Habari za saa hizi msomaji wa Jifunzeujasiriamaliblog
Juzi niliahidi tutaanza
usomaji wa Kitabu cha FIKIRI &
UTAJIRIKE(THINK & GROW RICH) ndani ya Mastermind Group la
Michanganuo-online na leo ndio ilikuwa siku rasmi ya kuweka ratiba na taratibu
za usomaji wa kitabu hicho kilichobadilisha maisha ya watu wengi mno duniani
kuliko kitabu kingine chochote kile katika tasnia hii ya fedha na mafanikio.
Si kitabu hiki tu bali ni
vitabu vyote, kusoma mpaka mtu umekimaliza chote huku ukiyatia katika vitendo
yale uliyojifunza kwa kweli kunahitaji kujitoa kwa hali na mali, utenge muda
pamoja na kuwa na mpango mkakati uliokuwa wazi kama ambao tutakwenda kuuweka
hapa leo.
Kitabu cha Think & Grow
Rich nakala ya kiingereza( English version) kina kurasa zipatazo 235 wakati
nakala ya kiswahili niliyotafsiri ina kurasa 420 hivyo unaweza kuona kwamba
kiswahili kinahitaji maneno mengi zaidi karibu mara 2 zaidi kuelezea dhana
ileile ambayo imeelezwa kwa kiingereza
Bila kupoteza muda mwingi
ndugu msomaji naomba nitoe utaratibu wa namna tutakavyoendesha zoezi letu hili
la usomaji wa kitabu hiki cha FIKIRI & UTAJIRIKE; ndani ya group hilo
1. Kila
siku tutasoma kurasa 6 za kitabu ikiwa ni nakala ya kiingereza, kwa watakaosoma
nakala ya kiswahili watatakiwa kusoma kurasa 10 mpaka 12.
2. Kila
siku tutakuwa tukipeana mirejesho ya kile tulichojifunza pamoja na ufafanuzi wa
mada ngumu kwa wale ambao watakutana na vikwazo mbalimbali ama kutokuelewa
baadhi ya maneno na sexntensi
3. Kila
mwisho wa Sura pia kutakuwa na muda wa kujadili sura husika, kupeana ufafanuzi
wa mada na maneno magumu kutoka kwa wadau tofautitofauti kwenye group
4. Kitabu
hiki huwezi ukakisoma mara moja tu kikakupa manufaa yanayotarajiwa,
inapendekezwa kurudiwarudiwa hata zaidi ya mara 3. Hivyo na sisi tutafanya
hivyo, mara ya kwanza lengo likiwa ni kuelewa mada mbalimbali na mara ya pili
kufanyia kazi mambo yale tuliyojifunza
5. Tunaanza
rasmi usomaji wa kitabu hiki kurasa 13 za utangulizi leo tarehe 20/6/2022.
Itachukua siku 2 kumaliza kurasa 13 ambapo kwa anayesoma nakala ya kiswahili ni
kurasa 26 naye atazisoma kwa siku 2 pia yaani leo na kesho
6. Jitahidi
usome angalao kurasa 3 asubuhi unapoamka, kurasa moja mchana na kurasa mbili
usiku kabla hujalala. Hata hivyo unaweza kutengeneza utaratibu wako mwenyewe
ilimradi kwa siku utimize zile kurasa 6
7. Unaposoma
jitahidi uwe na notebook kwa ajili ya kurekodi baadhi ya maneno au mistari ile
inayokugusa au iliyobeba ujumbe
Tumeweka katika group nakala
ya kitabu kwa kiingereza pamoja na nakala ya sauti. Kwa anayehitaji nakala ya kiswahili
anaweza kukipata kwa bei ya punguzo ya shilingi elfu sita tu(6,000/=) katika
mtandao wa GETVALUE kupitia link ifuatayo badala ya shilingi elfu 10 ya kawaida;
Fikiri
& Utajirike (Think & Grow Rich-Swahili edition)
Aidha bei hii ya punguzo ya
shilingi elfu 6 itadumu kwa muda mfupi sana kabla haijarudishwa ile ya kawaida ya
sh. Elfu 10, hivyo wahi mapema kupakua(kudownload)
nakala yako pale ukitumia smartphone
yako
0 Response to "USOMAJI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FIKIRI & UTAJIRIKE) KATIKA GROUP"
Post a Comment