Bila shaka umewahi kusikia maajabu mengi ya watu
waliofanikiwa kimaisha haraka au ndani ya muda mfupi kiasi kwamba mpaka hivi
leo hujaamini bado ikiwa mafanikio hayo yalitokana na juhudi za kawaida. Ni
desturi kwa Waafrika tulio wengi na pengine Binadamu wote wa Dunia ya Tatu kuwa
na imani mbalimbali zisizokuwa na uthibitisho kwamba mafanikio kimaisha kama hayo
lazima nyuma yake kuna nguvu za giza.
Sasa basi ikiwa siyo nguvu za giza ni nguvu gani hiyo
inayowezesha baadhi ya binadamu wenzetu kupata mafanikio ya haraka kimaajabu
namna hiyo? Utasikia mara huyu alianza
na genge tu, mara yule alianza na ufundi viatu nk. lakini sasa hivi ni matajiri
“wakutupa”
SOMA: Jinsi kiwanda kidogo kinavyoweza kukutoa kimaisha nakuwa tajiri wa kutupa
Kuna siri moja kubwa watu wengi hawajaigundua au wakati
mwingine hata wanapoigundua basi hawaitilii maanani kabisa. Kuna hatua katika
biashara mtu kamwe huwezi kulazimisha ikuletee mafanikio haraka. Nasema hivyo
kwani ni leo tu msomaji wangu mmoja alinipigia simu kutaka nimshauri afanyeje
baada ya biashara yake ya duka kuifunga mwezi mmoja tu baada ya kuifungua.
Maelezo yake kwa kina nitayaelezea hapa siku nyingine lakini ninachotaka kusema tu ni kwamba, hatua ya awali ya biashara yeyote ile inataka subira, kujitoa na ubunifu wa hali ya juu pasipo kujali ‘factors’ nyinginezo kama vile washindani, mtaji wa kutosha na eneo ulipo. Una washindani wengi, usikimbie kiholela wewe huna rasilimali za kutangatanga tafuta njia za kukabiliana nao, mtaji ni kidogo- zipo mbinu, eneo ni bovu lakini tayari umeshalivaa, utakimbia? Na ukikimbia je una pesa za pango kwenda kulipia kwingine haraka?. Niliwahi kuandika makala moja hii… Huna mtaji wa kutosha, hukopesheki?, jaribu njia ya kufunga mkanda (bootstrapping). ukiisoma unaweza kujua nasema kitu gani.
Bootstrapping ni dhana ya mtu kujipatia mtaji kwa njia
fupi lakini ngumu na inayohitaji ubunifu. Kwanini tunaona wanaofanikiwa haraka
wanafanya maajabu fulani pengine hata kudhania wanatumia nguvu za giza? ni kwa
sababu Bootstrapping ni ngumu na isiyoweza kuvumiliwa na kila mtu isipokuwa tu
wachache walioamua kujitoa kwelikweli wakisaidiwa na UBUNIFU.
SOMA: Maana kamili ya Ujasiriamali, ulikotoka, Ulipo na Unakoelekea Duniani
Ukweli ni kwamba hatua ya biashara mtu anapokuwa na mtaji
wa kutosha ni rahisi sana kuendesha na haiumizi tena kichwa ndio maana kila
anayefikia hatua hiyo wengine wote humchukulia kama mtu mjanja au mwenye akili
nyingi lakini ukweli ni mtu wa kawaida tu aliyefikia hatua ya biashara
isiyokuwa ngumu.
Pesa ni ngumu kupatikana hivihivi na bila ya mtaji-pesa tusidanganyane
dunia ya leo kufanikiwa biashara kwa
kiwango kikubwa ni ndoto za alinacha. Kuna mengi hapa ya kufafanua pamoja na
zile dhana kwamba, pesa si ishu bali ishu ni mawazo nk. lakini yote hayo
tutayapa muda wa kutosha siku nyingine au kwenye MASTERMIND GROUP letu Watsap
na Telegram(MICHANGANUO-ONLINE-2022)
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2022 njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima!
Tunaweza kwa kutumia biashara zilezile tulizonazo na
tunazoona hazitulipi kihivyo, kutafuta mtaji wa kutosha kufanya mambo makubwa
zadi. Ikiwa mtego mkubwa wa mafanikio upo katika MTAJI basi hatuna budi kutumia kila njia zinazoweza kutupatia
mitaji ya kutosha ili nasisi tuweze kufanya biashara za kijanja zenye mafanikio
makubwa yanayoeleweka.
Mwezi ule wa 11 nilifanya semina ya kuandika mchanganuo
wa biashara ya ufugaji wa kuku watu wengi wakaniona kama mwehu, “kutoka na biashara za kuku? huyu jamaa ana wazimu, kuku nafuga toka
utotoni na sijaona mafanikio yeyote”
alicomment msomaji katika forum moja nilikokuwa natangaza ile semina.
