Blog ya jifunzeujasiriamali mwaka wetu mpya wa 2022 tayari umekwishaanza na kama ilivyokuwa ada huwa kila mwaka kipindi kama hiki hapa kwenye Blogu natoa Dira itakayoenda kutuongoza kwa mwaka mzima zikiwemo kaulimbiu na malengo ya mwaka.
Kaulimbiu yetu mpya
ya mwaka huu ni; BADILISHA TABIA KUJENGA TIJA NA UFANISI ZAIDI. Kauli hii itakwenda
sambamba na ile ya mwaka jana ya "MTEJA NI KILA KITU, WAJALI WATEJA WAKO” Kwani
tija ni nini kwenye mafanikio kifedha? Tija maana yake ni faida. Na ufanisi ni
nini? Ufanisi maana yake ni ubora katika utendaji(efficiency). Kwa ujumla tunakwenda kujifunza utamaduni wa jinsi ya kujenga tija na ufanisi katika biashara au kazi zetu.
SOMA: Ukitaka mafanikio ya haraka mwaka 2021achana na mambo mengi komaa na siri hizi mbili (2) tu
Kwangu binafsi na
timu nzima ya Jifunzeujasiriamali mwaka 2021 unamalizika tukifurahia kutimiza
moja kati ya malengo muhimu kabisa tuliyokuwa tumejiwekea. Kukamilisha rasmi
kazi ya kukitafsiri kitabu cha Think & Grow Rich katika lugha ya Kiswahili.
Ikiwa wewe ni mfuatiliaji wa makala zangu, kwa kipindi kirefu kidogo uliona
sikuweza kuwa hewani kama ilivyopasa na sababu kubwa ilikuwa ni jukumu hilo la
kumalizia kutafsiri Fikiri & Utajirike
Napoleon Hill aliweza
kukamilisha kuandika kitabu hiki kwa miaka zaidi ya 20, mimi bila shaka kazi tu
ya kutafsiri isingeliweza kuwa ngumu na ya muda mrefu kiasi hicho lakini pia nathubutu
kusema kwamba haikuwa kazi nyepesi hata kidogo.
SOMA: 2021 amua hatma yako, tengeneza mwaka uliokuwa bora zaidi kushinda mingine yote
Katika safari hiyo nimegundua
kuna vitu vinne (4) ambavyo ikiwa kama nitakwenda kufanya mabadiliko kidogo
basi nitaongeza mara dufu ufanisi na tija katika shughuli zangu nyingine za
kujitafutia pesa. Nitakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wangu
mzima wa utendaji kazi na mambo haya yote nitakwenda kuyashirikisha moja kwa
moja kwa vitendo kwenye kundi langu, MASTERMIND GROUP la Michanganuo-online
kila siku tutakapokuwa tukijifunza elimu ya kifedha.
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake, njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima!
Kupitia mchakato
mzima wa kukitafsiri kitabu cha Think and Grow Rich nilikutana na changamoto
nyingi sana na nikajifunza pia mambo mengi kuhusiana na namna ya kujenga tija
na ufanisi katika kukamilisha malengo. Mengi nitayashirikisha kwenye makala
zangu zijazo katika blogu ya jifunzeujasiriamali lakini pia katika MASTERMIND
GROUP kila siku usiku tunapojadili michanganuo ya biashara za mtaji mdogo zenye
faida ya haraka.
Lengo kuu la mkakati
huu ni kubadilisha kabisa tabia za zamani na kujenga tabia mpya/mazoea ya
kiufanisi na tija kwenye kazi zangu. Kwa mfano kazi nilizokuwa nachukua mpaka
masaa 5 kuzikamilisha sasa hivi inakwenda kunichukua masaa 2 tu. Mkakati huu
pia utanisaidia kujenga mazoea ya kufanya vitu kila siku pasipo kuahirisha-ahirisha
ovyo pamoja na kujenga mifumo ya biashara zenye uwezo wa kuingiza pesa hata wakati nimelala usiku na familia yangu.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
Siyo kwamba naenda
kujaribu mfumo huu hapana, mbinu hizi tayari nimekwisha zifanyia majaribio,
nimethibitisha zinafanya kazi na zinanipa matokeo chanya.
Na
haya ndio mambo yenyewe manne (4) muhimu sana katika safari hiyo ya kutengeneza
tija na ufanisi mkubwa zaidi kifedha
1.
