Baada ya kumaliza kazi ya kufanya utafiti wetu kuhusiana na biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama na kupata taarifa mbalimbali, sasa tunaweza tukaanza kuandika mchanganuo wetu hatua kwa hatua. Zipo njia tano mtu unazoweza ukazitumia katika kuandika mpango wa biashara yeyote ile kama ifuatavyo;
1. Njia ya kutumia vipengele vya mpango wa biashata(Outlines) ambapo unaorodhesha vipengele vyote
kisha unaanza kuandika kwa undani kimoja baada ya kingine hadi unamaliza mpango
wako mzima
2. Kwa kutumia Vielezo(Templates); Njia hii unafuatisha maelezo yaliyokwishawekwa kwenye kurasa
kwa kuondoa au kubadilisha yale yaliyokuwepo na kuweka yakwako kulingana na
biashara yako
3. Kwa kutumia Michanganuo ya biashara nyingine iliyokwisha kuandikwa
tayari(Business plan samples); Hii unasoma michanganuo mbalimbali inayofanana na wakwako
unaotaka kuandika kisha unaandika wa kwako.
4. Kwa kutumia Programu maalumu za kompyuta za kuandika mpango wa
biashara(Business plan softwares); Hizi ni applications maalumu unazojaza taarifa za biashara
yako na kisha zenyewe zinakutengenezea mchanganuo wako yakiwamo na makisio ya
taarifa zote za mahesabu.
5. Kutumia mchanganyiko wa njia zaidi ya moja au zote zilizotajwa hapo juu.
Katika
mchanganuo wetu huu wa kuku wa nyama wa kuombea mkopo tutatumia njia ya
vipengele vya mpango wa biashara (Business plan outlines). Ingawa vifuatavyo
ndiyo vipengele vinavyounda mpango mzima wa biashara lakini siyo sheria kwamba
ni lazima kila kipengele ukiweke katika mpango wako hata kama kipengele
hakifanyi kazi katika biashara husika.
Weka tu vile
vipengele unavyoona vitafanya kazi au vitafaa kwenye aina ya biashara unayotarajia
kuifanya. Kumbuka lengo hasa la mpango wa biashara siyo kujaza kurasa maneno
matupu bali ni MATOKEO(results) mpango huo utakayoyaleta.
Hata hivyo
kulingana na hadhira au walengwa wa mchanganuo wako inawezekana wakawa
wanahitaji baadhi ya vipengele lazima viwekwe hivyo hauna budi kuviweka mfano
benki au taasisi unayoomba fedha inaweza kukuwekea sharti la kujumuisha
vipengele fulani katika mchanganuo wako.
VIPENGELE
RASMI VYA MCHANGANUO WA BIASHARA
1.0
MUHTASARI
2.0
MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA
2.1
Dhamira kuu
2.2
Malengo
2.3
Siri za mafanikio
2.4
Umiliki wa Biashara
2.5
Kianzio (kwa biashara mpya au historia kwa kampuni iliyokwishaanza zamani)
2.6
Eneo la biashara na vitu vilivyopo
3.0
MAELEZO YA BIDHAA / HUDUMA au VYOTE
3.1
Maelezo ya bidhaa/huduma
3.2 Sifa
za kiushundani au Utofauti wa bidhaa/huduma na za washindani wako
3.3
Vyanzo vya malighafi/bidhaa
3.4
Kopi za matangazo
3.5
Teknolojia
3.6
Bidhaa au Huduma za baadae
4.0
TATHMINI YA SOKO
4.1
Mgawanyo wa soko
4.2
Soko lengwa
4.2.1
Mahitaji ya soko
4.2.2
Mwelekeo wa soko
4.2.3
Ukuaji wa soko
4.3
Tathmini ya sekta
4.3.1
Washiriki katika sekta
4.3.2
Usambazaji
4.3.3
Ushindani
4.3.4
Washindani wako wakubwa
5.0
MIKAKATI NA UTEKELEZAJI
5.2
Mkakati wa soko
5.2.1
Kauli ya kujipanga katika soko
5.2.2
Mkakati wa bei
5.2.3
Mkakati wa matangazo/promosheni
