KITABU CHA BURE (FREE E-BOOK) JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO MFUPI WA BIASHARA YAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KITABU CHA BURE (FREE E-BOOK) JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO MFUPI WA BIASHARA YAKO

Kuandika mpango mfupi wa biashara /ukurasa mmoja wa mchanganuo

DOWNLOAD KURASA 7 ZA MWANZO ZA E-BOOK HII uzisome, utanufaika na template/kielezo kitakachokuwezesha kuandika mchanganuo mfupi (one page business plan) wa biashara yako (biashara ya aina yeyote ile) hata kama wewe ni mvivu kiasi gani kuandika.

E-Book hii ina kurasa 74 na hizi ni kurasa 7 pekee. Unaweza ukajipatia e-book hii nzima kwenye kifurushi maalumu cha (OFFA ya vitu 20) niliyoandaa kwa ajili ya wale wote wanaojiunga na Semina kubwa mwaka huu wa 2022 ya JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA katika MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE inayoanza rasmi siku ya Ijumaa jioni tarehe 1/4/2022

Semina/Course hii pamoja na vitu hivyo 20 ambavyo ni Vitabu 4, Michanganuo ya Biashara 12, Templates 2, somo maalumu 1 na kuunganishwa Mastermind group la Michanganuo-online mwaka mzima, kwa pamoja vitakuwezesha wewe kama Mjasiriamali kufahamu vyema na kwa urahisi jinsi ya kuandaa Mchanganuo wa biashara yeyote ile, iwe kubwa au ndogo, ya kuuza Bidhaa ama Huduma.

Aidha kwa yule mwenye ndoto ya kuwa Mtaalamu wa kuandikia Watu na Makampuni michanganuo kwa ajili ya biashara zao kama mimi mwenyewe nifanyavyo HAPA KWENYE KAZI ZETU, anaweza kutimiza ndoto hiyo bila wasiwasi wowote kupitia semina hii.

 

MAMBO 3 YA KIPEKEE KWENYE SEMINA YA MWAKA HUU: 

              i)      Hatuna cheti cha kawaida cha karatasi bali cheti cha ushiriki ni Mchanganuo wako mwenyewe wa biashara utakaoandika hatua kwa hatua huku tukikushika mkono. Mwisho wa semina kila mshiriki atakuwa na mchanganuo wake kamili mkononi.

 

              ii)     Ijapokuwa kozi hii ina muda maalumu wa kumalizika lakini mshiriki anaweza kujiunga siku yeyote kabla ya siku ya mwisho ya semina na akapata masomo yote ya sehemu iliyokwishafundishwa sawasawa tu na wale waliotangulia kujiunga huku akiendele na masomo yaliyobakia.

 

             iii)     Mkufunzi wa semina atakuwepo hewani siku zote za semina saa 1 – 6 usiku bila kujali kama ni muda wa masomo au la kusudi aweze kuwasaidia washiriki waliochelewa kujiunga na wale ambao watakuwa hawajaelewa baadhi ya vitu na wanahitaji muda wa ziada kufafanuliwa. Atakuwa akijibu kila swali litakaloulizwa na washiriki moja kwa moja kwenye Mastermind Group la Michanganuo-online.

 

             iv)    Tutatumia mtindo (Staili) mashuhuri sana iliyotumiwa na Napoleon Hill katika Kitabu cha Think and Grow Rich alipokuwa akifanya Mikutano na Washauri wake wa kufikirika (kwa wale waliowahi kusoma kitabu cha Think and Grow Rich Sura ya 14) mtindo huu ambao Kanuni ya mwisho ya 13 ya Matumizi ya Mlango wa sita wa fahamu (The sixth sense) hutumika unaweza kufanya maajabu makubwa sana katika mtu kujifunza jambo lolote lile jipya. Hivyo Hii ni semina ya kipekee sana haijawahi kutokea popote Tanzania wala A. Mashariki.

KWANINI NIMETUNGA E-BOOK YA ONE PAGE B/PLAN?

Kabla mtu hujajiunga na Corse hii wala kutoa elfu 10 yako kama ada, ni vizuri kwanza ukafahamu kuandika mchanganuo mfupi kabisa wa biashara yako (ONE PAGE BUSINESS PLAN) ambao mfano wake ndio niliouweka kwenye utangulizi wa kitabu hiki kwenye kurasa chache za mwanzo nilizotoa free, kisha maelezo kwa kina na mifano zaidi nikaviweka katika sura zinazofutata.

