Habari za jion hii Wanamichanganuo-oline wenzangu,
Natumaini sote
tupo poa.
Ni wangapi tumemaliza kusoma Utangulizi wa Fikiri &
Utajirike(Think & Grow Rich?
Ni wangapi tumesoma nakala ya kiswahili? Nadhani wengi
tutakuwa tumesoma nakala ya kiingereza kwani wengi bado hatukuwa tumejipatia
nakala ya kiswahili.
Niwaombe pia wale walionunua nakala ya kiswahili wakapata
changamoto ya kukidownload kama ndugu yangu Bernard Makachia. Hili si tatizo
kubwa tutalitatua na linatokana na kutokufuata vizuri utaratibu kama ulivyoelekezwa
kwenye website ya GETVALUE.
Kwa mfano mr. Bernard tayari kwenye system nimeona
amekwishalipia kitabu lakini tatizo lipo kwenye kulog in katika app ya Getvalue
au kukosea neno siri maana inatakiwa nenosiri unalojisajili nalo kwenye website
liwe ndilo hilohilo utakalo login nalo katika ‘APP’ halikadhalika na email nayo
ni hivyohivyo.
Tafadhali sana naomba tushee hapa kwenye group chochote
kile kuihusu sura hii ya kwanza iwe ni ujumbe ama hata kama ni lugha
imekutatiza mahali fulani unaweza kushea na wanamastermind wenzako ukapata
suluhisho.
Baadae kidogo nitashea yakwangu lakini hebu tuendelee na
mwingine yeyote mwenye mchango. Unaweza kuandika chochote ilimradi kihusiane
nah ii chapter. Kumbuka hii ni Sura ya
kwanza kabisa kwa kiingereza inaitwa INTRODUCTION na kwa kiswahili nilitafsiri
kama UTANGULIZI.
SURA
YA KWANZA KWA UFUPI
Sura hii ya kwanza ni kama mwandishi alitaka msomaji
kupata picha ya ujumbe wa kitabu kizima anataka kuzungumzia nini maana amegusa dhamira kuu ya kitabu chenyewe
kwamba mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu halisi kinachoweza
kushikika mfano wa pesa, majumba, magari
nk. kwa kutumia kanuni maalumu kama zilivyoelezwa kwenye sura 13 za kitabu hiki
ukiacha sura ya kwanza, na ile ya 15.
Ndio maana utaona pia hata baadhi ya mada
zilizozungumziwa humo na hata watu utakwenda kukutana nazo tena kwenyeSura za
kitabu zinazofuata kwa undani zaidi.
Hivyo basi kwa kifupi kabisa mimi nimejaribu ‘kusummarize’ sura hii katika mistari
michache ifuatayo;
v
Mawazo
yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu halisi kinachoshikika kama vile
mali au pesa kwa kutumia kanuni maalumu.
v
Chanzo kikubwa cha kuanguka ni tabia ya kukata tamaa baada ya kukutana na
vikwazo vya muda mfupi.
v
Badala
ya kukata tamaa unapoanguka, tumia uzoefu ulioupata kufanya vizuri zaidi.
v
Utajiri
unapoanza kukujia, huja kwa wingi kiasi
ambacho unaweza ukashangaa ni kwa nini haukuja siku zote ulizokuwa ukisubiri,
na utajiri huo huanza na wazo kichwani pamoja na lengo mahususi pasipo hata chembe ya kazi ngumu.
v
Mafanikio
humjia mtu anayewaza mafanikio, ubongo huambukizwa mawazo tunayofikiri midhili
ya sumaku, na sumaku hiyo huvuta nguvu, watu na mazingira yeyote yale
yanayohusiana na mafanikio.
v
Kwa
hiyo kabla hatujaanza kutengeneza utajiri ni sharti kwanza tuziambukize akili
zetu hamu/shauku kubwa ya kutaka kutajirika baada ya hapo, kuwa na
lengo na kisha kukomalia lengo hilo bila kukata tamaa mpaka pale
tutakapofanikiwa. Waambukize na watu wengine uliokuwa nao karibu (washirika)
ili wakusaidie kukamilisha lengo lako.
Natumaini kila
mmoja wetu atakuwa amekamilisha kusoma sura hii ya kwanza ya kitabu cha Think
& Grow Rich, INTRODUCTION/UTANGULIZI,
iwe ni kwa kiingereza ama kwa Kiswahili.
Leo tarehe
22/06/2022 tutaanza kusoma sura ya pili, DESIRE
/SHAUKU ambayo katika nakala ya kiingereza kuna kurasa 18 na ile ya
Kiswahili kurasa 32
Ina maana kwamba
itatuchukua siku 3 kumaliza sura hii, siku ya kwanza tutasoma hadi ukurasa wa
27 nakala ya kiingereza au ukurasa wa 52 kwa wanaofuatilia nakala ya
kishwahili.
Tukutane jioni
kwa ajili ya kupeana mrejesho wa hizi kurasa 6 za mwanzo za sura ya pili ya
kitabu chetu pendwa SHAUKU au DESIRE.
Kwa anayehitaji
kununua nakala ya kishwahili asiwe na wasiwasi, cha kufanya tu ni kuwa na
smartphone yako, bonyeza linki hii ifuatayo kisha utaingia website ya Getvalue
ukurasa wenye kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION kisha utafuata
taratibu mpaka umejisajili kwa email
yako na nenosiri, halafu utalipia shilingi elfu 6 bei ya punguzo badala ya elfu
10 ya kawaida.
Baada ya hapo
nenda play store kapakue APP ya GETVALUE, inafanana na website yake
kimuonekano lakini ni vitu viwili tofauti. Ukishaipakua tumia ileile email
na nenosiri ulizotumia mwanzoni kwenye website kulogin katika hiyo APP
na mwishowe utaweza kusoma kitabu chako bila wasiwasi wowote.
KUJIUNGA NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE
Ikiwa unapenda kujiunga na group letu la masomo, semina na kupata OFFA ya vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara za Kitanzania zilizo na faia, lipa ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha ujumbe wa wasap au sms usemao. "NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"
Nitakutumia kila kitu na kukuunganisha ba group muda huohuo
0 Response to "TULIVYOANZA USOMAJI WA KITABU THINK AND GROW RICH-SURA YA KWANZA-UTANGULIZI"
Post a Comment