Mawili Miongoni mwa matukio makubwa duniani yaliyotokea hivi karibuni ni lile la Ushindi wa Kundi la Talibani nchini Afghanistani lililokuwa likipigana na Muungano wa Majeshi ya NATO yaliyokuwa yakiongozwa na Marekani pamoja na tukio jingine la Ushindi wa Rais Hakainde Hichilema wa nchi ya Zambia aliyemshinda hasimu wake mkuu Rais Edgar Lungu anayeondoka madarakani.
Katika matukio yote haya mawili ingawa
hayana uhusiano wa moja kwa moja lakini kuna jambo moja kubwa sana
linayoyaunganisha. Yakiwa yametokea kwa nasibu ndani ya mwezi mmoja kuna kitu
kikubwa ambacho mtu yeyote yule, (kikundi au taasisi,)mwenye nia au malengo ya
kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani anaweza akajifunza.
Wanamgambo wa
Talibani kwa takribani miaka 20 kwa kutumia silaha duni, bila uwezo mkubwa
kifedha na kiuchumi wamekuwa wakipambana na na Majeshi ya NATO yaliyokuwa na nguvu
nyingi za kiuchumi, silaha, na hata ushawishi duniani kote. Ni kitu gani hicho
hatimaye kilichowasaidia wanamgambo hawa kuiteka nchi nzima ya Afghanistan tena
kwa siku 10 tu bila upinzani wowote toka kwa wapinzani wao NATO na majeshi ya
serikali ya Rais Ashraf Ghani?
SOMA: Muhammad Ali: uvumilivu, nidhamu, ujasiri, msimamo vilimpa ubingwa Kinshasa Zaire
Mwanasiasa Hakainde
Hichilema kwa muda wa miaka zaidi ya 15 amekuwa akiwania urais wa Zambia bila
ya mafanikio. Katika safari yake hiyo ya kusaka mafanikio amepitia kukatishwa
tamaa kwingi, changamoto za kila namna ikiwemo hata kubambikiwa kesi ya ugaidi
ambayo maana yake ni uhaini na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ingeliweza kuwa
adhabu ya kifo. Lakini licha ya misukosuko yote hiyo aliendelea tu kuwa
king’ang’anizi na uvumilivu wa hali ya juu bila ya kukata tamaa mpaka leo hii
ambapo amefanikiwa kufikia malengo yake ya kushika uraisi wa Taifa la Zambia.
Ukiwa na MSIMAMO “huwezi kudanganyika hata kwa mbegu za mtama”
Wamarekani walijaribu kuwahadaa Watalenani kwa kila njia ikiwemo hata kuahidi
kushea madaraka na serikali ya Kabul lakini katu hawakutetereka wala kulegeza
msimamo wao. Msimamo ni lazima uambatane na lengo kamili ambalo walikuwa nalo
tayari, lengo la kusimamisha utawala au serikali yao inayofutata Sharia za Kiislamu (Islamic Emirate of Afghanstan). Lengo kamili ni lazima pia
liambatane na mipango ya kivitendo itakayotekelezwa kulifikia lengo, na
Talibani utaona walikuwa na mikakati kadhaa ikiwemo mapambano na serikali na
majeshi ya NATO na propaganda mbalimbali zilizosaidia Jamii ya Waafghanistan
kuichukia serikali yao iliyokuwa imejaa vitendo vya rushwa na ufisadi
NATO: Rais Obama kila mtu anatakiwa apewe nafasi ya kurekebisha maisha yake
Ijapokuwa ushindi wa
Taliban kwa wengi unaweza usiwe ni jambo la kufurahisha hasa ukizingatia
historia na itikadi waliyo nayo dhidi ya haki za binadamu hususani wanawake na
watoto, lakini ukweli unabakia palepale kwamba ni kielelezo kizuri cha kuwa na MSIMAMO
katika mapambano ya kufikia lengo lolote lile maishani.
Aidha ushindi wa
Taliban siyo dalili njema hata kidogo kwa Dunia na hasa Afrika kunakoonekana
kuibuka kwa makundi ya kijihadi yaliyo na muelekeo na Itikadi za Al-Qaeda,
ISS(Dola la Kiislamu) na makundi mengine ya misimamo mikali kama Boko haram
Nigeria, Al-Shaababu kule Somalia na hata hapa jirani Msumbiji.
SOMA: Maziwa na asali vya Gadafi, Mubarak na Sadam Hussein vipo wapi?
Bila shaka makundi
haya yatapata motisha, nguvu na ari mpya baada ya kuona kumbe kwa MSIMAMO
kila kitu kinawezekana chini ya jua haijalishi ni muda gani utapita.
Hili laweza kugeuka janga na silaha moja hatari sana. Ni tishio kubwa
linaloinyemelea Dunia hasa Afrika ukanda wa Sahel
Silaha hii ya MSIMAMO
hakuna mahali popote imewahi kushindwa. Inapotumiwa kwa usahihi adui utamwona
akifunga virago vyake mwenyewe mithili ya NATO na Marekani kule Afghanistani au
Edgar Lungu wa Zambia alivyosalimu amri kwa hasimu wake Hichilema pasipo hata
kwenda mahakamani kupinga ushindi kama ilivyo kwa Wanasiasa wengi wa Afrika
wanaposhindwa chaguzi.
