Makala
ya leo nitakushirikisha kile nilichoandika katika ufunguzi rasmi wa MICHANGANUO
BUNIFU 10 YA BIASHARA ZINAZOONEKANA ZA KAWAIDA SANA LAKINI ZENYE FURSA KUBWA
KUTOKANA NA UBUNIFU ULIOTUMIKA. Katika Group la Michanganuo-online nimeandika
kama ifuatavyo;-
Leo ndio tunaanza rasmi masomo yetu ya Michanganuo kwa
mwaka huu ingawa tulishaanza pale Januari lakini kutokana na group kuwa
halikuwa na watu wa kutosha tukasitisha kidogo.
January niliahidi tutajadili kwanza Michanganuo 10 ya
biashara ndogondogo zenye ubunifu wa kipekee na tayari tulishaandika Mchanganuo
mmoja wa biashara ya kuuza dagaa mchele na samaki wa maji chumvi. Siku
ya leo tunakwenda kuona Mchanganuo wa biashara nyingine, nayo ni; BIASHARA YA
KUUZA MATUNDA KWA UBUNIFU KUONGEZA FAIDA MARA DUFU.
Biashara hizi unaweza ukaziona kama ni za kawaida sana na
zinafanyika na watu lukuki mitaani lakini sisi tumeamua kuzifanya tofauti
kabisa kuongezea ubunifu utakaozifanya ziwe ni za kipekee na zinazomlipa zaidi
yule anayeamua kuzifanya.
Kwa mtindo huo biashara hizi hizi ambazo watu wengi
wamekuwa wakizifanya miaka nenda, miaka rudi kwa minajili ya kupata tu mlo wa
kila siku sasa zitakwenda kuwa na uwezo wa kumfanya mjasiriamali mdogo
asiyekuwa na mtaji aweze kupata mtaji haraka huku akiipanua biashara yake au
kuanzisha biashara nyingine kubwa itakayomfanya hatimaye kupiga hatua kubwa
kiuchumi.
Kwahiyo unaweza ukasema michanganuo hii ama course hizi ni kimbilio la mjasiriamali
yeyote yule anayehangaika (kustruggle)
kupata mtaji wa kufanya biashara kubwa.
Katika Michanganuo hii nitatumia mtindo maalumu uitwao , One Page
Business Plan au kwa kiswahili Mchanganuo Mfupi wa Biashara. One page
simaanishi ni lazima uwe ni wa ukurasa mmoja tu hapana, ingawa pia unaweza
ukaufanya kuwa hivyo.
Hii ni aina ya mchanganuo mfupi, kidogo ungefanana na
Muhtasari ule wa kawaida wa Mpango wa biashara unaokaa pale mwanzoni mwa kila
mchanganuo wa biashara lakini huu unaweza kuwa mrefu hata zaidi ya page moja.
Nimeamua kutumia mtindo huu katika michanganuo hii 10 kwakuwa ni rahisi
mwanafunzi kuelewa misingi muhimu ya uandishi wa michanganuo ya biashara
kutokana na sababu kwamba vipengele vinavyotumika huwa ni vilevile sawa na
vinavyopatikana katika mchanganuo mrefu lakini maelezo yake huwa ni mafupi na
unaandika zile pointi muhimu tu kwanza. Baadae unaweza “ukauextend” ukaongeza
maelezo na mchanganuo huo ukawa mchanganuo kamili mrefu.
Mchanganuo mfupi wa Biashara unakidhi haja ileile ambayo
mchanganuo mrefu wa biashara ungekidhi, kwa mfano sehemu nyingi wanazoitisha mtu upeleka business
plan kama mabenki na Taasisi nyingine za fedha , wasomaji wa
michanganuo hiyo hupendelea zaidi kusoma
ufupisho wa mchanganuo unaopeleka ili kupata picha halisi ya biashara
yako na ufupisho huo unafanana sana na aina hii ya mchanganuo mfupi ninaouzungumzia.
Hata hivyo katika hili group letu tutaendelea kuwa na
vipindi vya masomo ya jinsi ya kuandaa michanganuo ya kawaida mirefu ya
biashara sawa na ile inayopatikana katika kitabu chetu cha Michanganuo ya Biashara na ujasiriamali.
Je, Kuna Tofauti gani kati ya Mchanganuo Mfupi na Mchanganuo Mrefu?
· Tofauti
kubwa ni wingi au uchache wa maelezo tu lakini aina zote mbili ni kitu kilekile
kimoja kwa maana ya maudhui kwani mchanganuo mfupi hugusa kila kipengele muhimu
kinachopatikana katika mchanganuo mrefu.
· Mchanganuo
mfupi huchukua muda mchache zaidi kuandaa
· Unaweza
kubadili mchanganuo mfupi kuwa
mchanganuo mrefu au kinyume chake pia
Faida za Mchanganuo mfupi;
· Humwezesha
mjasiriamali kupata picha kamili/ ramani
ya biashara yake kwa haraka
· Humwezesha
hadhira/msomaji wa mchanganuo wako kuifahamu biashara yako kwa urahisi.
