Habari za muda huu mpenzi
msomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali
Ni matumaini yangu unaendelea
vizuri, leo nimekuletea somo moja kutoka kitabu cha Think and Grow Rich somo
ambalo wakati mwingine tumekuwa sisi wenyewe tukilitumia kati harakati zetu za
kimaisha kila siku hasa kiuchumi.
“Hapana”
siyo lazima imaanishe kuwa jambo haliwezekani.”
Hivi ni ni mara ngapi umewahi
kukutana na neno hili HAPANA? Basi
hebu tuendelee kusoma nisijemaliza uhondo bure………!
Siku
moja mchana mtu mmoja aitwaye Darby alikuwa akimsaidia mjomba wake kusaga ngano
kwenye kinu cha zamani. Mjombake alikuwa na shamba kubwa ambalo ndani yake
waliishi wakulima wadogowadogo waliokodisha sehemu ya shamba hilo. Taratibu
mlango ulifunguliwa, na mtoto mdogo aliingia, alikuwa ni binti mdogo wa mmoja
kati ya wale waliokodisha shamba,(wapangaji) aliingia ndani na kuketi karibu na
mlango.
Mjomba
alipotazama na kumuona yule mtoto alimpayukia kwa kelele,
“Unataka
nini”
Kwa
unyenyekevu yule mtoto alimjibu,
“Mama
yangu anaomba umtumie senti hamsini”
“Sitamtumia”
Mjomba alimjibu kwa ukali. “Sasa hivi uondoke nyumbani” “Sawa Baba” Mtoto
alimjibu lakini wala hakusogea.
Mjomba
aliendelea na kazi yake, huku akizama kwenye kazi kiasi kwamba hakukumbuka tena
uwepo wa yule mtoto. Alipotazama na kumuona akiwa bado amesimama pale,
alimpigia kelele tena,
“Nilikuambia
uende nyumbani! Sasa ondoka au nitakuchapa” Yule binti alijibu “Ndiyo
Baba", lakini tena hakusogea hata inchi moja. Mjomba alidondosha chini
gunia la nafaka ambalo alikuwa anakaribia kulimimina kwenye kinu cha nafaka,
akachukua kipande cha fimbo na kuanza kumfuata yule mtoto huku usoni akiashiria
alikuwa ameghadhabishwa mno.
Darby
aliyekuwa ameketi pembeni aliishiwa na pumzi, bila shaka alihisi alikuwa karibu
kushuhudia mauaji ya mtoto mdogo. Alitambua mjombaake alikuwa ni mtu wa hasira
kali. Mjomba alipofika pale mtoto alipokuwa amesimama, mtoto haraka alisogea
mbele hatua moja, akamuangalia machoni na kupiga yowe mpaka mwisho wa sauti
yake nyembamba, “NI LAZIMA MAMA YANGU
APATE HIZO SENTI HAMSINI”
Mjomba
alisimama akamtizama kwa dakika moja, kisha taratibu akakiweka kile kipande cha
fimbo chini, akaweka mkono mifukoni akachomoa nusu dolla na kumpatia.
Mtoto
alizichukua zile pesa, na taratibu akarudi kuelekea mlangoni, kamwe hakuyatoa
macho yake kwa mjomba, mtu ambaye punde alikuwa amemshinda. Baada ya kuwa
ameishaondoka, mjomba aliketi chini juu ya boksi na kutazama nje kupitia
dirishani kwa zaidi ya dakika 10. Alikuwa akitafakari kwa heshima
iliyochanganyikana na hofu juu ya pigo alilokuwa amelipata toka kwa yule mtoto
mdogo.
Bwana
Darby, naye pia alikuwa akiwaza. Hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza
kushuhudia mtoto mdogo wa mpangaji kwa
makusudi akimfunza mtu mzima mwenye madaraka.
Je, yule mtoto aliwezaje kufanya
vile?
Ni
kitu gani kilichomfanya mjomba hasira kali zimtoke na kuwa mpole kama
mwanakondoo?
Ni
nguvu gani ya ajabu aliyotumia yule mtoto iliyomfanya mjomba kusalimu amri
mbele ya huyu mtoto?
