Somo
letu la kwanza kabisa lilikuwa na vitu hivi 5;-
1) Maana ya Mchanganuo / Mpango wa biashara
2) Majina mbalimbali ya
mpango wa biashara
3) Ni kina nani wanaohitaji
mpango wa biashara
4) Aina za michanganuo ya
biashara na tofauti zake.
5) Matumizi ya mpango wa
biashara
1. MAANA YA MPANGO WA
BIASHARA
Kwanza
kabla hatujajua maana yake niseme kwamba ukiona nimetumia neno Mchanganuo wa
biashara ni sawasawa na neno Mpango wa
Biashara, hivyo usije ukadhani ni vitu viwili tofauti hapana.
Mchanganuo wa biashara kwa
kimombo (Business plan) ni maandishi yanayoelezea kila jambo kuhusu biashara
unayoiendesha, mambo hayo ni, malengo, mikakati, bidhaa/hudumu utakayouza, soko
(wateja), shughuli mbalimbali za masoko na uongozi, gharama, mahitaji, na
masuala yote yanayohusiana na fedha.
Hata hivyo hakuna maana moja tu ya mpango wa biashara,
maana zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya mpango wenyewe kwani pia kama
tutakavyoona huko mbele kuna aina nyingi za mipango ya biashara. Hivyo hapa
chini nitaweka maana nyingine za mpango wa biashara ukiacha ile ya kwanza hapo
juu.
Mchanganuo wa biashara ni dira au
ramani ya biashara yako kuonyesha unakotoka na
unakokwenda. Basi.
AU
Mpango wa biashara ni jumla ya maelezo yote yanayoihusu biashara, kuanzia
malengo ya biashara mpaka mbinu mbalimbali zitakazotumika kufanikisha biashara
husika. Ni dira au ramani inayokuongoza katikabiashara yako kujua unatoka wapi
na unaelekea wapi.
AU
Mpango wa biashara ni andiko linaloelezea fursa ya kibiashara kwa
wawekezaji na taasisi za kifedha.
AU
Mpango wa biashara ni mpango kazi unaoonyesha kila shughuli
itakayofanyika katika biashara yako.
2. MAJINA MBALIMBALI YA MPANGO WA BIASHARA
Unaweza
kusikia sehemu mbalimbali yakitajwa maneno tofauti yanayomaanisha kitu kilekile
kimoja na mpango wa biashara ni hivyohivyo. Baadhi ya maneno yanayomaanisha au
kuhusiana kwa karibu na mpango wa biashara ni haya yafutayo;
· Mpango
wa biashara lenyewe
· Mchanganuo
wa biashara.
· Andiko
la biashara.
· Upembuzi
wa biashara
· Mpango
kazi
· Andiko la mradi.nk.
3. NI KINA NANI WANAOHITAJI MPANGO WA BIASHARA?
· Wale
wanaotaka kuanzisha biashara mpya
· Wenye
biashara zilizokwisha anzishwa siku nyingi
· Wawekezaji,
mameneja wa mabenki na wabia
· Wafanyakazi
katika taasisi mbalimbali
· Wanafunzi katika taasisi za elimu na vyuo
4. AINA ZA MICHANGANUO
YA BIASHARA NA TOFAUTI ZAKE.
Michanganuo
ya biashara ipo ya aina nyingi kulingana na ni malengo gani umekusudia
kuutumia;
i)
Kwa ajili ya matumizi ya ndani
ii) Kwa
ajili ya matumizi ya nje
iii) Kwa
ajili ya biashara mpya,
iv) Kwa
ajili ya kuendeleza biashara iiliyokuwepo,
v) Kwa
ajili ya bidhaa mpya katika soko,
vi) Kwa
ajili ya kutafuta masoko nk.
Yote
hiyo ni aina ya michanganuo ya bioashara na vipengele vyake huwa ni vile vile
ila tofauti yake tu ni kwamba kila aina huzingatia vipengele fulani zaidi
kuliko vingine, kwa mfano inategemewa kuwa mchanganuo kwa ajili ya biashara
mpya utakuwa na vipengele vichache tu wakati kwa biashara ya zamani vipengele
huwa vingi zaidi, kwa ajili ya matumizi ya ndani kwa mfano kuna vipengele
kabisa havina umuhimu wa kuviweka mfano, kipengele cha historia ya kampuni na
Bidhaa kutokana na sababu kuwa tayari wdau wa ndabi ya kampuni wanavifahamu
vizuri.
5. MATUMIZI YA MPANGO WA
BIASHARA
a) Kuanzisha
na kuendeleza biashara mpya;ni dira itakayokuongoza katika safari ya
kufanikisha biashara yako.
b) Kuweka
na kufafanua malengo pamoja na mikakati uliyojiwekea.
c) Kuombea
mikopo kutoka taasisi za fedha.
d) Kupima
utekelezaji wa malengo mara kwa mara pamoja na kufanya marekebisho pale ulipokosea.
e) Kuainisha
mikataba baina ya wabia.
f)
Kutathmini bidhaa mpya, kuzitangaza au
kupanua bidhaa za zamani.
g) Kuweka
viwango katika biashara/kampuni kwa
ajili ya kuiuza au kwa ajili ya maswala mengine ya kisheria.
h) Ni
kipimo cha uwezo wako kibiashara.
Mawasiliano
yetu ni; 0765553030 AU 0712202244
Kujiunga na semina mara moja pamoja na kutumiwa vitu 20
vya offa muda huohuo huku ukiendelea kujifunza mwaka mzima, lipia ada yako sh.
10,000/= kisha tuma ujumbe usemao, “NATAKA
SEMINA-2022 NA OFFA YA VITU 20”
OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO JUMLA ITEMS 20, INAYOISHA TAREHE 30/05/2022
1.
KITABU cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha
kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa
biashara (One Page Business Plan) -cha
kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
KITABU
mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN
ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza
5.
KITABU
cha
mwandishi Tim Berry cha JINSI YA
KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha
kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara
ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo
kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo
Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama-
kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku
wa nyama- kwa
kiingereza
11. Mchanganuo
Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai -
kwa kiswahili
12. Mchanganuo
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji
(KIBADA
WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo
wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa
kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo
wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo
cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa
kiingereza
20. Somo
maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. Kunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima
0 Response to "NINI MAANA YA MCHANGANUO WA BIASHARA? - SOMO LA KWANZA-2022"
Post a Comment