· Ni
rahisi kuandaliwa hata na mtu ambaye hana uzoefu mkubwa wa kuandaa michanganuo
mirefu ya kawaida
Kwanini
huwa tunaandika Michanganuo ya Biashara?
· Faida
ya kwanza na kubwa zaidi ya kuandika Mpango/Mchanganuo wa Biashara ni ili uweze
kutusaidia katika uendeshaji wa biashara zetu kwani mchanganuo wa biashara ni
sawa na ramani/dira inayotuonyesha njia kule tuendako kibiashara.
· Unapojifunza
au kuandika Mpango wa biashara ni sawasawa tu na mtu anayejifunza biashara
kwani mchanganuo hugusa kila kipengele kinachohusiana na biashara kuanzia
bidhaa/Huduma mpaka maswala ya fedha na Usimamizi.
· Umuhimu
mwingine ni kama vile, kuombea fedha mabenki au taasisi za kifedha, kuvutia
wabia, kwa ajili ya mafunzo nk.
Kwa maelezo hayo ndugu mdau
wangu wa Michanganuo-online nikuombe tu kwamba usikose mfululizo wa masomo haya
kila siku usiku kuanzia saa 2 mpaka saa 4. Pia tafadhali sana wajulishe na wale
uwapendao juu ya darasa hili la kipekee kwa mwaka 2022.
Kiingilio hiki cha shilingi
elfu 10 kwa mwaka mzima ukilinganisha na manufaa ya darasa hili vikiwemo vitabu
na Michanganuo, hakika unaweza kudhania ni karibu kabisa na bure.
· Je, ungependa
kuufahamu ni ubunifu wa aina gani uliotumika kwenye biashara hii ya kuuza
matunda?
· Na
je, ungependa kujifunza hatua kwa hatua jinsi mchanganuo wa biashara hii
unavyoandikwa?
· Na
je, Ungependa kuuliza swali lolote kuhusiana na biashara hii au mchanganuo wa
biashara kwa ujumla?
· Na
je, Ungependa kufahamu kwa kina hatua mbalimbali biashara inazopitia , siyo ya
matunda tu bali hata na aina nyinginezo za biashara ili uweze kuandaa mpango wa
biashara yeyote ile nyingine kwa wepesi?
Ikiwa majibu ni ndiyo basi
huna haja ya kuchelewa, jiunge na MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP LEO Kwa
kulipa kiingilio chako sh. Elfu 10 tu mwaka mzima. Namba zetu ni 0765553030 au
0712202244 Jina NI Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wasap au sms
usemao;
“NIUNGANISHE NA GROUP LA
MASOMO 2022 PAMOJA NA OFFA YA KUFUNGA USAJILI”
Nimetoa offa mara nyingi
siku zilizopita na wengi walizichangamkia, OFFA
hii hapa chini itakuwa ndio ya mwisho kwa kipindi cha hivi karibuni kwani pia
tunatarajia kufunga usajili rasmi wa Wanagroup ifikapo tarehe 15/3/2022 hivyo
unaweza kuona jinsi ambavyo nafasi ya kujiunga na group letu hili inavyozidi
kupungua.
Ningefurahi sana kuona pia
unapata masomo yote mazuri ya kipekee ndani ya MICHANGANUO-ONLINE kama
unavyopata masomo kupitia blogu yako hii.
NB:
Ikiwa utahitaji offa hii peke yake, hupendi kujiunga na magroup basi nijulishe
pia.
OFFA
YA KUFUNGIA USAJILI WA WANAGROUP LA MICHANGANUO-ONLINE MPAKA- 15/2/2022
1. KITABU cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili
2. KITABU:
MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
3. KITABU mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN
ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha
kiingereza
4. Mchanganuo
wa Biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza WINE na JUISI ya ROSELA-kiswahili
5. Mchanganuo
wa biashara: Kiwanda kidogo cha kukoboa Mpunga (Kikundi cha Akina Mama) -kwakiswahili
6. Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji
nafaka –(USADO Milling))-kwakiswahili
7. Michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku,
kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wakienyeji-yote
kwa kiswahili
8. Mchanganuo kamili wa kilimo cha tikitimaji
(KIBADA
WATERMELON)-kwa kiswahili
9. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa
Kiswahili & kiingereza
10. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
11. Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
12. Vielezo vya michanganuo
ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. -Kwa Kiswahili & kiingereza
13. Vipengele vya Mpango wowote
ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika
busiMchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika.
14. Somo
maalumu la mzunguko wa fedha. -Kwa
Kiswahili
15. Kuunganishwa
group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima
0 Response to "JE, UNAIJUA NJIA HII RAHISI ZAIDI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO?"
Post a Comment