA: Kanuni kuu ya mafaniki Duniani iliyo kubwa kuliko zote
Kwa
mujibu wa kitabu hicho amini katika kuweka malengo yako ukizingatia kanuni
iitwayo kwa kimombo S.M.A.R.T au kwa kiswahili tunaweza kuiita isivyorasmi “Ma.Pi.Fi.Fa.Mu”
kwa kirefu malengo yanapaswa yawe; Maalumu,
yawe yana Pimika, yawe yana Fikika, yanayoFaa na yenye Muda
maalumu wa utekelezaji;
S: Specific,
M: Measurable
A: Attainable/Relevant
T:
Time based
Kwa
mfano ikiwa una lengo la kupunguza deni unalodaiwa, badala tu ya kusema
utapunguza deni, sema ni kiasi gani hasa unachotaka kupunguza, lini na pia ni
kiasi gai unataka upunguze kwa siku, kwa mwezi na hata kwa mwaka ili kuweza
kumaliza deni lote unalodaiwa katika muda ule uliojiwekea katika lengo lako.
Au
inawezekana labda wewe lengo lako ni kujiwekea akiba ya fedha za kutosha
kununulia kiwanja kwa ajili ya kujenga nyumba ya kuishi au hata ya kupangisha
wapangaji wakuletee kodi kila mwisho wa mwezi. Hakuna ubaya wa kuwa na lengo
kama hilo lakini je, lengo lako hilo ni S.M.A.R.T? Unahitaji pesa kiasi gani
hasa? Ni lini na siku gani utazihitaji? Ni mabadiliko yapi uliyo tayari
kuyafanya kusudi uweze kulitimiza lengo lako hili?
2.
Fanya Ufuatiliaji.
Ikiwa
unataka mafanikio kwenye jambo lolote lile maishani, fanya ufuatailiaji! Ni
hivi, huwezi kujua ni wapi unakokwenda ikiwa hujui pale ulipo sasa. Mara
utakapokuwa umejiwekea lengo lako, fuatilia maendeleo yake na uyapime kulingana
na malengo MA.PI.FI.FA.MU (S.M.A.R.T) Kwenye jambo hili unatakiwa kutafuta njia
utakayoweza kuitumia kujua hasa umepunguza deni kiasi gani, ni kiasi gani
kilichosalia, umepunguza matumizi yako kiasi gani? Ni kiasi gani kimeongezeka
katika thamani ya mali zako unazozimiliki na ni kiasi gani pia mapato
yatokanayo na vitegauchumi vyako yameongezeka.
Mfano
mzuri ni pale mtu anapotunza kila rekodi ya miamala anayoifanya katika kitabu
ama daftari lake la mahesabu. Ikiwa hutafuatilia mahesabu yako ya fedha unaweza
siku moja ukaja kupata mshangao mkubwa pale utakapokuja kuamua kufuatilia.
Ikiwa unataka kuweka akiba, huna budi kwanza kufahamu matumizi yako ya kila
siku. Na ikiwa pia utataka kukuza mali zako ni lazima kila mwezi ufahamu ni
kiasi gani zimeongezeka.
3.
Fanya uwekaji Akiba kuwa Kipaumbele chako cha Kwanza
Kuweka akiba ndiyo njia ya kweli na ya uhakika
ya kutengeneza utajiri iliyofanyiwa majaribio na kutumiwa na watu wengi
duniani. Utamsikia kila mtu akisema lake, wengine watakuambia uweke akiba asilimia 10% ya mapato yako,
wengine asilimia 20% nk. Lakini kiukweli ikiwa utataka kujenga utajiri haraka
unaweza kuweka akiba hata asilimia zaidi ya 50% ikiwa mazingira yataruhusu.
4.
Lipa Madeni Unayodaiwa
Umeshaweka
akiba yako, sasa utaifanyia kitu gani? Ikiwa unayo madeni ni jambo zuri
ukayapunguza au kuyalipa yote kwanza. Haijawahi kutokea hata siku moja mtu
akatajirika angali ana madeni mabaya. Ukiwa na deni hutofautiani na mtu
aliyetia nanga ufukweni mwa bahari na wakati huohuo akitarajia kushinda mbio za
majahazi. Deni ni kizingiti kwenye safari yako ya kifedha. Anza kulipa madeni
yale yaliyokuwa na riba kubwa kwanza na ikiwezekaha hata yalipe yote ili uanze
freshi/upya.
5.
Wekeza pesa zako.
Na sasa umeshamaliza kulipa madeni yako yote,
unaweza ukasheherekea kidogo, lakini kumbuka huu ndio muda muafaka wa wewe
kufanya biashara na ongezeko la fedha zile ulizokuwa ukitumia kulipa madeni.
