Uchambuzi
Kwa kina Sura ya 11 ya kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI
EDITION) – Sehemu ya ii
Mwandishi amezungumzia
ngono kama kichocheo cha akili kati ya vichocheo vingine 9 vya akili ambavyo ni
hivi hapa chini;
1. Ngono
yenyewe (shauku ya mapenzi)
2. Upendo(Mapenzi)
3. Shauku
kali ya Umaarufu, cheo na fedha
4. Muziki
5. Urafiki
wa jinsia moja au wa jinsia tofauti
6. Ushirika
wa Kushauriana(Mastermind group)
7. Maumivu
ya pamoja kama yale wanayopata watu walio katika mateso
8. Kujishauri-binafsi
9. Hofu
10. Dawa
za kulevya na pombe.
Vichocheo nane kati
ya hivi asili yake ni chanya yaani ni vya kujenga wakati vichocheo viwili vya
mwisho ni vya kubomoa au hasi. Shauku ya kujieleza kingono hukaa kileleni
kabisa mwa vichocheo vingine.
Akili ya binadamu kwa
kawaida huwa ina tabia ya kuitikia kwa wepesi vichocheo hivi na kufunguliwa
mpaka kufikia kiasi cha juu kabisa cha mitetemo ijulikanayo kama shauku kali au
Ubunifu wa kujenga / kubomoa kulingana na aina ya kichocheo inachoitikia.
Majaribio ya
kisayansi juu ya historia za wanaume wenye mafanikio makubwa yamebainisha
ukweli ufuatao;
· Wanaume wenye mafanikio makubwa ni wale walio na asili ya mapenzi iliyokomaa vya kutosha au wanaume waliojifunza sanaa ya kugeuza fikra za mapenzi(ngono) kuwa katika vitu vingine vyenye faida. Hapa utaona kwamba wanaume kwa mfano mashoga au wasio na nguvu za kutosha za kiume huwa pia kufanikiwa kwao katika nyanja zingine ni vigumu.
· Wanaume
waliopata utajiri mkubwa na umaarufu kwenye fasihi, sanaa, viwanda, uhandisi na
fani nyinginezo walihamasishwa kutokana na nguvu ama ushawishi wa wapenzi wao /
wake zao.
Shauku ya kujieleza
kimapenzi ni ya asili na na kuzaliwa nayo, huwa haiwezi na haitakiwi
kukandamizwa wala kuzuiwa bali inatakiwa kupewa njia ya kutokea kupitia aina
chanya za kujieleza kimwili, kiroho na kiakili. Vinginevyo yenyewe kwa kutumia
mgeuko au mabadiliko tunayoyazungumzia kwenye hii sura itatafuta njia nyingine
ya kutokea kupitia njia hasi za kimwili zinazoonekana. Haina tofauti na mto wa
maji, hata uujengee bwawa kubwa, utauthibiti kwa muda fulani tu lakini maji ni
maji na itafika muda yatalazimisha njia ya kutokea.
Kuthibitisha ukweli
kwamba mhemko wa ngono ni nguvu isiyozuilika kwa binadamu na ni lazima mtu
akitaka kuizuia lazima atumie sanaa ya kuigeuza kuwa katika nguvu nyingine
chanya mwandishi anatoa mfano wa dume la ngombe au mnyama mwingine yeyote yule
anapohasiwa;
“Haribu matezi ya jinsia iwe ni kwa mwanaume au mnyama na utakuwa
umeondoa chanzo kikubwa cha vitendo” anaendelea kusemakwamba “Ng’ombe dume hugeuka kuwa mpole kama ng’ombe
jike baada ya kubadilishwa jinsia(kuhasiwa)”. Nguvu zote za kupambanandani
yake huondoka. Na mabadiliko ya jinsia ya kike pia yana matokeo sawa.
Katika sura hii
mwandishi ametaja mifano ya wanaume ambao mafanikio yao makubwa ya kushangaza
yanahusishwa moja kwa moja na ushawishi wa wanawake ambao waliamsha vitivo
jengefu vya akili zao kupitia msisimko wa hamu kubwa ya mapenzi. Mmoja wao alikuwa ni
kiongozi mashuhuri sana wa kijeshi wa karne iliyopita huko Ulaya, Napoleon
Bonapatre.