5.2.4
Programu za masoko
5.3 Mkakati wa mauzo
5.3.1
Makisio ya mauzo
5.3.2
Programu za mauzo
5.4
Mkakati wa ushirikiano
5.5
Vitendo na utekelezaji
5.5.1
Uendeshaji
6.0
MAELEZO YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI
6.1
Mfumo wa uongozi
6.2
Timu ya uongozi na wafanyakazi
6.3
Mpango wa mishahara
7.0
MPANGO WA FEDHA
7.1
Dhana/makisio muhimu
7.2
Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even Analysis)
7.3
Makisio ya faida na hasara
7.4
Makisio ya mtiririko wa fedha
7.5
Makisio ya mali na madeni (mizania ya
biashara)
7.6
Sehemu muhimu za biashara
8.0
VIELELEZO / VIAMBATANISHO
· Taarifa za mahesabu
ya fedha kwa undani
· Mahesabu yako ya
nyuma
· Leseni, vibali,
ripoti za kodi, hatimiliki na alama za biashara
· Mikataba mbalimbali
· Orodha ya mali na
vifaa mbalimbali(Dhamana)
· CV za viongozi na
wafanyakazi muhimu
· Kopi za matangazo ya
biashara
Ingawa
Muhtasari ndiyo sura au kipengele cha kwanza kabisa katika mlolongo wa
vipengele kama tulivyoona hapo juu, kwenye kuandika siyo lazima tuanze na
kipengele cha kwanza, tunaweza tukaanza na kipengele kingine chochote kile kati
ya hivyo vinane. Sisi katika mchanganuo wetu huu tutaanza na kipengele cha pili
cha MAELEZO YA BIASHARA / KAMPUNI.
Unapoanza
kuandika sura au kipengele chochote kile acha nafasi ya kuandika muhtasari wa
sura hiyo kisha ukishamaliza kuandika sura nzima ndipo unakuja kumalizia na
muhtasari huo. Jumla ya mihutasari yote 8 katika kila kipengele/sura ndiyo
inayokuja kuunda Muhtasari mkuu wa mchanganuo wako wote ambao ndio unaoanza
pale mwanzoni kabisa mwa mchanganuo wako.
Kwa kawaida
wawekezaji, taasisi za fedha na wakopeshaji wengine huwa wana kawaida ya kutaka
kusoma muhtasari tu wa mpango mzima wa biashara na watahitaji kusoma mpango
mzima mara chache sana hivyo unatakiwa muhtasari wako uuandike kwa umakini ili
uweze kubeba picha halisi ya mchanganuo wako mzima ikiwa ni pamoja na kuonyesha
kwa kifupi vile vipengele muhimu vinavyogusa mkopo au vinavyohitajika zaidi na
wawekezaji / taasisi au benki.
Benki
Ikiwa
unaandika mchanganuo wako kwa ajili ya kuomba mkopo benki au taasisi nyingine
yeyote ile ya kifedha ni lazima utambue kuwa benki au taasisi yeyote ya mkopo
hawawekezi kwenye biashara yako bali wanakukopesha na mwishowe urejeshe fedha
zao zote iwe biashara itafanikiwa au itafeli. Kwa hiyo watataka maelezo
yanayojitosheleza kwenye vipengele vinavyogusa biashara hasa umiliki, maombi ya
mkopo, matumizi ya mkopo, dhamana na jinsi utakavyorejesha fedha zao. Pia
watalenga kwenye kipengele cha makisio ya fedha hasa mtiririko wa fedha
utakavyokuwa.
Wabia/Wawekezaji
Kama
unalenga kuwavutia wawekezaji au wabia basi ni lazima uweke msisitizo kwenye
kipengele kinachoonyesha wewe ushiriki wako katika hiyo biashara ni kiasi gani
na pia mbia atapata asilimia ngapi ya umiliki. Wawekezaji na wabia pia
wanapenda kupata maelezo ya kutosha katika kipengee cha Uongozi na timu nzima
itakayohusika katika uendeshaji wa biashara, sifa, wasifu wao na uzoefu
waliokuwa nao kufanikisha biashara husika.