Kupunguza vidakizi (Distractions)
Wakati nikitimiza
majukumu yale ya msingi nitaondoa au kuzima kabisa baadhi ya mitandao ya
kijamii nisiyokuwa na umuhimu nayo. Hakuna sababu ya kufungua facebook,
tweeter, watsap, tick tock, redio, TV, au mtandao mwingine wowote ule wa
kijamii wakati nikitimiza kazi zangu muhimu, vitu hivi nitavitengea muda
maalumu au kutoshughulika navyo kabisa labda tu kuwe na ulazima sana. Sitazima
kabisa simu kwani nategemea kupokea email na simu muhimu za biashara. Aidha
sitatumia muda mwingi kwenye simu, sms watsap meseji au email zenye viashiria
vya kunipotezea muda(Spams) bali zile
tu zenye mlengo wa matatizo ya kweli ya wateja au zilizo na fursa kifedha.
2.
Kukamilisha kazi zangu haraka na mapema zaidi iwezekanavyo.
Nitaacha kabisa
mazoea ya kufanya kazi pale inaponilazimu na kufanya kazi kuwa ni jambo la
lazima kukamilika kwa muda ule niliojipangia kila siku na nitafanya hivyo mpaka
iwe mazoea kwangu. Hii itanisaidia sana kukamilisha zile kazi muhimu katika
masaa ambayo mwili unakuwa na nguvu na tija ya kiwango cha juu. Jioni baada ya
masaa hayo ndipo nitafanya zile kazi zisizokuwa na umuhimu mkubwa au kupumzika
kwa burudani. Nitajitahidi kuamka kila siku saa 11 alfajiri na kumalizia kazi
zangu muhimu saa 8 alasiri kabla sijajiingiza kwenye kazi au majukumu ya ziada.
3.
Kujifunza vitu vipya kila siku.
Hili ni jambo ambalo
sitakoma kulifanya kila siku maisha yangu yote. Kwenye ratiba yangu kila siku
ni lazima nihakikishe najifunza kitu kipya kuhusiana na kazi ninazozifanya
pamoja na kufanya marudio kwa baadhi ya mambo niliyowahi kujifunza siku za
nyuma vikiwemo vitabu maarufu nivipendavyo vikiwemo vya elimu ya kifedha
4.
Kufanya mazoezi na kula kwa usahihi.
Kila asubuhi
nitakapoamka hata kama sitakimbia mchakamchaka au kuruka kamba, nitajinyoosha
viungo vya mwili wangu angalao kwa dakika 15 hivi. Halikadhalika na jioni pia
nitatenga muda kama huo tena kwa mazoezi mepesimepesi. Nitajitahidi kula mlo
kamili kila siku, kunywa maji salama ya kutosha na kulala usiku angalao masaa 5
-6 kwa afya nzuri ya akili yangu. Kabla ya kulala nitafanya tafakuri na mwisho
kusali na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai.
……………mwisho……………
Ikiwa mpenzi msomaji
wangu utapenda na wewe kushiriki nami katika mfumo huu mpya wa maisha
nakukaribisha sana! Njoo kwenye MASTERMIND GROUP LETU mahali pekee mimi na
wanamastermind wenzangu tutakapoonyesha kwa vitendo kila siku namna mfumo huu
wa ufanisi na tija unavyofanya kazi.
Hapa nimeandika kwa
kifupi sana lakini kuna mambo mengi ndani ya Group tutayafanya katika kujenga
tija na ufanisi mkubwa kwenye biashara zetu na maisha kiujumla. Kuthibitisha
kweli tunakwenda kujenga tabia mpya za kimafanikio nitakuwa kila siku kwenye
blog ya jifunzeujasiriamali nikitoa taarifa kwa ufupi ya kile kinachoendelea
ndani ya Mastermind group hilo.
Ikiwa nimefanikiwa kukitafsiri
kitabu cha Fikiri na Utajirike chote, nina uhakika hakuna kitu
kinachoshindikana chini ya jua ikiwa mtu utaamua na ‘kufocus’ kwenye jambo moja
mpaka likamilike mfano malengo ya biashara ya kuingiza pesa kiasi fulani kwa
muda utakaoamua wewe mwenyewe.
Makala hii
imeandaliwa na;
PETER AUGUSTINO
TARIMO
Mwalimu na
Mhamasishaji wa Mafanikio
Simu/Watsap:
0765553030 au 0712202244
0 Response to "JINSI NITAKAVYOONGEZA TIJA ZAIDI NA UFANISI 2022 (HOW AM I GOING TO BE MORE PRODUCTIVE); MAMBO 4 MUHIMU SANA"
Post a Comment