Mengine
mawili ni semina ya kuandika michanganuo kama hukubahatika kuipata na la tatu
ni offa zetu za mara kwa mara lakini hii ikiwa ni ya kipekee zaidi kama
utakavyosoma mwishoni mwa makala hii.
Nikukaribishe
tuwe sote mpaka mwisho.
Hata kabla ya ‘janga’ hili la kiuchumi kuanza, bado wengi wetu tulikuwa na sababu
lukuki ni kwanini hatuna mafanikio, utajiri, furaha na upendo kama ambavyo
tungelipenda tuwe navyo. Kila mtu angelitoa sababu tofauti kwa hilo, wengine
wakisema, “ni shauri ya uchumi mbovu”, “kazi yangu siyo nzuri hailipi”, wengine
wangelalamikia mazingira ya biashara na kudai siyo rafiki kwao yanawarudisha
nyuma nk.
Kuna idadi kubwa sana ya watu ambao wangewalaumu watu
waliowazunguka kama vile ndugu, wenza, watoto, familia na hata marafiki wakidai
wao ndio chanzo cha kuporomoka au kudorora kwao kimafanikio. Na sasa hivi
tunaambiwa kuwa sababu ya hali ya kiuchumi kuzidi kuwa mbaya duniani na vitu
kupanda mno bei kunatokana na vita huko Ukraine pamoja na Covid 19. Unaweza
kushangaa kwani ngano na mchele si tunalima wenyewe hapahapa jamani?
Lakini mimi leo ningependa unione wa ajabu kidogo kwa
kukuambia kwamba; sababu zoote hizo ikiwemo na vita ya Ukrain na Corona, wala hazina
lolote lile la kufanya juu ya mafanikio yako katika nyanja zote ikiwemo
kiuchumi na tena nikuambie hakuna sababu yeyote kutokea nje yako wewe inayoweza
kukurudisha nyuma kimafanikio.
Tatizo kubwa lipo ndani yetu sisi wenyewe. Na kama
huamini hebu chunguza kipindi chote cha mdororo wa kiuchumi, je hawataibuka
watu na mafanikio katika nyanja mbalimbali? Je, ni kila mtu atakuwa akikosa
hela ya kula, kununulia mafuta na unga?
Falsafa hii ya Mafanikio nimejifunza kutoka kitabu
mashuhuri cha Think & Grow Rich, (Fikiri na Utajirike)
nakusihi sana kitafute ukisome kama hujakisoma, na si kama napigia debe nakala
ya kiswahili niliyotafsiri ili niuze, la hasha, kinapatikana pia bure kwa
kiingereza huko mitandaoni na unaweza kukitafuta audio au hata softcopy bila
gharama kubwa.
Falsafa hii inatuambia kwamba mtuhumiwa nambari moja wa
matatizo yetu mengi ni UBONGO wetu
wenyewe. ‘The way’ tunavyoyatazama
matatizo ndiyo tatizo lenyewe. Ubongo wa mtu una nguvu kubwa ya kumletea
mafanikio lakini pia Ubongo huohuo unaweza kumsababishia mtu maanguko makubwa
kiuchumi, kiafya na hata kijamii.
SASA
TUFANYEJE?
Dunia
ya mtu ya nje ni sawa na kivuli tu cha Dunia yake ya ndani. Badala
ya kuona vitu vikipanda bei na kusikitika tusijue la kufanya, tukae tubuni njia
za kuongeza vipato vyetu zaidi hasa kwa njia ya kufanya Biashara. Ikiwa vitu
vimepanda bei basi hata bidhaa na huduma unazouza lazima pia upandishe bei,
hivyo mimi hapo sioni kama kuna tatizo. Ikiwa kama huko nje wanatuletea mafuta
kwa bei kubwa wakisingizia vita ya Urusi na Ukraine, basi na sisi tuwauzie
korosho, kahawa na katani yetu kwa bei ileile ya juu.
Kwanini tusiwe kama Vladmir
Putin? Mataifa ya Magharibi wamemwekea vikwazo vikali yeye akawajibu kwa
kuwaambia, “sasa tuone gesi, petroli na ngano mtatoa wapi msipokula jeuri yenu”,
matokeo yake ndiyo mpaka huku na sisi tunalalamika kupanda bei kwa vitu
kulikopindukia, Ulaya yote na Marekani kilio ni hichohicho.
