Habari ndugu mdau wa blogu hii,
Tafadhali kabla hujasoma makala yangu ya leo kwanza
nikupe salamu fupi toka kwa ‘mentor’
wangu Mkuu Napoleon Hill, unaweza pia na wewe leo ukaamua kumfanya kuwa mentor
wako kwa kujiunga na Group letu la Kushauriana- MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND
GROUP. Group ambalo members wake wanaishi hata baada ya kufa kimwili hapa
duniani………...
Unaendeleaje
lakini na mapambano yako dhidi ya
umasikini? Bila shaka nitafarijika ukiniambia bado yanaendelea na moto ni
uleule haujapoa. Aisee tutafute pesa maanake matatizo mengi duniani yanatokana
na umasikini, ikiwa kina Bakhresa, Mo na Bill Gate moto haujapoa sembuse mimi
na wewe?
Tutafute
pesa kwa njia zozote kasoro tu zile haramu na njia moja kubwa zaidi ya zote ni
biashara au uwekezaji tu na si nyinginezo kama alivyonena Napoleon Hill katika
kitabu chake maarufu Think & Grow
Rich miaka zaidi ya 80 iliyopita, ujumbe huu umebeba maana ileile
utafikiria umetoka jana.
Asante
na karibu kwa makala yetu ya leo.
Semina ya masomo 11 ya msingi ya jinsi ya kuandika
mchanganuo wa biashara yeyote ile ya mwaka 2022 ilifanyika ndani ya group la
watsap la Michanganuo-online na tayari semina hiyo imeshamalizika huku
washiriki kila mmoja akijipatia nakala ya kitabu cha semina hiyo nzima.
SOMA: Kwanini kundi la kushauriana(Mastermind Group) ni muhimu kwa kila anayetafuta mafanikio?
Ikiwa kwa sababu yeyote ile hukuweza kushiriki semina hii
lakini ulikuwa na shauku ya kushiriki, leo ninayo habari njema kwako. Bado
unaweza ukaipata semina hiyo kama ilivyo katika mfumo wa kitabu-nakala
tete(softcopy. Kitabu hiki cha kurasa 50 kimerahisisha kwa kiasi kikubwa mno
kazi ya kujifunza namna ya kuandaa mpango wa biashara ya aina yeyote ile iwe
kubwa au ndogo.
Habari njema zaidi ni kwamba kitabu hiki kimeambatana na
OFFA ya kipekee sana ambayo sijawahi hata siku moja kutoa offa yenye kufanana
nayo kwa thamani. Ni kifurushi kamili cha course
ya uandishi wa Michanganuo kinachojumuisha kila kitu mtu anachohitaji kuandika
mpango wa biashara yake mwenyewe pasipo kuhitaji mwalimu au mtaalamu. (A complete course on Business Planning including
books, templates and B.plan Samples) Nimekuandalia materials zote
zinazohusiana na kuandaa mchanganuo wa biashara kwa kiswahili na kiingereza
sehemu moja.
Katika ile OFFA iliyopita ya vitu 20 pameongezeka vitu
vingine 2 ambavyo ni kitabu hiki cha Masomo
11 ya msingi ya jinsi ya kuandaa Michanganuo pamoja na kitabu kingine cha Semina ya Hesabu za Mpango wa Biashara kwa
kina( Advanced Business Plan Financials) ambacho bei yake halisi ni Tsh.
20,000/= Vitabu hivi viwili ni kama Mapacha kwa jinsi vinavyotegemeana.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako
Ukipata Kifurushi/Package hii hakuna mchanganuo wowote
ule wa biashara utakaokushinda kuandika, wala hauhitaji mtu wa kukuelekeza, na
hata kama utahitaji bado utakuwa upo ndani ya Mastermind group la
Michanganuo-online mwaka mzima ambapo utaweza kushea changamoto zako zozote
pamoja na members wengine nikiwemo pia mimi mwenyewe mwandishi wa vitabu na
michanganuo yote iliyopo kwenye hii package.