Nimefanya hivi kwani najua siyo kila mtu anapenda kuandika mchanganuo mrefu unaochukua muda mwingi wakati mwingine mpaka hata wiki moja kumaliza wakati ukurasa mmoja wa mchanganuo dakika 15 tu unaweza kufanya kazi ile ile mchanganuo mrefu unaweza kufanya mfano, kuonyesha wadau kama vile taasisi za kifedha, benki, wabia na hata kwa ajili tu ya uendeshaji mzuri wa biashara yako kiufanisi.

E-book hii inakupa misingi muhimu sana katika uandishi wa mpango wa biashara yako. Template niliyoiweka pale mwanzoni inakuwezesha kuandika vile vitu vya msingi kabisa katika mchanganuo wowote ule duniani kwa dakika zisizozidi 15 uwe ni mtaalamu wa kuandika michanganuo ama hujui chochote juu yake.

Mchanganuo mfupi (One Page Busines Plan) unaweza kuandika vipengele vichache kabisa vikaenea kwenye ukurasa mmoja tu sawa na mfano niliokuwekea kwenye utangulizi (template) hiyo au unaweza kuandika kurasa mbili tatu kama mifano mingine utakayoiona katika sura za kitabu (e-book) hiki zinazofuata, ni rahisi sana kuandika!

Hata ikiwa huna haja na Course hii basi nakusihi sana ukopi hiyo template hapo kwenye utangulizi wa kitabu kama ilivyo na ujaze vipengele vyake vyote ukivihusianisha na biashara yako, ukimaliza utakuwa tayari umepiga hatua moja kubwa sana katika kuifikisha biashara yako viwango vingine kwani zoezi hilo litakuwezesha kubaini maono na malengo uliyokuwa nayo juu ya biashara yako, ni wapi unataka kufika, ubayana (clarity) wa kile unachotaka kukifanya, mikakati yako mbalimbali, wateja na washindani wako, mtaji unaohitaji, gharama pamoja na mapato unayotazamia kuyapata.

Jipatie bure kabisa kurasa za mwanzo za e-book hii zikiwa na template / kielezo cha One Page Business Plan, ijaze template hiyo kwa umakini na utakuwa tayari umekwisha andika mchanganuo mfupi wa biashara yako hata ikiwa kama huna uzoefu wowote na michanganuo ya biashara.

Ukihitaji Kitabu kizima (E-BOOK HII) pamoja na OFFA ya Vitabu na Michanganuo halisi 20, jiunge na Semina yetu kubwa ya mwaka 2022 ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo kamili wa Biashara yeyote ile Hatua kwa hatua inayoanza leo tarehe 30/March 2022 jioni.

Kujiunga, Tuma ada ya Ushiriki Tsh. 10,000/= kisha Ujumbe wa wasap au sms usemao; NATAKA SEMINA KUBWA YA 2022 NA OFFA YA VITU 20. Ikiwa hupendi kujiunga na magroup ongeza hapo neno “BILA GROUP” na nitakuondoa kwenye group mara tu semina itakapomalizika. Kisha utatumiwa papo hapo offa zako zote 20 na kuungwa kwenye group na Channel ya masomo.

Ikiwa hutumii watsap wala Telegramu tutakutumia kila kitu kupitia njia ya email.

Nambari zetu za Simu ni; 0765553030 au 0712202244 jina ni PETER AUGUSTINO TARIMO.

OFFA hii ya vitu 20 ni kwa ajili ya watu 30 tu wa mwanzo na itamalizika rasmi tarehe 10 April 2022. Baada ya tarehe hii kujiunga na group kunaweza kukawepo lakini bila ya offa hii. Pia wakifika watu 30 mapema kabla ya tarehe 10 offa itakuwa imekomea hapo.

Semina hii Haitaathiri programu zetu nyingine za kawaida kwenye group za kila siku kama vile Michanganuo 10 bunifu na Masomo ya mzunguko wa fedha, vyote vitaenda sambamba.

 

Ifuatayo ni Listi ya Vitu 20 vya OFFA kubwa semina ya Kuandika Mchanganuo 2022;

  

                      1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                      2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

                      3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                      4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                      5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

                      6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

                      7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

                      8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

                      9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

                    10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

                    11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

                    12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

                    13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                    14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

                    15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

                    16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                    17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                    18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

                    19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

                    20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

                    21.    Kunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima


 

IMEANDALIWA NA;

PETER AUGUSTINO TARIMO

MTAALAMU WA MICHANGANUO YA BIASHARA.

(BUSINESS PLAN EXPERT)

 

0 Response to "KITABU CHA BURE (FREE E-BOOK) JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO MFUPI WA BIASHARA YAKO"

Post a Comment