Habari
za jioni Mwanamichanganuo-online mwenzangu,
Tukiwa
bado tunaendelea na usomaji wa kitabu chetu cha Think & Grow Rich leo
tarehe 23/6/2022 ni siku ambayo tulipaswa kusoma kurasa 6 za kitabu.
Kwa
wale wasomaji wa nakala ya kiingereza ukurasa wa 28 hadi wa 33 na wale wa
nakala ya kiswahili ukurasa wa 55 hadi wa 66
Binafsi
nitashea kidogo nilivyoelewa lakini pia na wewe naomba useme chochote kile
ulichojifunza katika kurasa hizi 6
Kurasa hizi zimeendelea
kusisitiza juu ya umuhimu wa mtu yeyote anayetaka kufanikiwa kuwa kwanza na SHAUKU KALI ya kile anachotamani
kuwa/kuwa nacho.
Akatolea mfano wa Waotaji ndoto wa zamani (dreamers) waliohusika na uvumbuzi wa vitu muhimu
kabisa dunia inavyojivunia hivi leo
kwamba haikuwa rahisi kwao kama ilivyo kwa waotaji ndoto wa leo, wengine hata
walidiriki kuonekana kama vile ni wenda wazimu kwa kuwa na mawazo au fikra
ngeni zisizotekelezeka mfano mvumbuzi wa redio bwana Marcon marafiki zake
walimpeleka wodi ya vichaa(‘mirembe’)
wakimtuhumu kuwa mawazo yake ya sauti kusafiri pasipo waya yalikuwa sawa na
uchizi.
Ipo pia stori ya mtoto
kiziwi, Blaire ambaye ni mtoto wa kumzaa wa mtunzi wa kitabu hiki mwenyewe Bwana
Napoleon Hill. Hapa Napoleon anazungumzia habari inayomhusu yeye mwenyewe binafsi
tofauti na stori zingine zote kwenye hiki kitabu hivyo unaweza kuona ni jinsi
gani Somo la SHAUKU ya kutaka kutimiza jambo Napoleon amelifafanua kwa uzuri.
Shauku yake ya kutaka mwanaye wa kumzaa asikie na kuzungumza imethibitisha
kanuni hii ya SHAUKU KALI kufanya kazi pasi na shaka yeyote ile.
Pointi muhimu tunazopata
kutoka kwenye hizi kurasa 6 ni hizi hapa;
i)
Ndoto
hazizaliwi hivihivi tu kivivu pasipokuwa na malengo
ii) Wale wote wanaofanikiwa katika maisha,
huanzia na mwanzo mbaya, na kupitia mapambano mengi yenye kuumiza moyo kabla
“hawajafika”.
iii) Mtu hashindwi bali hushindwa tu pale
atakapokubali kushindwa.
iv) Imani, ujasiri na uvumilivu ni hali ya
akili ambayo ukiichanganya na maarifa ya kazi ya kanuni zilizoelezwa, vingine
vyote utakavyohitaji vitakuja kwako utakapokuwa tayari kuvipata
v) Kila rafiki ambaye roho yako inamtamani
mwishowe atakukumbatia.
vi) Akili iliyofungwa haihamasishi imani,
ujasiri wala kuamini.
vii) Kumbuka, nguvu inayohitajika kuweka
malengo makubwa maishani katika kupata mali na utajiri ni sawasawa na ile
inayohitajika kuleta mateso na umasikini
viii) Mipaka yetu pekee ni ile tunayojiwekea
ndani ya akili zetu
ix) Shauku ikisaidiwa na imani haijui neno
liitwalo “haiwezekani”
x) kila mkosi huja ukiwa ndani yake umebeba
mbegu ya neema inayolingana na mkosi wenyewe
xi) Ulemavu unaweza kubadilika kuwa rasilimali.
Naomba
tafadhali tuendelee kujitahidi kusoma kitabu hiki kwani kina mafunzo ambayo
endapo yatafanyiwa kazi yana uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha ya mtu
Siku
ya kesho tarehe 24 tutamalizia Sura hii ya pili kwa kusoma kurasa zilizobakia
kuanzia ukurasa wa 34 – 39 kwa wasomaji wa nakala ya kiingereza na ukurasa wa
67 – 74
Nakala
yeyote ile utakayosoma iwe ni ya kiingereza au ya Kiswahili zote maudhui yake
ni yaleyale ‘mamoja’ pia hata AUDIO book kwa aliye na kifaa cha kusikilizia
vizuri nayo inafaa na hurahisisha sana usomaji kwani unaweza sikiliza hata muda
upo kwenye basi nk. kidownload ubadilishe kuwa mp3 kiwe katika simu au kompyuta
yako.
Kwa
anayehitaji nakala ya kiswahili asisahau kufuata linki hii, FIKIRI & UTAJIRIKE kisha malipo katika mtandao huo ambapo
bei bado ni ya OFFA shiingi elfu 6 tu badala ya shiingi elfu 10. Kabla ya
kulipia soma maelekezo jinsi ya kununua kitabu katika mtandao huo ili iwe
rahisi zaidi kwako
Kwa
yeyote yule anayenunua kitabu akapata changamoto tafadhali asisite kuwasiliana
na mimi ili tutatue changamoto husika.
KUJIUNGA NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE
Ikiwa unapenda kujiunga na group letu la masomo, semina na kupata OFFA ya vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara za Kitanzania zilizo na faia, lipa ada ya mwaka mzima shilingi 10,000/= kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha ujumbe wa wasap au sms usemao. "NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"
Nitakutumia kila kitu na kukuunganisha ba group muda huohuo
0 Response to "USOMAJI WA THINK AND GROW RICH SURA YA PILI SEHEMU YA 2-3"
Post a Comment