Si lazima ujiunge na group baada ya kulipia package yako,
wengine huwa tu hawapendi kuwa ndani ya magroup haya ya watsap, hivyo ikiwa
hupendi nijulishe nisikuunganishe nikutumie tu ‘items’ zako huku ukiendelea kuwa na mawasiliano ya karibu kabisa na
mimi kwa usaidizi wowote utakaohitaji mbele ya safari.
SOMA: Nguvu ya Ushirika, Umoja ni nguvu
Lakini pia habari moja ambayo si ya kuvutia sana ni
kwamba OFFA hii ni kwa watu wachache tu
watakaowahi kulipia shilingi elfu 10. Idadi maalumu hata baada ya masaa mawili
na OFFA itafungwa rasmi. Pia muda wa mwisho wa hii OFFA tulipanga uwe ni tarehe
15 June 2022, lakini imebidi tuongeze muda baada ya maombi mengi toka kwa wadau
wetu wa masomo kwa njia ya email waliosema muda ni mfupi mno.
Muda umeongezwa mpaka pale tutakapotoa taarifa nyingine
hivyo ni fursa kwa wale wote ambao walichelewa muda wa awali kulipia. OFFA
ikimalizika ina maana huwezi tena kupata vitabu na michanganuo iliyotajwa pale
chini mwishoni mwa hii makala kwa gharama ya shilingi elfu 10, utalazimika
kulipa kiasi kikubwa zaidi cha fedha au kuikosa kabisa offa yenyewe.
Hivyo nakusihi sana hasa wewe mdau wangu wa nguvu katika blogu
hii na masomo kwa e-mail, ikiwa ulikuwa na shauku ya kujiunga na Mastermind
group langu au kupata a complete course on business planning in
kiswahili & english, basi changamka sasa hivi uidake hii offa kabla
wajanja wengine kama wewe hawajakuzidi kete uje kulipa gharama kubwa bure
kupata vitu ambavyo ungeweza kuvipata kwa buku 10 tu.
SOMA: Tabia 9 zitakazobadilisha maisha yako kifedha
Kukuibia
tu siri za group ni kwamba, katika nusu ya pili ya mwaka huu wa
2022 tayari tumeongeza vipindi vya masomo, kwanza tunakwenda kuwa na programu
ya kusoma vitabu na bila shaka yeyote tutaanza na kitabu PENDWA cha pesa na mafanikio duniani kisichochuja kamwe cha THINK & GROW RICH (FIKIRI &
UTAJIRIKE) tafsiri kwa kiswahili ya kitabu halisi cha mwaka 1938 kama
kilivyoandikwa na NAPOLEON HILL na nilichokitafsiri mimi mwenyewe Peter Augustino
Tarimo mwaka 2021. Kama ulikuwa hujui, kitabu hiki katika top ten ya vitabu bora
zaidi duniani vya uchumi, fedha na mafanikio miaka yote(of all time) kimekuwa
kikiongoza kushika nambari 1
Tutakuwa tukikisoma katika lugha zote mbili kiswahili na
kiingereza kulingana na matakwa ya mtu mwenyewe atakavyojisikia huku mjadala
ukifanyika pia kwa mseto wa lugha zote mbili.
SOMA: Je, ipo kanuni ya mafanikio ya kifedha?: Mtazamo wa kisaikolojia
Pili tutaweka pia msisitizo katika Michanganuo mifupi na
rahisi ya biashara zile zilizokuwa na fursa kubwa ya kulipa haraka kwa
madhumuni makubwa ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo, wale wanaostruggle
(wanaotaabika kupata mitaji ya biashara zao) kutengeneza mitaji yao
wenyewe kwa njia rahisi sana pasipo kumtegemea mtu au taasisi yeyote ile.
Wajasirimali hawa kwanza hawana sifa ya kukopesheka
kabisa, na hiki ndiyo kikwazo chao kikubwa kabisa(their biggest obstacle),
pili hata wakikopeshwa mahali hawawezi wakapewa kiasi kinachoweza kutosheleza
mitaji ya biashara zao kwani wakopeshaji wengi wakiwemo hata na ndugu,marafiki
na jamaa zao wenyewe wanawatazama kwa jicho la wasiwasi mkubwa wakihofia
watakwenda kupoteza pesa hizo kwani hawana dhamana yeyote ile ya uhakika
waliyoiweka.
