MAWAZO 10 YA BIASHARA BUNIFU NDANI YA MICHANGANUO-ONLINE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAWAZO 10 YA BIASHARA BUNIFU NDANI YA MICHANGANUO-ONLINE

Ofa ya mwisho ya kufunga na kuanza mwaka

Habari ndugu msomaji wa makala hii,

Leo hii pamoja na ujumbe wa mawazo 10 bunifu ya biashara zinazolipa lakini pia nina habari njema sana kwako ya punguzo la bei ya Vitabu vyangu vyote na michanganuo ya biashara. Mara nyingi nimekuwa nikirudiarudia kutoa offa hii lakini hii ya kipindi hiki itakuwa ni ya mwisho kabisa mpaka tena mwakani kipindi kama hiki, hivyo mdau wangu muhimu wa masomo haya, kama unanifuatilia masomo ninayoyatoa sioni ni kwanini uachie fursa hii adhimu ipite hivihivi bila kuchukua hatua haraka. Mwisho wa offa ni tarehe 10/01/2022, ni siku 3 tu tokea leo.

Watu mara nyingi tumezoea kufanya biashara kwa staili ileile huku tukiendelea kupata matokeo yaleyale kila siku. Lakini kiini hasa cha Ujasiriamali ni kufanya mambo kwa ubunifu na hivyo ndivyo nilivyoanza mwaka huu wa 2022 kwa kuandaa mawazo ya biashara 10 ambazo unaweza kudhani ni biashara za kawaida tu lakini tofauti kubwa ipo kwenye  mbinu za kiubunifu zinazosababisha biashara hizo kuleta faida kubwa na haraka tofauti na vile ilivyozoeleka kila siku.

Jana tumeanza na biashara ya kuuza dagaa mchele na samaki wa majichumvi, biashara hii ukiifanya kimazoea hautakuwa tofauti na maelfu ya watu wanaoifanya kila siku, miaka nenda miaka rudi lakini ukitumia mbinu za kiubunifu wanazotumia baadhi ya wale waliofanikiwa kwenye biashara hii bila shaka utashuhudia tofauti kubwa. Karibu, masomo na michanganuo ya mawazo hayo yote nayaweka kila siku katika channel ya group letu la Michanganuo-online sambamba na masomo mengine yote ya zamani. Ubunifu wa biashara hizi unaweza ukautumia hata kwa biashara nyingine tofauti.

 

FURSA YA MWISHO YA KUPATA VITABU VYANGU VYOTE, MICHANGANUO NA KUUNGWA GROUP LA MASOMO MWAKA MZIMA KWA SHILINGI ELFU 11 PEKEE

Unalipia shilingi elfu 10 kupitia namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wasap au sms usemao “NATAKA OFFA YA MWISHO NA KUJIUNGA GROUP LA MICHANGANUO 2022” Ikiwa hutaki kujiunga na group unataka offa za vitabu na michanganuo tu basi tuma tu neno “NATAKA OFFA YA MWISHO 2022”

Muda huohuo nitakutumia vitu vyote kupitia email yako au watsap isipokuwa kitabu cha Think and Grow Rich ambacho nitakutumia link maalumu ya kukidownload kwa simu yako ya smartphone ukilipia sh. Elfu moja iliyobakia kwa mpesa, Tigo au Mitandao mingine ya simu za mkononi

Nakuhakikishia katika offa hii huna cha kupoteza zaidi ya kunufaika, ukinunua kitabu na michanganuo hiyo mmojammoja utalipa zaidi ya sh. Laki moja. Bado pia unakuwa na fursa ya kuwa ndani ya Mastermind group kwa mwaka mzima bila ya kulipia chochote zaidi.

Ukiwa kwenye group unaweza pia ‘kuaccess’ masomo mengine yote yaliyopita kupitia channel yetu maalumu ya telegramu

Mastermind Group Letu mwaka huu tunaliendesha ‘exactly’ kama lile la Napoleon Hill kwenye kitabu cha Think and Grow Rich Sura ya 18 alipounda kundi la mikutano ya kufikirika na watu mashuhuri kwa lengo la kujenga TABIA kupitia kujishauri binafsi (Autosuggesion) Mikutano hii ya kila siku ilimpa Napoleon Hill uwezo mkubwa waliokuwa nao ‘Mamentors’ wake hao kama vile kina Lincoln, Ford, Emerson na wengineo.

Vivyo hivyo na sisi tumeunda Baraza kama hilo linaloanza kila siku jioni saa 1 – saa 4 usiku mimi mwenyewe nikiwa mwenyekiti . Kujua zaidi juu ya Baraza hili nakushauri usome hiki kitabu cha Think and Grow Rich, kimejaa busara nyingi za kuishi maisha ya mafanikio. Na siyo lazima usome cha kiswahili nilichotafsiri mimi, tafuta hata cha kiingereza kinapatikana bure huko mitandaoni.

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema kwamba mwaka huu wa 2022 kama wewe ni mfuatiliaji wa masomo yangu na  haupo kwenye MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP utakuwa umekosa mambo mengi sana .


SOMA NA HIZI HAPA PIA;-

1. Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado

2. Unajua biasharayenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

3. Mbinu na mikakati ya kuikwamua biashara yako kwenye hali ngumu kipesa

0 Response to "MAWAZO 10 YA BIASHARA BUNIFU NDANI YA MICHANGANUO-ONLINE"

Post a Comment