Karibu ndugu msomaji tuendelee na somo letu la elimu ya pesa. Jana sehemu ya kwanza tulijifunza Usimamizi mzuri wa fedha binafsi na leo ni fedha za biashara. Asije kukudanganya mtu kuwa eti ipo siri ya utajiri wa haraka ama dawa ya mafanikio kwenye biashara iwe ni miti shamba au hata ramli zaidi ya uzingatiaji wa mbinu mbalimbali zinazosisitizwa na wataalamu wa biashara katika usimamiaji na matumizi bora ya fedha za biashara.
Sikushauri ufanye lakini: Ikiwa kwa sababu yeyote ile muhimu hauna muda wa kutosha kusoma kikamilifu makala zote hizi mbili hii ya leo na ile ya jana, nakushauri uzingatie tu sentensi hii moja ifuatayo;
[
Jitahidi kwa kila hali kupunguza matumizi na gharama za biashara lakini wakati
huohuo ukiendelea kutoa huduma/bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja
wako mwisho utafanikiwa ]
Unaposikia watu waliofuzu somo la jinsi ya kuondokana na
umasikini haraka, basi ujue watu hao walizingatia vilivyo elimu ya usimamizi wa
fedha na wakaweka katika vitendo elimu hiyo wakijua au hata wakiwa hawajui kama
wanachokifanya ni usimamizi mzuri wa fedha zao. Kuna watu walifanikiwa basi tu
kwa sababu ya ubahili wao huku wenzao wakiwacheka na kuwatania majina mbalimbali kama vile,
“wewe bahili kama mchagga”, sijui “shilingi ikidondoka skafuni bahati mbaya
ukiwa chumba cha operesheni hoi unazinduka” nk.
Unapokuwa na malengo mazuri ya kifedha katika biashara yako
na kuyasimamia vizuri, biashara yako itaweza kuepukana na matatizo yatokanayo
na mzunguko hasi wa fedha kwa kuhakikisha kwamba muda wote ina fedha za kutosha
kujiendesha. Kama mmiliki wa biashara ikiwa utashindwa kusimamia vizuri pesa biashara
yako inaweza ikakumbwa na matatizo yafuatayo;
i)
Biashara kukosa pesa
ii) Kushindwa
kuweka akiba
iii) Kuchelewesha
malipo ya bili mbalimbali
iv) Kulipishwa
faini za ucheleweshaji wa bili na madeni ya biashara
v) Kushindwa
kukopa mahali popote pale
vi) Kuharibu
mahusiano yako na wadau wengine wa biashara
vii) Kushindwa
kutengeneza faida
viii) Na
mwisho biashara kufilisika kabisa na kufa.
Kama ilivuo katika upande wa usimamizi wa fedha binafsi
na kweny upande wa usimamizi wa fedha za biashara nako kuna hatua au MISAMIATI
mikuu inayotumika nayo ni hii hapa chini;
i)
Kuweka malengo ya biashara
ii) Kupanga
bajeti inayotekelezeka
iii) Kurekodi
na kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya biashara
iv) Kupunguza
gharama na kuzidisha mapato
v) Kuweka
akiba
vi) Uwekezaji
– kufanya maamuzi mazuri katika uwekezaji wa fedha za biashara
Bajeti ni mipango, unapanga matumizi yako ya biashara au
gharama ziwe vipi kulingana rasilimali zilizopo na faida inayoingia. Rais mmoja
wa Marekani Benjamin Franklin aliwahi kusema hivi; “Kushindwa kupanga ni Kupanga
kushindwa”
Tofauti
kati ya Usimamizi wa fedha binafsi na Ule wa fedha za Biashara
Kama tulivyoona jana kwenye utunzaji na usimamizi wa
fedha binafsi za mtu mwenyewe, na kwa upande wa biashara pia kunahitajika
usimamizi mzuri wa fedha ili biashara ikue na isife. Njia za kusimamia na
kudhibiti matumizi ya fedha kwenye biashara zinafanana kwa kiasi kikubwa na
zile za mtu binafsi isipokuwa tu kuna tofauti kadhaa hasa katika utekelezaji
wake.
Kwa mfano wakati mtu binafsi yeye anaweza asimshirikishe
mtu mwingine katika zoezi la usimamiaji wa fedha zake, kwa upande wa biashara
mmiliki atahitajika kuwashirikisha wadau wengine mbalimbali wa biashara yake
hasa wafanyakazi na wasaidizi wanaohusika kwenye utendaji wa kila siku wa
shughuli za biashara. Tofauti pia ipo kwenye malengo yanayowekwa na kila
upande. Malengo ya kifedha ya mtu binafsi hayawezi yakafanana na malengo ya
kifedha ya biashara.