SOMA: Kati ya Obama na Putin ni nani anayeisaidia IS?
Hata katika mapambano
ya kawaida ya kusaka mafanikio kiuchumi na kimaisha kwa ujumla, silaha hii
inaweza ikatumika na kufanya maajabu! Katika kitabu mashuhuri cha THINK AND
GROW RICH silaha ya msimamo imepewa sura nzima ya 9. Unaweza kushangaa sana
busara hizi zilizoandikwa miaka mingi huko nyuma lakini leo hii zinafanya kazi
utadhani zimeandikwa jana tu.
Ukisoma ndani ya
kitabu hiki namna vile MSIMAMO ulivyo na nguvu katika
kufanikisha mambo unaweza kujilaumu sana nikwanini hukukisoma kitabu hiki pale
tu ulipoanza kujua kusoma na kuandika, leo hii usingekuwa pale ulipo.
Nimeweka nukuu chache
tu za baadhi ya aya za sura hiyo ya 9 hapa chini;
“MSIMAMO ni kigezo muhimu katika njia ya kugeuza SHAUKU
kuwa katika kipimo chake cha fedha. Msingi wa msimamo ni NGUVU YA UTASHI”
“Wengi
wa watu wapo tayari kutupilia mbali nia na malengo yao na kukata tamaa katika
dalili za mwanzo za upinzani au mkosi. Wachache huendelea licha ya upinzani
wote mpaka wanafikia lengo lao. Wachache ndio kina Ford, kina Carnegie, kina
Rockfellers na kina Edson.”
“Ikiwa unafuatilia kitabu hiki kwa lengo la kutumia
maarifa kinachotoa, jaribio la kwanza la msimamo
wako litakuja wakati utakapoanza kufuata hatua sita zilizoelezwa katika sura ya
pili. Ikiwa kama wewe siyo mmoja wa wawili kati ya kila watu mia ambaye tayari
una “lengo kamili” ambalo unalilenga
na mpango kamili kwa ajili ya
kulifikia, unaweza kusoma maelekezo na kisha kuendelea na ratiba zako za kila
siku, kamwe usifuate maelekezo hayo.”
“Jihusishe mwenyewe na Kundi la Kushauriana, na
jenga msimamo kupitia juhudi za
ushirikiano wa wanachama wa kundi hili. Utapata maelekezo ya ziada ya kujenga
msimamo katika sura ya 4 juu ya Kujishauri-binafsi na sura ya 12 juu ya Akili
ya ndani.
Fuata maelekezo yaliyotolewa katika hizi Sura mpaka
tabia yako ya asili ikabidhi kwa akili yako ya ndani picha halisi ya kitu
unachotamani. Kutoka hatua hiyo na kuendelea, hautalemazwa tena na ukosefu wa
msimamo.”
“Ni nguvu gani ya kimuujiza hutoa kwa watu wenye MSIMAMO uwezo wa kukabiliana na magumu?
Ubora wa MSIMAMO hutengeneza katika
akili ya mtu aina fulani ya shughuli za kiroho, kiakili, au kikemikali ambazo
humpa uwezo wa kuzifikia nguvu za Kiungu? “
“Je, Nguvu kuu isiyo na mipaka(MUNGU) kawaida
hujitupa yenyewe katika upande wa mtu ambaye bado anaendelea kupambana baada ya
kushindwa vita, huku dunia nzima ikiwa kinyume naye?”
Katika kitabu hicho
cha Think & Grow Rich (FIKIRI NA UTAJIRIKE) tafsiri orijino
kwa kiswahili ya mwaka 2021 Sura ya 9 ya MSIMAMO
inazungumzia maswala mengi wakiwemo watu mbalimbali mashuhuri Duniani
walivyotumia silaha ya MSIMAMO katika kufanikisha malengo yao wakiwemo Mitume,
Manabii na viongozi mbalimbali waliowahi kutokea Duniani mfano akina Mtume
Muhamad, Yesu Kristo, Mahatma Ghandi, Badhi ya wafalme na Marais wa Taifa la
Uingereza, Marekani na wengineo wengi.
SOMA: Je, wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya madogomadogo?
Kitabu cha Think
& Grow Rich ni watu wachache sana wanaoujua ukweli kwamba ndio kitabu cha
kwanza Duniani kilichoandika kwa ukamilifu zaidi kuhusiana na Elimu ya Fedha na
Mafanikio, kinatambulika dunia nzima kwamba ndiyo Baba wa vitabu vingine vyote
vya Mafanikio na ushahidi wa jambo hili utakutana nao kwa karibu kila mwandishi
au mhamasishaji wa elimu ya mafanikio duniani, wote wanakiri na wanakubaliana
na FALSAFA ya NAPOLEON HILL katika kitabu hiki na wengi wao mafundisho yao ni
yaleyale yanayopatikana katika kitabu hiki.