Lakini msomaji yule hajui ni nini kilichomkwamisha katika
ufugaji wake miaka yote hiyo tokea utotoni, ndio maana nikafanya semina ya
kuandika mchanganuo wa biashara ya kuku wa KUOMBEA
MKOPO BENKI. Utafanikiwaje kwa kufuga kuku majike 5 na jogoo 1 ukitumaini
watotoe mpaka wafike kuku 1000, si utaota mvi kabla lengo lako hilo
halijatimia?
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji wa kutosha ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini
Tufike mahali Watanzania tufikirie nje ya maboksi, bila
ya ubunifu na kutafuta mitaji ya uhakika mafanikio kibiashara tutaendelea
kuyasikia kwenye media. Ndio maana mwaka huu 2022 katika MASTERMIND GROUP LANGU nimeandaa biashara ndogondogo Bunifu nyingi
tutakazochanganua kila siku kwa lengo la kujijengea uwezo mkubwa kimtaji.
Hakuna jipya chini ya jua, biashara hizo ni zile zile tulizozizowea lakini KIPYA hapo ni UBUNIFU na njia mpya za kuzifanya zitakazowezesha mzunguko wa fedha
kwenda chapchap.
Nakukaribisha sana kwenye GROUP LANGU, mwaka huu litakuwa
tofaui sana na miaka mingine.
Katika kipindi chote cha uandishi wangu nimeandika vitabu
4 na kutafsiri kimoja. Vitabu hivi vina utajiri mkubwa wa Maarifa ya
ujasiriamali ninayoweza kusema ukivipata vyote hautahangaika kutafuta maarifa
kwingine labda tu utake mwenyewe.
Kwa siku 5 kuanzia leo tarehe 19/12/2021 mpaka 25/12/2021
nimetoa OFFA kwa mtu yeyote kujipatia vitabu vyangu hivyo vyote pamoja na
michanganuo ya biashara kama nitakavyoorodhesha hapo chini kwa Shlingi elfu 11 tu
! Gharama ya vitu vyote hivyo inafika shilingi laki moja siku za kawaida.
JINSI
YA KULIPIA OFFA HII
Unalipa shilingi elfu 10 kupitia namba 0765553030 au
0712202244 na jina ni Peter Augustino Tarimo
Punde tu baada ya malipo hayo, nitakutumia kwa njia ya
Email au Watsap vitabu na michanganuo yote kasoro kitu kimoja tu, KITABU CHA THINK AND GROW RICH CHA
KISWAHILI
Kwa kutumia ile sh. Elfu moja iliyobakia nitakutumia COUPON maalumu itakayokuwezesha
kukinunua kitabu hicho kutoka katika Mtandao wa GETVALUE kwa shilingi elfu moja tu badala ya shilingi elfu 15 bei
ya kawaida. Aidha ni lazima uwe na simu ya Smartphone kupata kitanu hiki.
NB: Unaweza kujipatia offa ya vitabu na michanganuo tu peke yake au pamoja na nafasi ya kujiunga na MASTERMIND GROUP
1. Kupata
vyote viwili tuma kwa sms au wasap maneno, “NATAKA OFFA NA KUUNGWA GROUP”
2. Kupata offa peke yake group hutaki tuma neno, “NATAKA OFFA TU”
*Ukiwa
na akaunti ya telegram unapata pia fursa ya kusoma masomo yetu yote ya fedha
tuliyojifunza siku za nyuma zaidi ya 70.
*Ikiwa
huna watsap wala telegramu, bado tunaweza kukutumia vitabu, michanganuo na
masomo kupitia e-mail yako
ORODHA YA VITU (ITEMS) PAPO KWA HAPO VYA
OFFA YENYEWE NI HIVI HAPA CHINI;
1. KITABU: THINK
& GROW RICH – SWAHILI EDITION –kiswahili
2. KITABU: MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIANALI (New special Edition 2021) - kiswahili
3. KITABU:
MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA - Kiswahili
4.
KITABU:
MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA – kiswahili
5. KITABU:
SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO KWA UFANISI– kiswahili
6. KITABU mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika
vyuo vikuu vingi duniani.- kiingereza
7. Semina
nzima ya siku 4 na Mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa Mayai kuomba
mkopo benki. -kiswahili
8. Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa
biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO
Milling))-kwa kiswahili
9. Mchanganuo kamili wa kilimo cha
Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kiswahili
10. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa Kiswahili
& kiingereza
11. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
12. Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE) -kwaKiswahili
13. Vielezo(Templates) za michanganuo
ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.- Kiswahili & kiingereza
14. Mchanganuo mfupi wa biashara
ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
15. Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza.
Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.
16. Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2022 (MICHANGANUO-ONLINE)
unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali
kwa ujumla
0 Response to "BIASHARA BUNIFU ZA MTAJI MDOGO ZINAVVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA MWAKA 2022"
Post a Comment