Badala ya kulialia vitu kupanda bei, dawa ni kukomaa tu
na biashara mpaka kieleweke, kama wewe ni mfanyabiashara fanya biashara kisasa,
ikiwa wewe ni mkulima lima kibiashara, mfugaji fuga kibiashara na ikiwa ni
mfanyakazi basi timiza wajibu wako kwa
ufanisi ili kutoa matokeo yanayotegemewa.
Juu ya yote njoo tujifunze biashara na jasiriamali pamoja
ndani ya Mastermind group la
Michanganuo-online. Nakuhakikishia katika michanganuo 22 ya biashara, 10 ya
kwenye kitabu na 12 isiyokuwa kwenye kitabu nitakayokutumia punde baada ya
kulipia ada ya kujiunga sh. Elfu 10,
ukiisoma hakuna biashara itaayokubabaisha kwani mchanganuo unagusa kila hatua
biashara inayopita kuanzia mtaji mpaka mauzo.
Tunayo pia semina ya jinsi ya kuandika mchanganuo wa
biashara yeyote ile inayoendelea kwenye group mwaka mzima. OFFA ya vitabu na
michanganuo, jumla yake ni vitu 20 kama
inavyoonekana hapo chini mwisho. Offa hii ni kwa watu 30 tu watakaowahi
kujiunga kabla ya siku ya tarehe 30/5/2022 hivyo wahi mapema ikiwa utaguswa na
offa hii, sipendi uje kunilaumu, sijui ..ooo…sikupata ujumbe au sababu nyingine
yeyote.
Gharamahalisi ya kila kitu pamoja na kuwa ndani ya group
la masomo kwa mwaka mzima ni zaidi ya shilingi 100,000/=(laki moja) lakini hapa
unalipia shilini elfu 10 tu! Hii ni fursa ya kipekee kabisa kuwahi kutolewa na
mtandao wa jifunzeujasiriamali.co.tz
Namba za malipo ni 0765553030
au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma
ujumbe wa “NATAKA SEMINA NA OFFA YA VITU
20”
Nitakutumia offa zote muda huohuo pamoja na kukuunganisha
na Group na Channel yetu ya masomo na semina.
Kumbuka pia baada ya kujifunza Semina nzima nitatoa kwa
kila aliyeshiriki zawadi ya vitabu vipya 2 vya semina hiyo, cha semina ya
masomo 11 ya msingi na kingine cha Hesabu za mchanganuo wa biashara kwa undani (Advanced Business Plan Financials).
Ukivipata hakuna mchanganuo wa biashara utakaokushinda kuandika. Vyote viwili
vipo tayari vikikusubiri umalize semina.
Vilevile kama ulikuwa hujui ni kwamba OFFA ya safari hii
nimelenga mtu yeyote anayetaka kufahamu michanganuo ya biashara kwa kina kabisa
na hata yule anayependa kuwa Mtaalamu(expert) wa kuandaa Michanganuo ya
biashara kama mimi nifanyavyo kwa ajili ya Makampuni na biashara za watu
binafsi.
Ifuatayo ni orodha ya ya
vitabu na michanganuo utakayotumiwa punde baada ya kulipia semina;
1.
KITABU cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha
kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa
biashara (One Page Business Plan) -cha
kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
KITABU
mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN
ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza
5.
KITABU
cha
mwandishi Tim Berry cha JINSI YA
KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha
kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara
ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo
kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo
Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama-
kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku
wa nyama- kwa
kiingereza
11. Mchanganuo
Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai -
kwa kiswahili
12. Mchanganuo
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa kilimo cha
matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo
wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa
kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo
wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo
cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa
kiingereza
20. Somo
maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. Kunganishwa
group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima.
Kumbuka mwisho wa offa hii ni tarehe 30 na watu wakitimia
30 itakwisha hata kabla ya siku hiyo kufika. Tafadhali mjulishe na yeyote
unayemjali juu ya habari hizi njema.
Ni mimi,
Peter .A.Tarimo
Mfasiri wa Kitabu cha Think & Grow Rich kwa
kiswahili, Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara na pia Mwandishi wa vitabu na
makala za Biashara na Ujasiriamali.
0 Response to "BEI NA GHARAMA ZA MAISHA ZINAZIDI KUPANDA JUU, TUFANYE NINI SASA?"
Post a Comment