Wakati semina
yetu ya Jinsi ya kuandaa mchanganuo wa Biashara ikiendelea siku tunajifunza
somo la Tatu kuhusiana na Cover page au Jalada la nje, kichwa cha mchanganuo na
Yaliyomo alitokea mdau mmoja na kutaka kufahamu zaidi juu ya Biashara ya duka
la rejareja marufu kama duka la mangi au duka la mahitaji ya nyumbani wengine
huliita duka la vyakula.
Hii ni kawaida
katika group letu la MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP kwani tumejiwekea
utaratibu kwamba mdau yeyote anapokuwa na jambo lake linalomsumbua asisite
kuuliza kusudi members na wawezeshaji wengine tuweze kumuondolea dukuduku lake.
Swali hili nililifananisha na hadi mbuzi kufia kwa muuza supu kwani muulizaji
hakuwa anafahamu kama ndani ya Group kulikuwa na Mtunzi wa Kitabu cha Biashara
ya duaka la rejareja ambaye ndiye mimi hapa.
Basi na mimi
sikuchelewa mara moja nikampa majibu kama ifuatavyo;
Mr. Julius binafsi mimi ninao uzoefu na biashara hii ya duka la
rejareja mtaani maarufu kama maduka ya vyakula ila kwa kweli siyo la jumla.
Ninachoweza kusema ni kwamba maduka haya ni moja ya biashara
rahisi sana kuanzisha kwamtaji wowote ule uliokuwa nao kwani siyo lazima uanze
na vitu vingi. Wapo wanaoanzia hata majumbani mwao kwa kuanza na mche mmoja wa
sabuni na mafuta ya kula ya kupima na mwisho wa siku mtu huyohuyo unakuja
kumkuta kakodi fremu mahali anamiliki duka la malaki kama si mamilioni ya pesa.
Tusiandikie mate na wino ungalipo, katika kitabu changu cha
MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA nilielezea “exactly” kwa picha jinsi
nilivyoanzisha duka langu mwenyewe la rejareja pale Msimbazi Kariakoo nikiwa na
mifuko miwili tu ya keki, soda kreti moja na pakiti 4 za biskuti tena nje
barazani, siyo kwenye fremu. Baada ya mwaka sikuwa tena mwenzio, nikawa tayari
nipo ndani ya kiduka changu cha rejareja na msaidizi juu!
Kitafute kitabu hiki ndani nimeweka mbinu nyingi huwezi kuzipata
popote na gharama yake ni shilingi elfu 6 tu soft copy toleo jipya la mwaka 2023, ukihitaji nijulishe.
Baada ya wadau
wengi kutoa oda zao kupata kitabu hiki niliwasihi tuwasiliane ili waweze kukipata
kitabu hiki ambacho ni moja ya vitabu vyangu bora zaidi kuandika kutokana na
uzoefu niliopitia mwenyewe na wala siyo tafiti za kwenye vitabu na google.
“Tuwasiliane Wakuu hiki kitabu is one of my masterpiece,
nimekitunga kutokana na uzoefu wangu binafsi kwa asilimia zaidi ya 80%” Niliwaambia.
0 Response to "NAOMBA UZOEFU KIDOGO KWA ANAYEFANYA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA (MAHITAJI YA NYUMBANI)"
Post a Comment