Kwenye upande wa biashara unaweza ukatumia mifumo ya
usimamizi wa hesabu kwa kompyuta(accounting
software) kusimamia fedha za biashara yako vizuri wakati kwa upande wa mtu
binafsi mifumo hii siyo kawaida sana kutumika na mara nyingi inapotumiwa basi
ni kwa kiwango kidogo na sanasana katika sura ya applications za kwenye simu za
kisasa/apps za simujanja.
Tofauti nyingine pia ipo kwenye dhana hizi mbili,
Kujilipa mwenyewe na kuwekeza faida katika biashara. Ingawa vitu hivi viwili
kimsingi vinafanyika katika pande zote mbili lakini havina maana inayofanana
kila upande. Kujilipa mwenyewe kwa upande wa mtu binafsi kunaweza
kukafananishwa na kule kujiwekea akiba ya dharura asilimia 20% wakati kujilipa
mwenyewe katika upande wa Biashara kunamaanisha mshahara unaojimegea kila mwezi
au kila siku kutokana na faida inayoingizwa na biashara.
Kwa ujumla tofauti zipo nyingi ingawa ni ndogondogo
lakini ni za msingi kabisa na hazipaswi kupuuzwa hata kidogo, ndio maana
itakuwa vizuri sana ikiwa mtu atasoma masomo yote haya mawili la jana na hiili
la leo kwa ukamilifu wake bila ya kuachia njiani.
Uhusiano
mkubwa uliopo kati ya Usimamizi mzuri wa fedha Binafsi na ule wa fedha za Biashara
Ingawa tunasema Fedha za biashara na fedha binafsi
zinapaswa kutenganishwa kama maji na mafuta lakini vitu hivi viwili ni kama
ndugu mapacha vile, mmoja akiumwa na mwingine atanyongonyea tu hata kama hana
homa.
Mara nyingi chanzo cha fedha za biashara huwa ni akiba
inayowekwa kutokana na fedha binafsi za mmiliki wa hiyo biashara wakati pia
fedha za mmiliki mfukoni mwake kuna wakati zinatokana na gawio la faida inayotokana
na biashara.
Nasisitiza faida au kwa maneno mengine ile fedha mmiliki
anayojilipa mwenyewe kutokana na faida ya biashara na wala siyo kutokana na
mtaji wa biashara. Kama hamna faida ni bora kabisa ukaahirisha kujilipa
mwenyewe. Hivyo AFYA NZURI ya fedha za kila upande ni jambo lenye manufaa
makubwa kwa mmiliki wa biashara, biashara yenyewe na wadau wengine mbalimbali
wa biashara.
Naona nisikuchoshe mno na maelezo hebu sasa moja kwa moja
nikakudondolee hatua kwa hatua mbinu maridhawa za matumizi na usimamizi bora
kabisa wa fedha za biashara. Zipo mbinu kubwa……………………..
Ndugu msomaji wangu, somo hili litakamilika leo katika MASTERMIND-GROUP letu la MICHANGANUO-ONLINE. Siyo masomo yote ndaniya hii blogu tunayoweka nusu, ni baadhi tu ya masomo kwa lengo la kuhamasisha wale walio na kiu ya kujifunza zaidi na kwa kina mada hizi kujiunga kwani siyo kila mtu anapenda kusoma aina ya mada zetu kwa kirefu, wengine wana interest na mada zingine tofauti.
Ndani ya group na channel yetu utapata somo hili likiwa kamili part I & part 2, pia unaweza ukalihifadhi katika kifaa chako, simu, flash au kompyuta kwa ajili ya matumizi ya baadae.
· Ili kujiunga na GROUP hili mshiriki analipa kiingilio cha mwaka mzima na kisha kuunganishwa na group la watsap lenye pia channel ya Telegram ya masomo mengine yote yaliyopita zaidi ya 70.
· Ukijiunga mapema unapata zawadi ya kitabu cha MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI BURE
Kujiunga na Group lipia kiingilio shilingi
elfu 10 kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao,
“NIUNGE MASTERMIND GROUP-2022”
Namba zetu ni; 0765553030 au 0712202244
JINA: Peter Augustino Tarimo
Vitabu vyetu hapo chini ukiwa popote pale nchini Tanzania na nje ya nchi tunakufikishia kwa uaminifu mkubwa, kuvipata wasiliana nasi kwa namba 0765553030 au 0712202244
Nimependezwa Sana na vitabu hivi
ReplyDelete