Bonapatre
alipohamasishwa na mke wake wa kwanza Bibi Josephine alikuwa ni mtu
asiyezuilika wala kushindika kwa urahisi lakini mara tu alipokuja kushawishika
kumuacha akamweka pembeni na kumchukua
kimada mwingine, anguko lake lilikuwa dhahiri, akatupwa kama mfungwa kwenye
Kisiwa cha St. Helen na huo ndio ukawa mwisho wake.
Hata katika vitabu
vitakatifu tunasoma nguvu za ushawishi wa ajabu wa mwanamke Delila kwa Samsoni,
lakini huu tunaweza tukauweka katika zile aina za ushawishi hasi.
Hata leo hii unaweza kuona mifano ya watu wengi maarufu
kama Wasanii, Wanamuziko na Wafanyabiashara wakubwa jinsi walivyoathiriwa na
kuwaacha wanawake wa ujana wao, mafanikio yao yamebadilika na kushuka chini
tofauti na vile walivyokuwa na ushawishi wa wapenzi wao wa mwanzo waliokuwa
wakiwapenda kwa dhati.
Wengine hata ikiwa kama
hawakushuka chini baada ya kuwaacha na mifano tunayo hata hapa Tanzania, lakini
ukweli unabakia palepale kwamba Wanawake wao hao wa kwanza ndio waliofungua
ukurasa wa mafanikio yao.
Mbali na kupata
mafanikio makubwa kutokana na shauku kubwa ya mapenzi, kuna watu wengine
hujishusha wenyewe kufikia hali ya wanyama wadogo kutokana na matumizi mabaya
ya nguvu hii kubwa.
Sababu kubwa kwanini kila penye mafanikio ya mwanaume
nyuma yake kuna mwanamke ni kuwamba, hamu ya kujieleza kimapenzi ndiyo mhemko
wenye nguvu zaidi na msukumo kuliko mihemko mingine yote ya binadamu. Na
kutokana na sababu hii kubwa, hamu hii inapotumiwa na kugeuzwa katika kitendo
kingine tofauti na vitendo vya kimwili inaweza ikampandisha mtu kufikia hadhi
ya juu kabisa iwe ni katika mafanikio kiuchumi au hata katika uongozi.
Mwandishi anazidi kubainisha watu zaidi waliopata
mafanikio makubwa baada ya ushawishi wa wanawake waliowapenda kwa kumtaja
mfanyabishara mmmoja wa Kimarekani aliyekiri kwamba Katibu Muhtasi wake
aliyekuwa anavutia ndiye aliyekuwa anahusika kwenye mipango yake mingi
aliyokuwa anaitengeneza. Alikiri kuwa uwepo wa mrembo huyo ulimuinua hadi
vileleni mwa Ubunifu Jengefu.
Anaendelea kusema kwamba mmoja wa watu waliofanikiwa
zaidi Marekani anawiwa na mafanikio yake mengi kwa ushawishi wa mwanamke kijana
mchangamfu sana ambaye alitumika kama chanzo chake cha ushawishi kwa zaidi ya
miaka 12
………………………………………………
Mpenzi
Msomaji wangu, tukutane Sehemu ya Tatu (iii) ya uchambuzi wa Sura hii ya 11 ya
kitabu cha FIKIRI & UTAJIRIKE.
Asante
sana!
Peter
A. Tarimo.
Njia
2 Unazoweza kukipata Kitabu kizima cha FIKIRI & UTAJIRIKE (Think & Grow
Rich-swahili edition
1. Nakalapepe(softcopy) kwenye Simujanja yako, Ingia katika mtandao huu wa GETVALUE na uweze kukipakua ndani ya muda mfupi.
2. Kitabu
cha karatasi (Hardcopy), wasiliana na sisi kwa namba 0765553030 au 0712202244
tutakuletea popote ulipo nchini Tanzania.
0 Response to "KWANINI WANAUME WENYE MAFANIKIO NA UTAJIRI MKUBWA CHANZO NI USHAWISHI WA WAPENZI / WAKE ZAO? (Sura ya 11 ii)"
Post a Comment