Kunufaika
zaidi na semina hii unahitaji kuwa na michanganuo ya Jane Fast Food na Jane
Restaurant katika lugha ya kiswahili na kiingereza.
Katika kila mpango wa biashara Muhtasari ni lazima uwepo pale mwanzoni kabisa na huandikwa baada ya kuandika sehemu nyingine zote. Kazi zake kubwa ni;
· kutoa picha kwa ufupi ya andiko lako zima kwa
kuangazia maeneo yote muhimu.
· Kumpa msomaji wa mpango wako uelewa wa jumla wa kile
unachotaka kumueleza kabla hata hajasoma andiko lenyewe zima
· Kumpa yule msomaji asiyekuwa na muda mwingi wa kusoma mchanganuo wako wote ufupisho utakaomsaidia kupata zile pointi muhimu.
Urefu wa Muhtasari tendaji
haupaswi kuzidi ukurasa mmoja au miwili na aya zinapaswa kuakisi sura za andiko
lako.
Katika Muhtasari wako
unatakiwa kuweka yafuatayo;
Utambulisho/utangulizi
Hapa unamdokezea msomaji wako
kile unachotaka kuandika katika aya moja. Kwa mfano kwemye Jane Restaurant
tumeanza na Dhamira ambayo ni “kuwapa
wateja wake mlo mzuri wenye afya katika mazingira mazuri na rafiki kwa bei
watakayoimudu” mstari huo unatosha kabisa kumjulisha msomaji juu ya ni nini
biashara yako inahusika nacho.
Biashara na Fursa iliyopo
Elezea kwa kifupi kuhusiana
na biashara au kampuni yako ukijumuisha jina la biashara, kile unachouza, unawauzia
kina nani na wako wapi. Yapo mengi kuhusiana na bidhaa au huduma unayouza
lakini weka maelezo kwa kifupi sana.
Tathmini ya soko na Sekta
Taja muelekeo au vitu muhimu
kwenye sekta na biashara uliyopo, nguvu zako za kiushindani dhidi ya washindani
na eleza kwa ufupi kuhusu wateja wako watarajiwa ubainishe ni kwanini wanunue kutoka
kwako na wala siyo kwa wapinzani wako.
Mikakati na Utekelezaji
Eleza kwa kifupi mkakati wako
wa masoko jinsi utakavyotangaza bidhaa/huduma zako na njia utakazotumia kuwafikia
wateja. Onyesha pia ratiba ya matukio muhimu kwenye biashara yako, mhusika
atakayesimamia pamoja na bajeti.
Usimamizi na Uendeshaji
Eleza kwa kifupi yale mambo
muhimu kuhusiana na timu yako ya utawala mfano wasifu wa waanzilishi wa
biashara au watendaji wakuu. Pia eleza kwa kifupi jinsi shughuli za kila siku
zinavyoendeshwa katika biashara yako mfano ikiwa utatumia njia fulani ya
kipekee au mfumo wa usimamizi unazitaja hapa.
Mpango wa Fedha
Hesabu kwenye mpango wako
zipo nyingi na huwezi kila moja ukaiweka katika muhtasari, fikiria mpango wako
ni kwa ajili ya nini, je ni wa kuombea fedha benki? kuvutia wabia? hivyo weka
kiasi cha fedha unachohitaji na kile ulichokuwa nacho tayari. Na ikiwa lengo la
mchanganuo wako ni kuonyesha tu jinsi utakavyoendesha biashara yako kwa
mafanikio basi weka katika muhtasari wako sehemu ya hesabu inayoonyesha ukuaji
wa biashara yako.
Hitimisho
Unaweza pia kuweka hitimisho
kwa kuandika sentensi chache fupi na zenye kushawishi zinazoelezea andiko lako
zima na kumwacha msomaji na hamu ya kutaka kuusoma mchanganuo wako mzima.
Hitimisho lisizidi aya moja.
0 Response to "SEMINA SIKU YA NNE: JINSI YA KUUANDIKA MUHTASARI TENDAJI (EXECUTIVE SUMMARY) -JANE RESTAURANT"
Post a Comment