KUHUSU SEMINA YA MWAKA HUU 2022
Semina ya kuandika mpango wa biashara au mchanganuo wa biashara, ni masomo ya kina 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara yatakayotolewa kwenye group hili la MICHANGANUO-ONLINE kila siku kwa washiriki watakaopenda kufuatilia masomo hayo sambamba na programu zetu nyingine kwenye group.
Kwa wanafunzi wapya watakaokuwa wakijiunga wanaweza kufuatilia semina katika channeli yetu ya telegramu au kutumiwa semina nzima katika email huku wakiendelea kusoma somo la kila siku toka kwa mkufunzi. Mwanagroup ambaye tayari amekwishaelewa masomo haya ana hiyari ya kutohudhuria somo la siku akaendelea kuhudhuria tu programu nyingine.
Washiriki wapo huru kuuliza swali lolote lile pale wanapokuwa hawajaelewa na mwisho wa semina kila mshiriki atakuwa ameandaa mpango wa biashara yake atakayochagua yeye mwenyewe huku akipewa usaidizi wa karibu na mkufunzi wa semina.
Tofauti na semina za
miaka mingine hii hakuna mshiriki atakayeachwa nyuma kwa namna yeyote ile
kutokana na vile wakufunzi walivyoamua kujitolea muda wao kuhakikisha lengo la
washiriki linatimia. Maswali yanakaribishwa muda wowote hata ikiwa kama siyo
muda maalumu wa masomo.
Ada ya kujiunga na semina ni sh. elfu 10 na inafanyika ndani ya Mastermind Group la Michanganuo-online kupitia watsap, Telegram na email. Watu 30 wa kwanza watajipatia Offa ya vitabu na michanganuo kamili ya biashara mbalimbali jumla vitu 20, pia kuungwa group la masomo ya kila siku kwa mwaka mzima.
Mwisho wa OFFA ya vitu 20 ni tarehe 30/5/2022
IFUATAYO NI RATIBA YA MASOMO
SOMO LA KWANZA
Maana ya
Mchanganuo/Mpango wa biashara
· Majina mbalimbali ya
mpango wa biashara
· Ni kina nani wanaohitaji
mpango wa biashara
· Aina za michanganuo ya
biashara na tofauti zake.
· Aina za Michanganuo ya
Biashara
· Matumizi ya mpango wa
biashara
SOMO LA PILI
Jinsi ya kuanza kuandika
mpango/mchanganuo wa biashara
· Unaanzaje kuandika
mapango wa biashara?
· Mawazo utayatoa wapi?
· Utafiti wa soko/biashara
au feasibility study
· Vipengele/sehemu za
mpango wa biashara
· Ni kipengele kipi huanza
na ni kipi humalizia.
SOMO LA TATU
Kasha la nje, kichwa cha
mchanganuo na Yaliyomo
Utajifunza ni vitu gani
hukaa nje kwenye jalada na namna ya kuvipanga
Pia utaona ni nini
huwekwa kwenye yaliyomo
SOMO LA NNE
Muhtasari.
· Ni vitu gani muhimu
vinavyounda Muhtasari?
· Mifano ya
muhtasari ya biashara mbalimbali
· Aina za muhtasari
· Muda muafaka wa kuandika
Muhtasari
· Mbinu za kuandika
Muhtasari utakaomfanya msomaji yeyote asiweze kukwepa kusoma mpango wako mzima.
SOMO LA TANO
Maelezo kuhusu biashara
au Kampuni
· Umiliki wa biashara:
kampuni, ubia au mtu binafsi
· Historia ya kampuni.
· Usajili wa biashara
· Jina na eneo biashara
ilipo
· Dhamira kuu
· Maono
· Malengo ya biashara
· Siri za mafanikio.
SOMO LA SITA
Maelezo kuhusu Bidhaa
· Bidhaa au huduma
utakazouza
· Kwanini wateja wanunue
kutoka kwako?
· Faida atakayipata mteja
kutokana na bidhaa au huduma zako
· Namna utakavyopata
malighafi au bidhaa na jinsi utakavyokidhi mahitaji ya wateja
· Teknolojia itakayotumika
· Mabadiliko ya bidhaa au
huduma katika soko kwa siku za baadae.
SOMO LA SABA
Mpango/Tathmini ya soko.
· Wateja wako ni kina
nani?
· Mahitaji ya wateja na
tabia zao
· Kwanini wanunue kutoka kwako
na siyo kwa washindani wako?
· Mwelekeo wa soko na
jinsi wateja walivyosambaa
· Ukubwa wa soko
unalomiliki
· Ukuaji wa soko
· Tathmini ya sekta
uliyopo
· Washindani wako wakubwa
· Tathmini ya Nguvu,
Udhaifu, Fursa na Vikwazo
SOMO LA NANE
Mikakati na utekelezaji.
· Mkakati wa masoko
· Bidhaa/Huduma,
· Bei,
· Matangazo,
· Eneo na Usambazaji
· Huduma kwa wateja
· Programu ya masoko
· Mkakati wa mauzo
· Makisio ya mauzo
· Programu za mauzo
· Utekelezaji/Uendeshaji
· Kazi za kila siku
· Mpango wa utekelezaji
vitendo na muda maalumu wa utekelezaji
SOMO LA TISA
Uongozi na Wafanyakazi
· Mchoro wa Utawala
· Timu ya viongozi, wasifu
wao na majukumu watakayohusika nayo
· Idadi ya wafanyakazi na
sifa zao
· Pengo la wafanyakazi na
mahitaji ya wafanyakazi ya siku za baadae.
· Jedwali la mishahara.
SOMO LA KUMI
Makisio ya Taarifa za
Fedha
· Unaingiza vipi fedha?
· Muhtasari wa mahitaji
yote ya fedha, vyanzo na matumizi yake
· Makisio ya gharama za
awali(unazolipa mara moja)
· Makisio ya
mali(rasilimali) za kudumu
· Makisio ya mauzo
· Makisio ya gharama za
mauzo
· Gharama za kudumu za
uendeshaji
· Makisio ya kodi na riba
ya mikopo
· Makisio ya Faida na
Hasara(Projected Profit & Loss)
· Makisio ya fedha taslimu
(Projected Cash Flow)
· Makisio ya mali na
madeni (Projected Balance Sheet)
· Tathmini ya mauzo
yatakayorudisha gharama zote (Break even analysisi)
· Uwiano wa Sehemu muhimu
za biashara (Business Ratio).
SOMO LA KUMI NA MOJA
Viambatanisho Muhimi
· Majedwali na vielelezo
· Leseni, vibali na
stakabadhi za kodi na benki
· Taarifa za mahesabu ya
nyuma
· Kopi za barua na
mikataba mbalimbali.
0 Response to "RATIBA YA SEMINA: JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO / MPANGO WA BIASHARA 2022"
Post a Comment