Juzi nilisema nitayajibu maswali na changamoto mbalimbali za wasomaji wa blogu hii walioniuliza hivi karibuni na huu ndio muendelezo wa majibu ya changamoto hizo. Msomaji huyu kupitia watsap aliuliza hivi, na nimeweka screenshot ya mawasiliano yangu na yeye pale chini;
(Huwa hatuutaji
utambulisho halisi wa muulizaji-swali pasipo idhini yake rasmi)
SWALI:
Samahani
Mkuu nimeaza biashara yangu ya Mtaji wa shilingi laki 4 nauza mahitaji ya nyumbani
ya kawaida mfano sukari mafuta nyanya na vingine, Changamoto yake nashindwa
kugawa mapato asilimia ngapi niweke kwenye Akiba na asilimia ngapi niweke
kwajili ya kununulia bidhaa zilizopungua dukani kwangu, naombaaaa ushauriii
mkuuu Mungu akubariki sana
MAJIBU:
Njema kabisa Mkuu, Karibu
Kiasi Cha akiba unachotakiwa kuweka kitategemea ni faida
kiasi gani unachoingiza kwenye biashara yako.
Ikiwa utakuwa na uhakika ni faida kiasi fulani unachopata kila siku basi kiasi hicho cha faida ndicho unachopaswa kukigawa kwa ajili ya
kuweka kama akiba na kingine kununulia bidhaa.
SOMA: Biashara ya urembo inalipa, ni ya pili kutoka haraka baada ya chakula, ni fursa kubwa
Hata hivyo pia kwa kuwa naona mtaji ni kidogo (laki 4)
kwa mujibu wa maelezo yako, sifikiri kama ni Jambo la busara kugawa faida na
kuiweka akiba mapema kiasi hicho badala yake nadhani unge’focus’ zaidi katika
kuongezea faida hiyo kwenye mtaji ili kuikuza zaidi biashara yako hii ya duka
la mahitaji ya nyumbani.
Aidha njia ya kufahamu ni faida kiasi gani ya duka lako unayopata kwa siku au kwa mauzo unayouza ni rahisi, tumia moja kati ya njia
hizo mbili hapo chini;
1. Andika
kila bidhaa inayouzika na kisha jioni wakati wa kufunga hesabu ukokotoe kila
bidhaa imechangia faida kiasi gani, kisha tafuta jumla ya faida ya bidhaa zote
zilizouzika kwa siku hiyo.
2. Njia
ya pili unaweza kukokotoa faida ya mauzo ya siku husika kwa kutumia asilimia ya
mauzo. Inafahamika bidhaa nyingi za rejareja huwa na faida wastani wa asilimia
25% mpaka 30% ya mauzo, hivyo chukua mauzo yote ya siku yazidishe mara asilimia
25% au 30% jibu ndio faida uliyopata na
ndipo Sasa unaweza kuamua ugawe kiasi gani hapo kwa ajili ya akiba na siyo
kuweka akiba mtaji wenyewe.
Hesabu hizi haijalishi ni duka la aina gani ilimradi ni
duka au biashara ya kuuza bidhaa za rejareja. Inaweza ikawa unataka kujua faida
ya duka la dawa muhimu, faida ya duka la vipodozi, faida ya duka la nguo, faida
ya duka la simu za rejareja, faida kwenye biahara ya kuuza sambusa nk. ilimradi
tu ni mahesabu ya duka la rejareja au biashara yeyote ile nyingine ya rejareja
unapofunga mahesabu jioni kwani mahesabu ya biashara zote za rejareja mfumo
wake ni uleule mmoja haubadiliki sana.
Asante sana!
………………………………………
Ukiwa na changamoto yeyote fupifupi kama hii unaweza
kuuliza muda wowote ule na nitakujibu haraka bila malipo yeyote.
Kwa maswali mengi zaidi au majibu kwa kina zaidi unaweza
kujiunga na MASTERMIND GROUP LA
MICHANGANUO-ONLINE kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu ada ya mwaka mzima
ambapo unapata na offa ya kitabu cha Michanganuo ya biashara bure.
Huku unaweza kuuliza chochote bila kikomo na unapata
fursa ya ‘kuaccess’ masomo zaidi ya 70 ya fedha pamoja na Michanganuo ya
biashara za kipekee zinazolipa Tanzania.
Kupata Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA kwenye simu au kompyuta lipa sh. 5,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jiana Peter Augustino Tarimo kisha ujumbe wa "NATAKA KITABU CHA DUKA LA REJAREJA" nitakutumia muda huohuo
Kwa kitabu Hardcopy (cha karatasi) utaletewa popote pale ulipo kwa sh. elfu 15, mikoani utaongeza gharama za basi.
WATSAP/CALL:
076555330 au 0712202244
Kwa vitabu zaidi na
Michanganuo mbalimbali ya biashara tembelea duka la mtandaoni, SMARTBOOKSTZ
Peter Tarimo
0 Response to "FAIDA DUKA LA MAHITAJI YA NYUMBANI: NIWEKE AKIBA KIASI GANI CHA MAPATO YA SIKU?"
Post a Comment