Baada ya
maelezo hayo machache hebu sasa tuanze kuandika vipengele vya mchanganuo wetu;
2.0
MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA
Sehemu hii ni kwa
ajili ya muhtasari mdogo wa Sura hii mara baada ya kumaliza kuandika sura yetu
nzima
2.1 Dhamira kuu (Mission statement)
Kwenye
dhamira kuu tutaandika, shughuli ile biashara inayokwenda kutekeleza ambayo ni;
“Kuzalisha na kusambaza bidhaa bora za kuku
zilizojaa virutubisho na protini ya kutosha kwa wateja wetu katika eneo la
Bagamoyo na maeneo mengine ya karibu”
2.2 Malengo.(Objectives)
Hapa tutayataja malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu ya biashara hii ambayo ni haya yafuatayo;
1. Kuomba mkopo benki wa shilingi
5,000,000/=
2. Kufuga kuku 2000 katika msimu mmoja
na kuku elfu 16 Kwa mwaka
3. Kutengeneza ajira ya kudumu kwa watu
wawili
4. Kutengeneza jina zuri la kampuni kwa wateja wetu kwa kuwauzia kuku walio na afya kwa bei nafuu.
2.3 Siri ya Mafanikio (Keys to success)
Katika siri
za mafanikio tutataja vile vitu ambavyo biashara inatarajia kuvipa kipaumbele
kusudi iweze kufanikiwa, vyaweza kuwa ni kitu chochote kile na hapa sisi
tutataja;
· Kununua chakula cha kuku kwa bei
nafuu ya jumla kutoka kiwandani moja kwa moja
· Banda la kuku kubwa na lililojengwa
kwa uimara linalotosha kuku 2000
· Uuzaji wa kuku kwa wakati katika wiki
ya 4 – 5
· Kutembelewa na afisa wa mifugo mara
kwa mara
· Kuzingatia kikamilifu kanuni za
ulinzi wa kuku dhidi ya maambukizi ya magonjwa (Strictly biosecurity measures)
2.4 Historia ya Kampuni
Kampuni ya
Tumaini Poultry ilianza rasmi shughuli za ufugaji wa kuku kwa ajili ya nyama
mnamo mwezi Desemba mwaka 2020 kwa kuanza na vifaranga 1000 wa siku moja.
Kampuni kwa mwaka 2022 imelenga kufuga kuku 2000 katika mzunguko mmoja wa siku 44 ambapo kwa mwaka mmoja kutakuwa na
mizunguko/misimu 8. Kampuni inamilikiwa
na Bwana Tumaini Masanja kwa asilimia zote 100% za hisa na imelenga kuomba
mkopo benki wa shilingi 5,000,000/= mwanzoni mwa mwaka 2022 utakaolindwa kwa
dhamana za kampuni na zile za mmiliki mwenyewe binafsi. Mradi huu upo katika
eneo la Kiromo karibu na barabara ya Bagamoyo kilomita 50 kutoka katikati ya
jiji la Dar es salaam.
2.5 Mahesabu ya kipindi kilichopita
(Past performance)
Kipengele
hiki chote kipo kwenye somo hili zima
katika group la masomo la mastermind Michanganuo-ONLINE
2.6 Maombi ya Mkopo.(Fund request)
Kipengele
hiki pia utakipata chote kwenye somo hili zima katika mastermind group la
michanganuo-ONLINE
2.7
Mahitaji ya Mradi
Kwenye
kipengele hiki tutachora jedwali linaloonyesha mahitaji yote ya mradi huu kwa
mwaka 2022 ili biashara iweze kutekeleza malengo iliyojiwekea kikamilifu. Hapa
tutaorodhesha mahitaji yote, kiasi cha fedha kitakachohitajika kugharamia
mahitaji hayo pamoja na chanzo cha fedha kwa ajili ya mahitaji hayo. Kujua
undani wa jedwali hilo pata semina hii nzima.
