SOMO LA 10
7.0 MAKISIO YA FEDHA
Mchanganuo wa biashara ni mchanganyiko wa maelezo na namba
zinazowakilisha hesabu na taarifa mbalimbali. Tangu sehemu zilizopita huko
nyuma tulikwishaanza kuona baadhi ya hesabu kwa mfano katika maelezo ya kampuni
tuliona jedwali la vyanzo vya mahitaji kwa biashara mpya pamoja na jedwali la
hesabu za kipindi cha nyuma kwa biashara ya zamani.
Tuliona pia hesabu ya makisio ya mauzo, gharama za mauzo, gharama
za uendeshaji na jedwali la mishahara kwenye kipengele cha uongozi na
wafanyakazi.
Katika kipengele hiki cha makisio ya fedha ndipo unapotakiwa
kuunganisha hesabu hizo nyingine ndogondogo zote na kutengeneza makisio ya
taarifa tatu muhimu ambazo ni, Faida na Hasara, Fedha taslimu na Mizania ya
biashara.
Kimsingi hesabu za mpango wa biashara ni tofauti na hesabu halisi
za kawaida za biashara kwani ni makisio, zinafanana tu kimuundo. Kwa hiyo mtu
hauhitaji kuwa mhasibu au mtaalamu wa biashara aliyebobea ndipo uweze kukisia
taarifa hizo ingawa pia mtu atahitajika kuwa na uelewa wa msingi wa hesabu za
biashara. Ikiwa unaandika mpango wa biashara na sehemu hii inakutatiza unaweza
ukamtafuta mtaalamu au mwenye uzoefu wa kutosha akakusaidia eneo hili.
Tofauti nyingine ni kwamba, hakuna mtu atakayeweza kukuwajibisha kisheria
kwa kukisia mahesabu ya mpango wa biashara yanayotofautiana na hesabu halisi
lakini katika uhasibu unaweza hata kufungwa jela kwa kuandika ripoti za hesabu
zisizokuwa sahihi.
Makisio ya mpango wa biashara mara nyingi huwa tofauti na hesabu
halisi wakati wa kutekeleza mpango na unatakiwa uwe unafanya mapitio kujua
mpango wako wa biashara na hali halisi vimepishana kwa kiasi gani na hivyo
ufanye kitu gani zaidi kurekebisha.
Vipengele vidogo
katika sehemu hii ni hivi vifuatavyo,…………………..
…………………….Inaendelea kwenye group la Michanganuo-online
Semina hii iliyofanyika
katika group la Michanganuo-online unaweza ukaipata muda wowote ule katika
mfumo wa e-book ukiwa mwanachama wa group hilo. Unaidownload katika channel
yetu ya telegram au pia tunaweza kukutumia moja kwa moja inbox katika watsap
ama email yako.
Kama unahitaji kupata
semina hii pamoja na masomo mengine yote yaliyowahi kufundishwa katika group
letu zaidi ya masomo 70 jiunge kwa kutoa kiingilio chako sh. Elfu 10 tu na ada
hii ni ya miezi 12/mwaka mzima.
Kulipia tumia namba
zetu, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na ujumbe watsap
au sms usemao “NATAKA SEMINA KUBWA YA KUANDIKA MICHANGANUO”
0 Response to "MPANGO WA FEDHA"
Post a Comment