Nina mtaji wa shilingi
milioni moja, mtaji wa laki moja, mtaji wa sh. laki mbili, mtaji wa elfu
hamsini(50,000/=) naomba ushauri nifanye biashara gani ya kunilipa nk. ni maswali yanayoulizwa mara nyingi sana
na wajasiriamali wengi mitandaoni na hata nje ya mtandao hiyo.
Binafsi mimi kama mshauri wa wafanyabiashara wadogo na wale wa kati nimewahi kukutana na maswali yanayofanana na hili zaidi ya mara 50 wengi nikiwajibu humubumu katika blogu ya jifunzeujasiriamali lakini wengine nawajibu tu hewani kupitia sms, watsap na simu ya kawaida ya mkononi.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma nipeni ushauri nina wakati mgumu
Mdau aliyejitambulisha kwa
jina moja la Kimaro karibuni naye aliniuliza kama ifuatavyo namimi kama kawaida
yangu sipendi kuongeza wala kupunguza maneno ya waulizaji maswali, nimekuwekea
hapo chini swali lake na majibu niliyomjibu kama ifuatavyo;
Swali:
Salama
mkuu
Naitwa
…Kimaro
Samahani
kuomba ushauri mkuu
Mimi
nina mtaji wa shilingi milioni moja (1000,000), naomba unipe ushauri nitafanya
biashara gani kwa mtaji huo
Majibu:
Ndugu yangu Kimario, suala la kuanzisha biashara halina
tofauti kubwa na suala la mtu kujichagulia mwenza/kuoa au kuolewa. Ni suala
ambalo mara nyingi halitaki mtu kutumia moja kwa moja ushauri wa mtu mwingine
hata ikiwa mtu huyo wa pili ni mzazi nikimaanisha mama yako au baba yako.
Sisemi ushauri wa watu wengine ni mbaya hapana, ila tumia ile falsafa maarufu
ya aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya nne Mh. JK. kumhusu mbayuyayu isemayo, Akili
ya kuambiwa changanya na za kwako.
SOMA: Nataka kufungua biashara ya steshenari mtaji milioni 1.5 nifanyeje?
Hii maana yake ni kitu gani? Akili ya kuambiwa maana yake
ni majibu ya utafiti utakayofanya kwenye lile jambo/biashara unayotaka
kuanzisha sawa tu na mchumba unayetaka kumchumbia. Namaanisha kwamba ukitaka
kuanzisha biashara yeyote ile au kuoa kuna jambo moja la msingi sana unalopaswa
kulifanya kusudi uweze kufahamu biashara sahihi ya wewe kuifanya au mchumba
sahihi anayeweza kuwa mke wako ni yupi.
UTAFITI
AMA UPEMBUZI YAKINIFU kwa mujibu wa Kitabu changu kikubwa cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kitabu kilichokuwa na kila kitu
mjasiriamali yeyote anachohitaji kufanya biashara ya kisasa, ndiyo jibu la
maswali yoote niliyotangulia kuyataja pale mwanzoni ya “Nina mtaji wa shilingi milioni kadhaa nifanye biashara gani, au nina
mtaji wa laki kadhaa nitafanya biashara ipi itakayonilipa vizuri.”
SOMA: Ishi kama Mbayuwayu, akili za kuambiwa changanya na za kwako
Kwahiyo Mr. Kimaro majibu yangu kwa kifupi sana mimi
nakushauri kama ulivyoniuliza unamaanisha sasa hivi unafanya utafiti wa wazo la
biashara itakayokufaa. Sasa binafsi siwezi kukujibu kafanye biashara fulani
labda genge, duka au saluni hapana, jibu la ni biashara ipi inakufaa linatakiwa
litokane na mazingira yakwako wewe mwenyewe unavyoishi. Chunguza ni mahitaji
gani katika jamii/eneo unaloishi watu wanataabika sana kuyapata, wazo la
biashara pia linaweza likatokana na ujuzi au taaluma uliyokuwa nayo, shuleni
ulikuwa unatamani sana kuja kufanya kitu gani? Je una kipaji chochote kile
unachoweza ukakigeuza kuwa biashara?.
Hebu fanya ziara maeneo mbali na pale unapoishi, je
hautagundua biashara ambazo hukuwa unazifahamu hapo kabla na ambazo unaweza
kwenda kuzifanya katika eneo jingine?. Unaweza kubuni kitu fulani kipya kabisa
kama Masudi kipanya alivyobuni gari la kutumia betri ya kuchaji kwa umeme
Tanzania?
Basi ndugu yangu Kimaro(“Boashee”) hizo ni baadhi tu ya mbinu mtu unaweza kuzitumia kupata
wazo la biashara ya ndoto yako sawa sawa
tu na jinsi ulivyompata mke wa ndoto yako(kama
tayari umeoa lakini, kama bado subiri usiwe na papara maisha siyo rehearsal).
SOMA: Mtaji wangu ni mdogo sana lakini nahitaji kufanya biashara na sina ajira naomba ushauri wako
Mbinu zingine na vitu kibao kuhusiana na biashara na ujasiriamali kwa ujumla unaweza ukazipata kwa uzuri zaidi kwenye kitabu chetu hicho cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ambacho kukipata ni rahisi sana, kwani kwa kulipia tu shilingi elfu 10 kwa namba 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo, nakutumia nakalatete ya kitabu hicho muda huohuo kwenye simu yako ya mkononi au kompyuta iwe ile ya mezani, tablet au mpakato.
Makala hii imeandaliwa na;
Peter Tarimo
Mtaalamu wa michanganuo ya biashara na mfasiri wa kitabu cha Think & Grow Rich katika lugha adhimu ya Kiswahili.
Call/Whatsap: 0712202244 / 0765553030
0 Response to "NINA MTAJI WA SHILINGI MILIONI MOJA (1000,000), NAOMBA USHAURI NITAFANYA BIASHARA GANI?"
Post a Comment