Vifaranga
Vitahitajika
vifaranga 2000 wa siku moja kutoka kwa
wakala anayeaminika wa kampuni ya kutotolesha vifaranga wa nyama. Kila
kifaranga kitagharimu shilingi 2,000/=
sawa na shilingi 4,000,000/= kwa vifaranga vyote 2000
Chakula
Kitahitajika
chakula starter mifuko 35 na finisher mifuko 45, chakula hiki kitaagizwa moja
kwa moja kutoka katika kiwanda cha kutengeneza chakula cha kuku kwa bei ya
kiwandani ya wastani wa shilingi 70,000/= starter na sh. 65,000/= finisher Kwa kila mfuko wa kilo 50.
Kwa mujibu
wa taarifa za utafiti wetu tulioufanya kule mwanzoni wakati tunaanza semina hii
ambapo kuku mmoja anakadiriwa kula kiasi cha chakula kilo mbili kwa muda wote
wa wiki 4-5, Jumla ya gharama zote za chakula pamoja na usafirishaji wake tangu
siku ya kwanza mpaka kuku wanauzwa wote zinakadiriwa kuwa shilingi 5,375,000/=
Maji
Kulingana na
utafiti tuliofanya kuku mmoja wa nyama kwa wiki zote 4 mpaka 5 anakadiriwa
kunywa kiasi cha maji lita 2, x kuku 2000 jumla ni lita 4000 za maji ambazo ni
sawa na madumu 200 ya lita 20. Bei ya dumu moja la maji inakadiriwa kuwa
shilingi 100, hivyo kwa muda wote gharama za maji ni shiingi 20,000/=
Mabanda:
Kuku 2000
kwa mujibu wa utafiti wetu kama unafuatilia semina hii toka mwanzo tuliona
wanahitaji mita za mraba 200, hili ni eneo lenye ukubwa sawa na nusu ya kiwanja
cha mita 20 kwa 20. Katika mradi huu mmiliki wake hatajenga mabanda yake
binafsi bali atakodisha mabanda yaliyokuwa tayari kwa shilingi 100,000 katika
mzungiko mmoja wa siku 44
Wafanyakazi
Watahitajika
wafanyakazi 2 wa kuhudumia mradi wa kuku na kila mmoja atalipwa shilingi
100,000/= kwa wiki zote 5 za mzunguko mmoja Jumla wote wawili watalipwa sh.
200,000/=
Madawa na chanjo:
Katika
mzunguko mmoja gharama za chanjo, madawa na vitamini kwa kuku wote 2000
zinakadiriwa kufikia shilingi 300,000/=
Viota
Kutakuwa na
viota 20 kila kimoja vifaranga 100. Gharama ya kutengeneza kiota kimoja
inakadiriwa kuwa ni shilingi 10,000 sawa na shilingi 200,000/= kwa viota vyote
20
Joto na mwanga
Vifaranga
wakiwa kwenye viota kwa siku 7 za mwanzo watahitaji taa wastani wa saa zote 24.