Maswali
haya na mengine kama hayo yalimulika ndani ya akili ya Darby, lakini hakuweza kupata
majibu mpaka miaka kadhaa baadaye alipokuja kusimulia hii habari.
Jibu
la swali hili litapatikana kwenye kanuni 13 zilizoelezewa ndani ya kitabu cha THINK AND GROW RICH(FIKIRI &
UTAJIRIKE). Jibu ni zima na lililokamilika. Lina maelezo ya kina na maelezo
yanayotosheleza kumfanya mtu yeyote aelewe na kuitumia nguvu kama hiyo hiyo
aliyoitumia mtoto mdogo kwa bahati tu pasipo yeye mwenyewe kufahamu kama
anaitumia.
Nguvu
hii isiyoweza kuzuilika mtu yeyote yule anaweza akaitumia katika kutimiza ndoto
yake yeyote ile katika maisha iwe ni kupata utajiri, au hata mafanikio katika
Nyanja ninginezo za kimaisha.
Kuna watu wengi
wamewahi kuitumia Nguvu hii na wakafanya maajabu hapa duniani wakiwemo kina Henry
Ford, Marcon, Wright Brothers , Thomas Edison na wengineo.
Ndugu msomaji Karibu sana kwenye group letu, tayari jana tumeanza rasmi usomaji wa kitabu cha
Think & Grow Rich, kitabu chenye majibu ya mambo mengi magumu
yanayotutatiza katika maisha yetu ya kila siku.
Unaweza
kufuatilia kitabu cha kiingereza PDF au Audio Book ambavyo vyote tunavitoa bure
kwenye group au ukaamua kufuatilia nakala ya kiswahili ambayo unaweza kuipata
kwa bei ya punguzo kwenye mtandao wa GETVALUE
Kujiunga
na Mastermind Group hili, lipia ada ya mwaka mzima shilingi elfu 10 tu ambapo
utapata na offa ya vitu 22, Vitabu,
Michanganuo na Seminars. Lipa kupitia namba 0712202244 au 0765553030
jina ni Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe usemao, “NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22” namimi nitakuunganisha
na kukutumia kila kitu muda huohuo.
Offa
hii imeongezewa muda kutokana na maombi ya wengi wa wadau wetu mliosema muda
ulikuwa hautoshi. Itaendelea kwa muda mfupi kabla haijaondolewa hivyo ni vizuri
kuwahi mapema.
Ndani
ya Mastermind Group la Michanganuo-online mbali na usomaji wa hiki kitabu cha
FIKIRI & UTAJIRIKE pia tunazo programu nyingine mbalimbali zinazolenga
kumjengea uwezo mjasiriamali mdogo na wa kati hasa kwenye eneo la kumiliki
mtaji wa uhakika kwenye biashara zake hata ikiwa hana dhamana za kutosha kukopa
mahali.
OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO INAYOISHIA KARIBUNI NI HII HAPA
CHINI;
1.
KITABU cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha
kiswahili
2.
KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa
biashara (One Page Business Plan) -cha
kiswahili
3.
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili
4.
KITABU
mashuhuri
zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN
ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza
5.
KITABU
cha
mwandishi Tim Berry cha JINSI YA
KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza
6.
Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha
kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili
7.
Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara
ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili
8.
Mchanganuo
kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili
9.
Mchanganuo
Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama-
kwa kiswahili
10. Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku
wa nyama- kwa
kiingereza
11. Mchanganuo
Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai -
kwa kiswahili
12. Mchanganuo
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili
13. Mchanganuo kamili wa kilimo cha
matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili
14. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) –kwa kiswahili
15. Mchanganuo
wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa
kiingereza
16. Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda
cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili
17. Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI
CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili
18. Kielezo cha mchanganuo
wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili
19. Kielezo
cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa
kiingereza
20. Somo
maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili
21. KITABU
CHA SEMINA: Masomo 11 ya michanganuo ya
Biashara
22. KITABU
CHA SEMINA: Hesabu za mpango wa biashara kwa kina(Advanced Business Plan
Financials)
0 Response to "NGUVU YA AJABU ALIYOTUMIA HUYU MTOTO UNAIFAHAMU?"
Post a Comment