Ikiwa kama kweli upo makini(serious) kujijengea utajiri unatakiwa kununua
vitegauchumi vile vilivyo na tabia ya kuongezeka thamani kadiri muda unavyopita
mfano ardhi, hisa za makampuni nk. na wala siyo vitegauchumi vile vinavyopungua
thamani kama vile gari, TV na Simu. Kitegauchumi kinachoongezeka thamani
chaweza pia kikawa ni biashara yeyote ile ilimradi tu iwe ni biashara
inayoingiza faida na siyo hasara.
SOMA: Wanaofanikiwa maishani wengi husema 'no'(hapana) kwa vitu hivi vitatu 3
Jitahidi
sana kuwekeza katika miradi isiyokuwa na hatari kubwa hasa ikiwa wewe ni
mwajiriwa usiyekuwa na muda mwingi wa kufuatilia vitegauchumi vyako au
uwekezaji.
6.
Tengeneza Kipato Zaidi.
Tayari uneshajiwekea malengo,Umefuatilia
malengo yako zikiwemo na hesabu za fedha zako vizuri, umeweka akiba asilimia
kubwa ya kutosha katika mapato yako ya kila siku, umelipa madeni yako na kufanya uwekezaji. Sasa ni nini kitafuata?
Kinachofuata ni kuzidisha mara dufu mzunguko wako wa uwekezaji na kuweka akiba
kwa kuongeza kipato chako.
Ikiwa wewe ni mwajiriwa mahali fulani fikiria ni nini utakachokifanya ili kuongeza thamani katika kampuni uliyopo, mfano kuongeza ujuzi/elimu nk. Kama ni mfanyabishara fikiria utafanya kitu gani kuongeza mauzo yako? Unaweza pia kufikiria kuhusu kufungua biashara ya pembeni zaidi ya ile uliyokuwa nayo au kazi unayofanya.
SOMA; Ujanja Matajiri wanaoutumia kupata pesa kutoka vyanzo vingi vya mapato.
Je, kuna kitu chochote kile una mapenzi nacho na ungependa
kuwashirikisha wengine mfano biashara mbalimbali za kwenye mtandao? Kwa kadri
utakavyojitahidi kwa kasi kuongeza kipato chako kwa njia mbalimbali ndivyo pia utakavyoweza
kuufikia uhuru wako wa kifedha haraka zaidi.
Hitimisho:
Kuna
njia nyingi za kutengeneza Utajiri, lakini mbinu na falsafa nilizozielezea
katika makala hii zimedhibitika kufanya kazi kwa watu wengi waliowahi kupata mafanikio
makubwa. Jambo la msingi tu ni wewe kuchukua hatua ya kwanza.
………………..mwisho…………………
BIDHAA
NA HUDUMA MBALIMBALI TUNAZOTOA
1. Kitabu cha THINK & GROW RICH kwa lugha ya Kiswahili sasa unaweza
kukipata popote pale ulipo. Kwa nakala tete(softcopy) bonyeza kiungo
kifuatacho, THINK & GROW RICH-SWAHILI-EDITION, na kisha fuata maelekezo, ukimaliza kulipia kupitia
mtandao wako wa simu utakidownload kwenye smartphone yako.
Kwa
nakala Ngumu(Hardcopy) kitabu kinapatikana kwa wakala wetu mkuu, Bright Bookshop & Stationery
iliyopo Mbezi-Kimara jirani na Sekondari ya St. Augustine au Kanisa la KKKT Mji
mpya. Unaweza kupitia njia ya Temboni au Kibanda cha Mkaa, Bei ya kitabu ni sh. 25,000/=
Kwa
Dar es salaa tunatoa huduma ya Delivery popote mteja alipo kwa gharama ya sh.
2000/=
Mikoa mingine yote Bara na Zanzibar tunatuma kwa mabasi au boti na gharama zote pamoja na kitabu ni Tsh.35,000/=
2. Vitabu vyetu vingine vyote pia
vinapatikana: MICHANGANUO & UJASIRIAMALI, DUKA LA
REJAREJA na MIFEREJI 7 YA PESA
3. Kujiunga na MASTERMIND Grop
letu la masomo ya fedha kila siku na michanganuo ya biashara zinazolipa
Tanzania katika group la whatsap & Channel ya telegram, lipia kiingilio cha
mwaka mzima sh. Elfu 10 tu kwa namba 0765553030 kisha tuma ujumbe, ‘NIUNGE NA
MASTERMIND GROUP 2021/2022’ kisha
nitakutumia bure vitabu na michanganuo pamoja na kukuadd katika hilo group na
channel ya telegram muda huohuo.
4. Na ile huduma ya kuandikiwa MCHANGANUO
WA BIASHARA(Business Plan) kwa biashara yeyote ile
kitaalamu nayo inapatikana kwa gharama ya asilimia 1% ya mtaji wa biashara
husika, lakini mazungumzo pia yapo.
MAWASILIANO YETU NI: 0765553030 au 0712202244
0 Response to "MAFANIKIO NA UTAJIRI: WATU WENGI UMETOKANA NA FALSAFA HIZI 7 ZA FEDHA "
Post a Comment