Taa 20 za watts 100 zitawaka kwa saa 24,
Taa 20 x 100w = 2000w / 2kW (Kilowat 1 = Watts 1000)
Hivyo
Kilowatt 2 x saa 24 x Siku 7 = 336kWh
Kilowatt-
Hour 1(1kWh) = Unit moja ya umeme, hivyo 336kWh = Units 336
Unit 1 =
shilingi 300, hivyo 336unit x 300 = Tsh. 100,800
Hivyo kwa
siku 7 gharama za umeme zitakuwa ni shilingi 100,800/=
Kwa siku 7
zinazofuata taa kwa ajili ya joto zitahitajika kwa wastani wa saa 12 tu kwa
siku ambapo ni sawa na nusu ya gharama iliyopatikana hapo juu = 50,400
Kuanzia wiki
ya 3 na kuendelea kuku watahitaji taa kwa ajili ya mwanga tu masaa ya usiku na
zitawashwa taa 10 tu katika banda zima kwa wastani wa masaa 10. = taa 10 za
watts 100 x saa 10 x siku 18 = 180kWh x 300 = 54,000
Jumla ya
gharama zote za mwanga na joto ni shilingi 205,200
Matandazo
Wastani wa viroba
30 vya maranda ya mbao vitahitajika katika mzunguko mmoja wa ufugaji na kila kiroba
kimoja kinagharimu shilingi 2000 x 30 = 60,000/=
Vyombo vya kulia chakula
Kila kuku
100 watahitaji kutumia wastani wa vilishio 2 mpaka 3 vya chakula, tukitumia
vilishio 3, kuku 2000 watahitaji jumla ya vilishio 60
Kilishio
kimoja huuzwa kwa bei kati ya shilingi 7,000 – 12,000 tunakadiria bei ya
shiilingi 9,000 kwa kila kilishio sawa na shilingi 540,000 kwa vilishio vyote
60
Vyombo vya kunywea maji
Kwa kila
kuku 100 watatumia wastani wa vinyweo 2 sawa na vinyweo 40 kwa kuku wote 2000.
Kinyweo kimoja ni kati ya shilingi 5,000 – 12,000, tukitumia shilingi 7,500 x
40 = 300,000/=
Kipimajoto (Thermometer)
Kitatumika
kipimajoto kimoja sh. 35,000/=
Gum boots
Pea mbili za
viatu vya kufanyia kazi bandani jumla shilingi 50,000/=
Jedwali la mahitaji (Gharama)
Jedwali
hili kamili unaweza ukaliona kwenye semina nzima iliyowekwa katika channel ya
group la Michanganuo-online
Chanzo cha mahitaji
Mtaji
wa mmiliki |
7,125,200 |
Mkopo
wa Benki |
5,000,000 |
JUMLA YA VYANZO VYOTE |
12,125,200 |
Mpaka hapo tumemaliza kujadili Sura au kipengele cha 2.0
cha BIASHARA/KAMPUNI, Kwahiyo tunaweza kuhamia katika kipengele kingine
chochote kile kati ya vile 8. Hapa sisi kwa mfano tumeamua tuendelee tu na
kipengele cha 3.0 cha BIDHAA/HUDUMA ambapo kama uonavyo kwenye mchanganuo wetu
tumetaja bidhaa yetu kuu kuwa ni kuku wa nyama lakini pia tuna bidhaa nyingine
ambayo ni mbolea ya kuku……
Kupata semina hii ikiwa kamili pamoja na mchanganuo wake
wote katika lugha 2, kiswahili na kiingereza karibu kwenye mastermind group,
mahali unapoweza kupata kila kitu unachohitaji kama mjasiriamali.
Wahi pia offa yetu hapo chini ya kupata vitabu vyetu vyote na michanganuo kabla haijamalizika.
ORODHA YA VITU (ITEMS) PAPO KWA HAPO VYA OFFA KUBWA NA YA MWISHO KWA MWAKA 2021;
1. KITABU: THINK & GROW RICH – SWAHILI EDITION –kiswahili
2. KITABU: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIANALI (New special Edition 2021) - kiswahili
3. KITABU: MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA - Kiswahili
4. KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA – kiswahili
5. KITABU: SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO KWA UFANISI– kiswahili
6. KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.- kiingereza
7. Semina nzima ya siku 4 na Mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa Mayai kuomba mkopo benki. -kiswahili
8. Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili
9. Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kiswahili
10. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza
11. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
12. Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE) -kwaKiswahili
13. Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.- Kiswahili & kiingereza
14. Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili
15. Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.
16. Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2022 (MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla
SOMA PIA NA HIZI:
0 Response to "HATUA KWA HATUA JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUKU WA NYAMA 2000 KUOMBA MKOPO TAASISI ZA FEDHA"
Post a Comment