SOMA: Je, Mtanzania unakopesheka na taasisi za fedha au benki?
Mchanganuo unaweza ukaonyesha wazi kabisa ili biashara fulani
itoboe inahitaji laki 6 au 7, lakini cha ajabu mkopeshaji(ndugu, jamaa, rafiki, Sacoss au Vikoba anampa laki mbili akimsisitizia
eti akomae nazo na kubana matumizi tu atatoboa. Mjasiriamali hawezi kukataa
pesa kwani yeye shida yake kubwa ni mtaji-pesa, huzipokea kwa shingo upande na
kwenda kuwekeza kwenye biashara yake liwalo na liwe.
Lakini ‘masikini’, hauwezi kupita muda mrefu kabla mtaji
huo haujakata kutokana na mzunguko mdogo wa pesa katika biashara ambayo
mjasiriamali anaitegemea kwa kila kitu, hana njia nyingine na hawezi kufa njaa
au ugonjwa na pesa anaziona.
Dawa hapo ilikuwa ni apate tu kiasi cha fedha
zinazotosheleza mahitaji ya kuanza hiyo biashara na mambo wala yasingeenda
mrama kutokana na biashara nayo kuwa ingelizalisha faida ya kutosha. Biashara
nyingi hufa kutokana na ufinyu wa mitaji-pesa
Basi tunakwenda kujadili exactly namna baadhi ya
biashara zinavyoweza kuzalisha faida kubwa kwa muda mfupi hata ikiwa mtaji ni
mdogo kiasi gani. Mtaji utakua
harakaharaka na kumpa mjasiriamali nguvu ya kwenda taasisi kubwakubwa za
kifedha kuchukua mikopo ya maana itakayompeleka viwango vingine, na hapa ndipo
utasikia, ooo, fulani kaingia sijui freemason, sijui madudu gani,
ilimradi tu wampake matope mtu aonekane siyo pesa zake halali.
SOMA: Biashara ya mtaji mdogo yenye faida kuwa zaidi Tanzania ilivyoshangaza darasa la Michanganuo
Hapa naomba nieleweke vizuri, hatuendi kujadili biashara
mpya kutoka mwezini au sayari nyingine hapana, biashara ni zilezile tulizozizoea
lakini tofauti moja tu ni kwamba tutaonyesha ni UBUNIFU gani mtu anaweza akautumia zikalipa haraka na pasipokuwa na
mtaji mkubwa.
Kulipia offa hii spesho nikutumie kila kitu sasa hivi
bila kuchelewa tumia namba zangu hizi, 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo,
kisha ujumbe wa watsap au sms usemao, “NITUMIE
OFFA YA VITU 22” na kama unapenda nikuunge pia na group ongeza hapo maneno,
“NA MASTERMIND GROUP”
Kwa mwaka huu wa 2022 hii ndiyo itakayokuwa OFFA yangu
kubwa ya mwisho, si kama hakutakuwa na offa nyingine ndogondogo hapana, ila hii
ndiyo offa ya kipekee na kubwa zaidi kuliko nyingine zote kwa mwaka huu na
pengine miaka mingine yote. Kumbuka offa ina ukomo wake wakitimia idadi fulani
tu ya watu. Hivyo kama unaihitaji huna sababu za kutokulipia sasa hivi.
Njoo jiunge sasa kwani hii ni fursa ya kipekee kabisa ya
kujifunza kwa kina na kuziishi falsafa za kitajiri ndani ya kitabu mashuhuri zaidi
cha fedha na mafanikio duniani, FIKIRI & UTAJIRIKE au hata wengine
wamediriki kukiita “MSAHAFU WA MAFANIKIO”
Ni mimi,
Peter
Augustino Tarimo
Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara na Mfasiri wa kitabu cha Think & Grow Rich(Fikiri & Utajirike) katika lugha adhimu ya Kiswahili.
0 Response to "JE, ULIKOSA SEMINA KUBWA YA UANDISHI WA MICHANGANUO YA BIASHARA 2022?"
Post a Comment