Binafsi wakati fulani
katika harakati za kusoma vitabu mbalimbali niligundua kwamba karibu kila
mwandishi nguli wa Elimu ya mafanikio duniani niliyemsoma anakiri kwa namna
moja au nyingine kwamba moja ya vitabu au watu waliomhamasisha zaidi kwenye
elimu ya fedha na mafanikio alikuwa ni Napoleon Hill na kitabu chake cha Think
& Grow Rich. Sasa nikawa najiuliza hivi:-
“Ikiwa kama kila mwandishi
mashuhuri wa mafanikio duniani anakiri kuhamasishwa na kitabu cha Napoleo Hill
cha Think & Grow Rich kwanini basi nisianze na kitabu hicho kwanza kukisoma
ndipo nisome hivyo vya waandishi wengine?”
Swahi hili ndilo
lililosababisha hatimaye mimi kuanza safari ya kukitafsiri kitabu hiki katika
lugha ya kiswahili kwani baada tu ya kumaliza kukisoma niligundua hazina kubwa
liyokuwa imejificha ndani ya kitabu hiki na ambayo kuna watu wengi walikuwa
wakiikosa kwasababu tu ya kushindwa kuelewa kiingereza sawasawa au kuona kazi
ngumu kusoma kwa lugha wasiyoizowea.
JINSI YA KUKIPATA KITABU CHA THINK AND GROW RICH-SWAHILI EDITION 2021 (FIKIRI & UTAJIRIKE)
KITABU
CHA KARATASI / HARD-COPY
(1)
Dukani(Bright Future Books & Stationery):
Lipo Mbezi Kimara, Kibanda cha Mkaa karibu na St. Augustino Sekondari TAGASTE,
Kituo cha bajaji – KWA MOTA. bei
dukani ni tsh. 20,000/=(Elfu ishirini tu)
(2)
Kuletewa mpaka ulipo: Kama upo Dar es salaam
tunakuletea kwa Tsh. 22.000/=(Elfu 22).
Ukiwa mikoa mingine tunatuma kwa mabasi
kwa Tsh. 30,000/= (Elfu 30)
KITABU
NAKALA-TETE / SOFTY-COPY
1. Kinapatikana
katika mtandao wa GETVALUE kwa anuani(link) ifuatayo ikiwa unatumia Simu ya
Smartphone,
FIKIRI
NA UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION 2021)
VITABU
NA HUDUMA NYINGINE TOKA KWETU
1) Vitabu
vyetu vingine vyote vinapatikana kwa mifumo yote, vya karatasi(hardcopy) lakini
pia Softcopy kupitia Email au Watsap.
2) Vya
karatasi unaweza kufika katika duka lililotajwa hapo juu(BRIGHT FUTURE BOOKS & STATIONERY) au ukawasiliana nasisi
tukakuletea ulipo.
3) Kwa Softcopy
Lipia kitabu husika kisha tutumie anuani yako ya email au namba ya watsap
tutakutumia kitabu/vitabu muda huohu.
Mawasiliano
yetu ni:
Simu
/ Watsap: 0765553030 au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo
KUANDIKIWA
MCHANGANUO/MPANGO WA BIASHARA (BUSINESS
PLAN)
(1) Tunatoa huduma ya kuandika mchanganuo / Mpango mzima wa biashara yeyote ile (Full business plan) kubwa na ndogo kwa gharama nafuu sana. Tunakutumia maswali yanayohusiana na biashara yako unajibu kwa kifupi, na kisha baada ya hapo kazi nyingine unatuachia sisi. Kuona baadhi ya kazi zetu tulizofanya bonyeza hapa
(2)
Tunafanya makisio katika Sehemu/Kipengele cha
Fedha cha Mchanganuo wa Biashara kwa yule ambaye ameshaandika sehemu nyingine
zote lakini kwa kipengele hiki akahitaji usaidizi. Gharama yake ni ndogo kulinganisha
na gharama ya kuandika mchanganuo mzima.
KUJIUNGA
NA GROUP NA CHANNEL YA MICHANGANUO-ONLINE (MASTERMIND-GROUP)
1) Kwa
shilingi elfu 10 (10,000/=) tu kwa mwaka mzima unajiunga na group la watsap
ambalo tunajifunza kila siku Michanganuo ya Biashara mbalimbali zenye ubunifu
kwa mtaji mdogo pamoja na Masomo yenye maudhui ya Fedha. Pia tunakuwa na semina
za mara kwa mara juu ya uandishi wa Michanganuo ya biashara.
Kujiunga na Group Lipia kiingilio chako kupitia namba 0765553030 au 0712202244 kisha tuma ujumbe; "NIUNGANISHE NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO2021"
SIMU: 0712202244
WATSAP: 0765553030
0 Response to "KAMA UNATAFUTA MAFANIKIO KUNA SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA KWA USHINDI WA TALIBANI AFGHANISTAN NA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA"
Post a Comment